Subscribe:

Ads 468x60px

BARAZA LA MADIWANI LAVUNJWA .

 Inawezekana ikawa Mwanzo ama baadhi wakarudi hasa kundi la viti maalum ambao wanategemea ushindi wa vyama vyao.
 Wananchi hawakuwa nyuma kufuatilia kikao hicho.
 Wanafuatilia mjadala

 Wageni mbalimbali walikuwepo
 Ng;oina akifungua kikao hicho cha mwisho.


KIKAO CHA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI CHATAWALIWA NA VITUKO,
Serengeti:Kikao cha kuvunja baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kimetawaliwa na vituko,ikiwemo madiwani kugoma kuingia ukumbini mpaka wajue hatima ya mafao yao,na Mwenyekiti kulia wakati akitoa hotuba ya mwisho.
Mgomo wa madiwani kuingia ukumbi wa halmashauri hiyo juzi ulianza saa 4 asubuhi  hadi 6:15 mchana ,huku watumishi,wageni waalikwa na wananchi wakiwa wamekaa ukumbini  kwa muda wote bila kutaarifiwa kinachoendelea.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya hiyo Mafutah Ally,aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng’oina,Mkurugenzi Mtendaji Naomi Nnko na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Stephen Kebwe walifanikiwa kuzima mgomo huo,baada ya kujadiliana kwa muda mrefu na  kuwapa utaratibu wa ulipaji wa mafao.
Dalili zamgomo zilianza mapema baada ya madiwani hao kuitana pembeni bila kujali itikadi zao na kuanza kuweka msimamo wa kutoingia mpaka wajue hatima ya malipo yao ya mwisho,na malipo ya madeni ya mikopo wanayodaiwa  katika benki za Nmb na Crdb  matawi ya Mugumu.
Samwel Gibewa aliyekuwa diwani wa kata ya Machochwe akiongea na blog hii  alisema  kuwa riba ya mikopo yao imeongezeka ,ikiwa ni nje ya mkataba wao,ongezeko ambalo lilipaswa kulipwa na Mkurugenzi .
“Hilo na  mafao yetu ndiyo yametufanya tukae nje mwa muda wote ili tujue hatima yake ,maana baraza linapovunjwa hata ufuatiliaji unakuwa mgumu….baada ya majadiliano ya muda mrefu na ufafanuzi ndiyo tumefikia uamzi wa kuingia ukumbini”anasema.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria waliliambia Blog hii kuwa wengi wanategemea fedha hizo ili ziwasaidie kwenye kampeini,kuambiwa zitatolewa baada ya uchaguzi ndiyo maana wakaweka msimamo.
Akisoma waraka toka ofisi ya Waziri Mkuu tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Mkurugenzi mtendaji Naomi Nnko alisema,posho za mwezi za madiwani zitalipwa hadi oktoba 30 na ndipo watalipwa na mafao yao ya mwisho.
“Kuhusu madeni ya madiwani yale waliyoingia wenyewe watalazimika kulipa ,lakini kama yapo ambayo halmashauri ilihusika ,yatalipwa kwa utaratibu husika,”alisema.
Katika hali isiyo ya kawaida na ambayo imeibua simanzi kwa madiwani waliomaliza muda wake ni kitendo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng’oina kumwaga machozi wakati anasoma taarifa ya baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
Ng’oina alimwaga machozi baada ya kuelezea alivyougua na madiwani wakamuuguza ,” wenzetu watatu kwa kipindi cha miaka mitatu waliaga maisha …mimi niliugua mkaniuguza kwa muda mrefu hadi nikapona,”alisema huku akitokwa machozi.
Hata hivyo alisema si vizuri kwa tukio hilo la yeye kumwaga machozi,lakini alisisitiza kuwa sasa amepona na alikuwa amefikia uamzi wa kutogombea,lakini wananchi wamemshauri agombee na hata madiwani wanaomba aendelee kuwa Mwenyekiti.
Kuhusu mafanikio kwa kipindi cha miaka mitano alisema wamejitahidi kujenga umoja wa madiwani bila kujali itikadi zao,na kuwa wametekeleza miradi mingi kwa ufanisi hali iliyosababisha kupata hati safi mwaka huu,na hawajawahi pata hati chafu.
“Kwa kipindi hicho tumefungua shule mbili za kidato cha tano na zinafanya vizuri,pia shule bora kitaifa kwa matokeo ya mwaka 2014 ilitoka wilayani hapa…pia shule mbili zilizofanya vibaya zimetoka hapa,”alisema.
Alisema ana imani wote watashinda kwenye chaguzi na watarudi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja kama walivyokuwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Nccr Mageuzi  wilaya ambaye pia alikuwa diwani wa kata ya Kisangura Tanu Mwita alipopewa nafasi ,alisema ili baraza hilo lifanye maamzi mazuri madiwani wa CCM wanapaswa kupunguzwa na wananchi ,kwa kuwa wamekuwa wakitumia wingi wao kupitisha hoja.
Mkuu wa wilaya hiyo  Mafutah aliwaomba wajiepushe na utoaji ahadi zisizotekelezeka ,kwa kufanya hivyo kunachangia migongano na jamii na kuisumbua serikali.
Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru wilaya Emmanuel Liguda alisema  hawatasita kuwakamata watakaokiuka sheria ya Takukuru na kuwataka waone  aibu kukamatwa na serikali yao kwa makosa ya kutoa rushwa
Mwisho.

 Inawezekana madiwani wengi wa viti maaluma wakapoteza nafasi zao,hapo wanaonekana kuwa na mawazo sana.
 Kamanda wa Takukuru wilaya Emmanuel Liguda akitoa tahadhari kwa watakaotoarushwa watakamatwa na serikali yao,hivyo waone aibu kukamatwa.
 Ded akisoma waraka toka Tamisemi unaoelekeza utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri baada ya kuvunjwa kwa baraza na pia mafao ya madiwani na stahiki zingine.
 Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu mkoa wa Mara akisisitiza matumizi mazuri ya fedha za miradi,licha ya kupata hati safi.
 Dk Kebwe akisisitiza jambo

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza John Ng'oina katikati,kulia Dc Mafutah na kushoto Ded Nnko wakifuatilia mijadala.
 Wengi wanawaza kama watavaa tena majoho hayo kwa kuwa upinzani ndani na nje ya chama chao ni mkubwa katika maeneo yao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Naomi Nnko kulia akiteta jambo na katibu tawala Cosmas Qamara wakati wa kikao cha kuvunja baraza la madiwani.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na mbunge wa jimbo hilo Dk Stephen Kebwe akielezea mikakati ya serikali kuboresha huduma za jamii.
 Mkuu wa wilaya Mafutah Ally akitoa nasaha kwa waliokuwa madiwani kuwa wakafanye kampeini kwa ustaarabu na serikali haitasita kuwakamata iwapo watakiuka sheria na taratibu za uchaguzi.

 Waliokuwa madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye kikao chao cha mwisho ,
 Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI Taifa Mosena Nyambabe akisalimia madiwani hao,tayari ametia nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.



UJENZI WA WODI LA AKINA MAMA KATA YA KISAKA WAANZA

 Wakazi wa kata ya Kisaka Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiwa kwenye kikao cha kujadili shughuli za maendeleo.
 Aliyekuwa diwani wa kata ya Kisaka wilaya ya Serengeti Chacha Togocho akielezea adhima yake ya kukamilisha wodi ya wanawake na watoto katika kata hiyo ili kupunguza matatizo ya kusafiri umbali mrefu wakati wa kujifungua,ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi desemba mwaka huu,anachangia sehemu kubwa ya mradi huo,wananchi wanatakiwa kutoa viashiria.
 Nasisitiza kuwa mnichague msinichague lazima nijenge wodi maana hapa ni nyumbani
 Wanaelekea eneo la mradi
 Watoto walipata zawadi zao ikiwa ni pamoja na kalamu .
 Someni sana maana ninyi ndiyo mtakuwa madiwani baadae, anasisitiza
 Nimedhamiria kujenga wodi hii kwa kushirikiana na marafiki zangu,ili akina mama wapate sehemu ya kujifungulia ,maana kukosekana kwa wodi wengi walikuwa wanahamia maeneo ya jilani na huduma ,anasisitiza.
 Watoto nao walishiriki kwenye mjadala huo kwa kuwa wana haki ya kutoa maoni,
 Msingi tayari umeishajengwa kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha ujenzi unakwenda kasi ili kufikia desemba kazi iwe imekamilika.
 Kazi hii italeta nafuu kwa wakazi wa kata hiyo
 Togocho anakabidhi mifuko mia ya saruji kwa vijiji vitanovya kata hiyo kwa ajili ya ujenzi na kukarabati majengo ya shule na nyumba za walimu
 Hongera sana maana unafanya kwa vitendo,
 Ushirikiano unatakiwa maana kazi hii ni yetu na wanufaika ni sisi sote ,anasisitiza Togocho.
Wananchi waliahidi kushikamana ili kukamilisha kazi hiyo.

MATUKIO MBALIMBALI WILAYANI SERENGETI.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Chamoto Mamlaka ya mji wa Mugumu wilaya Serengeti Rhobi Magoiga akikabidhi zawadi ya sh 25,000 kwa nahodha wa timu ya Magetta Fc baada ya kushinda mashindano ya Sabasaba.
 Rhobi akitoa zawadi ya soda kwa timu ya Magetta baada ya kuibuka washindi
 Mitambo ya Kampuni ya Samota Ltd kutoka Nzega ikisawazisha barabara ya mjini Mugumu wilaya ya Serengeti inayojengwa kwa kiwango cha lami nyepesi
 Mtambo ya Samota ikisawazisha barabara ikiwemo kubomoa majengo,vibanda vilivyojengwa katika hifadhi ya barabara
 Thomas Burito kada wa ACT WAZALENDO katikati akiwa na viongozi wa chama hicho wakati wa kuchukua fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo.
 Thomas akisaini kuchukua fomu ya kutaka kuteuliwa ndani ya chama hicho kuwania nafasi ya Ubunge ,anayeshuhudia ni katibu mwenezi wilaya Hamisi Lazaro
 Burito akielekea ofisi ya Act wilaya kuchukua fomu,msafara wake ulisimamiwa na kuongozwa na askari wa usalama barabarani
 Uboreshaji wa barabara unaendelea
 Burito anamwaga sera zake nini atawafanyia wakazi wa jimbo hilo iwapo atateuliwa na chama kisha kuchaguliwa na wananchi
 Huyo ni mmoja wa boda boda mjini Mugumu ambaye inadaiwa ni kada maarufu wa chama hicho,hapo akiwa eneo la ofisi ya wilaya hiyo mtaa wa NHC
 Pokea fomu kajaze kisha urudishe na ukiteuliwa peperusha vema bendera yetu,anasisitiza Katibu mwenezi wa wilaya Hamisi
 Msafara wa mtia nia ulipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo pikipiki,magari na muziki
 Msafara wa ACT Wazalendo
Mambo ya Act Wazalendo

PILIKA PILIKA ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA BUNDA

 Kikundi cha Tarumpeta wakiongoza maandamano wakati Dk Lucas  Webiro akirudisha fomu zakutaka kuteuliwa kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Bunda.
 Safari inakwenda ikiongezeka huku burudani zikihanikiza
 Boda boda nao hawakubaki nyuma katika kumsindikiza mtia nia huyo.
 Wanachama na mashabiki wa Chadema wengine walikuwa ofisi ya jimbo hilo wakisubiri mtia nia huyo
 Safari inaendelea kuelekea ofisi yajimbo la Chadema Bunda
 Dk Webiro akiwapungua mikono wananchi
 Wanachama,mashabiki na wananchi wakiwa ofisi ya jimbo hilo kushuhudia mtia nia akirudisha fomu
 Hata watoto walikuwepo
 Brudani ilipokolea kila mmoja aliingia kwa staili yake