MKUU WA SHULE,OFISA
ELIMU WATUHUMIWA KUCHOTA FEDHA ZA NYUMBA YA MWALIMU.
MEI 1,2013.
Serengeti.
WAKATI taifa likiwa kwenye kihoro cha matokeo mabaya ya
kidato cha nne,mkuu wa sekondari ya Nyambureti kwa kushirikiana na ofisa elimu sekondari
wilayani Serengeti wanatuhumiwa kula sh,mil.9 za ujenzi wa nyumba ya Mwalimu.
Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya
Mwalimu toka akaunti ya Maendeleo ya halmashauri hiyo,ikiwa ni kuchangia nguvu
za wananchi kwa ujenzi wa nyumba ya Mwalimu.
Ubadhirifu huo unadaiwa kumhusisha mkuu wa shule hiyo Patrick Majige kwa kushirikiana na ofisa elimu
sekondari William Makunja na kupelekea nyumba hiyo kutokujengwa.
Blogu hii ilibaini kuwa fedha hizo zilitolewa mwaka 2010 na
kuwekwa akaunti ya shule benki ya NMB tawi la Mugumu wilayani hapa,hazikufanya
kazi kusudiwa badala yake zilitumika kulipana
posho za safari zisizo na na wito
kwa idhini ya ofisa elimu sekondari.
Kwa mjibu wa uchunguzi wa blogu ulibaini tarehe 1,1,2011 akaunti hiyo ilikuwa
na kiasi cha sh,10,489,660= baada ya kupokea sh.mil.9 fedha za mradi na sasa
benki hakuna fedha na nyumba haijajengwa.
Blogu hii imeona ripoti ya mkaguzi wa ndani ya halmashauri hiyo
ikionyesha kwa kipindi cha januari 1/2011 hadi desemba 31.2012 posho za safari
zilikuwa zimegharimu sh.7,703,400=.
Safari zote zikiwemo za kuitwa wilayani ambazo ziligharimu
sh.1,254,000 hazikuwa na viambatanisho vya barua za wito zote
zikiidhinishwa na ofisa elimu sekondari ambaye pia hukaimu nafasi ya Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri mara kwa mara.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa fedha hizo zimetumika kinyume
cha lengo kusudiwa la ujenzi wa nyumba bila kufuata sheria,kanuni na taratibu
za kubadili matumizi ya fedha ya miradi husika.
Katika hitimisho la mkaguzi amebainisha kuwa mkuu wa shule
hiyo Majige anawajibika kwa kubadilisha matumizi ya fedha sh,mil.9 za ujenzi wa
nyumba ,malipo ambayo yameidhinishwa na wakuu wake wa idara wakijua fedha hizo
si za utawala.
Kuchulikuwa kwa fedha hizo kunakwamisha juhudi za wananchi
waliokuwa wameandaa viashiria kama mawe,mchanga na saruji mifuko 48 toka mwaka 2011ambayo iko hatarini kuharibika
kutokana na kukaa muda mrefu.
Ofisa elimu.
Ofisaelimu shule za sekondari William Makunja ambaye hukaimu
nafasi ya Mkurugenzi Mara kwa mara alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusiana na
tuhuma hizo kwanza alisita kisha akasema”shule gani hiyo Nyambureti…nilikuwa
sijui nitafuatilia ili kujua kama nyumba haijajengwa”alisema.
Alipotakiwa kufafanua kama ameishampitishia fedha mkuu wa shule na kwa kazi zipi ,hakukubali wala kukataa,bali
alibaki kushangaa kuhusu mwandishi kupata taarifa hizo.
Mkuu wa sekondari.
Majige ambaye ni mtuhumiwa wa ufujaji huo alipotafutwa kwa
simu yake ya mkononi na kuulizwa atoe
ufafanuzi kuhusiana na tuhuma hizo
akasema”nipo hapa Mugumu..ulikuwa unataka kujua suala la nyumba ya
Mwalimu…niko Mwanza ,unataka kujua fedha za nyumba….mimi nasema,aaah….sihusiki”alisema
kwa kusitasita.
“Haya mambo tunatakiwa tuonane ili tuongee vizuri….maana haya
mambo si mazuri …umepata wapi hizo habari zote….mimi sihusiki wala
sijui….lakini ninge…”akakata simu bila kumalizia sentensi yake.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Good Pamba
hakupatikana ofisi kwa kile kilichodaiwa kuwa yuko Musoma kikazi,hata hivyo
anadaiwa kutokuchukua hatua licha ya kukabidhiwa taarifa ya ukaguzi.
Diwani.
Nicholaus Maro diwani wa kata hiyo anasema kutokana na
ukosefu wa nyumba za walimu amepokea walimu wawili waliopangia hapo wanaishi kwake,huku
akisisitiza kuwa tatizo hilo linapelekea walimu kuikimbia shule hiyo.
“Kama fedha zinaletwa za kujenga nyumba ya mwalimu ,mkuu
anashilikiana na afisa wake wanakula fedha hizo,mamlaka ziko kimya ….hii
inakatisha tamaa ,na wanaoathirika ni watoto wetu kitaaluma …hili
hatutalinyamazia”amedai.
Mwisho.