Saturday,
August 22, 2015
Na Serengeti Media Centre(SMC)
Agosti 22,2015.
Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 vyama vya CCM,CHADEMA na
CUF vilitoa ahadi mbalimbali ambazo
walipanga kuzitekeleza katika kipindi cha miaka mitano.
Ahadi ambazo zililenga kutoa majawabu ya matatizo ya Ujinga,Umaskini,maradhi na kuimarisha
utawala bora kwa jamii.
Kabla ya kuja na ahadi mpya katika kampeini ambazo zimeanza
,hawajarudi kwa wananchi kama sehemu ya tathimini nini tuliahidi,tumetekeleza
nini,bado nini,je kuna changamoto mpya,badala yake ndimi zao uhubiri mafanikio
tu, kana kwamba waliyoyafanya yako mbinguni ambako hatujafika.
Kazi nyingi zilizofanyika ,utekelezaji wake umewahusisha
wanancha kwa nguvu na michango yao,sioni mantiki ya kuja na maneno mengi kwa kuwa walishiriki
katika utekelezaji wake, tunategemea waje waseme kwa yake ambayo hayakufanyika
ni kero kwa jamii,kwanini hayakufanyika,na kuna mkakati gani.
Serengeti Media Centre(SMC)inawarudisha kwenye ahadi za vyama
vya CCM,CUF na CHADEMA walizotoa mwaka 2010
ili wananchi waone kilichoahidiwa ,kilichotekelezwa na nini wanaleta
kipya,je kimezingatia matatizo yao ama yameachwa.
CCM.
Chama cha Mapinduzi (CCM)kupitia aliyekuwa mgombea wake
Jakaya Kikwete alitoa ahadi 75 kubwa ,ambazo kama zingetekelezwa taifa
lingesonga mbele na kuinua uchumi wa jamii.
Ujenzi
reli mpya kutoka Dar es salaam mpaka mikoa ya kanda ya Ziwa(Nzega),Mikoa ya
Tanga kuwa jiji la viwanda(Tangamjini)Tabora kutumia maji ya ziwa
Victoria(Igunga)kulipa madeni ya chama cha Ushirika Mkoa wa
Shinyanga(SHIRECU)Shinyanga.
Kumaliza
migogoro ya ardhi nchini(Dodoma)Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono(Dodoma
mjini)Kuwapatia trekta wakulima –kata ya Mrijo(Dodoma)Wananchi kutoondolewa
Ranchi ya Misenyi(Kagera)Kujenga uwanja wa ndege Misenyi(Kagera).
Kupanua
uwanja wa Ndege Bukoba(Bukoba mjini)Kujenga uwanja wa Ndege mkubwa
Kigoma(Kigoma mjini)Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda(Kagera)Mikoa ya Kagera,Kigoma,Lindi,Rukwa
na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya Taifa ya Umeme(Kagera)Kuimarisha
Takukuru kwa miaka mitatu(Kagera).
Hukumu kwa
waliopatikana na hatia ya kuua
albino(Mbeya)Kununua Meli kubwa kuliko Mv Bukoba(Kagera)Kuanzisha benki
ndogondogo kwa ajili ya wajasiliamali,Serikali kusaidia vyama vya Ushirika
(Mwanza)Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi
maalum chenye vifaa kupambana na waharifu(Mwanza),Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya
Mkoa (Geita)Kulinda Muungano kwa gharama zote(Pemba).
Kuwajengea
nyumba waathirika wa mafuriko ya Kilosa(Morogoro)Kununua Meli mpya kubwa Ziwa Nyasa(Mbeya mjini)Kujenga bandari
Kasanga(Rukwa)Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano (Songea)Kufufua Mgodi wa
Makaa ya Mawe Kiwira(Mbeya)Kuzuia hatari ya Kisiwa cha Pangani
kuzama(Tanga)Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa
vijijini(Iringa)Kujenga barabara yenye kiwango cha Lami kutoka Same mpaka
Kisiwani,Kihunio na kuunganisha na barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam(Same).
Kuboresha
barabara za Igunga (Tabora)Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari
zenye upungufu mkubwa wa walimu(Kisesa Magu),Kusambaza vyandarua viwili kwa
kila Kaya(Mbeya Mjini),Kuzipandisha hadhi hospitali maalum saba nchini kuwa za
rufaa ili kupunguzia mzigo hospitali ya taifa ya Muhimbili(MNH)(Hydom Wanyama).
Kulinda
amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini,kikabila na kisiasa(Musoma)Kulinda
haki za walemavu (Makete),Kujenga barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha
Lami urefu wa kilometa 109(Iringa mjini),Kuenga barabara ya Lami Musoma –Mto wa
Mbu(Arusha mjini),Kuanzisha jimbo la Ulyankulu(Shinyangamjini).
Kujenga
barabara ya lami Manyoni Kigoma(Kaliua Tabora)Kukarabati barabara ya Arusha
Moshi(Moshi mjini)Kuboresha barabara ya Handeni ,Kondoa mpaka Singida (Dodoma)Kuwafidia wanakijiji ng’ombe
waliokufa wakati wa kiangazi mwaka 2009(Longido),Vijiji vyote vilivyoko
kilometa 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria Shinyanga-Kahama kuunganishiwa
Maji,(Shinyanga).
Tatizo la
umeme kufika kikomo novemba 2010 mkoa wa Arusha(Arusha mjini)Kukopesha wavuvi
zana za kilimo (Busekela wilaya ya Musoma)Kuwapatia maji wakazi wa
Longido(Longido)Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa hifadhi ya Taifa
ya Serengeti(Ngorongoro),Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo
kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri,(Mbulu Arusha).
Kusambaza
umeme,utoaji wa huduma za afya,na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na
utoaji wa ruzuku kwa wakulima 2010-2015(Babati mjini)Kuongeza mara tatu
wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo na kilimo kwa mfumo wa Vocha
-(Iringa),Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika(Iringa mjini),Kulinda
usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-(Ifunda).
Kutokomeza
Malaria 2015(Bunda Mara)Kuwapa wanawake nafasi zaidi(Iringa)Kuisaidia Zanzibar
kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii(Kibandamaiti mjini Zanzibar),Kusaidia
Zanzibar kila panapohitajika msaada(Kibandamaiti Zanzibar)Serikali kujenga upya
bandari ya Mbambabay(Ruvuma)Ununuzi wa Meli Mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400(Mbambabay Ruvuma).
Kufufua
chama kikuu cha Ushirika cha wakulima wa Mbinga(Ruvuma),Hakutakuwa na umwagaji
wa damu baada ya uchaguzi wa 2010(Dar es Salaam),Mtwara kuwa mji wa
viwanda(Mtwara)Ujenzi wa kiwanda cha dawa ya viluwiluwi vya mbu,hospitali ya
Tumbi kuwa ya Mkoa(Kibaha),Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo
maalum la viwanda(Kibaha)Ujenzi wa reli kutoka Ubungo hadi Tegeta(Dar es
Salaam).
Kujenga
kiwanda cha kusindika matunda mkoani Pwani(Kibaha)Kuhifadhi zao la mpunga
katika ghala la Taifa (Malinyi),kujenga daraja la Kilombero lenye ukubwa wa
mita 400(Morogoro)na kuboresha barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe(Kilombero)
CHADEMA.
Dk Wilbroad Slaa akinadi sera za chama cha Demokrasia na
Maendeleo mwaka 2010 alitoa ahadi 18 kubwa ,iwapo wangeshinda ambazo
zingesaidia kukuza uchumi wa taifa na wananchi.
Kurudisha
fedha za mradi wa Rada(Moshi),Kushughulikia suala la taasisi ya kuweka na kuvuna pesa (DECI-Uwanja wa
Mashujaa Moshi),Kujenga nchi isiyo na ufisadi(Mwanza)Kufufua Tanganyika ili
irejee mezani kujadili Muungano na Zanzibar(Ifakara)Kufufua uchumi wa nchi kwa
kutumia rasilimali zilizopo(Arusha) Kukata asilimia 20 ya mshahara wa
Rais(Mwanza),Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15(Arusha).
Kuweka
Mwenge wa uhuru jumba la Makumbusho(Kilimanjaro),Kutoa huduma bora za afya
bure(Mwanza )Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi(Tarime)Kufuta walimu wote wa cheti
cha stashahada shule za sekondari na kuleta walimu walio na shahada
(Arusha)Kutoa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita(Morogoro).
Kutoa
huduma za afya bure kuanzia kituo cha afya hadi hospitali ya rufaa(Mwanza)Kutoa
ruzuku taasisi za kidini(Ifakara)Kusambaza magari aina ya shangingi kwa jeshi
la polisi ili wakamatie wahalifu badala ya mawaziri kuyatumia(Ifakara)Mfuko wa
saruji na bati kuuzwa sh 5,000(Bukoba)Kufuta pocho ya chai serikalini.
CHAMA CHA
WANANCHI(CUF)
Tofauti na wagombea wengine Profesa Ibrahimu Lipumba
alitoa 10 kubwa ambazo angepata ridhaa
zingesaidia kutatua matatizo yanayoikabili nchi na jamii.
Kubadili
Katiba na kumteua Dk Mohamed Shein kuwa Makamu wa Rais(Unguja)Elimu ya bure
kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu(Tanga)Kubana matumizi kwa kupunguza
ukubwa wa baraza la Mawaziri(Tanga)Kuunda serikali shirikishi(Mtwara)Kusimamia
raslimali(Tanga),Kuimarisha miundo mbinu(Kidongo chekundu).
Kusimamia
na kuboresha afya(Kidongo Chekundu)Kuboresha kilimo,viwanda na
uwekezaji(Mtwara)Kudhibiti uuzaji wa zao la Korosho(Mtwara)na Mfuko maalum wa
kusomesha walemavu.
Tusubiri
ahadi za Mwaka huu zitakazodumu kwa kipindi cha miaka mitano,Tutaendelea
kuwaletea taarifa mbalimbali kadri kampeini zinavyoendelea ili wananchi waweze
kuchukua uamzi sahihi wakati wa kupiga kura.