Subscribe:

Ads 468x60px

askari Senapa waua jangili na kukamata bunduki smg AK47 risasi 258


ASKARI SENAPA WAUA JANGILI,WAKAMATA BUNDUKI SMG AK 47 ,RISASI 258.
Na Mwandishi wetu-Serengeti.
Novemba 30,2012.

ASKARI wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti wamefanikiwa kumuua mtuhumiwa mmoja wa ujangili ,kukamata silaha ya kivita aina ya Smg AK 47,risasi258 , meno mawili ya tembo na msumeno wa kukatia meno ya tembo na shoka.

Tukio limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma linadaiwa kutokea novemba 29,majira ya saa 12;30 jioni katika eneo la Itaro ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,eneo ambalo kumewekwa Faru waliotolewa Afrika Kusini,maarufu kama Faru wa JK.

Alisema aliyeuawa hajafamika ingawa anakisiwa kuwa na umri kati ya miaka 27,33 na kuwa katika majibizano hayo alipigwa risasi mguu wa kulia iliyopelekea kufa na wenzake wanakisiwa kuwa wanne kukimbia ,na hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo.

Habari za uhakika kutoka eneo la tukio zinadai kuwa askari wa hifadhi hiyo wakiwa doria walisikia milio ya bunduki na kufuatilia walikuta kundi kubwa la majangili wanaokadiriwa kufikia watano  wakiwa na silaha za kivita wameishaua tembo mmoja na wametoa meno.

“Walianza kutushambulia kwa risasi,kukatokea majibizano makali yaliyochukua muda ambayo yanaonyesha kuwa walikuwa na risasi za kutosha kwa kuwa walikuwa na silaha za kivita,mmoja akawa amepigwa risasi na kuanguka …wenzake walipoona hivyo wakakimbia mmoja akiwa na bunduki,”kulisema chanzo kimoja cha uhakika.


“Maiti hiyo imehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali teule ya Nyerere ddh,haijatambuliwa ,inaonekana si mtu wa maeneo haya hali ambayo inaonyesha ukubwa wa mtandao huo kutoka mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na wenyeji wa maeneo,kasi yao kuingia inakwenda sambamba na uingizaji silaha kutoka mikoa iliyoko pembezoni mwa mipaka ya nchi jilani”kilisema chanzo hicho.

Mganga mkuu wa Hospitali hiyo dk,Kelvin Mwasha amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa marehemu huyo”amefikishwa hapa usiku wa manane na ameletwa na askari polisi…hawajaja polisi kwa ajili ya uchunguzi,tunawasubiri maana hatuwezi kusema kilichosababisha kifo bila kufanya uchunguzi”alisema daktari.

Mtandao wa ujangili ambao umesambaa hifadhi za taifa ,mapori ya akiba na maeneo ya wazi unadaiwa kufadhiliwa na wafanya biashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi ambao wanahusishwa kuwa na ushirikiano wa karibu na baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi,mahakama,maliasili ,uhamiaji na ofisi za wanasheria wa serikali na Tra.

Uhusiano huo huwawezesha kusafirisha shehena za meno ya tembo kwa kupita mipakani,bandarini,na kupeleka nje ya nchi,kasi hiyo ikienda sambamba na uingizaji wa silaha za kivita kwa ajili ya kazi hiyo.

Wakati huo huo mtu mmoja ambaye hajatambuliwa aliuawa na wananchi baada ya kukutwa akiiba mabati kwenye jengo la mtu aliyejulikana kwa jina Jumanne Kagosi katika kijiji cha Kwangwa kata ya Kigera Manispaa ya Musoma.

Kamanda Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea novemba 29,majira ya saa 10 jioni mwaka huu na kuwa wananchi waliamua kuchukua sheria mkononi na kumpiga hadi kufa ,na kuomba wananchi wasijichukulie sheria mkononi badala yake wafikishwe kwenye vyombo husika.

Mwisho.


0 comments:

Post a Comment