Subscribe:

Ads 468x60px

WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII KUNOLEWA


Journo Tourism ‘kufunda’ wanahabari
Na Mwandishi wetu –Serengeti
Februari 17,2013.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Maliasili na Utalii Tanzania (Journo
Tourism), kimeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini
yatakayofanyika wilaya ya Serengeti mkoani Mara mwishoni mwa mwezi
huu.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Julius Magodi amewaambia waandishi wa habari kuwa  mafunzo hayo yanatarajiwa   kuanza Februaria 25 hadi 28 mwaka huu mjini Mugumu.

Amesema  lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea wanahabari uwezo
wa kuandika habari za maliasili na utalii kwa usafaha zaidi, kuzilinda
na kufichua hujuma, ambazo zinakwamisha maendeleo ya sekta ya utalii
nchini.

Pia waweze kupata uwezo  wa kuandika kwa kina habari zinazohusu
utalii na vivutio vyake pamoja na maliasili za taifa.

Aliongeza kuwa Journo Tourism, kimedhamiria kuwapika waandishi wa
habari, wawe chachu ya kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, ili
kukuza utalii na mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

Magodi alifafanua kwamba waandishi wa habari kupitia taaluma yao wana
jukumu kubwa la kulinda maliasili na kuvitangaza vivutio vya utalii
vilivyopo na vile ambavyo havifahamiki, hatua ambayo licha ya kukuza
uchumi wa taifa, itasaidia pia kuzalisha nafasi za ajira hasa kwa
vijana.

Magodi amesema mafunzo hayo yataendeshwa na baadhi ya wadau wa utalii
nchini, ambao watatoa mada mbalimbali kwa washiriki.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa shirika hilo Anthony Mayunga alibainisha kuwa maandalizi ya mafunzo hayo yanaendelea vizuri na kuwa tayari wataalam kutoka Tanapa,Bodi ya Utalii Tanzania,Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,Frankfurt Zoological Society(FZS)Mawalla ,Singita Grumeti wanatarajiwa kushiriki kwa kutoa mada.
“Lengo la kuwaleta wataalam hao ni kusaidia waandishi kutofautisha Tanapa,Mamlaka ya Ngorongoro,Mapori ya akiba na Hifadhi za jamii(WMA)ingawa wote wanahifadhi lakini wanaongozwa kwa sheria na kanuni tofauti…itawasaidia kujua na kuandika habari kwa usahihi”alisema.
Alisema waandishi hao watatoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa shirika hilo ni la kitaifa na watapata siku ya kuzuru moja ya hifadhi baada ya mafunzo ili kujifunza kwa vitendo.
Mwisho.

Mwisho.

0 comments:

Post a Comment