Subscribe:

Ads 468x60px

AUAWA BAADA YA KUKUTWA NDANI YA DUKA AKIJARIBU KUIBA.


AUAWA BAADA YA KUKUTWA NDANI YA DUKA AKIJARIBU KUIBA.
Juni 26,2013
Serengeti:
WAKAZI wa kijiji cha Nyamakendo kata ya Machochwe wilaya ya Serengeti wamemuua mkazi mmoja wa kijiji cha Machochwe baada ya kufungiwa ndani ya duka la Mwalimu mkuu shule ya Msingi Manyata katika jaribio la wizi.
Diwani wa kata hiyo Samwel Gibawa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juni 25,2013 majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Manyata ,na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Bageni Mwita Manko(19),akiwa na wenzake wawili  wakiwa wameisha vunja kufuli la duka la Mwalimu Mkuu Manyata Matiko Ryoba kwa nia ya kuiba.
Alisema kabla ya kutokea tukio hilo,Mwalimu Ryoba alifunga duka na kwenda nyumbani kwake,ili kutoa nafasi kwa  vijana wake wanaolala dukani ,hata hivyo alirudi ghafla dukani na wakati anasukuma mlango akabaini uko wazi na kuna mtu kwa ndani.
“Alijaribu kusukuma ndani kukawa na mtu naye anazuia mlango…akaamua kufunga komeo kwa nje huku akipiga yowe….watu wakajitokeza ,watuhumiwa wengine wawili waliokuwa nje wakakimbia…ikatolewa amri ajisalimishe akagoma,wakabomoa mlango na kuanza kumshambulia hadi akakata roho”alisema diwani.
Alisema baadhi ya silaha zilizokutwa eneo hilo ni visu na nondo wanazotumia kuvunjia makufuli,hata hivyo alikiri kukithiri kwa vitendo vya wizi wa kubomoa maduka na vibanda vya biashara katika kata hiyo.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa uchunguzi wa awali umekamilika na kuruhusu ndugu waendelee na mazishi,huku wakidai wanaendelea kuwasaka walitoroka .
Mwisho.