WAKAMATWA NA SMG,RISASI 96 NYARA IKIWEMO MAYAI YA MBUNI,
Na Anthony
Mayunga-serengeti
Oktoba 29,2012.
WATU watatu wakazi wa
kitongoji cha Mageriga kijiji cha Motukeri kata ya Natta wilayani Serengeti
wamekamatwa na bunduki ya kivita aina ya Smg ,risasi 96,vipande 10 vya nyara za nyama pori na mayai 4 ya mbuni.
Tukio limetokea ikiwa ni siku chache katika kijiji cha
Makundusi kata hiyo tembo watatu walidaiwa kuuawa kwa njia ya sumu na meno yake
kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na watuhumiwa walikamatwa kwa kati ya
oktoba 25 na 26 katika maeneo tofauti ya wilaya za Serengeti na Bunda.
Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa za wananchi polisi na
Tanapa ambao baada ya kukithiri matukio ya ujangili wanahaha kila kona
kuhakikisha mtandao huo unadhibitiwa kabla ya kuleta madhara makubwa.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Sabasaba Nyagekubwa (31)aliyekutwa na silaha
na risasi hizo zikiwa chini ya godoro wamelalia na kuwataja wenzake ambao ni Pius Mayengo mkazi wa
Kyandege wilayani Bunda na Timoth mkazi
wa Kisii Kenya.
Mkisii huyo alidai kuwa yeye alifika kwa mtuhumiwa huyo
kutoa mahari baada ya kumtorosha binti wa mtuhumiwa e ,madai ambayo yanapingwa
na baadhi ya majilani kwa madai kuwa huo ni mtandao wao wa kuvusha nyara kwenda nchini Kenya .
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinadai kuwa
Nyagekubwa alikamatwa oktoba 25 majira ya saa 11 alfajiri akiwa kwa hawala yake
na kuwampeleka nyumbani walipokuta silaha na risasi zikiwa zimefungwa kwenye
mfuko.
Bunduki hiyo aina ya SMG inadaiwa ni ya kisasa kwa kuwa ina stendi za kusimamisha wakati wa
kutenda uharifu,inadaiwa kuingizwa nchini kutokea nchi za Rwanda na Burundi kupitia
Kigoma na mtu mmoja ambaye inadaiwa aliingia kijijini hapo akijifanya mganga wa
kienyeji(Sangoma)
Sangoma huyo ambaye jina lake limehifadhiwa anasakwa alitajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye
aliyeingiza silaha na risasi kwa lengo la kuwindia tembo na uhalifu mwingine na
kuwa hata soko la nyara ndiye anajua.
Watuhumiwa walikutwa harusini .
Kwa mjibu wa habari hizo inasemekana watuhumiwa wengine
walifanikiwa kutoroka baada ya kukutwa kwenye harusi na polisi katika kudhibiti
watu wote watuhumiwa wakafanikiwa kutoroka .
Wengine walitaarifiwa
kwa simu na kutoroka na nyara.
Habari hizo zinasema kuwa
watuhumiwa wengine walitaarifiwa na hawala wa Nyagekubwa kwa njia ya simu baada ya polisi kuchukua simu
ya mtuhumiwa na wengine huku moja ikifichwa ndiyo ilisaidia watuhumiwa kutoroka
na nyara walizokuwa nazo.
Mtuhumiwa anakesi
mbili za nyara kwa majina tofauti.
Imebaini kuwa mtuhumiwa Nyangekubwa anakabiliwa na kesi
mbili za kukutwa na nyara kwa majina tofauti na moja akidaiwa kuruka dhamana na
alipokamatwa kwa tukio kama hilo aliandika jina lake halisi.
Kesi ya kwanza aliandika jina la Ndalahwa Makaranga tukio la mwaka 2010 ambalo aliruka dhamana.
Silaha za kivita
huingizwa kutokea Kigoma.
Matukio ya watu kuingiza silaha kutokea mkoani Kigoma
yanazidi kushika kasi kwa ajili ya uwindaji wa tembo na uhalifu
mwingine,ikiwemo mtandao uliowahi kutikisa bunge lililopita kwa kuwataja
watuhumiwa ambao walipewa dhamana kinyamera licha ya kukamatwa na Smg 4 na
risasi zaidi ya 460.
Watuhumiwa walifutiwa
kesi.
Hata hivyo wale watuhumiwa waliokamatwa na shehena ya silaha
hizo na kelele kusambaa hadi bungeni walifutiwa mashitaka kinyamera katika
mazingira ambayo inadaiwa kutawaliwa na rushwa kwamba hawana mashitaka ya
kujibu.
Kuachiwa kwao kuliibua maswali mengi kutoka Tanapa kwa kuwa
wanakamata watuhumiwa na vielelezo
ikiwemo bunduki za kivita lakini polisi huwaachia linadaiwa kusimamiwa na
aliyekuwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Serengeti,ambaye kutokana na kashifa hiyo
ameshushwa cheo na kupelekwa ofisi ya kamanda wa upelelezi mkoa wa kipolisi
Tarime na Rorya.
Hata hivyo baada ya kubainika waliachiwa kwa mazingira ya
rushwa watuhumiwa baadhi walikamatwa tena kwa maelekezo ya ngazi za juu za
jeshi la polisi na wako chini ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara huku
wakiendelea kuwasaka wengine.
Mwisho,itaendelea.
0 comments:
Post a Comment