Subscribe:

Ads 468x60px

TUJIKUMBUSHE AHADI ZILIZOTOLEWA MWAKA 2010 KABLA YA KUPOKEA ZA 2015



Saturday, August 22, 2015
 Na Serengeti Media Centre(SMC)
Agosti 22,2015.

 
Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 vyama vya CCM,CHADEMA na CUF vilitoa ahadi mbalimbali ambazo  walipanga kuzitekeleza katika kipindi cha miaka mitano.
Ahadi ambazo zililenga kutoa majawabu ya matatizo  ya Ujinga,Umaskini,maradhi na kuimarisha utawala bora kwa jamii.
Kabla ya kuja na ahadi mpya katika kampeini ambazo zimeanza ,hawajarudi kwa wananchi kama sehemu ya tathimini nini tuliahidi,tumetekeleza nini,bado nini,je kuna changamoto mpya,badala yake ndimi zao uhubiri mafanikio tu, kana kwamba waliyoyafanya yako mbinguni ambako hatujafika.
Kazi nyingi zilizofanyika ,utekelezaji wake umewahusisha wanancha kwa nguvu na michango yao,sioni mantiki  ya kuja na maneno mengi kwa kuwa walishiriki katika utekelezaji wake, tunategemea waje waseme kwa yake ambayo hayakufanyika ni kero kwa jamii,kwanini hayakufanyika,na kuna mkakati gani.
Serengeti Media Centre(SMC)inawarudisha kwenye ahadi za vyama vya CCM,CUF na CHADEMA walizotoa mwaka 2010  ili wananchi waone kilichoahidiwa ,kilichotekelezwa na nini wanaleta kipya,je kimezingatia matatizo yao ama yameachwa.
CCM.
Chama cha Mapinduzi (CCM)kupitia aliyekuwa mgombea wake Jakaya Kikwete alitoa ahadi 75 kubwa ,ambazo kama zingetekelezwa taifa lingesonga mbele na kuinua uchumi wa jamii.
Ujenzi reli mpya kutoka Dar es salaam mpaka mikoa ya kanda ya Ziwa(Nzega),Mikoa ya Tanga kuwa jiji la viwanda(Tangamjini)Tabora kutumia maji ya ziwa Victoria(Igunga)kulipa madeni ya chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga(SHIRECU)Shinyanga.
Kumaliza migogoro ya ardhi nchini(Dodoma)Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono(Dodoma mjini)Kuwapatia trekta wakulima –kata ya Mrijo(Dodoma)Wananchi kutoondolewa Ranchi ya Misenyi(Kagera)Kujenga uwanja wa ndege Misenyi(Kagera).
Kupanua uwanja wa Ndege Bukoba(Bukoba mjini)Kujenga uwanja wa Ndege mkubwa Kigoma(Kigoma mjini)Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda(Kagera)Mikoa ya Kagera,Kigoma,Lindi,Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya Taifa ya Umeme(Kagera)Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu(Kagera).
Hukumu kwa waliopatikana na hatia ya kuua  albino(Mbeya)Kununua Meli kubwa kuliko Mv Bukoba(Kagera)Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiliamali,Serikali kusaidia vyama vya Ushirika (Mwanza)Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na waharifu(Mwanza),Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya Mkoa (Geita)Kulinda Muungano kwa gharama zote(Pemba).
Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko ya Kilosa(Morogoro)Kununua Meli mpya kubwa  Ziwa Nyasa(Mbeya mjini)Kujenga bandari Kasanga(Rukwa)Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano (Songea)Kufufua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira(Mbeya)Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani kuzama(Tanga)Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini(Iringa)Kujenga barabara yenye kiwango cha Lami kutoka Same mpaka Kisiwani,Kihunio na kuunganisha na barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam(Same).
Kuboresha barabara za Igunga (Tabora)Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa walimu(Kisesa Magu),Kusambaza vyandarua viwili kwa kila Kaya(Mbeya Mjini),Kuzipandisha hadhi hospitali maalum saba nchini kuwa za rufaa ili kupunguzia mzigo hospitali ya taifa ya Muhimbili(MNH)(Hydom Wanyama).
Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini,kikabila na kisiasa(Musoma)Kulinda haki za walemavu (Makete),Kujenga barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha Lami urefu wa kilometa 109(Iringa mjini),Kuenga barabara ya Lami Musoma –Mto wa Mbu(Arusha mjini),Kuanzisha jimbo la Ulyankulu(Shinyangamjini).
Kujenga barabara ya lami Manyoni Kigoma(Kaliua Tabora)Kukarabati barabara ya Arusha Moshi(Moshi mjini)Kuboresha barabara ya Handeni ,Kondoa mpaka  Singida (Dodoma)Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliokufa wakati wa kiangazi mwaka 2009(Longido),Vijiji vyote vilivyoko kilometa 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria  Shinyanga-Kahama kuunganishiwa Maji,(Shinyanga).
Tatizo la umeme kufika kikomo novemba 2010 mkoa wa Arusha(Arusha mjini)Kukopesha wavuvi zana za kilimo (Busekela wilaya ya Musoma)Kuwapatia maji wakazi wa Longido(Longido)Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti(Ngorongoro),Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri,(Mbulu Arusha).
Kusambaza umeme,utoaji wa huduma za afya,na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji wa ruzuku kwa wakulima 2010-2015(Babati mjini)Kuongeza mara tatu wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo na kilimo kwa mfumo wa Vocha -(Iringa),Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika(Iringa mjini),Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-(Ifunda).
Kutokomeza Malaria 2015(Bunda Mara)Kuwapa wanawake nafasi zaidi(Iringa)Kuisaidia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii(Kibandamaiti mjini Zanzibar),Kusaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada(Kibandamaiti Zanzibar)Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay(Ruvuma)Ununuzi wa Meli Mpya yenye  uwezo wa kubeba tani 400(Mbambabay Ruvuma).
Kufufua chama kikuu cha Ushirika cha wakulima wa Mbinga(Ruvuma),Hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi wa 2010(Dar es Salaam),Mtwara kuwa mji wa viwanda(Mtwara)Ujenzi wa kiwanda cha dawa ya viluwiluwi vya mbu,hospitali ya Tumbi kuwa ya Mkoa(Kibaha),Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalum la viwanda(Kibaha)Ujenzi wa reli kutoka Ubungo hadi Tegeta(Dar es Salaam).
Kujenga kiwanda cha kusindika matunda mkoani Pwani(Kibaha)Kuhifadhi zao la mpunga katika ghala la Taifa (Malinyi),kujenga daraja la Kilombero lenye ukubwa wa mita 400(Morogoro)na kuboresha barabara za vijijini kwa kiwango cha  changarawe(Kilombero)
CHADEMA.
Dk Wilbroad Slaa akinadi sera za chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka 2010 alitoa ahadi 18 kubwa ,iwapo wangeshinda ambazo zingesaidia kukuza uchumi wa taifa na wananchi.
Kurudisha fedha za mradi wa Rada(Moshi),Kushughulikia suala la taasisi ya  kuweka na kuvuna pesa (DECI-Uwanja wa Mashujaa Moshi),Kujenga nchi isiyo na ufisadi(Mwanza)Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili Muungano na Zanzibar(Ifakara)Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo(Arusha) Kukata asilimia 20 ya mshahara wa Rais(Mwanza),Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15(Arusha).
Kuweka Mwenge wa uhuru jumba la Makumbusho(Kilimanjaro),Kutoa huduma bora za afya bure(Mwanza )Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi(Tarime)Kufuta walimu wote wa cheti cha stashahada shule za sekondari na kuleta walimu walio na shahada (Arusha)Kutoa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita(Morogoro).
Kutoa huduma za afya bure kuanzia kituo cha afya hadi hospitali ya rufaa(Mwanza)Kutoa ruzuku taasisi za kidini(Ifakara)Kusambaza magari aina ya shangingi kwa jeshi la polisi ili wakamatie wahalifu badala ya mawaziri kuyatumia(Ifakara)Mfuko wa saruji na bati kuuzwa sh 5,000(Bukoba)Kufuta pocho ya chai serikalini.
CHAMA CHA WANANCHI(CUF)
Tofauti na wagombea wengine Profesa Ibrahimu Lipumba alitoa  10 kubwa ambazo angepata ridhaa zingesaidia kutatua matatizo yanayoikabili nchi na jamii.
Kubadili Katiba na kumteua Dk Mohamed Shein kuwa Makamu wa Rais(Unguja)Elimu ya bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu(Tanga)Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la Mawaziri(Tanga)Kuunda serikali shirikishi(Mtwara)Kusimamia raslimali(Tanga),Kuimarisha miundo mbinu(Kidongo chekundu).
Kusimamia na kuboresha afya(Kidongo Chekundu)Kuboresha kilimo,viwanda na uwekezaji(Mtwara)Kudhibiti uuzaji wa zao la Korosho(Mtwara)na Mfuko maalum wa kusomesha walemavu.
Tusubiri ahadi za Mwaka huu zitakazodumu kwa kipindi cha miaka mitano,Tutaendelea kuwaletea taarifa mbalimbali kadri kampeini zinavyoendelea ili wananchi waweze kuchukua uamzi sahihi wakati wa kupiga kura.