MMILIKI WA VIWANJA 250 HAJULIKANI SERENGETI..
Februari 17,2013.
KAMATI ya ardhi wilaya ya Serengeti haina viwanja vya kugawa
kutokana na halmashauri kutokuwa na uwezo wa kutunza maeneo na kuyafanyia
mpango wa kuyapima kutokana na ukata unaoikabili idara ya ardhi.
Kutokana na ukata huo wakazi wengi wa mji wa Mugumu
wamejimilikisha maeneo kinyamera ama
wengine wanagawiwakinyume cha utaratibu na wataalam wa idara hiyo na kupelekea
kukithiri kwa migogoro ya ardhi.
Kwa mjibu wa Taarifa ya afisa ardhi wilaya Orwaka Nyamususa
kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo amebainisha kuwa vitalu J na K
katika maeneo ya Magereza na Matare viwanja vina milikiwa kimila na wananchi
ikiwa ni kinyume cha utaratibu.
Na kuwa serikali ilipaswa kuvitambua na kwa msingi huo
haipati kodi ya ardhi ,na kikubwa ni kuwa hawana vifaa vya kupimia kama
darubini ya kisasa ili wazalishe viwanja na matokeo ni ujenzi holela katika
maeneo ambayo hayajapimwa.
“Halmashauri haina takwimu sahihi kuhusu kodi kwa mwaka…viwanja
vyenye kumb.932 kitalu A,B,C,D,E,F,G,H,J,na K viwanja 250 kitalu A-G mmiliki
wake hajulikani…vingine hakuna takwimu sahihi kodi wanayotakiwa kulipwa wala
ukubwa wa viwanja”amebainisha.
Na kuwa kumbukumbu zinazotakiwa ni kubaini viwanja vilivyopimwa,andaliwa,hati
miliki,barua za toleo,visivyoendelezwa,waliokiuka masharti ya
uendelezaji,zinazolipiwa kodi ,zisizolipiwa ,maeneo hatari kwa makazi ,zenye
mashauri mahakamani na migogoro ya umiliki.
Pia miliki zilizotolewa kituo cha uwekezaji(TIC)mashamba
yaliyopimwa,hati miliki za kimila yaliyohaulishwa na kimilikishwa au
yaliyotelekezwa.
Pamoja na kuwa na mchakato wa kuifanya mamlaka ya mji mdogo
kuwa mamlaka maeneo mengi ya wazi yanavamiwa na kugeuzwa makazi kinyamera na
wanaoongoza mchezo huo ni viongozi wa serikali hali ambayo inadaiwa kuchangiwa
pia na idara hiyo ya ardhi.
Aidha inadaiwa kuwa watalaam wa idara hiyo wamejimilikisha
viwanja vingi kinyamera ambavyo huvitumia kwa kuuza kwa watu na hiyo inachangia
kutokuwepo kwa kumbukumbu sahihi za wamilikaji wa baadhi ya viwanja .
Licha ya kutambua matatizo hayo ambayo yanapelekea kukithiri
kwa migogoro baadhi ya watumishi wanaohusika wanalindwa na baadhi ya madiwani
kwa misingi ya ukabila ,na hatua huchukuliwa haraka kwa wale ambao si wazawa wa
wilaya hiyo wanapobainika kukosea ,lakini kwa wazawa hulindwa na matokeo yake
halmashauri hiyo inashitakiwa katika mabaraza ya ardhi na wananchi.
Mwisho.
1 comments:
Hii kazi kwa mwendo huo tutafika kweli?
Post a Comment