MAUAJI
Mnamo tarehe 01.12.2012 majira ya saa 00.30 hrs huko Kampuni ya
Nyanza road katika kijiji cha Nyatwali kata ya kunzugu, Tarafa ya Serengeti,
Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara Mtu mmoja aitwaye ROHITA GANTIRALALL umri 20yrs, msimamizi wa shamba, aliuwawa
kwa kupigwa risasi chini ya kidevu na majambazi ambao waliiba simu yake ya
mkononi aina ya NOKIA. Majambazi hao
waliokuwa takribani sita (6) kabla ya tukio hili walifyatua risasi hewani na
kuvunja mlango wa nyumba kwa kutumia jiwe kubwa maarufu kama “Fatuma”. Walimshambulia PATEL VISHAL VINUBHAI na kumjeruhi usoni, kichwani, na mkono wa kulia kwa
kutumia nondo kasha kumpora fedha taslimu Tshs. 500,000/= na US DOLLAR 600
pamoja na simu mbili, JAGINAL NARAM Umri 23yrs, msimamizi wa shamba alijeruhiwa kichwani, usoni kwa kutumia
npondo na kuporwa simu – Sum sung, VINUDI RAMJI Umri 45yrs, msimamizi wa shamba alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na
kuporwa simu moja aina ya NOKIA. PATEL
VISHAL VINUBAL alilazimishwa
atoe fedha za mishahara nae kwa kujitetea aliwaeleza fedha ziko ofisini ambako
ni kilometa moja toka wanapoishi. Wakiwa njiani kuelekea kwenye ofisi hiyo
waliona Askari Polisi, wakamwachia na kutokomea gizani. Uchunguzi na
ufuatiliaji wa kina umeanza kufanyika. Wito yeyote anayekusudia kusafirisha
fedha kiwango kikubwa aombe ulinzi wa Polisi wenye silaha.
ABSALOM A. MWAKYOMA – S.A.C.P
KAMANDA
WA POLISI ‘M’ MARA, MUSOMA
0 comments:
Post a Comment