Dawa ya
sangoma yawageukia wanafamilia, wapata kichaa
Kwa ufupi
- Filamu
hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume (Omwando) wanaoishi Kenya,
kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia ndugu yao.
Mwalimu aliyetumia uchawi kuwaroga wezi, amejikuta
akiwaroga shemeji zake waliopata uchizi
Butiama. Ilikuwa kama simulizi ya kwenye filamu, baada ya
mganga wa kienyeji aliyeletwa toka Kenya kuja kuwaroga wezi walioiba nyumbani
kwa Mwalimu mstaafu, Raphael Omwando (60), baada ya dawa yake kuwatia uchizi
ndugu wa mke mkubwa wa aliyeibiwa.
Mwalimu Omwando ambaye ana wake wawili alivamiwa na
wezi waliomwibia pikipiki na mali nyingine, ikiwemo kumjeruhi yeye (Omwando) na
mkewe mkubwa. Mke mdogo aliyemuoa hivi karibuni anaishi kwenye nyumba nyingine
na hakuweza kuvamiwa na wezi hao, lakini mke mkubwa alipigwa hadi kulazimika
kupewa matibabu hospitali.
Watu walio karibu na familia hiyo walisema
kutokuelewana kati ya mke mkubwa na mdogo, kulimfanya mke mkubwa aliyejeruhiwa
na majambazi kumtuhumu mke mdogo kwamba alishirikiana na majambazi hao.
Filamu hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume
(Omwando) wanaoishi Kenya, kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia
ndugu yao.
“Sijui nimefikaje hapa hospitali…maana kumbukumbu
zinaishia pale nilipolazimishwa kunywa dawa na mganga wa kienyeji (Sangoma)
anayedaiwa kutokea nchini Kenya …ili wezi wa pikipiki na vifaa vya mwalimu
mstaafu virudishwe,” hiyo ni kauli ya mmoja kati ya watu wanne waliolazwa
hospitali kwa madai ya kurukwa na akili.
Boniphace Joseph (20)huku akisitasita, anasema
ana habari kabla ya kunywa dawa lakini baada ya kunywa hakumbuki kilichoendelea
mpaka alipopata fahamu na kuona watu wanamshangaa naye akiwashangaa.
Msira Magesa (17) anasema yeye baada ya kunywa
alitoka kwenda kwenye shughuli zake, ghafla akazidiwa na kupewa dawa ya
kutuliza maumivu aina ya panadol hali ikazidi kuwa mbaya na kufikishwa
hospitali kwa matibabu
Hali ilivyokuwa
Julai 5, majira ya saa 5:15 usiku mwaka huu,
Mwalimu mstaafu, Raphael Omwando (60) alivamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa
majambazi, wakamkata yeye, mkewe akapigwa na majambazi hao na baada ya kipigo
waliiba pikipiki, mabegi ya nguo, sola, sanduku dogo la kuhifadhia nyaraka,
simu ya mkononi na vitu vingine.
Omwando kutokana na majeraha aliyoyapata
akapelekwa hospitali ya mkoa alikolazwa kwa matibabu, lakini ndugu zake
wanaoishi Shirati na wale wanaoishi nchini Kenya baada ya kupata taarifa
waliamua kuchukua mganga wa kienyeji kutoka Kenya, ambaye aliwahakikishia kuwa
wahusika baada ya saa 3 watarudisha vitu walivyoviiba wakiwa wamejitwisha na
pikipiki wakiwa wanaisukuma.
Mganga huyo alieleza dalili za awali
zitakazowapata wezi hao kuwa ni kuchanganyikiwa, wengine watakuwa wanakula
nyasi kama ng’ombe. Mganga huyo alitoa tangazo kwamba Julai 9 majira ya
saa 9:00 alasiri wanakijiji wote wajitokeze kunywa dawa hiyo ili kuwapata
wahusika.
Vituko vyao walikojoleana, kutapikiana
Mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo ambaye
hakutaka jina lake litajwe anasema, walipofikishwa hapo aliogopa,“ walikuwa
wanakojoleana midomoni, wanatapikiana, huku wakiongea lugha za ajabuajabu,
tuliogopa maana ni tukio la kwanza kutokea,” anasema.
Anasema walipewa dawa za kuwafanya walale lakini
wakaonekana wanaendelea kuongea wengine kukimbia huku wakidai kuna watu
wanataka kuwaua, lakini sasa wametulia wanaongea wenyewe.
Shuhuda mwingine Isa Magesa anayemuuguza ndugu
yake anasema Matiko, mmoja wa waathirika hao alikuwa akikimbia kasi kwenda nje
huku akipiga kelele, “Nililazimika kutoa msaada, nilipomkamata alionekana ana
nguvu sana huku akisema…acheni kuniua…hao wanakuja kuniua…nisaidie …wabaya hao,
huku akionyesha kwa vidole lakini wao hawawaoni,” anasema.
Mganga Mfawidhi.
Dk Iragi Ngerageza, Mganga Mfawidhi Hospitali ya
Mkoa, anasema vijana hao walifikishwa hapo wakiwa hawajitambui huku ikidaiwa
kuwa walipewadawa na mganga wa kienyeji na kuwapokea wakiwa na hali mbaya
na kuwa hali hiyo bado wanaendelea kuichunguza.
“Inakuwa vigumu kujua madhara ya hiyo dawa, kama
tungeweza kuipata na kupeleka kwa mkemia ingetoa majibu, lakini kwa sasa sisi
tunaendeleakuwatibu…lakini ni hatari maana kama walikunywa wakafikia hatua hiyo
lazima kuna kitu, ikipatikana itatusaidia,” anasema.
Mke wake akamatwa.
Pilly Esther mke mdogo wa Mwalimu Omwando
amekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo, kusaidia kumpata mganga
aliyehusika na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Butiama.
Hata hivyo akizungumzia tukio hilo anasema,
wakati mume wake anavamia yeye alikuwa kwake na alisikia kelele za mbwa, lakini
hakuelewa kilichotokea mwishoni akapigiwa simu na mke mkubwa kuwa wamevamiwa na
kuumizwa. “Ndugu wa mume wangu akiwemo mke mkubwa ambaye ni Mjaluo wa kwao
walinituhumu mimi kuwa ndugu zangu ndiyo wameiba mali kwa kuwanimeolewa hivi karibuni..au
mpenzi wangu wa zamani ndiye amehusika, nilipokataa wakasema wanakuja na mganga
kutoka Kenya ambayeanatoa majibu haraka,” anasema.
Anasema mganga aliomba mtendaji kualika wananchi
wote lakini akakataa wakafika kama 40 wakiwemo kinamama, lakini kabla ya kutoa
dawa akawaanasema wahusika ni kama anawaona hapo anawaomba wasinywe dawa,
ajabuwaliopata madhara ni ndugu wa mke mkubwa.
Wagonjwa hao ni vijana wanne wa Kijiji cha
Kirumi Kata ya Bukanga, Tarafa ya Makongoro, Wilaya ya Butiama, mkoani
Mara waliolazwa hospitali ya Mkoa wa Mara baada ya kunywa dawa hiyo na kupoteza
fahamu huku wakionekana kama mazuzu (Mazombi).
Waathirika
Matiko Joseph (25) anasema yeye alilazimishwa
kunywa dawa nyingi pamoja na makapi yake,” …Baada ya kumtajia mganga hivyo
akasema ninyi kunyweni nyingi…dawa ilikuwa na ukakasi ilinikereketa sana. Baada
ya kunywa niliondoka lakini baadaye hali ikabadilika sana,” anasema na
kuongeza,
“Nilishtukia niko hospitali tayari ikiwa ni siku ya
pili …Nikisimuliwa ilivyokuwa nazidi kushangaa…huyo mganga alilenga kutuua
kabisa….maana wakati anatoa dawa alisema atakayepata madhara hatapona hata
akipelekwa wapi mpaka vitu virudi ama fedha…akaondoka kwenda Kenya na hakuacha
simu wala jina lake kujulikana,” anasema Joseph huku akipumua kwa harakaharaka.
Tura Joseph (30) anasema wengine walikunywa kidogo
lakini wao wana ndugu walilazimishwa kunywa zaidi kwa kile kinachodaiwa kuwa
walihisiwa kula njama za kumdhuru shemeji yao, na ndiyo walidhurika zaidi.
Anasema baada ya kunywa alihisi kitu kinamkaba
shingoni na kuishiwa nguvu, akawa hoi na kuanza kuongea maneno yaliyowatia
shaka, ndugu wakawabeba kwa bajaji hadi hospitali.
“Inakuwa vigumu kujua madhara ya hiyo dawa, kama
tungeweza kuipata na kupeleka kwa mkemia ingetoa majibu, lakini kwa sasa sisi
tunaendeleakuwatibu…lakini ni hatari maana kama walikunywa wakafikia hatua hiyo
lazima kuna kitu, ikipatikana itatusaidia,” anasema.
Mke wake akamatwa.
Pilly Esther mke mdogo wa Mwalimu Omwando
amekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo, kusaidia kumpata mganga
aliyehusika na anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Butiama.
Hata hivyo akizungumzia tukio hilo anasema,
wakati mume wake anavamia yeye alikuwa kwake na alisikia kelele za mbwa, lakini
hakuelewa kilichotokea mwishoni akapigiwa simu na mke mkubwa kuwa wamevamiwa na
kuumizwa. “Ndugu wa mume wangu akiwemo mke mkubwa ambaye ni Mjaluo wa kwao
walinituhumu mimi kuwa ndugu zangu ndiyo wameiba mali kwa kuwanimeolewa hivi
karibuni..au mpenzi wangu wa zamani ndiye amehusika, nilipokataa wakasema
wanakuja na mganga kutoka Kenya ambayeanatoa majibu haraka,” anasema.
Anasema mganga aliomba mtendaji kualika wananchi
wote lakini akakataa wakafika kama 40 wakiwemo kinamama, lakini kabla ya kutoa
dawa akawaanasema wahusika ni kama anawaona hapo anawaomba wasinywe dawa,
ajabuwaliopata madhara ni ndugu wa mke mkubwa.
MUUGUZI AKICHUKUA VIPIMO KUBAINI CHANZO CHA UGONJWA WA WAKAZI HAO.