Subscribe:

Ads 468x60px

PICHA ZA MATUKIO YA TAMASHA LA 16 LA NCHI ZA MAJAHAZI NGOME KONGWE

PROFESA MARTIN MHANDO MKURUGENZI WA ZANZIBAR INTERNATION FILM FESTIVAL(ZIFF) AKIONGEA NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA KENYA OFISI ZA ZIFF NGOME KONGWE ZANZIBAR
MMOJA WA WASHINDI WA AWARD ZA NCHI ZA MAJAHAZI
WASHINDI WA AWARD MBALIMBALI WA TAMASHA LA 16 ZA NCHI ZA MAJAHAZI KATIKA PICHA YA PAMOJA NGOME KONGWE
WASHINDI WA AWARD MBALIMBALI KATIKA PICHA YA PAMOJA

MAMBO YA ZANZIBAR


SAFARI ILIKUWA NZURI KWA MAONGOZI YA MUNGU
HAPO NI NGOMA KONGWE ZANZIBAR,ENEO MAARUFU SANA KWA HISTORIA YA KISIWA HICHO,WATALII WENGI HUFIKA ENEO HILO KWA AJILI YA KUPATA HISTORIA HIYO,MATAMASHA MBALIMBALI HUANDALIWA HAPO

SAFARI YA ZANZIBAR KUPITIA KIA

 MUNGU NI MWEMA TUNAWASILI KIA TUNASUBIRI NDEGE KWENDA ZANZIBAR VIA UWANJA WA MWALIMU NYERERE DSM
 SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE
 KIA TUKITOKEA MWANZA
 MAMBO YA SAFARI
 KIA NI PAZURI,HALI YA HEWA BARIDI KIDOGO
 KUELEKEA MAPUMZIKO KIA
 ENEO HILI LINAVUTIA ZAIDI,
 NIMEPAPENDA HAPA
MMOJA WA WAFANYAKAZI WA KIA,

WAFUGAJI WAIPA SERIKALI ANGALIZO KUNUSURU VURUGU


WAFUGAJI walioko kando  ya mapori ya akiba ya Ikorongo na
Grumeti wilaya za Serengeti na Bunda wameitaka  serikali kuwachukuliahatua askari wa mapori hayo wanaoshirikiana na Kampuni ya SingitaGrumeti Reserves wanaohusishwa na utesaji wananchi na mauaji ya mifugo wanapowakamata.

Mbele ya viongozi wa serikali ,madiwani na Kampuni ya Singita Grumeti Reserves kwenye ukumbi wa Mandela Issenye wakati wa Kongamano lililoandaliwa na shirika la Maendeleo ya Wafugaji Jamii yaWataturu(Shimwajawa)wafugaji walisema hali ilipofikia inahatarisha uhifadhi kwa kuwa hakuna ushirikiano pande hizo mbili.

Gidai Murasi(75) mfugaji kutoka Hunyari wilayani Bunda kwa hasira alinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa “ili tuendelee tunahitaji ardhi,siasa safi,watu na uongozi bora…tatizo ni uongozi bora…kama inafikia wahifadhi wanaua ng’ombe wetu ili tuwe masikini….kuna mapato gani ya uhifadhi yanaweza kutuhudumia sisi kwa umaskini
wanaotusababishia?”alihoji.

Alisema  wafugaji hao  ni kama hawako Tanzania ,maana kwa umri wake hajaona taifa linalowafanya wananchi wake kuwa maskini…”mimi sijasoma…maisha yangu yote ni ng’ombe,natunza na kusomesha watoto kwa mifugo…hivi kwa nini mnatengeneza majambazi…nchi hii itakuja kuwa navita mbaya sana”alisema.

Murasi alisema serikali inatambua tatizo lao ni malisho hasa baada ya
kuchukua maeneo yao na kuwa hifadhi,wakati wa kiangazi hali huwa mbaya zaidi,lakini kama kungekuwa na uhusiano wangeruhusiwa kuingia hatua chache na kunywesha mifugo kwa kuwa mto walioutegemea nao ulichukuliwa na hawakuchimbiwa malambo.

Esther Balebe mkazi wa Issenye alisema mahusiano mabaya yaliyopo kwa wahifadhi na wafugaji yanachangia kukithiri kwa ujangili,kwa kuwa hata akina mama wakienda kuokota kuni  wanadhalilishwa wanapigwa na kutendewa mambo yasiyofaa.

Joash Tangera alisema udhaifu wa serikali utakuja kuibua matatizo
makubwa kati ya pande hizo,kwa kuwa hiyo ni vita ya ndani ,lakini iko siku itakuja kuwa kubwa,wafugaji hawapendi kuingiza mifugo hifadhini lakini tatizo kubwa ni malisho,baada ya eneo lao kuchukuliwa na kuwa kwa mahusiano wangeruhusiwa kuchungia mita chache wakati wa kiangazi.

Walihoji sababu za serikali kuwafidia wafugaji wa Monduli baada ya
ng’ombe wao kufa kwa ukame,wakati nao wana matatizo kama hayo,wengine wanauawa na pia wanyama wanaua watu,mifugo na kula mazao na hakuna fidia iliyowahi tolewa.

Gijeshi Gambarara mkazi wa Iharara alisema ng’ombe wake watatu
walifukuzwa kwa helkopita yaSingita Grumeti Reserves  na kushuka
karibu upepo ukawapelekea kuzama mtoni na kufa,huku shamba lake la ekari 10 likiwa limeliwa na wanyama pori,lakini hajawahi pata
msaada,na kuwa uwekezaji huo haufai kwa jamii.

Wafugaji walisema mpango wa mwekezaji ni kuua mifugo yao ,hata kwenye mipango yake hakuna mkakati wa kusaidia wafugaji.

Baadhi walisema serikali isisubiri matatizo kama ya Mtwara ndio
ichukue hatua bali wakae chini watafute ufumbuzi wa pande hizo,kwa kuwa madhara yake ni makubwa ikiwemo ongezeko la ujangili wa tembo kwa kuwa jamii haioni faida ya kutoa ushirikiano kwa sekta inayowatia umaskini.

Mwenyekiti wa Shimwajawa Gohebu Gorobani na katibu wake Mnada Mayonga walisema lengo la kukutanisha wahifadhi,wafugaji na serikali ni kutafuta muafaka kwa maslahi ya taifa kwa kuwa kuna kila dalili za uvunjifu wa amani.

Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Serengeti ambaye ni afisa tarafa ya
Grumeti Paulo Shanyangi alisema njia hiyo inalenga kuleta muafaka, serikali itachukua hatua za haraka ili kuleta mahusiano,akiitaka kampuni ya Singita Grumeti kusaidia wananchi upande wa malambo ya maji.

Kwa upande wa Kampuni ya Singita Grumeti waliomba suala hilo
lisichukuliwe kwa jazba madhara yake ni makubwa kwa kuwa watakaoumia ni vijana wao ,kwa kuwa mwekezaji hakuja na watu wake,bali watumie njia ya kuzungumza kwa kuwataja wahusika hatua zichukuliwe.

Hivi karibuni askari hao wametuhumiwa kuua ng’ombe 51 na wengine 100 kupotea mali ya Kiteku Meshinya mkazi wa Mariwanda wilayani Bunda,baada ya kuwakamata na kisha kuwafukuza kwa magari na kuzama mto Rubana.

Mwanzoni mwa mwaka huu ng’ombe zaidi ya 40 mali ya Kijiji mkazi wa Motukeri waliuawa kwa mtindo huo,na mwaka 2008 ng’ombe 65 wa Gorobani Marosina walizamishwa mtoni,huku ikidaiwa kijana mmoja naye alikufa maji baada ya kumkimbiza na kutumbukia mtoni.

Hata hivyo uongozi wa Senapa,ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi halmashauri ya Bunda hawakuhudhuria kongamano hilo licha ya kuwa na taarifa.

Mwisho.
 WAFUGAJI WAKATI WA KONGAMANO LILILOWAKUTANISHA NA WAHIFADHI NA VIONGOZI WA SERIKALI CHINI YA SHIRIKA LA SHIMWAJAWA ISSENYE WILAYANI SERENGETI
 MMOJA WA WAFUGAJI KUTOKA MARIWANDA WILAYANI BUNDA AKIELEZA MIKASA IWAKUTAYO WAFUGAJI
HATA AKINA MAMA WAFUGAJI HAWAKUSITA KUSEMA WANAVYOTENDEWA NA WAHIFADHI WAWAKAMATAPO HIFADHINI WAKIWA NA MIFUGO AMA WANASENYA KUNI

BUSTANI ZINALIPA KULIKO UVUVI RORYA

 MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA BADILIKA FOUNDATION  MOSES WAMBURA AKIONGEA NA MMOJA WA VIONGOZI WA KIKUNDI CHA WAKULIMA WA UMWAGILIAJI SONGAMBELE KIJIJI CHA MUHUNDWE KATA YA KYANG'OMBE SUBA WILAYA YA RORYA.
 BWAWA LA MAJI KWA AJILI YA UFUGAJI WA SAMAKI NA UMWAGILIAJI WABUSTANI LA KIKUNDI CHA GRA KATIKA KIJIJI CHA KINESI WILAYANI RORYA
 BUSTANI YA KIKUNDI CHA GRA KINESI WANAOHUDUMIA WATOTO YATIMA NA WALE WA MAZINGIRA MAGUMU
 HAPA NINAONGEA NA KIJANA MHITIMU WA KIDATO CHA SITA AMBAYE NI MWANACHAMA WA KIKUNDI CHA SONGAMBELE,AMBAYE ANADAI BUSTANI NI AJIRA TOSHA
I
 WAKATI MWINGINE MNALAZIMIKA KUFANYIA MAZUNGUSZO SHAMBANI BILA KUJALI JUA ,HAPA NI KIKUNDI CHA JITUME MUHUNDWA WILAYA YA RORYA AMBAO WAMELIMA MAHINDI NA VIAZI,KAMA ZAO LA BIASHARA
BUSTANI YA WANA GRA KIJIJI CHA KINESI WILAYANI RORYA.

SAFARI WILAYANI RORYA KWA USAFIRI WA FERI ZIWA VICTORIA NI UTALII TOSHA

 MTOTO AKIJARIBU KUPANDA JUU KWA NAHODHA WA KIVUKO CHA MV RORYA
 BEACH YA KINESI HUWAVUTA WATU WENGI WAKIWEMO WATOTO AMBAO HUCHEZA FUKWENI,NI ENEO AMBALO LINALOPENDEZWA ,BAADHI YA WATU HUFIKA ENEO HILO KUPUMZIKA WAKIWEMO WAGENI TOKA NJE YA NCHI
 WATOTO WAKILOA SAMAKI ZIWA VICTORIA ENEO LA KINESI WILAYANI RORYA
 KISIWA HIKI KIKO KATIKATI YA ZIWA VICTORIA WILAYANI RORYA KINATARAJIWA KUJENGWA HOTELI YA KITALII KAMA FURSA YA UTALII .
 BAADHI YA ABIRIA NA WANAOSUBIRI WAGENI WAKIWA ENEO LA BANDARI MUSOMA MJINI WAKATI FERI  IKITOKEA RORYA IKIKARIBIA KUTIA NANGA .
HAPA BODA BODA WANAWAHI ABARIA KUTOKA KINESI TAYARI KWA KUWAPELEKA MAENEO MBALIMBALI MJINI MUSOMA.

SAFARI YA RORYA KUTEMBELEA VIKUNDI VYA KILIMO CHA MBOGA MBOGA

 NIKIWA WILAYANI RORYA NIMEKUTANA NA WANAKIKUNDI CHA BUSTANI CHA WAUSO SONGAMBELE KATA YA KYANG'OMBE TARAFA YA SUBA
 MAHOJIANO YANAENDELEA SHAMBANI
 BAADA YA KAZI NINAPATA MUDA WA KUPUMZIKA BEACH YA KINESI NIKISUBIRI USAFIRI
 ENEO HILI LINA UPEPO MWANANA TOKA ZIWA VICTORIA
 KAZI NA DAWA MSOSI HUO UNAPATIKANA BEACH YA KINESI,NASI HATUKUBAKI NYUMA KATIKA KUREKEBISHA AFYA ZETU
 BAADA YA CHAKULA NILIANZA SAFARI YA KWENDA KUPANDA FERI TAYARI KWA KUELEKEA MUSOMA MJINI,IKIWA SIKU YA KWANZA,
SIKUWA PEKEE YANGU KUPANDA FERI,TAYARI ABIRIA WAMEISHAPANDA TAYARI KWA KUANZA KUKATA MAWIMBI MAZITO,MUNGU ALIKUWA UPANDE WETU TUKAFIKA SALAMA,ASHUKURIWE.

BIASHARA YA MKAA LICHA YA KUTOKUTOZWA KODI,HUCHANGIA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA


 MIONGONI MWA BIASHARA AMBAYO HAITOZWI KODI NI MKAA,HAPA MMOJA WA WAUZA MKAA ANADAI KWA TRIPU MOJA ANAPATA ZAIDI YA SH.50,000 NA ANA UWEZO WA KUSOMBA ZAIDI YA MARA MBILI.
LICHA YA KUTOTOZWA KODI BIASHARA HIYO LAKINI INACHANGIA UHARIBIFU MKU WA MAZINGIRA,WAKATI MKAKATI WA KUPANDA MITI UKIBAKI KWENYE MAKABRASHA WAKATI WA SIKU YA MAZINGIRA DUNAINI ,KILA WILAYA IKIDAI IMEPANDA MITI MIL.1.5
FRANSISCA NA ALICE NI WATOTO WANGU,AMBAO KILA JIONI WANAKUWA NA DARASA LA KUJIFUNZA KOMPUTA ,MAANA TEKNOLOJIA NDIYO MAMBO YOTE KWA ULIMWENGU WA LEO.

AUAWA BAADA YA KUKUTWA NDANI YA DUKA AKIJARIBU KUIBA.


AUAWA BAADA YA KUKUTWA NDANI YA DUKA AKIJARIBU KUIBA.
Juni 26,2013
Serengeti:
WAKAZI wa kijiji cha Nyamakendo kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti wamemuua mkazi mmoja wa kijiji cha Machochwe baada ya kufungiwa ndani ya duka la Mwalimu mkuu shule ya Msingi Manyata katika jaribio la wizi.
Diwani wa kata hiyo Samwel Gibawa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juni 25,2013 majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Manyata ,na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Bageni Mwita Manko(19),akiwa na wenzake wawili  wakiwa wameisha vunja kufuli la duka la Mwalimu Mkuu Manyata Matiko Ryoba kwa nia ya kuiba.
Alisema kabla ya kutokea tukio hilo,Mwalimu Ryoba alifunga duka na kwenda nyumbani kwake,ili kutoa nafasi kwa  vijana wake wanaolala dukani ,hata hivyo alirudi ghafla dukani na wakati anasukuma mlango akabaini uko wazi na kuna mtu kwa ndani.
“Alijaribu kusukuma ndani kukawa na mtu naye anazuia mlango…akaamua kufunga komeo kwa nje huku akipiga yowe….watu wakajitokeza ,watuhumiwa wengine wawili waliokuwa nje wakakimbia…ikatolewa amri ajisalimishe akagoma,wakabomoa mlango na kuanza kumshambulia hadi akakata roho”alisema diwani.
Alisema baadhi ya silaha zilizokutwa eneo hilo ni visu na nondo wanazotumia kuvunjia makufuli,hata hivyo alikiri kukithiri kwa vitendo vya wizi wa kubomoa maduka na vibanda vya biashara katika kata hiyo.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa uchunguzi wa awali umekamilika na kuruhusu ndugu waendelee na mazishi,huku wakidai wanaendelea kuwasaka walitoroka .
Mwisho.

MKUU WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUIBA VIFAA MBALIMBALI VYA SHULE,


MKUU WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUIBA VIFAA MBALIMBALI VYA SHULE,
Serengeti:
ALIYEKUWA Mkuu wa shule ya Sekondari Machochwe wilayani Serengeti Epifan John anatuhumiwa kuiba  vifaa  mbalimbali vya shule  ikiwemo laptop,magodoro,madawati,viti vya plastiki na vifaa vingine.
Uongozi wa  kata ya Machochwe ,ofisi ya elimu sekondari,halmashauri na  Mkaguzi wa hesabu wa ndani  umethibitisha kutokea  wizi wa vifaa hivyo.
Kwa mjibu wa ripoti ya mkaguzi iliyothibitishwa na ofisi ya elimu sekondari imebainisha vifaa vilivyopotea kuwa ni viti vya mbao kwenye mabano( 86),na kubaki 44,madawati (98)  yameibiwa na kubaki 153,viti vya plastiki (33 ) kubaki 67 na magodoro (61) na kubaki 107.
Vifaa vingine anavyotuhumiwa kuiba ni komputa mpakato(laptop) zote (6 )zilizotolewa na wafadhili mbalimbali kwa ajili ya watoto kujifunzia,komputa kubwa desk top (1) na kubaki 7,Cpu (5)Monitor (5)Keybod 5 zote zilizokuwepo.
Diwani wa kata hiyo Samweli Gibewa ameiambia blog  kuwa wizi  huo umebainika mwaka jana wakati anahama,huku  Mkuu wa sekondari aliyehamia hapo Emmanuel Mgini akishiriki kuficha ukweli kwa  kusaini makabidhiano vitu ambavyo havipo kwa lengo la kumlinda.
“Niliita bodi ,pamoja na WDC tukakaa na kubaini upotevu wa vitu hivyo… mtuhumiwa akawa hatoi ushirikiano baada ya kuhamishiwa sekondari ya Mbalibali,Mgini alikiri kudanganywa na mwenzake …nikatoa taarifa halmashauri,mkaguzi wa ndani alipotumwa akabaini upotevu huo”anasema  na kuongeza
“Leo(jana )tuna kikao cha WDC nimemwalika Mwenyekiti wa halmashauri maana taarifa ya mkaguzi tunayo sasa …maana suala hili linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu…wazazi wanachangia vitu,walimu wanageuza miradi yao”anasema.
Mwalimu John alipoulizwa alikiri vifaa hivyo kutoweka,”ni kweli havipo lakini viko kwenye nyumba za walimu…vitarudishwa …maana wengine walikuwa masomoni….nikuahidi kuwa vitarudishwa hivyo vifaa maana nimeishapata taarifa ya mkaguzi…nimeitwa kwenye kikao nitawaambia kuwa nitarudisha”alisema.
Alipotakiwa kufafanua ilikuwaje akabidhi vitu ambavyo havipo,na toka mwaka 2012 alipohama ameombwa arudishe bila mafanikio,alisema,”nakwambia vifaa vitarudi baadhi kama magodoro yapo yaliyokwisha “alisema bila kufafanua mangapi yalibaki.
Alipotafutwa siku moja baada ya kikao kutoa ufafanuzi kama amerudisha kama alivyoahidi,alijibu kwa ujumbe mfupi wa simu “kuwa na subira nitakujibu”.
Uchunguzi wa Blog hii umebaini  mwalimu huyo aliandikiwa barua ya kutakiwa kueleza mali hizo zilipo akapewa siku 30 ,hakujibu akaandikiwa barua ya kusudio la kuchukuliwa hatua za kisheria ,lakini akarejesha Laptop 6 mbovu zikakataliwa.
Aidha mkuu wa shule aliyepo Mgini ameazimiwa na kikao cha halmashauri achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushiriki wizi huo kwa kusaini  vitu hewa,hali ambayo inaonyesha walikuwa na dhamira moja.
Uchunguzi zaidi umebaini katika kikao cha kamati ya Uchumi,ardhi na Mazingira ya baraza la madiwani iliyoketi juni 25 mwaka huu imeazimia Mwalimu huyo kuvuliwa madaraka,ndani ya siku 30 awe amerudisha vitu vyote vilivyopotea,au apelekwe mahakamani.
Sekondari ya Machochwe ndiyo inaongoza kwa kuchangia harambee nyingi,na  ilikuwa miongoni mwa shule mbili na Natta zilizoandaliwa kuwa kidato cha tano na sita,na baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kata hiyo kuchukuliwa na Chadema , baraza la madiwani liikabadili uamzi na kuchagua shule zingine ambazo hazikuwa zimeandaliwa .
Wimbi la wakuu wa shule kufuja mali za umma linaendelea kutikisa wilaya hiyo hasa ,hivi karibuni aliyekuwa mkuu wa sekondari Nyambureti Patrick Majige kwa kushirikiana na ofisa elimu sekondari William Makunja walichota sh.mil.9 za ujenzi wa nyumba na haikujengwa,baada ya ukaguzi kubaini alihamishiwa Mugumu sekondari,kisha kusimamishwa.
Hata hivyo baada ya kusimamishwa  aliwasilisha barua ya kustaafu na kupitishwa,huku ofisa aliyeidhinisha fedha za ujenzi wa nyumba kutumiwa kwa posho za safari akiendelea na kazi kama kawaida.
Sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta 6 za vipaumbele ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika semina ya wakuu wa mikoa aliahidi atakaye shindwa kusimamia atafukuzwa kazi.
Mwisho.