Subscribe:

Ads 468x60px

Journalists' tax administration training to increase public call for accountability




By Prosper Makene
8th May 2014


Tax administration training is been offered to more than 400 journalists from across the country and is expected to build their capacity to monitor good governance aspects in the sector, encourage compliance, conduct investigative stories and expose tax evaders.

The resulting detailed reporting is expected to give the public better understanding of the sector allowing them to call for accountability of collected funds because it is their money, the facilitators say.

The training is organised by the Tanzania Tax Writers’ Network (Tawnet) and is meant to ensure reporters have the required knowledge to cover the subject.

Making the announcement at the start of the week in Dar es Salaam during the opening of the two-day Tax Administration Training session, Tawnet Managing Director Judica Tarimo said the plan will empower reporters to cover the subject much more comprehensively.

Tarimo said the training will also result in a network of competent reporters noting that: “The network is an important step in the country’s strategies to improve tax reportage.”

“The network will provide for vibrant and extensive reporting on tax issues and will enable the trained reporters to collect and disseminate (through their media outlets) information of public interest on tax issues,” he went on to explain.

Finance Deputy Minister Adam Malima, who graced the two-day training, told participants that training members of the media will increase awareness of tax issues in the community.

“Mass media is a key coordinator between the two sides…tax education for the community is very much needed because paying tax is not a matter of how well one is doing financially but an obligation,” Malima said.

However he expressed disappointment over what he termed as ‘media’s failure to report losses’ that resulted from recent slow downs and closure of shops as traders contested the use of Electronic Fiscal Devices (EFDs).

“The closure of shops has a lot of impact on the national economy, but most of the reporting was based on supporting the move and ignored the impact on the economy,” he lamented.

“Education imparted on the media should continue in a way that explains how the country can get out of dependence on donors and emphasize on government operations to be financed by taxes collected from the public,” he said.

Detailing on the training, Tawnet Managing Director Tarimo said the trained reporters will now be equipped to pursue investigative stories on tax and that way, encourage tax compliance.

According to him, through the resulting educative stories and by also recognising the ‘best taxpayers’ then others will be encouraged to emulate.  
SOURCE: THE GUARDIAN
More News
 

Kila Mtanzania ana deni la Sh. 470,000





Ni mgawanyo wa deni la taifa la trilioni 21.2


Deni  la Taifa limeendelea kupaa na sasa limefikia Sh. trilioni 21.2 kiwango ambacho kama kikigawanywa kwa kila Mtanzania wanaofikia milioni 45 kwa sasa kwa usawa, kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111.

Kiwango hicho cha deni kimepanda kutoka Sh. trilioni 16.98 cha mwaka wa fedha 2011/12.

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, aliweka hadharani deni hilo jana wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini hapa juu ya ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2012/13 ambayo inaishia Juni 30, mwaka jana. Ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni.

Utouh alisema ongezeko hilo limesababishwa na mikopo kutoka kwenye mabenki na nchi wafadhili kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo.

Utouh alisema deni la nje limefikia Sh. trilioni 15 hadi Juni 30, 2013  ambalo ni ongezeko la Sh. trilioni 3.0 kutoka Sh. trilioni 12.43 kwa mwaka 2011/12, wakati lile la ndani limefikia Sh. trilioni 5.78 ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 1.23 kutoka Sh. trilioni 4.55 kwa mwaka 2011/12.

 “Ni maoni yangu kwamba, pamoja na deni la Taifa kuongezeka, uchumi wa nchi nao umekuwa ukiimarika kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Utouh.

MISAMAHA YA KODI
Akizungumzia misamaha ya kodi, CAG alisema ukaguzi huo umebaini kuwa hadi kufikia Juni 30, mwaka jana Sh. trilioni 1.52 zilitolewa kama misamaha ya kodi.

 Alisema mwenendo umeonyesha kuwa kiasi hicho kimepungua kutoka Sh. trilioni 1.81 mwaka 2011/12 hadi Sh. trilioni 1.52 mwaka 2012/13 ambao ni upungufu wa Sh. bilioni 290.60 (asilimia 16).

 “Hivyo naipongeza serikali kwa hatua walizochukuwa kupunguza misamaha ya kodi kwa kiasi hicho ikilinganishwa na bajeti nzima ya serikali kwa mwaka 2012/13, misamaha ya kodi ambayo ilifikia asilimia 10 ya bajeti yote,” alisema.  Alishauri serikali izidi kupunguza kasi ya misamaha ya kodi ili fedha hizo zibakie serikalini na kufanya shughuli za maendeleo.

MWENYEKITI PAC
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alipongeza ukaguzi huo kubaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kunusuru fedha za walipakodi.

Alisema ripoti hiyo itaanza kufanyiwa kazi kuanzia sasa hadi Novemba ili kutoa maelekezo kwa hatua mbalimbali ambazo serikali itapashwa kuzichukua.Akizungumzia misamaha ya kodi, Zitto, alisema pamoja na kupunguza kiasi hicho hadi kufikia asilimia tatu ya pato la taifa, lakini bado ni kikubwa na kushauri ifikie asilimia moja ya pato la taifa.

Alisema wanakusudia kuwasilisha muswada wa mfumo mpya wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) wenye lengo la kudhibiti misamaha ya kodi, ambao alisema unapigwa vita na baadhi ya wabunge na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa madini.

 HATI CHAFU
Utouh alisema serikali imetoa hati za ukaguzi 961 kati ya hizo, 131 zimetiliwa shaka wakati nane zikiwa haziridhishi na mbaya zikiwa sita.

Alisema ukaguzi huo ulifanywa kwa halmashauri 140, wizara na idara na taasisi za serikali 117, mashirika na taasisi za umma 93, miradi ya wafadhili 611 na kubaini kasoro hizo.

Alisema pamoja na kuwapo kwa hati hizo chafu na zisizoridhisha, mwelekeo wa hati za ukaguzi kwa ujumla unaonyesha kuimarika kwa utendaji wa serikali katika kusimamia makusanyo ya mapato na matumizi ya rasilimali za umma ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alisema katika wizara na Idara za Serikali zilikuwa 117 na kuwa walibaini hati 85 zinaridhisha, hati 30 zenye mashaka, hati isiyoridhisha ilikuwa moja na hati mbaya moja.

Kwa upande wa halmashauri, alisema zilikaguliwa 140 na kubaini hati zinazoridhisha 112, zenye mashaka 27, isiyoridhisha bila kuwapo mbaya wakati. Kwenye mashirika ya umma taasisi zilizokaguliwa zilikuwa 93 hati zinazoridhisha zilikuwa 92, yenye shaka moja, hakukuwa na hati siyoridhisha wala mbaya.

 Katika miradi ya wafadhili iliyokaguliwa ni 611 na kupata hati zinazoridhisha 527, zenye shaka 73, zisizoridhisha sita na mbaya tano.

 Alisema hati zenye shaka kwa upande wa serikali kuu zimeongezeka kutoka tano mwaka 2011/12 hadi kufikia 30 mwaka 2012/13 kiliwango ambacho kimeongezeka mara tano.
 

JK: Mishahara itapanda na itapunguzwa kodi




Rais Jakaya Kikwete akiangua kicheko wakati walimu (juu), walipokuwa wakipita kwa maandamano, huku wakiimba ‘Shemeji mshahara bado’ wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. Walimu walimwita shemeji kwa kuwa mkewe, Salma ni mwalimu kitaaluma. Picha na Silvan Kiwale 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Mei2  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Tofauti na wafanyakazi wengine ambao walipita mbele ya mgeni rasmi bila kusimama, walimu walisimama kwa dakika moja kuhakikisha ujumbe huo unamfikia.
Dar/mikoani. Rais Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.
Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.
“Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo,” alisema.
Huku akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais Kikwete alisema: “Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo.”
“Kwa nyongeza iliyofanywa mwaka jana, hivi sasa Serikali inatumia asilimia 44.9 ya Bajeti kulipa mishahara ambayo ni asilimia 10 ya Pato la Taifa.”
Akifafanua namna Serikali ilivyofikia uamuzi wa kuongeza mishahara kwa mwaka huu, Rais Kikwete alisema kulikuwa na mjadala mkali baina ya wafadhili waliodai nyongeza ni kubwa mno.
“Ni kweli mapato yetu ni madogo lakini kwa kuwa mishahara ni midogo, lazima tuendelee kuongeza, hata hicho kidogo lazima ukitoe ili uijenge ile nafuu, alisema bila kutaja kiwango kitakachoongozwa.
“Hata sasa kumekuwa na ubishi mkali kati ya Wizara ya Utumishi na Hazina kuhusu nyongeza ya mwaka huu iwe mpaka kiasi gani, nikaingilia kati nikakubaliana na utumishi, Hazina walikuwa wanataka ipingue kidogo,” alisema.
Walimu na shemeji yao
Suala la mshahara lilijitokeza kwa namna nyingine kwenye maandamano ya wafanyakazi pale walimu walipoamua kusimama mbele ya jukwaa kuu na kumweleza Rais Kikwete ambaye walimtaja kama shemeji yao, kwamba hawajapata mshahara wa Aprili wakimtaka aingilie kati.
“Shemeji, shemeji, shemeji, hatujapata mishahara yetu ya Aprili, tunaomba utusaidie,” walitoa ujumbe huo kwa njia ya wimbo.
Tofauti na wafanyakazi wengine ambao walipita mbele ya mgeni rasmi bila kusimama, walimu walisimama kwa dakika moja kuhakikisha ujumbe huo unamfikia.
Wakati hayo yakitokea, Rais Kikwete na viongozi wengine walikuwa wakicheka huku wakiwaangalia walimu hao waliokuwa wakiendelea kuimba wimbo huo.
Ajira kwa wageni
Rais Kikwete aliagiza yafanyike marekebisho kwenye sheria ya vibali vya ajira ili kudhibiti ongezeko la wafanyakazi wa kigeni nchini ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.
Aliagiza hatua hiyo itekelezwe haraka hata ikibidi kwa kupeleka bungeni hati ya dharura ili kuhakikisha jambo hilo linaanza mara moja.
Malalamiko ya Tucta
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema pamoja na ongezeko la mishahara kufanyika kila mwaka, limekuwa dogo mno kiasi cha kushindwa kufikiwa kima cha chini ya mshahara kinachotakiwa.
Alisema kwa upande wa sekta binafsi, Serikali imeongeza mshahara kutoka Sh100,000 hadi Sh450,000 mwaka jana, huku sekta ya kilimo ikiwa ya mwisho kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi.
“Hali hii imesababisha kuwapo kwa upungufu mkubwa wa wafanyakazi mashambani na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao,” alisema na kuongeza:
“Tunapenda kuikumbusha Serikali kwamba kumlipa mfanyakazi mshahara unaokidhi mahitaji muhimu ya maisha siyo jambo la fadhila, bali ni mojawapo ya haki za msingi za binadamu zinazosisitizwa na jumuiya za kimataifa.”
Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Hafsa Mtassiwa alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi zikiwamo za kodi ya mishahara kuwa juu na kwamba inazifanyia kazi.
Mbeya
Mratibu wa maadhimisho hayo mkoani Mbeya, Joseph Sayo ameiomba Serikali iache kuwanyonya wafanyakazi na kuwa mwajiri msumbufu kuliko wengine nchini.
“Serikali inadaiwa na wafanyakazi fedha nyingi na pia inawakopa wafanyakazi kwa njia mbalimbali zikiwamo za kupitia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii na kushindwa kurudisha kwa wakati,” alisema.
Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewataka waajiri kufuata sheria na taratibu za kazi katika kuhakikisha kuwa wanawalipa wafanyakazi wao stahili zao ikiwamo nyongeza ya mishahara, kupandishwa vyeo na motisha kwa wanaostahili.
Geita
Wafanyakazi mkoani Geita, wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi mbalimbali ilizotoa kuboresha maisha yao, hivyo kulazimika kufanya kazi kwenye mazingira magumu.
Morogoro
Mratibu wa Tucta Mkoa wa Morogoro, Charles Luvunzu amesema rushwa na ukosefu wa uadilifu ni miongoni mwa mambo yanayokiukwa na waajiri wengi licha ya vyama vya wafanyakazi kuyapigia kelele.
Shinyanga
Tucta imewataka waajiri kuacha tabia ya kuwafukuza wafanyakazi kama kuku. Imeshauri wakae meza moja kujadiliana ili kutatua matatizo yanayowakabili sehemu za kazi.
ratibu wa Tucta Mwanza, Evarist Mwalongo ameutaka uongozi wa mkoa kuwachukulia hatua za kisheria waajiri wasiofuata sheria za kazi huku akiitaka Serikali kubadilisha sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ili itoe mafao mazuri kwa wastaafu na kiwango cha kodi kwenye mshahara kipungue hadi asilimia moja.
Mara
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Henjewelle amewaagiza waajiri kuwalipa wafanyakazi masilahi yao kwa wakati ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara kazini.
Imeandikwa na Goodluck Eliona, Raymond Kaminyoge, Aidan Mhando, Salum Maige, Happy Lazaro, Ernest Magashi, Dinna Maningo, Veronica Modest, Lilian Lucas, Stella Ibengwe, Lauden Mwambona na Salim Mohammed



 

JK aunda Tume kuchunguza Operesheni Tokomeza Ujangili



Rais Jakaya Kikwete 
Na Mwandishi Wetu Mwananchi

Posted  Mei3  2014  saa 9:40 AM
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi, kuhusu vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ilisema, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Vilevile, Rais Kikwete amewateua Jaji Mstaafu Stephen Ihema na Jaji Mstaafu Vincent Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Hatua ya Rais Kikwete kuunda tume hiyo inakuja baada ya Operesheni Tokomeza Ujangili kusitishwa na Bunge kutokana ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu wakati wa utekelezaji wake.
Operesheni hiyo iliayoanza Oktoba 2013 na kusitishwa Nobemba 4 mwaka jana, ndiyo iliyowang’oa mawaziri wanne kwa kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wake.
Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, na kutaja majukumu ya tume hiyo kuwa ni pamoja na kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.
Majukumu mengine ni kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza na kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.
Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.
Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.