Subscribe:

Ads 468x60px

UTOAJI ELIMU JUU YA RASIMU YA PILI WAFANYIKA SERENGETI

 KAZI YA UTOAJI ELIMU NA UGAWAJI WA MACHAPISHO ULIOFANYWA NA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU(LHRC)ULIANZA HIVI
 KAZI YA UGAWAJI WA MACHAPISHO KWA WAKAZI WA MJI WA MUGUMU WILAYA YA SERENGETI UNAENDELEA ,LENGO LIKIWA NI KUJENGA UELEWA WA RASIMU YA PILI NA KUFUATILIA MJADALA UNAOENDELEA ILI WAKATI WA MAAMZI WAJUE WANAPIGIA KURA MAMBO GANI.
 WATU WANAENDELEA KUSOMA MACHAPISHO ILI KUJENGA UELEWA
 MAMBO YANAENDELEA.
 WANANCHI WALIJITOKEZA KWA WINGI
MIJADALA YA WAO KWA WAO ILIENDELEA.

Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Chadema Serengeti

Viongozi wa chadema Serengeti baada ya uchaguzi
Safu ya viongozi wa Chadema wilaya ya Serengeti

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Serengeti
Pilika pilika zikiendelea ndani ya Ukumbi wa Anita Motel
Upigaji wa kura ukiendelea
Ulinzi wa kura uliimarishwa

UCHAGUZI CHADEMA WILAYA YA SERENGETI MKOAWA MARA


 BAADHI YA WAJUMBE WAKIWA WANAKAMILISHA TARATIBU ZA KUJAZA FOMU ZAO
 UJAZAJI FOMU UNAENDELEA

 HAPA WAJUMBE WANAINGIA UKUMBINI

 WAJUMBE WAKIWA WANAFUATILIA MAELEZO
NAMALIZA MUDA WANGU ,KAULI YA MWENYEKITI

Ojadact yamtaka Sitta kufuta kauli dhidi ya vyombo vya habari



Na Mwandishi wetu
10th August 2014
Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (Ojadact), kimemuonya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kumtaka kufuta kauli yake aliyotoa kutaka vyombo vya habari vidhibitiwe.

Akizungumza na wanahabari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa  chama hicho, Edwin Soko, alisema kauli hiyo ya Sitta inafananishwa na ‘mhalifu’ ambaye hana maumivu na watu wake.

“Haiwezekani amwagize waziri anayesimamia masuala ya habari avidhibiti vyombo vya habari, kuingiliwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya anapaswa alaumiwe yeye,” alisema Soko.

Soko alisema kauli hiyo ni ya uchochezi inayokwenda kinyume na Katiba ya nchi ya mwaka 1977 Ibara ya 18(1) inayotoa uhuru wa kutoa maoni, kutoa na kupokea habari, na jambo alilolifanya Sitta ni kinyume na kuvunja sheria za nchi.

Alisema katika mchakato wowote wa kutunga katiba, vyombo vya habari vinakuwa mstari wa mbele kuwapa nafasi wataalamu, wanasiasa na wananchi kujadili juu ya mchakato unavyokwenda na matarajio ya kupata katiba mpya, na hilo la Sitta linazalisha uhasama baina ya watawala na vyombo vya habari.

“Sitta hakuwa na sababu ya kuvishambulia vyombo vya habari na kutaka vidhibitiwe, hilo si jukumu lake bali msingi mkubwa ni kupata muafaka wa pande mbili zilizosigana kati ya Ukawa na wajumbe waliowengi wakiongozwa na wale wa CCM,” alisema.

Pia, alisema kauli hiyo ni ya kidikteta ambayo mizizi yake ni ukandamizaji wa haki ya wananchi katika kushiriki kutoa maoni yao kupitia mijadala na makongamano ambayo kimsingi wananchi wa kawaida wanapata nafasi ya kutoa maoni yao.

Alisema wanahabari wa mtandao huo wamesikitishwa na uelewa mdogo wa Mwenyekiti wa Bunge hilo juu ya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari na inaonyesha ukandamizwaji wa vyombo vya habari kupitia  sheria ya nchi kama sheria ya magazeti  ya 1976, sheria ya  usalama wa Taifa ya  1970, sheria  ya magereza ya 1967, ‘penal code’  ya 1945  na nyinginezo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI