Subscribe:

Ads 468x60px

NDUGU WAUA NA KUJERUHIANA KWA DENI LA SH,20,000



NDUGU MMOJA AFA WAWILI WAJERUHIWA WAKIDAINA  SH.20,000
Serengeti:DENI la sh.20.000 limesababisha ndugu  watatu wa kitongoji cha Nyasuma kijiji cha Borenga kata ya Kisaka wilaya ya Serengeti kukatana mapanga na mmoja kufariki huku wawili wakilazwa katika hospitali teule ya Nyerere ddh chini ya  ulinzi wakiwa na hali mbaya.
Tukio hilo la aina yakelinadaiwa kutokea septemba 23 majira ya saa 12:00 jioni nyumbani kwa Muhochi Hacheri limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali teule ya Nyerere ddh,na kumtaja aliyefariki kuwa ni Julius Mwikwabe (20)aliyefariki,na majeruhi hao kuwa ni Mwikwabe Mwikwabe(40)Magubo Mwikwabe(29).
Magubo ambaye ni mtuhumiwa akiwa amelazwa kitanda namba 8 na kaka yake wakiuguza majeraha alisema ,alikuwa akimdai mdogo ambaye ni marehemu  sh,20,000 baada ya kumuuzia baiskeli aina ya Swala kwa sh,40,000 na kulipa nusu ,alipomdai ndipo kukaibuka ugomvi na kusababisha kifo na majeruhi kwao .
“Toka mwezi mei namdai pesa hizo akawa mkaidi…septemba 19 nilikwenda kudai akaahidi kesho yake angelipa  hakulipa…septemba 23 tulipokutana akanitolea majibu mabaya…nilimchapa fimbo nne kama mdogo wangu…akatoka kimya akaenda kunoa panga na jioni akaja nikiwa kwa Hacheri na kufika na kunikata kwa panga mgongoni chini ya bega la kushoto”alisema majeruhi huyo.
Alisema ndipo naye akachukua panga alilokuwa nalo kwa nia ya kujihami,lakini mdogo wake huyo ambaye ni marehemu alinyanyua panga amkate tena,”aliponyanyua mkono anikate nikamkata mkono wa kushoto ukaning’inia na damu zikawa zinavuja sana..alifariki baada ya kufika hospitalini”alisema.
Naye Mwikwabe Mwikwabe kaka mkubwa wa familia hiyo alisema ,akiwa nyumbani kwake alipata taarifa ya ugomvi wa wadogo zake ,”lengo likiwa ni kuwaamua…nikiwa katika pilika pilika hizo Julius(marehemu)alinikata sehemu ya bega la kushoto kwa nyuma huku akidai ni bahati mbaya,”alibainisha.
Alisema kitendo cha kukatwa kilimfanya aanze kujihudumia huku wadogo zake wakiendelea kupambana na matokeo ya ugomvi huo wamempoteza mdogo wao.
Muuguzi wa zamu wodi ya wanaume Hellen Mosha alisema kuwa Julius alifariki muda mfupi kabla ya kupata matibabu na chanzo kikiwa ni kuvuja damu sana kutokana na kuchelewa  kufikishwa hospitalini.
Polisi wilayani hapa wamesema watuhumiwa hao wawili wanatibiwa wakiwa chini ya ulinzi wakati uchunguzi zaidi ukiendelea wa kubaini mhusika aweze kufikishwa  mahakamania.
Mwisho. 

MWIKWABE MWIKABE NA MASUBO MWIKWABE AMBAO NI MTU NA MDOGO WAKE WAKAZI WA KIJIJI CHA BORENGA KATA YA KISAKA WILAYANI SERENGETI WAKIWA WAMELAZWA WODI LA WANAUME KITANDA NAMBA 8 HOSPITALI TEULE YA NYERERE DDH KUFUATIA UGOMVI BAINA YAO ULISABABISHWA NA DENI LA SH.20.000 NA KUPELEKEA MDOGO WAO JULIUS MWIKWABE KUFARIKI .


 WAMELAZWA WAKIWA WAMEFUNGWA PINGU KUTOKANA NA TUHUMA ZA MAUAJI YA MDOGO WAO

NEMBO YA WILAYA YA SERENGETI

MSANII MASUI HAMISI MARARE AKIBORESHA PICHA YA TWIGA AMBAYO NI NEMBO YA WILAYA YA SERENGETI

WADAU WA ELIMU WAKUTANA SERENGETI

Klabu ya Haki Elimu ya wanafunzi wa Mugumu B wilayani Serengeti wakiigiza jinsi baadhi ya wazazi walivyokikwazo cha elimu kwa watoto wa kike ,
Wanaendelea kutoa ujumbe namna wanavyokutana na vikwazo kutoka kwa baadhi ya wazazi wenye mlengo wa kuwaoza mapema
hapo ni ujumbe tu
Mkurugenzi wa Haki Elimu Elizabeth Msokia akielezea changamoto za elimu wilayani Serengeti wakati wa mdahalo wa wazi wa elimu  kwa wadau wa elimu,marafiki wa elimu,walimu,watendaji wa serikali na madiwani waliofanyikia shule ya Mugumu B.
mjadala unaendelea
Wadau wakifuatilia mjadala huo
Jamani hali si nzuri kwenye sekta ya Elimu ni kauli ya Mkurugenzi wa Haki Elimu

SINGITA GRUMETI RESERVES YATOA MSAADA WA VIFAA SETCO

 MKURUGENZI WA UTALII KAMPUNI YA SINGITA GRUMETI RESERVES JASON TROLLIP AKIMKABIDHI MKURUGENZI WA CHUO CHA UTALII SERENGETI(SETCO)SAMWEL PETER MARWA KITABU IKIWA NI SEHEMU YA MSAADA WALIOTOA WA ZAIDI YA MIL.7 KWA CHUO HICHO.


 MBALI NA VITABU WAMETOA PIA OVENA
 KOMPUTA NI SEHEMU YA VIFAA WALIVYOTOA
 MMOJA WA WANACHUO AKIPOKEA KITABU KWA FURAHA

 POKEA VITI NI KAULI YA MKURUGENZI WA UTALII WA SINGITA
HAO NI BAADHI YA WANACHUO WA SETCO

AKATA MIGUU NG'OMBE 27


AKATA MIGUU NG’OMBE 27 BAADA YAJARIBIO LA KUMUUA MAMA YAKE KUSHINDWA,
“Mtuhumiwa aliiba kuku anayeatamia na kuuza kwa sh.7.000 akanunua gongo,alipoulizwa akampiga mama yake aliyejiokoa kwa kumkamata nyeti kijana wake”
Septemba 21,2013

MKAZI wa kijiji cha Bwitengi kata ya Manchira wilayani Serengeti Witiribani Thomas Barangwa (30)anatuhumiwa kukata  miguu ng’ombe 27 wenye thamani ya zaidi ya sh,mil.5kufuatia ugomvi baina yake na mama yake aliyemtuhumu kuiba na kuuza  kuku kwa ajili ya kupata pesa ya kununulia pombe.

Tukio hilo ambalo limezua mjadala  kutoka kwa wananchi linadaiwa kutokea septemba 19 majira ya saa 7:00 usiku mwaka huu katika kitongoji cha Mewara limethibitishwa na Mwenyekiti na ofisa mtendaji wa  serikali ya kijiji Daud Manteni na Antony Makuru,na kuwa mtuhumiwa ametoroka anatafutwa.

Akielezea mkasa huo ofisa mtendaji alisema mtuhumiwa huyo aliamua kukata miguu ng’ombe hao baada ya kumsaka mama yake mzazi NyambiseThomas Barangwa na dada yake Loyce Thomas Barangwa waliompiga kutokana na kosa la kuiba kuku aliyekuwa ameatamia na kumuuza  kwa sh.7.000 na kwenda kunywa pombe za kienyeji.

“Katika ugomvi huo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kumwangusha mama yake na kuanza kumkaba shingo…dada yake akaingilia kati, hata hivyo mama yake alipoona amezidiwa akamkaba sehemu za siri kwa nguvu na kumwachia…mtuhumiwa akakimbilia ndani na kuchukua silaha na kuanza kuwasaka awakate”alisema.

Makuru alisema mtuhumiwa alichukua panga kwa lengo la kumuua mama na dada yake ambao walikimbia na kujificha,na wanakijiji wakijitokeza kwa wingi kutoa msaada.

“Baada ya kuwakosa na kuona wananchi wamejitokeza kuwasaidia hasira zake zilihamia zizini na kuanza kukata ng’ombe mmoja baada ya mwingine mali ya baba yake…waliowekeshwa na wa kwake watatu hakuwagusa”alisema.

Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa mtuhumiwa aliuza kuku anayeatamia na kuwa mchezo huo ulikuwa wa mara kwa mara na fedha zote akazitumia kwa kununua gongo,na alipoulizwa alikuwa mkali na kuwatishia.

“Akishakunywa pombe ni mkali sana si kwa mama yake wala majilani…na anatumia nafasi hiyo kwa kuwa wanaishi na mama yake tu…kwa kweli tukio alilofanya ni la kipekee na halijawahi kutokea kijijini hapa”alibainisha jilani ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Kutokana na tukio hilo wafanya biashara wa bucha wanadaiwa kununua ng’ombe hao kwa bei ya chini kwa kuwa hawakuwa na uwezekano wa kupona kutokana na jinsi walivyokuwa wamejeruhiwa,pia wakazi wa kijiji hicho walinufaika kwa kupata nyama.

Polisi wilayani hapa wanaendelea na msako dhidi ya mtuhumiwa na wanaomba wananchi watoe ushirikiano ili aweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Mwisho.


MAHAFALI SAUT

DK.SAFARI WA CHUO KIKUU SAUT AKINIKABIDHI CHETI CHA KUHITIMU MAFUNZO YA MWAKA MMOJA YA HABARI ZA BIASHARA ZA UCHUNGUZI .
 HONGERA SANA KWA KUFUZU MAFUNZO YA UCHUNGUZI ANASEMA DK.SAFARI















MAHAFALI TWIBHOKI PRE PRIMARY-SERENGETI

MAANDAMANO YA KUINGIA UKUMBINI
WA KWANZA KULIA NI WILBROAD ANTHONY MAYUNGA

WILBROAD AKIONGOZA MAANDAMANO YA KUINGIA UKUMBINI
MAMBO YANAZIDI KUNOGA
HUYO NDIYE MAYUNGA JUNIORAdd caption

MAMA YAKE AKIMPONGEZA KIJANA WAKE
HONGERA MWANANGU KWA KUHITIMU NA KUIBUKA BINGWA WA TAALUMANI MANENO KUTOKA KWA MAMA YAKE
HONGERA NA PONGEZI HAZIKUACHANA


HUYO NI MDOGO WAKE NA WILBROAD ANAITWA FRANSISCA ANTHONY MAYUNGA AKISHUHUDIA HUKU NAYE AKIAHIDI KUFUATA NYAYO ZA KAKA YAKE MWAKA KESHO

KAKA NIMEKUKUBALI NI MANENO YA FRANSISCA

FRANSISCA AKIWA MENEJA WA MJADALA WAKATI WAKIONYESHA WAGENI WAALIKWA KUWA WANAWEZA ,
MJADALA UNAENDELEA MENEJA ANAUSIMAMIA VILIVYO
NI WAKATI MUAFAKA WA KUJALI AFYA WILBROAD ANAONGOZA WENZAKE
WAKATI MWINGINE HUAMUA KUPOOZI KAMA ALIVYO NASWA NA BLOG HII

WWAZAZI MBALIMBALI WALIKUWEPO KUWAPONGEZA WATOTO WAO

WWILBROAD ANAPOKEA CHETI CHA KUHITIMU PIA ALIPEWA CHETI CHA TAALUMA (HISTORY
KKAKA POKEA ZAWADI KUMBUKA MWAKANI NAMI MUNGU AKIJAALIA UJE UNITUZE,FRANSISCA AKIMWAMBIA KAKA YAKE
WILBROAD AKIWA NA MAMA YAKE NA MDOGO WAKE WA MWISHO ALICE AMBAYE ALIFIKA KUSHUHUDIA MAHAFALI YA KAKA YAKE.ption


HHONGERA WILBROAD