Wananchi hawakuwa nyuma kufuatilia kikao hicho.
Wanafuatilia mjadala
Wageni mbalimbali walikuwepo
Ng;oina akifungua kikao hicho cha mwisho.
KIKAO CHA KUVUNJA
BARAZA LA MADIWANI CHATAWALIWA NA VITUKO,
Serengeti:Kikao cha
kuvunja baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara
kimetawaliwa na vituko,ikiwemo madiwani kugoma kuingia ukumbini mpaka wajue
hatima ya mafao yao,na Mwenyekiti kulia wakati akitoa hotuba ya mwisho.
Mgomo wa madiwani
kuingia ukumbi wa halmashauri hiyo juzi ulianza saa 4 asubuhi hadi 6:15 mchana ,huku watumishi,wageni
waalikwa na wananchi wakiwa wamekaa ukumbini
kwa muda wote bila kutaarifiwa kinachoendelea.
Hata hivyo Mkuu wa
wilaya hiyo Mafutah Ally,aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John
Ng’oina,Mkurugenzi Mtendaji Naomi Nnko na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Stephen Kebwe walifanikiwa kuzima
mgomo huo,baada ya kujadiliana kwa muda mrefu na kuwapa utaratibu wa ulipaji wa mafao.
Dalili zamgomo zilianza
mapema baada ya madiwani hao kuitana pembeni bila kujali itikadi zao na kuanza
kuweka msimamo wa kutoingia mpaka wajue hatima ya malipo yao ya mwisho,na
malipo ya madeni ya mikopo wanayodaiwa katika benki za Nmb na Crdb matawi ya Mugumu.
Samwel Gibewa aliyekuwa
diwani wa kata ya Machochwe akiongea na blog hii alisema kuwa riba ya mikopo yao imeongezeka ,ikiwa ni
nje ya mkataba wao,ongezeko ambalo lilipaswa kulipwa na Mkurugenzi .
“Hilo na mafao yetu ndiyo yametufanya tukae nje mwa
muda wote ili tujue hatima yake ,maana baraza linapovunjwa hata ufuatiliaji
unakuwa mgumu….baada ya majadiliano ya muda mrefu na ufafanuzi ndiyo tumefikia
uamzi wa kuingia ukumbini”anasema.
Baadhi ya wananchi
waliohudhuria waliliambia Blog hii kuwa wengi wanategemea fedha hizo ili
ziwasaidie kwenye kampeini,kuambiwa zitatolewa baada ya uchaguzi ndiyo maana
wakaweka msimamo.
Akisoma waraka toka
ofisi ya Waziri Mkuu tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi)Mkurugenzi mtendaji Naomi Nnko alisema,posho za
mwezi za madiwani zitalipwa hadi oktoba 30 na ndipo watalipwa na mafao yao ya
mwisho.
“Kuhusu madeni ya
madiwani yale waliyoingia wenyewe watalazimika kulipa ,lakini kama yapo ambayo
halmashauri ilihusika ,yatalipwa kwa utaratibu husika,”alisema.
Katika hali isiyo ya
kawaida na ambayo imeibua simanzi kwa madiwani waliomaliza muda wake ni kitendo
cha aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Ng’oina kumwaga machozi
wakati anasoma taarifa ya baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
Ng’oina alimwaga
machozi baada ya kuelezea alivyougua na madiwani wakamuuguza ,” wenzetu watatu
kwa kipindi cha miaka mitatu waliaga maisha …mimi niliugua mkaniuguza kwa muda
mrefu hadi nikapona,”alisema huku akitokwa machozi.
Hata hivyo alisema si
vizuri kwa tukio hilo la yeye kumwaga machozi,lakini alisisitiza kuwa sasa
amepona na alikuwa amefikia uamzi wa kutogombea,lakini wananchi wamemshauri
agombee na hata madiwani wanaomba aendelee kuwa Mwenyekiti.
Kuhusu mafanikio kwa
kipindi cha miaka mitano alisema wamejitahidi kujenga umoja wa madiwani bila
kujali itikadi zao,na kuwa wametekeleza miradi mingi kwa ufanisi hali
iliyosababisha kupata hati safi mwaka huu,na hawajawahi pata hati chafu.
“Kwa kipindi hicho
tumefungua shule mbili za kidato cha tano na zinafanya vizuri,pia shule bora
kitaifa kwa matokeo ya mwaka 2014 ilitoka wilayani hapa…pia shule mbili
zilizofanya vibaya zimetoka hapa,”alisema.
Alisema ana imani wote
watashinda kwenye chaguzi na watarudi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja kama
walivyokuwa.
Hata hivyo Mwenyekiti
wa Nccr Mageuzi wilaya ambaye pia
alikuwa diwani wa kata ya Kisangura Tanu Mwita alipopewa nafasi ,alisema ili
baraza hilo lifanye maamzi mazuri madiwani wa CCM wanapaswa kupunguzwa na
wananchi ,kwa kuwa wamekuwa wakitumia wingi wao kupitisha hoja.
Mkuu wa wilaya hiyo Mafutah aliwaomba wajiepushe na utoaji ahadi
zisizotekelezeka ,kwa kufanya hivyo kunachangia migongano na jamii na kuisumbua
serikali.
Kwa upande wake Kamanda
wa Takukuru wilaya Emmanuel Liguda alisema hawatasita kuwakamata watakaokiuka sheria ya
Takukuru na kuwataka waone aibu
kukamatwa na serikali yao kwa makosa ya kutoa rushwa
Mwisho.
Inawezekana madiwani wengi wa viti maaluma wakapoteza nafasi zao,hapo wanaonekana kuwa na mawazo sana.
Kamanda wa Takukuru wilaya Emmanuel Liguda akitoa tahadhari kwa watakaotoarushwa watakamatwa na serikali yao,hivyo waone aibu kukamatwa.
Ded akisoma waraka toka Tamisemi unaoelekeza utaratibu wa uendeshaji wa halmashauri baada ya kuvunjwa kwa baraza na pia mafao ya madiwani na stahiki zingine.
Mdhibiti na mkaguzi wa hesabu mkoa wa Mara akisisitiza matumizi mazuri ya fedha za miradi,licha ya kupata hati safi.
Dk Kebwe akisisitiza jambo
Aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza John Ng'oina katikati,kulia Dc Mafutah na kushoto Ded Nnko wakifuatilia mijadala.
Wengi wanawaza kama watavaa tena majoho hayo kwa kuwa upinzani ndani na nje ya chama chao ni mkubwa katika maeneo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Naomi Nnko kulia akiteta jambo na katibu tawala Cosmas Qamara wakati wa kikao cha kuvunja baraza la madiwani.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na mbunge wa jimbo hilo Dk Stephen Kebwe akielezea mikakati ya serikali kuboresha huduma za jamii.
Mkuu wa wilaya Mafutah Ally akitoa nasaha kwa waliokuwa madiwani kuwa wakafanye kampeini kwa ustaarabu na serikali haitasita kuwakamata iwapo watakiuka sheria na taratibu za uchaguzi.
Waliokuwa madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye kikao chao cha mwisho ,
Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI Taifa Mosena Nyambabe akisalimia madiwani hao,tayari ametia nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment