Na Mwandishi wetu
10th August 2014
Chama cha Waandishi wa
Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania
(Ojadact), kimemuonya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta
kumtaka kufuta kauli yake aliyotoa kutaka vyombo vya habari vidhibitiwe.
Akizungumza na wanahabari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa chama hicho, Edwin Soko, alisema kauli hiyo ya Sitta inafananishwa na ‘mhalifu’ ambaye hana maumivu na watu wake.
“Haiwezekani amwagize waziri anayesimamia masuala ya habari avidhibiti vyombo vya habari, kuingiliwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya anapaswa alaumiwe yeye,” alisema Soko.
Soko alisema kauli hiyo ni ya uchochezi inayokwenda kinyume na Katiba ya nchi ya mwaka 1977 Ibara ya 18(1) inayotoa uhuru wa kutoa maoni, kutoa na kupokea habari, na jambo alilolifanya Sitta ni kinyume na kuvunja sheria za nchi.
Alisema katika mchakato wowote wa kutunga katiba, vyombo vya habari vinakuwa mstari wa mbele kuwapa nafasi wataalamu, wanasiasa na wananchi kujadili juu ya mchakato unavyokwenda na matarajio ya kupata katiba mpya, na hilo la Sitta linazalisha uhasama baina ya watawala na vyombo vya habari.
“Sitta hakuwa na sababu ya kuvishambulia vyombo vya habari na kutaka vidhibitiwe, hilo si jukumu lake bali msingi mkubwa ni kupata muafaka wa pande mbili zilizosigana kati ya Ukawa na wajumbe waliowengi wakiongozwa na wale wa CCM,” alisema.
Pia, alisema kauli hiyo ni ya kidikteta ambayo mizizi yake ni ukandamizaji wa haki ya wananchi katika kushiriki kutoa maoni yao kupitia mijadala na makongamano ambayo kimsingi wananchi wa kawaida wanapata nafasi ya kutoa maoni yao.
Alisema wanahabari wa mtandao huo wamesikitishwa na uelewa mdogo wa Mwenyekiti wa Bunge hilo juu ya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata habari na inaonyesha ukandamizwaji wa vyombo vya habari kupitia sheria ya nchi kama sheria ya magazeti ya 1976, sheria ya usalama wa Taifa ya 1970, sheria ya magereza ya 1967, ‘penal code’ ya 1945 na nyinginezo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment