Subscribe:

Ads 468x60px

TUNAMSIFU MUNGU









wanakwaya siku

Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana


Na Mwinyi Sadallah,Mwananchi

Posted  Jumapili,Decemba29  2013  saa 15:43 PM
Kwa ufupi
  • Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.
Aliapishwa jana kuwa mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Zanzibar.
Zanzibar. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.
Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.
Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.
Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati  Mzee Abeid Amani Karume.
“Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi,” alisema.
Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.
Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo. Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.

Uhaba wa madarasa wakosesha Wanafunzi 16,482 kuingia sekondari


Posted  Decemba28  2013  saa 9:28 AM

 Na Goodluck Eliona, Mwananchi
Kwa ufupi
  • Wanafunzi hao ni kati ya 844,938 waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba 11 na 12, 20013, ambapo 427,609 walifaulu kwa kupata alama A na C, ambayo ni sawa na asilimia 50.61 ya ufaulu.
Dar es Salaam. Serikali imetangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani, huku 16,482 wakishindwa kuchaguliwa kutokana na uhaba wa madarasa.
Wanafunzi hao ni kati ya 844,938 waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba 11 na 12, 20013, ambapo 427,609 walifaulu kwa kupata alama A na C, ambayo ni sawa na asilimia 50.61 ya ufaulu ikiwa ni ongezeko la asilimia 19 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini alisema jumla ya wanafunzi 867,983 walisajiliwa kufanya mtihani huo, lakini wanafunzi 23,045 hawakufanya kutokana na utoro, vifo na ugonjwa.
Alisema kuwa kutokana na ongezeko la fursa ya utoaji wa elimu ya sekondari nchini, wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali awamu ya kwanza huku zaidi ya 16,000 wakikosa kuchaguliwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa 412.
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 96.15 ya wanafunzi waliofaulu mtihani. Kati ya wanafunzi hao wasichana ni 201,021 sawa na asilimia 95.9 na wavulana ni 210,106 sawa na asilimia 96.3,” alisema Sagini na kuongeza kuwa:
“Ninaziagiza Halmashauri zilizobaki katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo Machi 2013.”
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana, idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza imeongozeka kwa asilimia 31.37.
Alisema kuwa mtihani huo ambao ulifanyika Septemba 11 na 12, mwaka huu, ulisahihishwa kwa kutumia teknolojia ya kompyuta ‘Optical Mark Reader (OMR)’.
“Mwanafunzi aliyepata alama ya juu kabisa kwa upande wa wavulana alipata 244 kati ya 250 huku msichana akipata 241. Mwaka 2012 alama ya juu ilikuwa 237,” alisema.
Akizungumzia vitendo vya udanganyifu kwenye mtihani huo, Sagini alibainisha kuwa wanafunzi 13 wamefutiwa matokeo yao, ambayo ni idadi ndogo ikilinganishwa na watahiniwa 219 waliofutiwa matokeo mwaka 2012.
“Napenda kutoa wito kwa walimu, wazazi na jamii kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani vinatoa taswira mbaya kwa taifa na kuwafanya watoto wetu wawe tegemezi zaidi kuliko kujituma na kujibidiisha katika masomo,” alisema.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo hakutaja viwango vya ufaulu kwa kila somo kama ambavyo imezoeleka katika mitihani iliyotangulia wala mkoa uliofanya vizuri au vibaya. Matokeo ya mwaka huu yanaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi walioshindwa kufanya mtihani imepungua kwa wanafunzi zaidi ya 6,000 ikilinganishwa na 29,012 ambao hawakufanya mtihani huo mwaka jana.

Huku idadi ya wasichana na wavulana walioshindwa kufanya mtihani ikipungua kutoka wasichana 12,501 mwaka jana hadi 9,781 mwaka huu na wavulana 16,511 hadi 13,264.
Matokeo hayo yameshindwa kufikiwa kwa malengo ya mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao uliwataka walimu kuhakikisha kuwa wanapandisha kiwango cha ufaulu hadi kufikia asilimia 60.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa BRN kwenye sekta ya elimu jijini Dar es Salaam, Agosti mwaka huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, alisema kuwa kiwango hicho cha ufaulu kilitakiwa kuanza kutumika mwaka huu. Aliwapongeza walimu, walimu wakuu, kamati za shule, waratibu wa Elimu Kata, Viongozi wa Halmashauri na wadau wote wa elimu ambao wanasimamia na kuendesha utoaji wa elimu nchini.
Akisoma hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, bungeni Dodoma mwaka huu, Dk Kawambwa alisema kuwa serikali itafanya ufuatialiaji wa namna ya uendeshaji wa mitihani ya darasa la nne, mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Mitihani mingine aliitaja kuwa ni wa ufundi stadi katika Halmashauri tisa ambazo ni Temeke, Ilala, Kinondoni, Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini, Bagamoyo na Kisarawe, ili kubaini wanafunzi wenye matatizo katika ujifunzaji.

Jairo, Nyoni wasafishwa kimyakimya


Jairo alisimamishwa kazi kutokana na  tuhuma za kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha Bajeti ya  Wizara ya Nishati na Madini, katika mwaka wa Fedha 2011/2012 . 
Na Elias Msuya, Mwananchi

Posted  Decemba28  2013  saa 9:11 AM
Kwa ufupi
  • Serikali iliahidi kuwasilisha  taarifa bungeni ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge kuhusu Jairo na wengine, ambayo bado hayajasomwa
  • Ikulu yasema hawana hatia, Ramo Makani ashangaa Bunge halijapata taarifa  

Serikali imewasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo huku ikimpandisha cheo aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa.
Nyoni alisimamishwa kazi pamoja na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa  na wote kwa pamoja walikuwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma.
Jairo kwa upande wake alisimamishwa kazi kutokana na kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bajeti ya wizara yake, katika mwaka wa fedha 2011/2012 na sasa ameondolewa kwenye utumishi wa umma, huku Bunge likiwa bado halijapata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yanayomuhusu.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katibu Mkuu Kiongozi
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia gazeti hili kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.
“Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa kuazima watumishi wa umma.
Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na kule TRA hakuwa na tatizo,” alisema Balozi Sefue.
Kuhusu Dk Mtasiwa alisema: Uteuzi wa Dk Mtasiwa ulikuwa wazi na hata alipoapishwa mambo yote yalitangazwa hadharani.” Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: “Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma.” Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.
“Siyo kwamba ameajiriwa TRA, amerudi tu kwenye ajira yake ya zamani, alikuwa akifanya kazi hapa akaazimwa na sasa amerudi,” alisema Kayombo na kuongeza: “Kwani amefanya kosa gani? Kuna mashtaka yoyote aliyofanya unaweza kuyathibitisha?”
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bernard Mchomvu ambaye alisema Nyoni alishasafishwa na Serikali ndiyo maana wamempokea. “Yule aliazimwa tu na Serikali…Sasa kama Serikali imesham-clear sisi tutamkataaje?” alihoji na kuongeza:
“Kwa sababu sikumwomba huyo mtu, nimeambiwa kwamba huyo yuko safi mimi nifanyeje? Unajua watu wanafurahia wengine wakipata matatizo, hata kama mtu ameua, basi walete ushahidi. Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu.”
Jitihada za kumpata Nyoni kupitia simu yake ya mkononi hazikuzaa matunda, baada ya simu yake kupokelewa na sauti ya kiume iliyosema kuwa namba imekosewa.
Hata alipotafutwa kwa namba nyingine, simu ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa Wizara ya Afya na kwamba namba hiyo kwa sasa haitumii tena. Alipotafutwa kwa njia ya simu, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah, alisema suala hilo aulizwe msemaji wa Serikali juu ya Bunge.
“Ongea na msemaji wa Serikali juu ya mambo ya Bunge,” alijibu kwa njia ya ujumbe wa simu.
Lukuvi
Naye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hayuko ofisini.
“Niko ‘airport’ nasafiri kwenda South Africa, msinipigie simu, siko ofisini hadi mwezi ujao (Januari),” alisema Lukuvi na kukata simu yake.
Awali alipoulizwa kwa njia ya simu baada ya mwandishi kuelezea suala hilo alisema ana kazi nyingi na kwamba apigiwe baadaye.
Makani azungumza
Mwenye wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza tuhuma hizo, Ramo Makani, ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, akizungumza na gazeti hili kuwa: “Ni kweli mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza suala hilo, kwa utaratibu kamati kama hiyo huundwa kwa kanuni za Bunge kwa kupewa majukumu maalumu… Kama mbunge tu ningefurahi kusikia taarifa ya Serikali bungeni baada ya kupata taarifa ya Bunge,” alisema Makani na kuongeza:
“Serikali iliahidi kuleta taarifa bungeni ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge. Mimi sikumbuki kama taarifa hiyo imeshasomwa bungeni, labda wewe mwenzangu umebahatika kuisikia. Kwa hiyo bado tunasubiri… Kama Serikali imechukua hatua, mimi sijui.”
Tuhuma za Nyoni
Nyoni alituhumiwa kutenda makosa saba ambayo yaliainishwa wakati wa mgomo wa madaktari ulioanza Januari mwaka jana, hali iliyomlazimisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutangaza kumsimamisha kazi ili uchunguzi uweze kufanyika.
Baadhi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili ni pamoja na kujilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) nje ya mshahara aliokuwa akilipwa na Serikali, kutengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na ofisa ununuzi wake kwa kujiweka yeye mwenyewe.
Tuhuma nyingine zilikuwa kulazimisha Wizara ya Afya kununua sare za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za ununuzi.
Katika mikutano yote inayofanyika wizarani, alikuwa akilazimisha Kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa zabuni ya kutoa huduma ya chakula kwa washiriki tangu alipotua wizarani kama Katibu Mkuu.
Sakata la Jairo
Hatua ya kumwondoa Jairo katika utumishi wa umma nayo imefanyika kimyakimya kwani Serikali hadi sasa haijawasilisha bungeni majibu ya maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo ambalo pia liliwagusa watumishi wengine wa Wizara ya Nishati na Madini. Maazimio hayo ni yale yaliyotokana na matokeo ya uchunguzi  wa Kamati Teule ya Bunge   iliyoongozwa na Makani na kubainisha kuwapo kwa makosa ya kiutumishi na kijinai ambayo yangewafikisha baadhi ya watumishi hao katika vyombo vya sheria.
Mbali na Jairo, kamati hiyo ilipendekeza kuwajibishwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.
Hata hivyo, ni Jairo pekee kati ya hao aliyewajibishwa kwa kusimamishwa kazi na baadaye kuondolewa katika wadhifa wake. Luhanjo alistaafu utumishi wa umma bila kuchukuliwa hatua zozote wakati Utouh anaendelea na wadhifa wake.
Pia katika taarifa yake, Kamati Teule ilisema utaratibu wa uchangishaji wa fedha Sh418.081 milioni uliofanyika katika Wizara ya Nishati na Madini haukuwa na uhalali kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni za Fedha za Umma.
Pamoja na mambo mengine, Bunge liliazimia kwamba ufanyike ukaguzi wa kiuchunguzi (forensic audit) kwa matumizi ya Sh214 milioni, ambazo kati ya hizo Sh126 milioni Kamati Teule ilikataa maelezo ya matumizi yake na Sh88 milioni ni zile zinaotajwa kwamba zilitumika katika kugharimia semina kwa wabunge.
Azimio jingine ni lile lililoitaka Serikali iviagize vyombo vya dola kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kughushi na ubadhirifu zilizoelezwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kama ilivyoelekezwa.
Baada ya kufikiwa kwa maazimio hayo, Serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe iliahidi kuyafanyia kazi na kuwasilisha majibu bungeni.
“Kwa sababu ya ukubwa na uzito wa taarifa hii, ni vigumu kuitolea majibu yote hapa hapa, ninachoweza kufanya ni kuipokea pia tutakapokuja katika Mkutano wa Sita, tunatarajia kuleta majibu ya hoja zilizomo kwenye taarifa hii,” alisema Chakawe ambaye sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria.

Human rights violations still rampant in Bunda


By Waryoba Yankami

25th December 2013

Women harassment in Bunda district, Mara region has continued to be an acceptable culture despite efforts deployed by human rights activists, the government and the international community.

This kind of women or children harassment is not a new thing whereas people are practicing it and viewing it as normal and acceptable style of living that they have to carry out in their daily life. 

That is not enough, indigenous of that area have automatically passed it to be part of life.

A survey conducted between  November and  December this year  by The Guardian in collaboration with Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) and The United Nations Population Fund (UNFPA) in Bunda’s  three wards of  Mihingo, Kunzugu and Hunyari has revealed  that  Gender Based Violence (GVB) is  still a big problem.

Over 83 cases of women and children battering were reported at Bunda police station, whereby out of the reported cases, only one case was taken to court at the duration of two years. The number of cases reported is very low compared to the situation on the ground.

Authorities in the district from local governments to district level, police and activists have virtually surrendered admitting that the war to end women battering and other kinds of harassments is a total failure.

Some women believe that being beaten or harassed is part and parcel of life. Interestingly, when a girl is married she is normally informed that she will have to take it easy when she is married because she will surely be beaten by her husband.  

Children are also facing beatings especially when their parents are not in good terms. These children end up in being street children and denied of the right to education.

Shida Simon who is a resident of Mihingo  has been in wedlock for nine years now with her husband. She  said that since 2005 to now has experienced  harassment by her spouse.

 Shida added that from that day onwards harassments began whereby her properties that she had obtained from small businesses that she was doing was taken away by the man.

“I was selling cassava. My husband knew that I had money with me and therefore wanted me to give him all the money. When I refused she started beating me,” she said.

“When I could not tolerate any more, I decided to run away to my father. That is where my husband (Kabalana) came and started insulting my father, speaking abusive language against my father,” she narrated.

She continued narrating that it is when her spouse  entered into his father in-law’s house and took her out by force demanding  that she ran away with his money while it was not true.

Shida added that last year she grew cotton but all the money (200,000)  accrued from  the selling of cotton was confiscated by his spouse. 
  
They have always been reconciliated by family members from either side but to no avail. 

Reconciliation is one of the factors that put many women at risk. This is because family members resolve matters related to harassments instead of taking them to law bodies which could give harassing men a bigger punishment.

Until November 29 this year she was sustaining injuries after she was severely beaten by her husband. The case was in the court at Nyamuswa primary court. Shida was  demanding divorce. 

She added that in the beginning when quarrels in the family began, she went to Mugeta police station asking that her husband be arrested  but the police did not give her good cooperation.

 Kabalana was therefore not arrested. This gives many men in the district a leeway to harassing  women, according to Shida.

Children is another group is facing  harassment.  Ghati Kibhokora a grandmother at Mihingo went at Mihingo police station with her grandson who had been beaten by his father Seleman Nyange. 

She   asked the police to go and arrest the son’s father. Unfortunately the police did not assist the grandmother.

District Community Development Officer (DCDO) Caroline Wanzagi admitted that there is much GBV in that district going on but said many of the cases were being solved at family level. 

Wanzagi said that last year three women were beaten to death including one who dragged was by a car because of her husband’s jealousy.

When quarrels take place in the family between father and mother, children also become victims. As a result children decide to ran away from their homes.

Although the number of street children is increasing every year, the district lacks a center to keep them, something that leads children to ran to DCD offices for assistance.

Wanzagi said that there are many NGOs which have registered to assist fighting against GBV,  but have fails to bring changes. They have decided stay silent get funds from donors for the work. 

Corporal Rita Charles from Gender and Children desk at Bunda police station admitted  that there is a presence of gender violence, whereas over 83 cases on women harassment were reported in her office although the number is too low compare to the actual number of cases taking place in the area.

The war against GBV is very difficult because so many cases are being solved at family level while others are not taken to police or courts while others lack evidence. This is because many victims withdraw from their cases.

Copl. Charles however added that about 25 cases only from the gender desk were taken to court in the duration of two years out of 83 cases that were reported, Victims withdrawn from cases due to reasons of forgiving each other and others failing to attend in the court hearing.

Bunda district court magistrate Saidi Kassonso who reported at that court on July this year said he has experienced only one case of couples who fought and the husband beat a wife and broke the jaw and the wife cut husband’s fingers.

Kassonso admitted that many of GBV cases are not reaching court because people of Bunda lack the culture of taking their cases before the law bodies for further judgments but they are solving their disputes at family level and in a traditional way.

TAMWA Executive Director, Valarie Msoka said the effects of violence on a victim’s health are severe. In addition to the immediate injuries from the assault, battered women may suffer from chronic pain, gastrointestinal disorders, psychosomatic symptoms, and eating problems. 

She said that  although psychological abuse is often considered less severe than physical violence, health care providers and advocates around the world are increasingly recognizing devastating mental health effects of domestic violence, including anxiety, post-traumatic stress disorder, and depression. 

Women who are abused suffer an increased risk of unplanned or early pregnancies and sexually transmitted diseases, including HIV/AIDS.

 As trauma victims, they are also at an increased risk of substance abuse. Women are particularly vulnerable to attacks when pregnant, and thus may more often experience medical difficulties in their pregnancies.

As the World Health Organization notes, domestic violence also has significant indirect costs for society. 

Domestic violence can be fatal; women are both intentionally murdered by their partners and lose their life as a result of injuries inflicted by them.
SOURCE: THE GUARDIAN
More News


Electricity tariffs to go up by 40 per cent on January 1



By Ludger Kasumuni,The Citizen Reporter

Posted  Tuesday, December 24  2013 at  08:34
In Summary
  • Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) claims that it would post a loss of Sh1.6 trillion ($1 billion), between October 2013 and December 2015, if its request to raise power tariff by 90 per cent hits a snag. In its application submitted to the regulator, Energy and Water Regulatory Authority (Ewura), Tanesco wants a tariff increase of 90 per cent effective October, this year.The proposed rise would be implemented within three years—from October 2013 to 1 January, 2015.
Related Stories
Dar es Salaam. Electricity consumers will mark New Year with a heavy burden of meeting energy costs in the wake of a steep increase in power tariffs announced yesterday by Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Ewura).
Ewura Director of Economic Regulation Felix Ngamlagosi, said yesterday that tariffs had been increased by an average of 40 per cent for domestic users, and the new rates would come into effect on January 1, 2014.
This means that domestic consumers – those who use up to 75 units of electricity per month – will now pay Sh100 per unit, up from Sh60. Initially, this group had those who used less than 50 units.
Those who consume anything above 75 units but who are within the domestic consumption category will pay Sh350 for a unit, Sh77 more than the previous rate.
According to Mr Ngamlagosi, the new rates for all categories of electricity consumers will last for three years. This means that Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) will only be allowed to ask for another tariff increase after December 31, 2016. In line with the new tariffs, power users in the T-1 category, who used to pay Sh221 for every unit of electricity they consume, will now pay Sh306 per unit (38.46 per cent or Sh85 more. The T-1 segment is applicable to groups of customers who use power for general purposes, including residential, small commercial and light industrial use, public lighting and billboards. This is the group to which the majority of electricity consumers in the country belong.
Similarly, consumers who fall under T-2 will, starting next month, pay Sh205 for every unit of electricity they consume, up from Sh132.
T-2 is applicable for general use where power is metered at 400V and average consumption is more than 7,500kWh per meter reading period and demand doesn’t exceed 500KVA per meter reading period.
According to the rates approved by Ewura yesterday, consumers in the T-3 category will from next month be paying Sh45 more to buy a single unit of electricity. Their new rate will be Sh163. Before the new rates, they were paying Sh118 for a unit. T-3 refers to consumers within the general use category where power is metered at a high voltage line of 11KV and above.
In the same vein, those categorized under T-3 HV will have to pay Sh159 instead of Sh106 per unit (an increase of Sh53).
“This order shall come into force on January 1, 2014…The approved tariffs imply an average increase of Sh39.19 per cent compared to the current tariffs,” reads part of the Ewura statement.
 “The approved tariffs and charges shall remain in force until December 31, 2016 unless results of cost of services study that will be undertaken in 2015 will recommend new tariffs,” the statement further says.
Ewura further said that the new rates were determined by the new formula for fixing power tariffs which was adopted from the 2012 cost of service study performed by an independent consultant, AF-MERCADOS which takes into account sustainability of electricity services in the country.
The new tariffs fixed by the regulator are in response to applications filled by the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), in October this year requesting Ewura to hike power tariff at 67.87 per cent effective from October 2013, 12.27 per cent effective from January 2014 and another increase of 9.17 per cent effective from January 2015.
Moreover, Ewura director of electricity business, Mr Anastas Mbawala, said that in imposing such power rates, the regulator had also imposed 10 terms of reference for Tanesco, one being the power utility parastatal to submit to the authority a monthly report on actual generation and planned generation of electricity and second to ensure that the projects are implemented in line with the Power System Master Plan.
Other terms of reference include; submission of quarterly reports on the supply and reliability of data of 11kv, 33kv, 132kv and 220kv by region for verification including total number of customer interruptions and total customers served, submission of demand side management, revenue management, reducing technical and non-technical revenue losses, fighting illegal connections and electricity theft and submission of report of installation of LUKU metres and Automatic Meter Readers.
Other terms are submission of quarterly reports on collection of revenue from debtors, enhanced customers education of their rights, submission of application of tariff adjustments in line with changes in fuel cost, inflation and currency fluctuations, providing the regulator with information on business performance and submission of implementation plan of this order before 31st March 2014.
Commenting on the hiked power tariffs, the president of the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA), Mr Peter Chisawilo, said that members of the business community were set to meet to discuss the matter so that they decide on how to move forward.
Mr Chisawilo said that it was imperative for members of the business community to know the impact of the hiked power tariffs on the competitive strength of commodities produced in the country in the East African market.
“We will definitely meet to discuss the implications of the new power tariffs on the business performance in our country in relation to our counterparts under the East African Community,” he said.

Mapigano yaua wakulima wanne


23/12/2013 | Posted by Danson Kaijage |  

MGOGORO kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto, Manyara umeingia sura mpya baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuwavamia wakulima na kusababisha vifo vya watu wanne.
Taarifa ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akilimali Mpwapwa, ilieleza kati ya watu hao, watatu walikufa hapo hapo na mmoja akiwa njiani kupelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma na majeruhi saba.
Alisema usiku wa kuamkia Jumamosi, wafugaji waliingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima katika eneo la Kijiji cha Olupoponyi, Kitongoji cha Kalakala.
Alisema kitendo hicho ndicho kilichosababisha wakulima nao kuanza kuwazuia wafugaji na mifugo yao kutolisha mimea yao, lakini baada ya hapo wafugaji walionekana kuwa wabishi na kuanza kuwashambulia.
“Kutokana na majibishano kati ya wafugaji na wakulima ilisababisha wakulima watatu kupoteza maisha na majeruhi saba ambao walilazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto,” alisema.
Mauaji hayo yalitokea Kijiji cha Olupoponyi, Kitongoji cha Kalakala ambapo Mbunge wa Kiteto na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Benedict Ole-Nangoro (CCM) anaishi.
Imeelezwa jamii ya wafugaji wa Kimasai waliwavamia wakulima wakiwa katika vibanda vyao wamelala, saa 7 usiku na kuanza kuwashambulia kwa mapanga, sime, mikuki, visu na risasi.
Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema kitendo ambacho kinafanywa na wafugaji dhidi ya wakulima ni cha kinyama zaidi.
Hata hivyo, alieleza kushangazwa na serikali kufumbia macho mgogoro huo ambao kimsingi ni wa miaka mingi.
“Wafugaji wa jamii ya Kimasai wamekuwa wakiwaua wakulima mara kwa mara na wala suala hili si geni, viongozi wa ngazi ya juu wamekuwa wakiambiwa masuala haya, lakini kinachoshangaza ni kuona ukimya wa viongozi,” alisema.
Mbali na hilo, alimshambulia mbunge wa Kiteto, Ole-Nangoro kuwa ni kati ya viongozi wanaochochea chuki na kukuza ukabila katika Wilaya ya Kiteto.
Hivi karibuni, Ndugai alifanya mkutano na wakulima katika mji mdogo wa Kibaigwa, wilayani Kongwa na kuwaeleza kuwa Wilaya ya Kiteto kwa sasa imechafuka kutokana na viongozi wake kuwa na tabia ya kuendekeza ukabila.
Mbali na kuwepo na vitendo vya ukabila na ubaguzi, aliwataja Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Elaston Mbwilo kuwa wanahusika kwa kiasi kikubwa kuchochea mgogoro kutokana na kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji.

Mikoani washangilia mawaziri kung’oka


Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Decemba23  2013  saa 9:33 AM
Kwa ufupi
  • Diwani wa Nyanungu, wilayani Tarime Mkoa wa Mara, Samson Mang’enyi alisema operesheni hiyo ilifanywa kwa uonevu na kuwaathiri wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Serengeti.
Mikoani: Wananchi katika mikoa mbalimbali nchini wameshangilia kung’olewa kwa mawaziri wanne, yakiwa ni matokeo ya uchunguzi wa Bunge kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili.

Diwani wa Nyanungu, wilayani Tarime Mkoa wa Mara, Samson Mang’enyi alisema operesheni hiyo ilifanywa kwa uonevu na kuwaathiri wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Serengeti.
Mang’enyi alidai kuwa askari wa wanyama pori wamekuwa wakiwapiga risasi raia na mifugo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kinyama kina mama na watoto ambao walikuwa wakiingia katika Bonde la Nyanungu kuokota kuni.
“Miaka yote hapa kijijini tulikuwa tunategemea Bonde la Nyanungu katika kulishia mifugo yetu, kulima na kina mama na watoto kuokota kuni, lakini baada ya kutangazwa Operesheni Tokomeza, kwa kweli hii nchi haina ubinadamu kwa baadhi ya watu,” alisema diwani huyo.

Mkazi mwingine wa kata hiyo, Caro Chacha alisema afya yake kwa sasa inazidi kuzorota baada ya kuchapwa viboko visivyo na idadi na baadhi ya askari wanyama pori wa Hifadhi ya Serengeti (Senapa) alipokuwa akiokota kuni katika Bonde la Nyanungu.

“Kwa kweli kipigo nilichokipata sitakisahau katika maisha yangu. Nilikuwa nanyonyesha lakini nilishindwa hata kunyonyesha mtoto, hata namna ya kujisaidia haja ndogo nilishindwa. Ila Mungu ni mkubwa,” alisema na kuongeza:

“Askari hao walifikia hatua na kutuvua nguo zote, tukabakia uchi wa mnyama kama tulivyozaliwa, jamani inauma sana kwani pale walikuwapo watoto, walitufanyia vitendo vya ajabu sana. Walitaka hata kutubaka ila walishindwa baada ya kuona tumeishiwa nguvu kwa mateso ya muda mrefu.”

Ruvuma
Mkoani Ruvuma, wananchi wamekuwa na maoni yanayokinzana, baadhi wamepongeza uamuzi wa Bunge na baadaye Serikali, wakati wengine wameeleza kusikitishwa.

Mkazi wa Tunduru, Ajiri Omary Kalolo alisema anaunga mkono uamuzi wa mawaziri kuondolewa madarakani akisema naye ni mmoja wa watu walioteswa na askari waliohusika na Operesheni Tokomeza Ujangili.

Kalolo alisema mbali na mateso aliyopata, aliwekwa mahabusu, kunyang’anywa fedha na kushinda njaa.

“Ninaunga mkono kung’olewa mawaziri wenye dhamana. Hili ni funzo, kwani nchi ingekufumbua macho tatizo hili tungeweza kufika pabaya zaidi ingawa najua wapo askari ambao wametesa wananchi kwa matakwa yao na hawakutumwa kufanya hivyo, tunaiomba Serikali iwachukulie hatua zaidi,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma, Andrew Kuchonjoma ambaye pia alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa siku tatu kwa kosa la kukutwa na mbao, alielezea kusikitishwa kwake na  kung’olewa kwa mawaziri kwa makosa yaliyofanywa na watendaji waliopo chini yao.

Alisema hatua ya mawaziri kung’oka haitoshi badala yake akataka Serikali iwachukulie hatua askari wote waliofanya vitendo vya ukatili.
Morogoro
Katika Wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro, baadhi ya wananchi wameeleza kufurahishwa kwao na uamuzi wa Serikali wa kuwawajibisha mawaziri hao wakisema operesheni hiyo ilisababisha vifo vya watu na wanyama na kwamba hata walipolalamika hawakusikilizwa.
Mmoja wa watu aliyedai kwamba ndugu zake waliuawa katika operesheni hiyo, Hamis Kewala alisema suala la kumalizika kwa ujangili linahitaji umakini kwani wahusika walio wengi wamekuwa wakitumia mbinu mpya kuua tembo na kusafirisha meno hayo, huku wasiohusika wakiumizwa bila hatia.
Mkazi mwingine, Mohamed Nguku alisema: “Vita hii sasa itakosa nguvu, suala la msingi ni kuhakikisha usimamizi wa hali ya juu na umakini, halafu taratibu na sheria za nchi kwa wanaopewa dhamana kufanya kazi hizi lazima zifuatwe na siyo kufanya wanavyojua wao”.
Agosti 12 mwaka huu, Mkazi wa Tarafa ya Mwaya wilayani Ulanga, January Gunena alikamatwa na kupelekwa katika kambi ya mateso iliyokuwa katika Hifadhi ya Selous na  kuteswa na baadaye alifariki dunia.
Wengine waliopatwa na mateso hayo ni madereva wanaoendesha magari yanayofanya safari kati ya Ifakara, Mahenge na Mwaya ambao wakiwa safarini walikuwa wakisimamishwa na askari kuhojiwa lakini wengine wakiishia kupata vipigo na kuporwa fedha.
Imeandikwa na: Florence Focus (Tarime), Joyce Joliga (Songea), Lilian Lucas (Morogoro).

Kisumo amtaka Kikwete kuwaiga waliomtangulia


Na Daniel Mjema, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Decemba23  2013  saa 9:29 AM
Kwa ufupi
  • “Kwangu mimi sifa kubwa zaidi ni kwa Kinana... itakuwa upuuzi chama kinachotawala kikaacha haki yake ya kuwatetea wanyonge kwa kupima utendaji wa wale kiliowapa dhamana ya uongozi,” Kisumo
Moshi. Mwanasiasa mkongwe, Peter Kisumo amesema kuna tatizo katika uchujaji (vetting) wa watu wanaoteuliwa kushika madaraka ya umma wakiwamo mawaziri na kutaka mfumo huo urekebishwe.

Pia Kisumo alisema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuiga mfano wa marais waliomtangulia kwa kuchukua hatua za kuwaondoa mawaziri wanaochafua taswira ya nchi badala ya kusubiri Bunge.

Akizungumza jana, Kisumo alisema ni lazima uchujaji wa watu wanaoteuliwa kuwa mawaziri na watumishi wengine wa ngazi za juu uzingatie uadilifu na siyo mapenzi ya Rais pekee.

Kisumo alikuwa akizungumzia hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wanne iliyotangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge.

Kisumo alisema ni lazima vyombo vya kumshauri Rais vifanye kazi yake kwa masilahi ya nchi vinginevyo Watanzania wataendelea kushuhudia mawaziri waking’oka kwa kushindwa kuwajibika.

Alitolea mfano kuwa  Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kumteua Chediel Mgonja (marehemu) kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga lakini akamwondoa kabla ya kumwidhinisha.

Kisumo alisema wakati wa Nyerere na hata awamu ya Benjamin Mkapa (1995-2005), wapo mawaziri waliowajibishwa na Rais lakini awamu zote mbili za Rais Kikwete mambo yako tofauti.

“Wakati wa Nyerere akipata taarifa kuwa taswira ya nchi inaharibika alikuwa anawaita na kuwataka wamuandikie barua ya kujiuzulu lakini awamu zote hizi za Kikwete mambo yanaanzia bungeni,” alisema na kuongeza:

“Kusubiri hadi upate shinikizo la Bunge wakati una uwezo wa kuwaondoa watu wako mapema haipendezi sana… haya nayaona awamu ya Kikwete.”

Mwanasiasa huyo alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa kufanya kazi ya kutathmini utendaji wa Serikali akisema hajawahi kupatikana katibu mkuu wa aina yake tangu 1995.

“Kwangu mimi sifa kubwa zaidi ni kwa Kinana... itakuwa upuuzi chama kinachotawala kikaacha haki yake ya kuwatetea wanyonge kwa kupima utendaji wa wale kiliowapa dhamana ya uongozi,” alisema.

Pinda: Watumishi 866 wamechukuliwa hatua kwa ubadhirifu wa fedha


Na Jacqueline Massano
22nd December 2013

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Watumishi 866 wa serikali wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa ubadhirifu wa fedha katika halmashauri mbalimbali nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akisoma hotuba ya kuahirisha shughuli za Mkutano wa 14 wa Bunge lililofanyika mjini hapa.

Pinda alisema watumishi waliohusika na ubadhirifu wa mali na fedha za Umma wamechukuliwa hatua mbalimbali zikiwemo kusimamishwa kazi, kushushwa vyeo na kufikishwa mahakamani.

Aidha, alisema kesi za watumishi hao ziko katika mahakama na katika vyombo vya nidhamu vya Halmashauri na Tume ya Utumishi wa Umma kulingana na makosa yao.

Alisema kutokana na hali hiyo, kati ya mwaka 2011/12 hadi Septemba, mwaka huu jumla ya wakurugenzi 52, wakuu wa idara 65 na watumishi wengine 746 wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa ubadhirifu wa fedha katika halmashauri mbalimbali nchini.

“Waliofukuzwa kazi ni 232, waliosimamishwa 186, waliovuliwa madaraka 33, waliopunguziwa mshahara 1, walioshushwa cheo 32, walipewa onyo 113, waliofikishwa mahakamani 233 na waliofikishwa polisi na Takukuru 36.

“Serikali itaendelea kuhimiza nidhamu katika matumizi ya kifedha na vilevile itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watumishi wote watakaokuwa wabadhirifu,” alisema.

Aidha, alisema pamoja na hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa watumishi hao mmoja mmoja, serikali imeendelea kuchukua hatua nyingine mbalimbali kukabiliana na tatizo la ubadhirifu wa mali za umma katika halmashauri.

Pinda alizitaja hatua za kukabiliana na ubadhirifu huo kuwa ni kuongeza uwezo kwa kuajiri wahasibu wa kutosha katika halmashauri, kuanzisha kamati za mapato na matumizi katika ngazi zote za halmashauri na kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa kamati za mapato na matumizi za halmashauri zote.

Alitaja mbinu nyingine zinazotumika ni kufanya ukaguzi maalum kubaini ufisadi na ubadhirifu wowote uliojitokeza.

“Kwa mfano katika mwaka wa fedha 2011/12 kumefanyika ukaguzi maalum kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa 14 ambazo ni Kilindi, Kiteto, Muheza, Ruangwa, Musoma, Kilwa, Temeke, Singida, Arusha, Mvomero, Morogoro, Dodoma, Mbarali na Bunda,” alisema.

Pinda aliahirisha Bunge hilo hadi Mei 6 mwakani katika mkutano wa 15 wa bajeti.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI