Subscribe:

Ads 468x60px

ZIARA YA WAZIRI MKUU WA THAILAND

 BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WALIOAMABATANA NA WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHINAWATRA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA ASKARI POLISI UWANJA WA NDEGE SERONERA  ULIOKO HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
 WAZIRI MKUU WA THAILAND YINGLUCK SHINAWATRA AKISHUKA UWANJA WA NDEGE WA SERONERA KWA AJILI YA SIKU MOJA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
 WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI DK,MARY NAGU AKISHUKA UWANJA WA NDEGE WA SERONERA NDANI YA HIFADHI YA SERENGETI AKIAMBATANA NA WAZIRIMKUU WA THAILAND
 WAZIRI MKUU WA THAILAND AKISALIMIA VIONGOZI MBALIMBALI
 BAADHI YA VIONGOZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MKUU WA MKOA WA MARA WAKIMSUBIRI WAZIRI MKUU WA THAILAND
 WAZIRI MKUU AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI.

 WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMISI KAGASHEKI AKIONGOZANA NA MGENI WAKE WAZIRI MKUU WA THAILAND UWANJA WA NDEGE SERONERA
 BAADHI YA WAGENI WALIOAMBATANA NAYE
 HATA HAO WALIKUWEPO
 WAZIRI MKUU WA THAILAND AKIWA FOUR SESSION SAFARI HOTEL LTD ZAMANI BILLILA
 TEMBO NI KIVUTIO HOTELINI HAPO
 TEMBO
 TEMBO WAKINYWA MAJI
 ANAANGALIA TEMBO
 HATA HAO WALISHANGAA TEMBO
 UTALII
 WANAFUATILIA MATUKIO KWA MBALI
 KAZI ZINAENDELEA KAMA KAWAIDA KARIBU NA WANYAMA
RAHA YA SERENGETI HIYO,JAMANI MSIWAUE TEMBO NI KIVUTIO

MAZEOZI YA KUJILINDA

 WATOTO WANGU WAKIWA KATIKA MAZOEZI YA UKAKAMAVU.

ZOEZI HILO SASA NI KWA FAMILIA NZIMA KWA LENGO LA KUJILINDA.

UKAKAMAVU

 JAMANI NI MAZOEZI YA UKAKAMAVU MAANA KUNG;OA MENO NA KUCHA KUMENIFANYA NIANZE MAZOEZI YA KUJIHAMI
NDIVYO ILIVYO

KAAMPUNI YA SINGITA GRUMETI RESERVES WILAYANI SERENGETI YAKABIDHI MADAWATI NA VITABU

 MKURUGENZI WA UTALII KAMPUNI YA SINGITA GRUMETI RESERVES JASON TROLLIP BAADA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WALIMU NA VIONGOZI WA KIJIJI CHA NATTA BAADA YA KUKABIDHI MADAWATI 30,MEZA 1,KITI KIMOJA NA VITABU VYA SAYANSI 241 KWA SHULEYA MSINGI MLIMANI NA SEKONDARI ZA ISSENYE NA RIGICHA WILAYANI SERENGETI
 WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MLIMANI KATA YA NATTA WILAYANI SERENGETI WAKIWA WAMEKALIA MADAWATI WALIYOPEWA NA KAMPUNI YA SINGITA GRUMETI RESERVES INAYOMILIKI HOTEL YA SASAKWA YA NYOTA TANO
WANAFUTINZI WA SHULE YA MSINGI MLIMANI WILAYANI SERENGE

MAGEREZA WALIOKAMATWA NA TWIGA WATIMULIWA KAZI



JESHI la Magereza nchini limewafukuza kazi askari watatu na kumsimamisha kazi afisa wake mmoja kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Mbali na hatua hiyo pia Mkuu wa gereza la Kiteto, Mrakibu wa Magereza Ally Sauko, amevuliwa madaraka na kurejeshwa katika Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara akisubiri hatua ya mamalaka ya kinidhamu dhidi yake kwa kutumia madaraka vibaya.
Askari waliofukuzwa kazi ni Sajenti Ketto Ramadhan, Koplo Silvester Dionice na Wada Barik huku afisa aliyesimamishwa kazi ni Joseph Kimaro ambaye ni mrakibu Msaidizi wa Magereza akifunguliwa mashtaka ya kinidhamu.
Taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa uchunguzi wa awali ulibaini ukiukwaji wa taratibu na maadili ya jeshi la Magereza na kwamba askari hao watapelekwa mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika .
Askari hao kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi wanadaiwa kukamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati Julai 23 mwaka huu wakiwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 55.
Inadaiwa askari hao wakiwa na gari la magereza Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili STK 4394 walikamatwa wakiwa wamepakia Twiga wawili, Majike mawili ya Swala Palapala na mbuni wawili.
Watuhumiwa walipopekuliwa katika gari walikutwa na kibali kilichoombwa na Hassan Omari kikiwaruhusu kuwinda nyati mmoja na pundamilia wawili.
Katika tukio hilo watuhumiwa wengine waliokamatwa ni Abubakari Ngaula, Hamza Ndachi, Saidi Idd na Husein Gola ambao pia walikutwa na bunduki ya aina ya SR mali ya Jeshi la Magereza pamoja na Rifle moja.


SAFARI YA UTALII

 Basi la Bunda Express baada ya kuungua moto likielekea jijini Arusha
 Kila mtu kwenye utalii ana kitu kinachomkonga moyo wake,hapo anapiga picha ndege wakiwa ndani ya viota vyao Lango la Naabi hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
 Ndege hao wapole wamekuwa ni kivutio kwan watalii mbalimbali
 Hapa tumashughulika na kubadilisha gurudumu la gari letu baada ya kupasuka na kusukwa sukwa lakini Mungu alikuwa upende wetu,na safari ikaendelea.
 Wanakamilisha taratibu za kuingia hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro wengine wakielekea hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
 Ukifika lango la Naabi kuna jumbe mbalimbali zinazoelekeza fursa na taratibu uwapo hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
 Ndege wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni rafiki wa binadamu ,kama inavyoonekana hapo.
Tembo licha ya kushambuliwa sana na majangili,bado wanapatikana kwa wingi hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

UTALII

 WATALII KWA KIPINDI HIKI NI WENGI SANA ,ASUBUHI LANGO LA NGORONGORO MSONGAMANO NI MKUBWA SANA
 HAPA WATU WA MATAIFA MBALIMBALI TUNAKUTANA KWA LENGO MOJA LA UTALII,UWE WA NJE WA NDANI NI UTALII TU
 TUKISUBIRI UTARATIBU KWA KUZINGATIA ALIYEINGIA WA KWANZA ANAHUDUMIWA KWANZA
 KUNA KITU KINAENDELEA HAPO NI UFUATILIAJI KWA MAKINI
 MABAKI YA BASI LA BUNDA EXPRESS LILILOUNGUA JUZI MALANJA LIKIENDA ARUSHA ,ABIRIA WALIPONA MIZIGO YOTE IKATEKETEA,HUENDA BODI LIKAUZWA KAMA VYUMA CHAKAVU
LANGO LA NGORONGORO

Mjane wa askari aliyefia Darfur atupiwa virago




 

  • Amina Juma 
  • Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waombolezaji waliokuwa nyumbani kwa marehemu Visiga, Kibaha zinasema baadhi ya wanandugu walimkana Amina siku chache baada ya kutangazwa vifo hivyo.
Kibaha/Tanga. Hata kabla ya maziko askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa Darfur, Sudan hayajafanyika, mchumba wa mmoja wa wapiganaji hao, Amina Juma ameonja chungu nyingine baada ya kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu mwenza wake.
Amina ambaye inadaiwa kuwa alikuwa akiishi na Fortunatus Msofe aliyekuwa askari katika Kambi ya Msangani, 36KJ Pwani alisema jana: “Kumekuwa na mzozo wa hali ya juu na ndiyo maana tumeshindwa hata kufika Uwanja wa Ndege kuupokea mwili na hata kesho (leo) sidhani kama nitakwenda... kuna mtafaruku mkubwa wa kifamilia.”
Baada ya kutimuliwa, Amina ambaye hawakuwahi kupata mtoto na marehemu Msofe, alilazimika kuondoka kwenye nyumba hiyo na kwenda Mlandizi kwa wazazi wake.
“Nimeishi na Msofe kwa miaka mitatu, akiwa kambini mimi niko hapa na wakati mwingine alikuwa analala huku... lakini leo wamenitimua,” alisema huku akilia.
Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waombolezaji waliokuwa nyumbani kwa marehemu Visiga, Kibaha zinasema baadhi ya wanandugu walimkana Amina siku chache baada ya kutangazwa vifo hivyo.
Ilidaiwa kwamba Amina alitimuliwa katika nyumba hiyo Ijumaa iliyopita, saa saba mchana baada ya ndugu watatu wa marehemu kufika hapo wakitokea Tanga.
Walipofika inadaiwa kuwa walitangaza kusitishwa msiba huo katika nyumba hiyo na kutangaza kutomtambua mke huyo.
Watu hao waliwaeleza waombolezaji kuwa walitumwa na baba mzazi wa marehemu, Willbad Msofe kutoka Kange, Tanga kufika Kibaha kusitisha msiba uliokuwa ukiendelea nyumbani kwa mtoto wake huyo.
Inadaiwa pia kuwa katika msafara huo,  alikuwapo mdogo wa marehemu ambaye aliwahi kuishi kwa miaka miwili na Amina hapo Visiga.
Ilidaiwa kuwa walipofika nyumbani hapo walionana na mfiwa, Amina na wazazi wake ambao pamoja na majirani na watu wengine wengi, walikuwa wakimfariji binti yao huyo.
Mmoja wa waombolezaji alisema baada ya salamu wanandugu hao walianza kuulizia mali za marehemu na walikuwa wakimuuliza Amina ambaye aliwaleza kila kitu kilipo na baada ya hapo ndipo walipomweleza kuwa wametumwa na baba wa marehemu kuwa watu hawatakiwi kuomboleza kwenye eneo hilo kwani msiba upo Tanga tu ambako ndiko iliko familia yake.
Alipoulizwa baba wa marehemu, Mzee Msofe alisema: “Mimi ndiye niliyeagiza nyumba ifungwe na ukweli ninamfahamu Amina, lakini simtambui kama mkewe kwa kuwa hawajafunga ndoa... Hata wewe si unayafahamu haya? Uchumba si ndoa na ukifunga ndoa ndipo unatambulika rasmi,” alisema.
Akiwa kwa wazazi wake Mlandizi jana, Amina alisema:
“Namwachia Mungu maana hayo yote nashangaa yanatokea wakati huu mume wangu ‘Fortu’ amekufa, mbona kipindi chote cha miaka mitatu iliyopita familia ya Tanga dada zake na mdogo wake tuliishi nao vizuri kwangu nilipokuwa na marehemu? Nimeishi na ndugu wote lakini hawakuwahi kuhoji, hata nilipokwenda na mume wangu Kange baba na mama Msofe nilikaa nao zaidi ya wiki na hawakunikana, ila nashangaa,” alisema na kulia kwa uchungu.
Akizungumzia kitendo hicho, baba yake Amina, Juma Juma alisema: “Nimeshangaa hizi taarifa. Tulikuwa tunajiandaa kupokea msiba wa mwanetu, lakini leo yanakuja mengine kwa kweli imetushangaza sana.”
“Nasubiri baada ya kumzika marehemu, nitazungumza nao... Kinachonishangaza ni kwamba walituandikia barua ya kumposa binti yangu na tukawajibu na gharama zilikuwa Sh1.2 milioni... Tutazungumza, ngoja hili lipite kwanza,” alisema mzee Juma.
Maisha ya Amina na ‘Fortu’
Akisimulia maisha yao, Amina alisema: “Tulianza kuishi Mbezi Luis mwaka 2010 katika nyumba ya kupanga na nikamshawishi tununue kiwanja na kwa kuwa mimi ni mwenyeji wa Kibaha, niliwatumia marafiki wa familia yangu Mlandizi wakatafutia eneo na mwaka 2011 tulipata na tukaanza ujenzi.
“Tukiwa Mbezi, tulianza kufyatua matofali kisha ujenzi ukaanza Visiga mwaka 2012 mwanzoni na  Septemba mwaka huo tulihamia kwenye nyumba yetu na hapo ndiyo ilikuwa makazi yetu hadi marehemu anaondoka kwenda Darfur.
“Wakati wote huo ‘Fortu’ alikuwa keshaniposa na hata barua zote za posa zipo na tulikuwa tukisubiri utaratibu wa kijeshi marehemu kukamilisha miaka sita ya kukaa kambini kisheria ndipo aruhusiwe kuoa.
“Fortu alikamilisha miaka hiyo mwaka 2012 mwishoni na wakati akijiandaa kwa kufunga ndoa ndipo ikatokea safari ya Darfur mwanzoni mwa mwaka huu na tukakubaliana tusitishe kwanza akirudi tukamilishe, lakini haikuwa.... Halafu wananifukuza wanasema hawanijui,” alieleza huku akiangua kilio

BARAZA LA KATIBA LA LHRC LAANZA KAZI YA KUCHAMBUA RASIMU YA KATIBA

 BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZA LA KATIBA LA LHRC WAKISIKILIZA KWA MAKINI UFUNGUZI ULIOFANYWA NA MKURUGENZI WA LHRC DR,KIJO BISIMBA KATIKA VIWANJA VYA OFISI HIZO KINONDONI
 WAANDISHI WAKIFUATILIA MATUKIO YOTE
 DR.KIJO BSIMBA MKURUGENZI WA LHRC WAKATI ANAFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA KATIBA LA LHRC
 WAJUMBE WAKIWA KWENYE MAKUNDI WAKICHAMBUA RASIMU YA KATIBA
 MJADALA WA KUNDI LA MASUALA MTAMBUKA YALIYOMO NDANI YA RASIMU YA KATIBA CHINI YA WAKILI SHILINDE UKIENDELEA
MJADALA WAENDELEA