Subscribe:

Ads 468x60px

UJANGILI WACHAFUA SIFA YA TANZANIA KWA NCHI ZA ULAYA NA ASIA.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMISI KAGASHEKI AKIJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MKAKATI WA SERIKALI WA KUKABILIANA NA KASI YA UJANGILI ,KWENYE VIWANJA VYA HOTELI YA MOUNT MERU JIJINI ARUSHA AMBAPO ALISEMA VITENDO HIVYO VIMEICHAFUA TANZANIA KWA MATAIFA YA AMERIKA,ULAYA NA ASIA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WABUNGE WALIOSIMAMA KWENYE UKUMBI WA MOUNT MERU HOTEL SIKU YA KUTANGAZA VIVUTIO VILIVYOSHINDA KWENYE MAAJABU SABA YA ASILI AMBAPO TANZANIA ILIIBUKA KIDEDEA KWA VIVUTI VITATU VILIVYOSHINDANISHWA KUSHINDA.

UJANGILI WACHAFUA SIFA YA TANZANIA KWA NCHI ZA ULAYA NA ASIA.
Na Anthony Mayunga-Arusha.
Februari 17,2013.
SERIKALI ya Tanzania inahusishwa na vitendo vya ujangili na uuzaji wa meno ya tembo nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wake na wadau wa sekta ya utalii kwenye ukumbi wa hoteli ya Mount Meru jijini Arusha alisema tatizo hilo limeichafua nchi.
Alisema kwa nchi za Marekani na barani Asia sifa ya Tanzania kwa suala la ujangili ni mbaya kwa kuwa inahusishwa na vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi.
“Hatuwezi kukubali kubeba sifa mbaya hiyo.. wanatusema sana wenzetu huko nje…hata wadau wa sekta ya utalii kwenye kikao wamesema…wakihusisha baadhi ya watendaji wa serikali na mtandao huo”alisema.
Kagasheki alisema mtandao wa ujangili ni mkubwa tena unatumia silaha za kivita ambazo zinatishia uhai wa askari wa hifadhi hizo na kuwa tayari mkakati wa kuunganisha nguvu za pamoja umekamilika ili kuhakikisha wanatokomeza mtandao huo.
“Ni mtandao mkubwa lakini hautatushinda lazima utokomezwe maana tusipofanya hivyo sifa tulizopata kwa vivutio vyetu kushinda kwenye mashindano ya vivutio bora vya asili Afrika hautakuwa na maana …lazima tulinde raslimali hizi zinazochangia pato kuwa kwa taifa”alibainisha.
Aliwaonya baadhi ya watumishi wanaoshirikiana na wahujumu uchumi kuwa hatua kali zitachukuliwa kwao,huku akisisitiza kuwa wanakusudia kurekebisha sheria ili ziwe kali kwa wanaokamatwa kwenye makosa hayo.
Kuhusu suala la silaha zinazotumiwa na majangili alisema zinatishia usalama wan chi kwa kuwa wanatumia silaha kali za kivita ambazo zinatakiwa kudhibitiwa.
Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa idara yake imejipanga kusafisha watendaji wasiokuwa waadilifu kwa kuwa baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wameishapoteza imani na idara hiyo kutokana na urasimu wa watendaji kitendo alichosema atakikomesha mara moja.
Februari 11 mwaka huu Vivutio vya Mlima Kilimanjaro,Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilitangazwa kuwa washindi kwa vivutio vya maajabu saba ya asili.
Mbali na hivyo pia mto Nile kwa Uganda,maporomoko ya Zambia,Jangwa la Sahara vilikuwa miongoni mwa vilivyoshinda ,mashindano yaliyoandaliwa na shirika la Seven Natural Wonders of Afrika la Taxes Nchini Marekani ,ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikabidhi tuzo kwa washindi.
Mwisho.


0 comments:

Post a Comment