Subscribe:

Ads 468x60px

UJANGILI WACHAFUA SIFA YA TANZANIA KWA NCHI ZA ULAYA NA ASIA.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMISI KAGASHEKI AKIJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MKAKATI WA SERIKALI WA KUKABILIANA NA KASI YA UJANGILI ,KWENYE VIWANJA VYA HOTELI YA MOUNT MERU JIJINI ARUSHA AMBAPO ALISEMA VITENDO HIVYO VIMEICHAFUA TANZANIA KWA MATAIFA YA AMERIKA,ULAYA NA ASIA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WABUNGE WALIOSIMAMA KWENYE UKUMBI WA MOUNT MERU HOTEL SIKU YA KUTANGAZA VIVUTIO VILIVYOSHINDA KWENYE MAAJABU SABA YA ASILI AMBAPO TANZANIA ILIIBUKA KIDEDEA KWA VIVUTI VITATU VILIVYOSHINDANISHWA KUSHINDA.

UJANGILI WACHAFUA SIFA YA TANZANIA KWA NCHI ZA ULAYA NA ASIA.
Na Anthony Mayunga-Arusha.
Februari 17,2013.
SERIKALI ya Tanzania inahusishwa na vitendo vya ujangili na uuzaji wa meno ya tembo nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wake na wadau wa sekta ya utalii kwenye ukumbi wa hoteli ya Mount Meru jijini Arusha alisema tatizo hilo limeichafua nchi.
Alisema kwa nchi za Marekani na barani Asia sifa ya Tanzania kwa suala la ujangili ni mbaya kwa kuwa inahusishwa na vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi.
“Hatuwezi kukubali kubeba sifa mbaya hiyo.. wanatusema sana wenzetu huko nje…hata wadau wa sekta ya utalii kwenye kikao wamesema…wakihusisha baadhi ya watendaji wa serikali na mtandao huo”alisema.
Kagasheki alisema mtandao wa ujangili ni mkubwa tena unatumia silaha za kivita ambazo zinatishia uhai wa askari wa hifadhi hizo na kuwa tayari mkakati wa kuunganisha nguvu za pamoja umekamilika ili kuhakikisha wanatokomeza mtandao huo.
“Ni mtandao mkubwa lakini hautatushinda lazima utokomezwe maana tusipofanya hivyo sifa tulizopata kwa vivutio vyetu kushinda kwenye mashindano ya vivutio bora vya asili Afrika hautakuwa na maana …lazima tulinde raslimali hizi zinazochangia pato kuwa kwa taifa”alibainisha.
Aliwaonya baadhi ya watumishi wanaoshirikiana na wahujumu uchumi kuwa hatua kali zitachukuliwa kwao,huku akisisitiza kuwa wanakusudia kurekebisha sheria ili ziwe kali kwa wanaokamatwa kwenye makosa hayo.
Kuhusu suala la silaha zinazotumiwa na majangili alisema zinatishia usalama wan chi kwa kuwa wanatumia silaha kali za kivita ambazo zinatakiwa kudhibitiwa.
Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa idara yake imejipanga kusafisha watendaji wasiokuwa waadilifu kwa kuwa baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wameishapoteza imani na idara hiyo kutokana na urasimu wa watendaji kitendo alichosema atakikomesha mara moja.
Februari 11 mwaka huu Vivutio vya Mlima Kilimanjaro,Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilitangazwa kuwa washindi kwa vivutio vya maajabu saba ya asili.
Mbali na hivyo pia mto Nile kwa Uganda,maporomoko ya Zambia,Jangwa la Sahara vilikuwa miongoni mwa vilivyoshinda ,mashindano yaliyoandaliwa na shirika la Seven Natural Wonders of Afrika la Taxes Nchini Marekani ,ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikabidhi tuzo kwa washindi.
Mwisho.

WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII KUNOLEWA

Journo Tourism ‘kufunda’ wanahabari
Na Mwandishi wetu –Serengeti
Februari 17,2013.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Maliasili na Utalii Tanzania (Journo
Tourism), kimeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini
yatakayofanyika wilaya ya Serengeti mkoani Mara mwishoni mwa mwezi
huu.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Julius Magodi amewaambia waandishi wa habari kuwa  mafunzo hayo yanatarajiwa   kuanza Februaria 25 hadi 28 mwaka huu mjini Mugumu.

Amesema  lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea wanahabari uwezo
wa kuandika habari za maliasili na utalii kwa usafaha zaidi, kuzilinda
na kufichua hujuma, ambazo zinakwamisha maendeleo ya sekta ya utalii
nchini.

Pia waweze kupata uwezo  wa kuandika kwa kina habari zinazohusu
utalii na vivutio vyake pamoja na maliasili za taifa.

Aliongeza kuwa Journo Tourism, kimedhamiria kuwapika waandishi wa
habari, wawe chachu ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, ili
kukuza utalii na mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

Magodi alifafanua kwamba waandishi wa habari kupitia taaluma yao wana
jukumu kubwa la kulinda maliasili na kuvitangaza vivutio vya utalii
vilivyopo na vile ambavyo havifahamiki, hatua ambayo licha ya kukuza
uchumi wa taifa, itasaidia pia kuzalisha nafasi za ajira hasa kwa
vijana.

Magodi amesema mafunzo hayo yataendeshwa na baadhi ya wadau wa utalii
nchini, ambao watatoa mada mbalimbali kwa washiriki.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa shirika hilo Anthony Mayunga alibainisha kuwa maandalizi ya mafunzo hayo yanaendelea vizuri na kuwa tayari wataalam kutoka Tanapa,Bodi ya Utalii Tanzania,Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Frankfurt Zoological Society(FZS)Mawalla ,Singita Grumeti wanatarajiwa kushiriki kwa kutoa mada.
“Lengo la kuwaleta wataalam hao ni kusaidia waandishi kutofautisha Tanapa,Mamlaka ya Ngorongoro,Mapori ya akiba na Hifadhi za jamii(WMA)ingawa wote wanahifadhi lakini wanaongozwa kwa sheria na kanuni tofauti…itawasaidia kujua na kuandika habari kwa usahihi”alisema.
Alisema waandishi hao watatoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa shirika hilo ni la kitaifa na watapata siku ya kuzuru moja ya hifadhi baada ya mafunzo ili kujifunza kwa vitendo.

VIWANJA 250 SERENGETI MMILIKI HAJULIKANI

MMILIKI WA VIWANJA  250 HAJULIKANI SERENGETI..
Februari 17,2013.
KAMATI ya ardhi wilaya ya Serengeti haina viwanja vya kugawa kutokana na halmashauri kutokuwa na uwezo wa kutunza maeneo na kuyafanyia mpango wa kuyapima kutokana na ukata unaoikabili idara ya ardhi.
Kutokana na ukata huo wakazi wengi wa mji wa Mugumu wamejimilikisha maeneo kinyamera  ama wengine wanagawiwakinyume cha utaratibu  na wataalam wa idara hiyo na kupelekea kukithiri kwa migogoro ya ardhi.
Kwa mjibu wa Taarifa ya afisa ardhi wilaya Orwaka Nyamususa kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo amebainisha kuwa vitalu J na K katika maeneo ya Magereza na Matare viwanja vina milikiwa kimila na wananchi ikiwa ni kinyume cha utaratibu.
Na kuwa serikali ilipaswa kuvitambua na kwa msingi huo haipati kodi ya ardhi ,na kikubwa ni kuwa hawana vifaa vya kupimia kama darubini ya kisasa ili wazalishe viwanja na matokeo ni ujenzi holela katika maeneo ambayo hayajapimwa.
“Halmashauri haina takwimu sahihi kuhusu kodi kwa mwaka…viwanja vyenye kumb.932 kitalu A,B,C,D,E,F,G,H,J,na K viwanja 250 kitalu A-G mmiliki wake hajulikani…vingine hakuna takwimu sahihi kodi wanayotakiwa kulipwa wala ukubwa wa viwanja”amebainisha.
Na kuwa kumbukumbu zinazotakiwa ni kubaini viwanja vilivyopimwa,andaliwa,hati miliki,barua za toleo,visivyoendelezwa,waliokiuka masharti ya uendelezaji,zinazolipiwa kodi ,zisizolipiwa ,maeneo hatari kwa makazi ,zenye mashauri mahakamani na migogoro ya umiliki.
Pia miliki zilizotolewa kituo cha uwekezaji(TIC)mashamba yaliyopimwa,hati miliki za kimila yaliyohaulishwa na kimilikishwa au yaliyotelekezwa.
Pamoja na kuwa na mchakato wa kuifanya mamlaka ya mji mdogo kuwa mamlaka maeneo mengi ya wazi yanavamiwa na kugeuzwa makazi kinyamera na wanaoongoza mchezo huo ni viongozi wa serikali hali ambayo inadaiwa kuchangiwa pia na idara hiyo ya ardhi.
Aidha inadaiwa kuwa watalaam wa idara hiyo wamejimilikisha viwanja vingi kinyamera ambavyo huvitumia kwa kuuza kwa watu na hiyo inachangia kutokuwepo kwa kumbukumbu sahihi za wamilikaji wa baadhi ya viwanja .
Licha ya kutambua matatizo hayo ambayo yanapelekea kukithiri kwa migogoro baadhi ya watumishi wanaohusika wanalindwa na baadhi ya madiwani kwa misingi ya ukabila ,na hatua huchukuliwa haraka kwa wale ambao si wazawa wa wilaya hiyo wanapobainika kukosea ,lakini kwa wazawa hulindwa na matokeo yake halmashauri hiyo inashitakiwa katika mabaraza ya ardhi na wananchi.
Mwisho.

NDOO AMBAPO BAADA YA KUJIFUNGUA ALIMUUA MTOTO NA KUMTUMBUKIZA KISHA AKAFUNIKA

MTOTO HUYO ALIZALIWA MZIMA NA AFYA TELE LAKINI MAMA YAKE AKAAMUA KUMKATILI KWA KUMUUA
ANNA CHACHA AMA KURWA SELE MKAZI WA MTAA WA BOMANENGETII MJINI MUGUMU WILAYANI SER AMBAYE AMEHITIMU KIDATO CHA NNE NATTA SEKONDARI 2012 AKIWA MJAZMITO NA BAADA YA KUJIFUNGUA AKAMUUA MWANAE NA KUMTUMBUKIZA NDANI YA NDOO LAKINI PAMOJA NA KUKIRI MBELE YA JAMII NA POLISI INADAIWA WALIMWACHIA BAADA YA NDUGU ZAKE KUWAKATIA RUSHWA HATUA AMBAYO INAPIGIWA KELELE  NA WANANCHI

VIVUTIO VYA TANZANIA VYAONGOZA

MIONGONI MWA BURUDANI ZILIZOPAMBA SIKU YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA MAAJABU SABA YA AFRIKA VILIVYOSHINDA HOTEL YA MOUNT MERU ARUSHA

BAADHI YA WAGENI WALIOHUDHURIA WAKIWEMO MABALOZI KUTOKA NCHI MBALIMBALI

MIZIKI YA BAKURUTU ILIWAINUA WATU VITINI WAKIWEMO WAZEE WA ZAMANI WAKIONGOZWA NA JAMES LEMBELI MBUNGE WA JIMBO LA KAMAHA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI ,MALIASILI NA MAZINGIRA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA,WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA UGANDA,WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA TANZANIA BALOZI KHAMISI KAGASHEKI NA RAIS WA KAMPUNI YA AFRICAN WONDERS WAANDAJI WA MASHINDANO HAYO DR IMLER WAKIFUATILIA BURUDANI

MKURUGENZI WA TANAPA ALLAN KIJAZI AKIWA AMEONYESHA TUZO MAALUM YA USHINDI WA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI AMBAYO ILIPIGIWA  KURA NYINGI SANA

MKURUGENZI MKUU WA TANAPA ALLAN KIJAZI MARA BAADA YA KUPOKEA HATI MAALUM YA USHINDI WA HIFADHI YA MLIMA KILIMANJARO WENGINE NI WAZIRI MKUU PINDA,WAZIRI WA UTALII UGANDA,RAIS WA KAMPUNI ILIYOANDAA MASHINDANO HAYO DR IMLER
WAZIRI KAGASHEKI AKITETA JAMBO NA DR IMLER

Bonde la Ngorongoro huvuta watalii wengi

watalii wakiangalia wanyama na vivutio vingine kama uoto wa asili na ndege ndani bonde la Ngorongoro