Subscribe:

Ads 468x60px

JANGILI ALIYEKUTWA NA SMG AFUNGWA MIAKA 15 JELA

 ALIYEKUTWA NA BUNDUKI YA KIJESHI,RISASI 96 NA NYARA ZA TAIFA AFUNGWA
MIAKA 15 JELA.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Oktoba 30,2012.

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Serengeti imemhukumu  mkazi
mmoja wa kijiji cha Motukeri kata ya Natta wilayani hapa kwenda  jela miaka
15 kwa  makosa ya kukutwa na bunduki ya kivita aina ya smg,risasi 96 na
nyara za taifa.

Aliyekumbwa na adhabu hiyo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Franco
Kiswaga ni Sabasaba Nyagekubwa(31) baada ya kukiri makosa yote manne
yaliyokuwa yanamkabili alipofikishwa mahakamani oktoba 29 mwaka huu.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Kiswaga alisema mahakama hiyo imemtia
hatiani mtuhumiwa huyo baada ya kukubali makosa manne yaliyokuwa
yanamkabili ikiwemo kula njama za kuingia hifadhini bila kibali.

Makosa mengine ikiwa ni kukutwa na silaha ya kivita aina ya SMG ambaye
kisheria hapaswi kukaa nayo raia ,kukutwa na risasi 96 kinyume cha
sheria na kukutwa na nyara za taifa vipande 10 vya nyama ,mikia 6 ya
nyumbu  na mayai manne ya mbuni.

“Kutokana na makosa hayo ambayo ni kinyume cha sheria na ambayo
yanaonekana kukithiri unahukumiwa kwenda jela miaka 15 ili iwe
fundisho kwa wengine ,kwa kuwa hatujui hiyo silaha kwa muda uliokaa
nayo umeitumiaje”alisema hakimu.

Katika utetezi wake mtuhumiwa aliomba mahakama imuhurumie kwa kuwa ni
kosa lake la kwanza kukaa na bunduki ya kijeshi  na hakuweza kuisumbua
mahakama na ndiyo maana aliposomewa makosa yake alikubali yote.

Mapema  oktoba 29 mwaka huu mwendesha mashitaka mrakibu msaidizi wa
polisi Alfred Marimi aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa
oktoba 25,majira ya saa 11 alfajiri mwaka huu katika kijiji cha
Motukeri alikamatwa akiwa na silaha,risasi na nyara za taifa.

Mbali nay eye watuhumiwa wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni
Timoth Omoke(20) mkazi wa Kisii nchini Kenya na Pius Mayenga mkazi wa
kijiji cha Kyandege wilayani Bunda ambaye alikana mashitaka yote na
kurudishwa mahabusu hadi novemba 13,2012 itakapotajwa tena.

Mtuhumiwa baada ya kukubali kosa kesi hiyo iliahirishwa hadi oktoba 30
2012 siku moja kwa ajili ya hukumu,hata hivyo kosa moja la kukutwa na
nyara bado linaendelea  novemba 13  mwaka huu kwa kuwa ni uhujumu uchumi wanasubiri kibali
ili iweze kusikilizwa.
Raia wa Kenya naye ahukumiwa.
Wakati huo huo Omoke raia wa Kisii nchini Kenya aliyekutwa nyumbani
kwa Nyagekubwa amehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela ama kulipa faini
ya tsh,250,000= baada ya kubainika kuishi nchini bila kibali.

Omoke ambaye kibali chake kilibainika kuisha toka oktoba 7 mwaka huu
amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa kiasi hicho.

Mwisho.

wakamatwa na smg,rissasi 96 na nyara za taifa

WAKAMATWA NA SMG,RISASI 96 NYARA IKIWEMO MAYAI YA MBUNI,
Na Anthony Mayunga-serengeti
Oktoba 29,2012.

WATU watatu  wakazi wa kitongoji cha Mageriga kijiji cha Motukeri kata ya Natta wilayani Serengeti wamekamatwa na bunduki ya kivita aina ya Smg ,risasi 96,vipande 10  vya nyara za nyama pori na mayai 4 ya mbuni.

Tukio limetokea ikiwa ni siku chache katika kijiji cha Makundusi kata hiyo tembo watatu walidaiwa kuuawa kwa njia ya sumu na meno yake kuchukuliwa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na watuhumiwa walikamatwa kwa kati ya oktoba 25 na 26 katika maeneo tofauti ya wilaya za Serengeti na Bunda.

Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa za wananchi polisi na Tanapa ambao baada ya kukithiri matukio ya ujangili wanahaha kila kona kuhakikisha mtandao huo unadhibitiwa kabla ya kuleta madhara makubwa.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni  Sabasaba Nyagekubwa (31)aliyekutwa na silaha na risasi hizo zikiwa chini ya godoro  wamelalia na kuwataja  wenzake ambao ni Pius Mayengo mkazi wa Kyandege wilayani Bunda na  Timoth mkazi wa Kisii Kenya.

Mkisii huyo alidai kuwa yeye alifika kwa mtuhumiwa huyo kutoa mahari baada ya kumtorosha binti wa mtuhumiwa e ,madai ambayo yanapingwa na baadhi ya majilani kwa madai kuwa huo ni mtandao wao wa kuvusha  nyara kwenda nchini Kenya .

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinadai kuwa Nyagekubwa alikamatwa oktoba 25 majira ya saa 11 alfajiri akiwa kwa hawala yake na kuwampeleka nyumbani walipokuta silaha na risasi zikiwa zimefungwa kwenye mfuko.

Bunduki hiyo aina ya SMG inadaiwa ni ya kisasa  kwa kuwa ina stendi za kusimamisha wakati wa kutenda uharifu,inadaiwa kuingizwa nchini  kutokea nchi za Rwanda na Burundi kupitia Kigoma na mtu mmoja ambaye inadaiwa aliingia kijijini hapo akijifanya mganga wa kienyeji(Sangoma)

Sangoma huyo ambaye jina lake limehifadhiwa  anasakwa alitajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye aliyeingiza silaha na risasi kwa lengo la kuwindia tembo na uhalifu mwingine na  kuwa hata soko la nyara ndiye anajua.

Watuhumiwa  walikutwa harusini .

Kwa mjibu wa habari hizo inasemekana watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka baada ya kukutwa kwenye harusi na polisi katika kudhibiti watu wote watuhumiwa wakafanikiwa kutoroka .

Wengine walitaarifiwa kwa simu na kutoroka na nyara.

Habari hizo zinasema kuwa  watuhumiwa wengine walitaarifiwa na hawala wa Nyagekubwa  kwa njia ya simu baada ya polisi kuchukua simu ya mtuhumiwa na wengine huku moja ikifichwa ndiyo ilisaidia watuhumiwa kutoroka na nyara walizokuwa nazo.

Mtuhumiwa anakesi mbili za nyara kwa majina tofauti.

Imebaini kuwa mtuhumiwa Nyangekubwa anakabiliwa na kesi mbili za kukutwa na nyara kwa majina tofauti na moja akidaiwa kuruka dhamana na alipokamatwa kwa tukio kama hilo aliandika jina lake halisi.

Kesi ya kwanza aliandika jina la Ndalahwa Makaranga  tukio la mwaka 2010 ambalo aliruka dhamana.

Silaha za kivita huingizwa kutokea Kigoma.
Matukio ya watu kuingiza silaha kutokea mkoani Kigoma yanazidi kushika kasi kwa ajili ya uwindaji wa tembo na uhalifu mwingine,ikiwemo mtandao uliowahi kutikisa bunge lililopita kwa kuwataja watuhumiwa ambao walipewa dhamana kinyamera licha ya kukamatwa na Smg 4 na risasi zaidi ya 460.

Watuhumiwa walifutiwa kesi.
Hata hivyo wale watuhumiwa waliokamatwa na shehena ya silaha hizo na kelele kusambaa hadi bungeni walifutiwa mashitaka kinyamera katika mazingira ambayo inadaiwa kutawaliwa na rushwa kwamba hawana mashitaka ya kujibu.

Kuachiwa kwao kuliibua maswali mengi kutoka Tanapa kwa kuwa wanakamata watuhumiwa  na vielelezo ikiwemo bunduki za kivita lakini polisi huwaachia linadaiwa kusimamiwa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Serengeti,ambaye kutokana na kashifa hiyo ameshushwa cheo na kupelekwa ofisi ya kamanda wa upelelezi mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya.

Hata hivyo baada ya kubainika waliachiwa kwa mazingira ya rushwa watuhumiwa baadhi walikamatwa tena kwa maelekezo ya ngazi za juu za jeshi la polisi na wako chini ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara huku wakiendelea kuwasaka wengine.

Mwisho,itaendelea.

mwanafunzi atuhumiwa kwa kuua kwa mshare familia yake yakimbia kwa kuhofu kuuawa

MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,
Na Anthony Mayunga-Serengeti.
Oktoba 27,2012.

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na kufa papo hapo.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2 mwaka huu  usiku nyumbani kwa marehemu Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya nyumba yake.

“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana huenda wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.

Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko julikana.

“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.

Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo ameyasikia.

“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na majilani,nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio hilo,tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila hata kuwaeleza sababu”alisema.

Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.

Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa  kidato cha pili Mugumu  sekondari  wilayani wilayani hapa  Mwang’omba Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya  kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)

Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu  ths 5,000  na katika kudaiana wakakorishana ndipo akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.
Mwisho.

FAMILIA YA MWANAFUNZI ANAYETUHUMIWA KUUA KWA MSHARE YATOWEKA KIJIJINI
KWA HOFU YA KUUAWA.
NaAnthony Mayunga-Serengeti
Oktoba 28,2012.
FAMILIA ya mwanafunzi wa kidato cha tatu sekondari ya Busawe wilayani
Serengeti Peter Lucas Wambura(17)anayesakwa  na polisi kwa tuhuma za
kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18)imetoweka kijijini
hapo na malizao zikiwemo kuku kwa hofu ya kuuawa.

Kutoweka kwao kunadaiwa kutokea oktoba 27,usiku mwaka huu baada ya
kubaini kuwa Mangali ameaga dunia kufuatia  kupigwa mshare wa sumu
kifuani na mtuhumiwa akimtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi na mdogo
wake anayesoma kidato cha pili sekondari ya Busawe.

Kwa mjibu wa habari kutoka kijijini hapo zilizothibitishwa na kamanda
wa tarafa hiyo Inspekta Abdallah Idd ambaye alikuwa eneo la tukio
zinadai kuwa familia hiyo ilitokomea kusikojulikana wakiwa wamebeba
kila kitu ikiwemo kuku.

Hofu yao ikiwa wananchi wangeweza kuwadhulu kwa kitendo kilichofanywa
na kijana wao ,tukio ambalo linadaiwa kushuhudiwa na mama wa mtuhumiwa
akimpongeza kijana wake kwa kumchoma mshare Mangali kwa kuwa alikuwa
alikuwa anachangia kuharibu mwenendo wa mtoto wake kimasomo.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio marehemu Mangali alikwenda kwao na
mtuhumiwa kwa lengo la kukutana na mpenzi wake huyo,tukio lililomuudhi
mtuhumiwa na kuchukulia kama dharau kwa familia kwa kuwa walikuwa
wameishamkata uhusiano wa mapenzi na binti huyo kwa kuwa ni
mwanafunzi.

“Walipigana kwanza hapo nje kwa kuwa wote walikuwa kama wanalingana
,mtuhumiwa baada ya kuona amezidiwa nguvu aliingia ndani na kutoka na
upinde na mshare mwenzake akidhani ana tania ndipo akamchoma kifuani
,lakini akafanikiwa kuuchomoa na kutoa taarifa kwao kwa kuwa ni
majilani”alisema mmoja wa wanafamilia jina limehifadhiwa.

Hata hivyo familia ya marehemu ilimwita mama wa mtuhumiwa ambaye
alisema alichokuwa anatafuta amekipata,wakati wanajiandaa kwenda
hospitali aliaga dunia kwa kile kinachodaiwa alizidiwa na sumu yam
share huo.

Hata hivyo jamii imesema itamnasa mtuhumiwa na familia hiyo kwa kuwa
hawataweza kukwepa zaidi ya kuchelewa kukamatwa,kwa kuwa tukio hilo ni
la kusikitisha na ambalo liliibua hisia kali za watu.

Habari za uhakika zinadai kuwa kutoroka kwa familia hiyo kulitokana na
hisia za kuweza kuuawa kwa kuwa si watu wa jamii hiyo na ukoo wa
aliyeuawa ni mkubwa ,huenda wakawa wamekimbilia maeneo mengine huku
mtuhumiwa akawa hakuambatana nao.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi kuwa
tukio hilo lilitokea oktoba 26,majira ya saa 2 usiku mwaka huu
nyumbani kwa marehemu likihusishwa na migogoro ya mapenzi.
 
MUUZA UREMBO ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA AKIMPAKA RANGI ZA KUCHA MKE WA BODABODA.
Na Anthony Mayunga-Mara
Oktoba 29,2012.

BODA BODA wa baiskeli mtaa wa Nyasho C,Manispaa ya Musoma anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujeruhi watu watatu waliokuwa wanamzuia asimkate kwa panga  muuza urembo baada ya kumkuta akimpaka mke wake rangi ya kucha.

Tukio hilo limetokea oktoba 27 majira ya saa 6 mchana mwaka huu katika maeneo ya Nyansho C’katika manispaa hiyo limethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma.

Kamanda huyo amemtaja mtuhumiwa anayeshikiliwa kuwa  ni Chacha Wandiba Masincha(25)ambaye ni boda boda wa baiskeli ambaye aliwajeruhi kwa kuwakata na panga watu watatu ambao walifikishwa hospitali kwa matibabu  wakatibiwa na kuruhusiwa.

“Mtuhumiwa alimkuta muuza urembo ambaye aliombwa na mke wa mtuhumiwa Anita Chacha(19)akitaka kumpaka rangi mke wake alichukua panga kwa lengo la kumkata ndipo watu wakajitokeza kusaidia asilete madhara “alisema kamanda.

Alisema katika purukushani hizo watu watatu waliokatwa  ni Nyairabu Mwita(22)mkulima na mkazi wa Nyasho C’,Kichonge Wandiba(19)mkulima mkazi wa eneo hilo na Marwa Wambura(20)ambaye ni boda boda eneo hilo.

“Majeruhi wametibiwa katika kituo cha afya Nyasho na kuruhusiwa kuondoka kwa kuwa hali zao hazikuwa mbaya ,lakini mtuhumiwa tunaye na tunategemea kumfikisha mahakamani taratibu zikikamilika”alibainisha kamanda Mwakyoma.

Hata hivyo muuza urembo alikimbia na kuacha mali zake ambazo ziliharibiwa na mtuhumiwa ambaye alionekana kupandwa na hasira kwa kile kilichobainika kuwa ni wivu wa kimapenzi dhidi ya mkewe.

Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa tatizo ni wivu wa kimapenzi na kutoaminiana kati yake na mkewe kwa kuwa mfumo wa wanawake kupakwa rangi ni la kawaida siku hizi.

Mwisho.

mwanafunzi atuhumiwa kwa kuua kwa mshare