Subscribe:

Ads 468x60px

MACHIMBO YA KOKOTO YAUA WAWILI,MMOJA MAJERUHI WOTE WA FAMILIA MOJA.

JOSEPH WAMBURA NDUGU WA MAREHEMU NA MAJERUHI AKIWA AMELAZWA WODI LA WANAUME BAADA YA KUPOTEZA FAHAMU MUDA MFUPI TU BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA VIFO.

Julai 14,2013.
Serengeti:WATU wawili wakazi wa kitongoji cha Kanisani kijiji cha Matare Mamlaka ya mji wa Mugumu wilayani Serengeti wa familia moja  wamekufa na mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto.
Tukio hilo limethibitishwa na polisi,uongozi wa kitongoji na Hospitali teule ya Nyerere ddh limetokea julai 14 majira ya saa 4:10 asubuhi mwaka huu katika eneo la machimbo ya kokoto,wakati wakiwa wanachimba.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Juma Mahando amewataja waliofariki kuwa ni Rhobi Mwita Nyantori(45)ambaye alifia eneo la tukio,Nyahiri Chacha Mwita(41)ambaye amefariki baada ya kupata huduma na majeruhi ni Wegesa Mwita(39)ambaye amelazwa.
Akisimulia mkasa huo kwa kugugumia Wegesa ambaye ni majeruhi alisema wenzake walikuwa ndani ya shimo nay eye akiwa pembeni akisubiri mzigo wa kokoto aweze kutoa nje ghafla walianguliwa na kifusi chote na kuwafunika.
“Udongo wote umenifunika..kilichosaidia pembeni kulibaki kama uwazi,lakini waliokuwa ndani humo umewapiga wakiwa wameinama na kuanguka…watu waliokuwa nje waliona na kupiga kelele wakajitokeza watu wakatupa msaada…nahisi maumivu makali kiunoni na mbavu”alisema kwa kugugumia.
Mganga wa zamu dk,Amosi Kittoh amesema kilichopelekea kifo cha Rhobi ni kuumia kifuani na Nyahiri alipata madhara makubwa kwenye uti wa mgongo .
Dk ,Kittoh amesema kuwa tukio hilo limesababisha ndugu wa marehemu hao Joseph Wambura kupoteza fahamu na wamemlaza wodi ya wanaume kwa ajili ya matibabu.
Akizungumzia machimbo hayo Mwenyekiti wa kitongoji hicho Mahando alisema novemba 2009 watu wawili wa familia moja waliangukiwa na kufariki,ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya vifo na serikali ikayafunga.
Hata hivyo alisema watu walikuwa wakienda kuchimba kama wizi kujipatia riziki,hata hivyo baadhi ya wananchi walisema serikali inafahamu kuwa machimbo hayo yanaendelea kwa kuwa kokoto huuzwa hadharani,huku hata viongozi wa wilaya wakiwa ni wateja wao na ndiyo maana yameendelea kwa kipindi chote bila kuwakamata wahusika.
Mwisho.
Wegesa Mwita(39)mmoja wa majeruhi ambaye amelazwa,katika hospitali teule ya Nyerere ddh baada ya kuangukiwa na kifusi wakichimba kokoto,akisukumwa na mwenyekiti wa kitongoji cha kaniasani Matare wilayani Serengeti Juma Mahando.



 Wegesa Mwita(39)majeruhi katika tukio hilo.
 BAADHI YA NDUGU WAKILIA BAADA YA KUTAARIFIWA KUFARIKI KWA NYAHIRI CHACHA MWITA(41)

SANGOMA NUSURA ASABABISHE MAAFA KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA KIRUMI WILAYANI BUTIAMA




 MATIKO JOSEPH MKAZI WA KIRUMI WILAYANI BUTIAMA AKIWA WODI YA WANAUME HOSPITALI YA MKOA WA MARA BAADA YA KUPOTEZA FAHAMU MUDA MFUPI TU BAADA YA KUNYWESHWA DAWA NA MGANGA WA KIENYEJI ANAYEDAIWA KUTOKA NCHINI KENYA KWA LENGO LA KUBAINI WEZI WALIOMWIBIA MKAZI MMOJA WA KIJIJINI HAPO.
Dawa ya sangoma yawageukia wanafamilia, wapata kichaa  
Kwa ufupi
  • Filamu hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume (Omwando) wanaoishi Kenya, kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia ndugu yao.
Mwalimu aliyetumia uchawi kuwaroga wezi, amejikuta akiwaroga shemeji zake waliopata uchizi
Butiama. Ilikuwa kama simulizi ya kwenye filamu, baada ya mganga wa kienyeji aliyeletwa toka Kenya kuja kuwaroga wezi walioiba nyumbani kwa Mwalimu mstaafu, Raphael Omwando (60), baada ya dawa yake kuwatia uchizi ndugu wa mke mkubwa wa aliyeibiwa.
Mwalimu Omwando ambaye ana wake wawili alivamiwa na wezi waliomwibia pikipiki na mali nyingine, ikiwemo kumjeruhi yeye (Omwando) na mkewe mkubwa. Mke mdogo aliyemuoa hivi karibuni anaishi kwenye nyumba nyingine na hakuweza kuvamiwa na wezi hao, lakini mke mkubwa alipigwa hadi kulazimika kupewa matibabu hospitali.
Watu walio karibu na familia hiyo walisema kutokuelewana kati ya mke mkubwa na mdogo, kulimfanya mke mkubwa aliyejeruhiwa na majambazi kumtuhumu mke mdogo kwamba alishirikiana na majambazi hao.
Filamu hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume (Omwando) wanaoishi Kenya, kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia ndugu yao.
“Sijui nimefikaje hapa hospitali…maana kumbukumbu zinaishia pale nilipolazimishwa kunywa dawa na mganga wa kienyeji (Sangoma) anayedaiwa kutokea nchini Kenya …ili wezi wa pikipiki na vifaa vya mwalimu mstaafu virudishwe,” hiyo ni kauli ya mmoja kati ya watu wanne waliolazwa hospitali kwa madai ya kurukwa na akili.
Boniphace Joseph (20)huku akisitasita, anasema ana habari kabla ya kunywa dawa lakini baada ya kunywa hakumbuki kilichoendelea mpaka alipopata fahamu na kuona watu wanamshangaa naye akiwashangaa.
Msira Magesa (17) anasema yeye baada ya kunywa alitoka kwenda kwenye shughuli zake, ghafla akazidiwa na kupewa dawa ya kutuliza maumivu aina ya panadol hali ikazidi kuwa mbaya na kufikishwa hospitali kwa matibabu
Hali ilivyokuwa
Julai 5, majira ya saa 5:15 usiku mwaka huu, Mwalimu mstaafu, Raphael Omwando (60) alivamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wakamkata yeye, mkewe akapigwa na majambazi hao na baada ya kipigo waliiba pikipiki, mabegi ya nguo, sola, sanduku dogo la kuhifadhia nyaraka, simu ya mkononi na vitu vingine.
Omwando kutokana na majeraha aliyoyapata akapelekwa hospitali ya mkoa alikolazwa kwa matibabu, lakini ndugu zake wanaoishi Shirati na wale wanaoishi nchini Kenya baada ya kupata taarifa waliamua kuchukua mganga wa kienyeji kutoka Kenya, ambaye aliwahakikishia kuwa wahusika baada ya saa 3 watarudisha vitu walivyoviiba wakiwa wamejitwisha na pikipiki wakiwa wanaisukuma.
Mganga huyo alieleza dalili za awali zitakazowapata wezi hao kuwa ni kuchanganyikiwa, wengine watakuwa wanakula nyasi kama ng’ombe. Mganga huyo alitoa tangazo kwamba  Julai 9 majira ya saa 9:00 alasiri wanakijiji wote wajitokeze kunywa dawa hiyo ili kuwapata wahusika.
Vituko vyao walikojoleana, kutapikiana
Mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema, walipofikishwa hapo aliogopa,“ walikuwa wanakojoleana midomoni, wanatapikiana, huku wakiongea lugha za ajabuajabu, tuliogopa maana ni tukio la kwanza kutokea,” anasema.
Anasema walipewa dawa za kuwafanya walale lakini wakaonekana wanaendelea kuongea wengine kukimbia huku wakidai kuna watu wanataka kuwaua, lakini sasa wametulia wanaongea wenyewe.
Shuhuda mwingine Isa Magesa anayemuuguza ndugu yake anasema Matiko, mmoja wa waathirika hao alikuwa akikimbia kasi kwenda nje huku akipiga kelele, “Nililazimika kutoa msaada, nilipomkamata alionekana ana nguvu sana huku akisema…acheni kuniua…hao wanakuja kuniua…nisaidie …wabaya hao, huku akionyesha kwa vidole lakini wao hawawaoni,” anasema.
Mganga Mfawidhi.
Dk Iragi Ngerageza, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa, anasema vijana hao walifikishwa hapo wakiwa hawajitambui huku ikidaiwa kuwa walipewadawa na mganga wa kienyeji na kuwapokea wakiwa na hali mbaya  na kuwa hali hiyo bado wanaendelea kuichunguza.
“Inakuwa vigumu kujua madhara ya hiyo dawa, kama tungeweza kuipata na kupeleka kwa mkemia ingetoa majibu, lakini kwa sasa sisi tunaendeleakuwatibu…lakini ni hatari maana kama walikunywa wakafikia hatua hiyo lazima kuna kitu, ikipatikana itatusaidia,” anasema.
Mke wake akamatwa.
Pilly Esther mke mdogo wa Mwalimu Omwando amekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo,  kusaidia kumpata mganga aliyehusika na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Butiama.
Hata hivyo akizungumzia tukio hilo anasema, wakati mume wake anavamia yeye alikuwa kwake na alisikia kelele za mbwa, lakini hakuelewa kilichotokea mwishoni akapigiwa simu na mke mkubwa kuwa wamevamiwa na kuumizwa. “Ndugu wa mume wangu akiwemo mke mkubwa ambaye ni Mjaluo wa kwao walinituhumu mimi kuwa ndugu zangu ndiyo wameiba mali kwa kuwanimeolewa hivi karibuni..au mpenzi wangu wa zamani ndiye amehusika, nilipokataa wakasema wanakuja na mganga kutoka Kenya ambayeanatoa majibu haraka,” anasema.
Anasema mganga aliomba mtendaji kualika wananchi wote lakini akakataa wakafika kama 40 wakiwemo kinamama, lakini kabla ya kutoa dawa akawaanasema wahusika ni kama anawaona hapo anawaomba wasinywe dawa, ajabuwaliopata madhara ni ndugu wa mke mkubwa.

Wagonjwa hao ni vijana wanne wa Kijiji cha Kirumi  Kata ya Bukanga, Tarafa ya Makongoro, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara waliolazwa hospitali ya Mkoa wa Mara baada ya kunywa dawa hiyo na kupoteza fahamu huku wakionekana kama mazuzu (Mazombi).
Waathirika
Matiko Joseph (25) anasema yeye alilazimishwa kunywa dawa nyingi pamoja na makapi yake,” …Baada ya kumtajia mganga hivyo akasema ninyi kunyweni nyingi…dawa ilikuwa na ukakasi ilinikereketa sana. Baada ya kunywa niliondoka lakini baadaye hali ikabadilika sana,” anasema na kuongeza,
“Nilishtukia niko hospitali tayari ikiwa ni siku ya pili …Nikisimuliwa ilivyokuwa nazidi kushangaa…huyo mganga alilenga kutuua kabisa….maana wakati anatoa dawa alisema atakayepata madhara hatapona hata akipelekwa wapi mpaka vitu virudi ama fedha…akaondoka kwenda Kenya na hakuacha simu wala jina lake kujulikana,” anasema Joseph huku akipumua kwa harakaharaka.
Tura Joseph (30) anasema wengine walikunywa kidogo lakini wao wana ndugu walilazimishwa kunywa zaidi kwa kile kinachodaiwa kuwa walihisiwa kula njama za kumdhuru shemeji yao, na ndiyo walidhurika zaidi.
Anasema baada ya kunywa alihisi kitu kinamkaba shingoni na kuishiwa nguvu, akawa hoi na kuanza kuongea maneno yaliyowatia shaka, ndugu wakawabeba kwa bajaji hadi hospitali.
“Inakuwa vigumu kujua madhara ya hiyo dawa, kama tungeweza kuipata na kupeleka kwa mkemia ingetoa majibu, lakini kwa sasa sisi tunaendeleakuwatibu…lakini ni hatari maana kama walikunywa wakafikia hatua hiyo lazima kuna kitu, ikipatikana itatusaidia,” anasema.
Mke wake akamatwa.
Pilly Esther mke mdogo wa Mwalimu Omwando amekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo,  kusaidia kumpata mganga aliyehusika na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Butiama.
Hata hivyo akizungumzia tukio hilo anasema, wakati mume wake anavamia yeye alikuwa kwake na alisikia kelele za mbwa, lakini hakuelewa kilichotokea mwishoni akapigiwa simu na mke mkubwa kuwa wamevamiwa na kuumizwa. “Ndugu wa mume wangu akiwemo mke mkubwa ambaye ni Mjaluo wa kwao walinituhumu mimi kuwa ndugu zangu ndiyo wameiba mali kwa kuwanimeolewa hivi karibuni..au mpenzi wangu wa zamani ndiye amehusika, nilipokataa wakasema wanakuja na mganga kutoka Kenya ambayeanatoa majibu haraka,” anasema.
Anasema mganga aliomba mtendaji kualika wananchi wote lakini akakataa wakafika kama 40 wakiwemo kinamama, lakini kabla ya kutoa dawa akawaanasema wahusika ni kama anawaona hapo anawaomba wasinywe dawa, ajabuwaliopata madhara ni ndugu wa mke mkubwa.
 
MUUGUZI AKICHUKUA VIPIMO KUBAINI CHANZO CHA UGONJWA WA WAKAZI HAO.

DAWA YA KUBAINI WEZI YAWAFANYA WACHANGANYIKIWE

MUUGUZI KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MARA AKICHUKUA DAMU KWA AJILI YA VIPIMO KWA MMOJA WA WALIONYWESHA DAWA NA MGANGA KIENYEKI KIJIJI CHA KIRUMI WILAYA YA BUTIAMA ,LENGO LIKIWA NI KUNASA WEZI WALIOMWIBIA MWALIMU MSTAAFU RAPHAELOMWANDO,BADALA YA VITU VILIVYOIBIWA KURUDISHWA NDANI YA SAA 3 VIJANA WANNE WALICHANGANYIKIWA KATI YA WATU ZAIDI YA 35 WALIOKUNYWA.

TAMASHA LA ZIFF


SAFARI YA KUREJEA JIMBONI

 BAADA YA KUKAMILISHA MAJUKUMU ZANZIBAR,HAPO NIKO UWANJA WA NDEGE NIKISUBIRI MUDA MUAFAKA WA KUANZA SAFARI YA KUREJEA JIMBONI

SAFARI INAANZA TARATIBU YA KUREJEA JIMBONI
 KAMA ILIVYO NYUKI WENGINE WANAINGIA WENGINE WANATOKA NDIVYO SAFARI ILIVYOKUWA.
 BAADHI YA ABIRIA KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI .
 KILA ASUBUHI PILIKA PILIKA ZA MAISHA HAZIKOSI KARIBU NA BANDARINI ZANZIBAR
 MUNGU ALIKUWA UPANDE WETU KWA KUTUWEZESHA KUSAFIRI SALAMA ZANZIBAR HADI MWANZA.
 MR,PETER NI MIONGONI MWA WAFANYAKAZI WA NDEGE YA PRECISION ANAYEJUA WAJIBU WAKE AWAPO KAZINI.
 MMOJA WA WASANII MAHIRI WA NGOMA AFYA THEATRE TROUPE WALIOBURUDISHA KWENYE MAONESHO YALIYOANDALIWA NA ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL (ZIFF)AMBAO WALIKUWA WAANDAAJI WA KOZI YETU KWA KUSHIRIKIANA NA TMF.
HAKUNA UCHAWI NI BURUDANI ZA ASILI HAPO

UTALII WA NDANI

 BIDHAA HIZO HUTENGENEZWA NA WAJASILIAMALI ZANZIBAR NI KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII WA NJE NA NDANI
 MCHEZO WA BAO NI MAARUFU SANA NASI HATUKUBAKI NYUMA KUSHIRIKI KUCHEZA
 FORODHANI NI ENEO MAARUFU KWA VYAKULA VYA KILA AINA JIONI,WATU WA MATAIFA MBALIMBALI HUJIPATIA VYAKULA .
MSAFARA WA RAIS WA ZANZIBAR UNAKUWA NA MAGARI MACHACHE SANA WAKATI ZIARA YA MKUU WA MKOA KWA TANZANIA BARA HUSHEHENI MAGARI MENGI BILA SABABU ZA MSINGI,KUNA MAMBO YA KUJIFUNZA HAPA.

HABARI ZANZIBAR



HABARI ZANZIBAR

BAADHI YA WAANDISHI WAHABARI WAKIFUATILIA MADA KUTOKAKWA MWEZESHAJI HAMZA KASONGO
ZANZIBAR BEACH RESORT NI ENEO ZURI KWA UTALII

PILIKAPILIKA ZA ZANZIBAR

 KITUO KIKUBWA CHA MAGAZETI MJINI ZANZIBAR KIKO OLD DISPENSARY WAUZAJI HUPATA MGAO ,
 HAPA TUKIWEKA AFYA VEMA ZANZIBAR BEACH RESORT

PILIKAPILIKA ZA BANDARINI ZANZIBAR

MATUKIO MBALIMBALI ZANZIBAR

 WAANDISHI WA HABARI WANAOHUDHURIA MAFUNZO YA CRITICAL JOURNALISM YALIYOANDALIWA NA ZIFF /TMF WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUFUNZI  OLD DISPENDANSARY ZANZIBAR
 PICHA YA PAMOJA
 FORODHANI ENEO MAARUFU KWA ZANZIBAR HAPO WATU WA NATAIFA MBALIMBALI HUKUSANYIKA JIONI KWA AJILI YA KUPATA CHAKULA CHA KILA AINA ,PANAPENDEZA
 DANNY SCHECHTER EDITOR IN CHIEF,MEDIA CHANNEL.ORG,NEWS DISSECTOR'BLOG; KUTOKA USA AKITOA MADA KWA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR
 TAMASHA LA ZIFF AWARDS NIGHT NGOME KONGWE