BIDHAA HIZO HUTENGENEZWA NA WAJASILIAMALI ZANZIBAR NI KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII WA NJE NA NDANI
MCHEZO WA BAO NI MAARUFU SANA NASI HATUKUBAKI NYUMA KUSHIRIKI KUCHEZA
FORODHANI NI ENEO MAARUFU KWA VYAKULA VYA KILA AINA JIONI,WATU WA MATAIFA MBALIMBALI HUJIPATIA VYAKULA .
MSAFARA WA RAIS WA ZANZIBAR UNAKUWA NA MAGARI MACHACHE SANA WAKATI ZIARA YA MKUU WA MKOA KWA TANZANIA BARA HUSHEHENI MAGARI MENGI BILA SABABU ZA MSINGI,KUNA MAMBO YA KUJIFUNZA HAPA.
HABARI ZANZIBAR
BAADHI YA WAANDISHI WAHABARI WAKIFUATILIA MADA KUTOKAKWA MWEZESHAJI HAMZA KASONGO
ZANZIBAR BEACH RESORT NI ENEO ZURI KWA UTALII

PILIKAPILIKA ZA ZANZIBAR
KITUO KIKUBWA CHA MAGAZETI MJINI ZANZIBAR KIKO OLD DISPENSARY WAUZAJI HUPATA MGAO ,
HAPA TUKIWEKA AFYA VEMA ZANZIBAR BEACH RESORT
PILIKAPILIKA ZA BANDARINI ZANZIBAR
HAPA TUKIWEKA AFYA VEMA ZANZIBAR BEACH RESORT
MATUKIO MBALIMBALI ZANZIBAR
WAANDISHI WA HABARI WANAOHUDHURIA MAFUNZO YA CRITICAL JOURNALISM YALIYOANDALIWA NA ZIFF /TMF WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUFUNZI OLD DISPENDANSARY ZANZIBAR
PICHA YA PAMOJA
FORODHANI ENEO MAARUFU KWA ZANZIBAR HAPO WATU WA NATAIFA MBALIMBALI HUKUSANYIKA JIONI KWA AJILI YA KUPATA CHAKULA CHA KILA AINA ,PANAPENDEZA
DANNY SCHECHTER EDITOR IN CHIEF,MEDIA CHANNEL.ORG,NEWS DISSECTOR'BLOG; KUTOKA USA AKITOA MADA KWA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
TAMASHA LA ZIFF AWARDS NIGHT NGOME KONGWE

MAFUNZO YA CRITICCAL JOURNALISM ZANZIBAR YAENDELEA
HELENE THOMAS MWANDISHI WA HABARI TOKA AUSTRALIA AKITOA MADA KWA WAANDISHI WA HABARI WA NDANI NA NJE YA NCHI WANAOHUDHURIA MAFUNZO YA CRITICAL JOURNALISM ILIYOANDALIWA NA ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL KWA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA MEDIA FUND UKUMBI WA OLD ZAHANATI ZANZIBAR
MADHARI YA BANDARI YA ZANZIBAR
MOJA YA KAZI ZINAZOTENGENEZWA NA WAKAZI WA ZANZIBAR,HUUZWA KWA WAGENI HASA WATALII ,HAPO NI OLD DISPENSARY ZANZIBAR
KAZI NA DAWA HAPA WATU MBALIMBALI WAKIPATA CHAKULA HOTELINI,KWA KIPINDI HIKI WATALII NI WENGI ZANZIBAR

PICHA ZA MATUKIO YA TAMASHA LA 16 LA NCHI ZA MAJAHAZI NGOME KONGWE
PROFESA MARTIN MHANDO MKURUGENZI WA ZANZIBAR INTERNATION FILM FESTIVAL(ZIFF) AKIONGEA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA KENYA OFISI ZA ZIFF NGOME KONGWE ZANZIBAR
MMOJA WA WASHINDI WA AWARD ZA NCHI ZA MAJAHAZI
WASHINDI WA AWARD MBALIMBALI WA TAMASHA LA 16 ZA NCHI ZA MAJAHAZI KATIKA PICHA YA PAMOJA NGOME KONGWE
WASHINDI WA AWARD MBALIMBALI KATIKA PICHA YA PAMOJA

MAMBO YA ZANZIBAR
SAFARI ILIKUWA NZURI KWA MAONGOZI YA MUNGU
HAPO NI NGOMA KONGWE ZANZIBAR,ENEO MAARUFU SANA KWA HISTORIA YA KISIWA HICHO,WATALII WENGI HUFIKA ENEO HILO KWA AJILI YA KUPATA HISTORIA HIYO,MATAMASHA MBALIMBALI HUANDALIWA HAPO
SAFARI YA ZANZIBAR KUPITIA KIA
MUNGU NI MWEMA TUNAWASILI KIA TUNASUBIRI NDEGE KWENDA ZANZIBAR VIA UWANJA WA MWALIMU NYERERE DSM
SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE
KIA TUKITOKEA MWANZA
MAMBO YA SAFARI
KIA NI PAZURI,HALI YA HEWA BARIDI KIDOGO
KUELEKEA MAPUMZIKO KIA
ENEO HILI LINAVUTIA ZAIDI,
NIMEPAPENDA HAPA
MMOJA WA WAFANYAKAZI WA KIA,

WAFUGAJI WAIPA SERIKALI ANGALIZO KUNUSURU VURUGU
WAFUGAJI walioko kando ya mapori ya akiba ya Ikorongo
na
Grumeti wilaya za Serengeti na Bunda wameitaka serikali kuwachukuliahatua askari wa mapori hayo wanaoshirikiana na Kampuni ya SingitaGrumeti Reserves wanaohusishwa na utesaji wananchi na mauaji ya mifugo wanapowakamata.
Mbele ya viongozi wa serikali ,madiwani na Kampuni ya Singita Grumeti Reserves kwenye ukumbi wa Mandela Issenye wakati wa Kongamano lililoandaliwa na shirika la Maendeleo ya Wafugaji Jamii yaWataturu(Shimwajawa)wafugaji walisema hali ilipofikia inahatarisha uhifadhi kwa kuwa hakuna ushirikiano pande hizo mbili.
Gidai Murasi(75) mfugaji kutoka Hunyari wilayani Bunda kwa hasira alinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa “ili tuendelee tunahitaji ardhi,siasa safi,watu na uongozi bora…tatizo ni uongozi bora…kama inafikia wahifadhi wanaua ng’ombe wetu ili tuwe masikini….kuna mapato gani ya uhifadhi yanaweza kutuhudumia sisi kwa umaskini
wanaotusababishia?”alihoji.
Alisema wafugaji hao ni kama hawako Tanzania ,maana kwa umri wake hajaona taifa linalowafanya wananchi wake kuwa maskini…”mimi sijasoma…maisha yangu yote ni ng’ombe,natunza na kusomesha watoto kwa mifugo…hivi kwa nini mnatengeneza majambazi…nchi hii itakuja kuwa navita mbaya sana”alisema.
Murasi alisema serikali inatambua tatizo lao ni malisho hasa baada ya
kuchukua maeneo yao na kuwa hifadhi,wakati wa kiangazi hali huwa mbaya zaidi,lakini kama kungekuwa na uhusiano wangeruhusiwa kuingia hatua chache na kunywesha mifugo kwa kuwa mto walioutegemea nao ulichukuliwa na hawakuchimbiwa malambo.
Esther Balebe mkazi wa Issenye alisema mahusiano mabaya yaliyopo kwa wahifadhi na wafugaji yanachangia kukithiri kwa ujangili,kwa kuwa hata akina mama wakienda kuokota kuni wanadhalilishwa wanapigwa na kutendewa mambo yasiyofaa.
Joash Tangera alisema udhaifu wa serikali utakuja kuibua matatizo
makubwa kati ya pande hizo,kwa kuwa hiyo ni vita ya ndani ,lakini iko siku itakuja kuwa kubwa,wafugaji hawapendi kuingiza mifugo hifadhini lakini tatizo kubwa ni malisho,baada ya eneo lao kuchukuliwa na kuwa kwa mahusiano wangeruhusiwa kuchungia mita chache wakati wa kiangazi.
Walihoji sababu za serikali kuwafidia wafugaji wa Monduli baada ya
ng’ombe wao kufa kwa ukame,wakati nao wana matatizo kama hayo,wengine wanauawa na pia wanyama wanaua watu,mifugo na kula mazao na hakuna fidia iliyowahi tolewa.
Gijeshi Gambarara mkazi wa Iharara alisema ng’ombe wake watatu
walifukuzwa kwa helkopita yaSingita Grumeti Reserves na kushuka
karibu upepo ukawapelekea kuzama mtoni na kufa,huku shamba lake la ekari 10 likiwa limeliwa na wanyama pori,lakini hajawahi pata
msaada,na kuwa uwekezaji huo haufai kwa jamii.
Wafugaji walisema mpango wa mwekezaji ni kuua mifugo yao ,hata kwenye mipango yake hakuna mkakati wa kusaidia wafugaji.
Baadhi walisema serikali isisubiri matatizo kama ya Mtwara ndio
ichukue hatua bali wakae chini watafute ufumbuzi wa pande hizo,kwa kuwa madhara yake ni makubwa ikiwemo ongezeko la ujangili wa tembo kwa kuwa jamii haioni faida ya kutoa ushirikiano kwa sekta inayowatia umaskini.
Mwenyekiti wa Shimwajawa Gohebu Gorobani na katibu wake Mnada Mayonga walisema lengo la kukutanisha wahifadhi,wafugaji na serikali ni kutafuta muafaka kwa maslahi ya taifa kwa kuwa kuna kila dalili za uvunjifu wa amani.
Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Serengeti ambaye ni afisa tarafa ya
Grumeti Paulo Shanyangi alisema njia hiyo inalenga kuleta muafaka, serikali itachukua hatua za haraka ili kuleta mahusiano,akiitaka kampuni ya Singita Grumeti kusaidia wananchi upande wa malambo ya maji.
Kwa upande wa Kampuni ya Singita Grumeti waliomba suala hilo
lisichukuliwe kwa jazba madhara yake ni makubwa kwa kuwa watakaoumia ni vijana wao ,kwa kuwa mwekezaji hakuja na watu wake,bali watumie njia ya kuzungumza kwa kuwataja wahusika hatua zichukuliwe.
Hivi karibuni askari hao wametuhumiwa kuua ng’ombe 51 na wengine 100 kupotea mali ya Kiteku Meshinya mkazi wa Mariwanda wilayani Bunda,baada ya kuwakamata na kisha kuwafukuza kwa magari na kuzama mto Rubana.
Mwanzoni mwa mwaka huu ng’ombe zaidi ya 40 mali ya Kijiji mkazi wa Motukeri waliuawa kwa mtindo huo,na mwaka 2008 ng’ombe 65 wa Gorobani Marosina walizamishwa mtoni,huku ikidaiwa kijana mmoja naye alikufa maji baada ya kumkimbiza na kutumbukia mtoni.
Hata hivyo uongozi wa Senapa,ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi halmashauri ya Bunda hawakuhudhuria kongamano hilo licha ya kuwa na taarifa.
WAFUGAJI WAKATI WA KONGAMANO LILILOWAKUTANISHA NA WAHIFADHI NA VIONGOZI WA SERIKALI CHINI YA SHIRIKA LA SHIMWAJAWA ISSENYE WILAYANI SERENGETIGrumeti wilaya za Serengeti na Bunda wameitaka serikali kuwachukuliahatua askari wa mapori hayo wanaoshirikiana na Kampuni ya SingitaGrumeti Reserves wanaohusishwa na utesaji wananchi na mauaji ya mifugo wanapowakamata.

MMOJA WA WAFUGAJI KUTOKA MARIWANDA WILAYANI BUNDA AKIELEZA MIKASA IWAKUTAYO WAFUGAJI
HATA AKINA MAMA WAFUGAJI HAWAKUSITA KUSEMA WANAVYOTENDEWA NA WAHIFADHI WAWAKAMATAPO HIFADHINI WAKIWA NA MIFUGO AMA WANASENYA KUNI
Subscribe to:
Posts (Atom)