MKUU WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUIBA
VIFAA MBALIMBALI VYA SHULE,
Serengeti:
ALIYEKUWA Mkuu wa shule ya
Sekondari Machochwe wilayani Serengeti Epifan John anatuhumiwa kuiba vifaa mbalimbali vya shule ikiwemo laptop,magodoro,madawati,viti vya
plastiki na vifaa vingine.
Uongozi wa kata ya Machochwe ,ofisi ya elimu
sekondari,halmashauri na Mkaguzi wa
hesabu wa ndani umethibitisha kutokea wizi wa vifaa hivyo.
Kwa mjibu wa ripoti ya mkaguzi
iliyothibitishwa na ofisi ya elimu sekondari imebainisha vifaa vilivyopotea
kuwa ni viti vya mbao kwenye mabano( 86),na kubaki 44,madawati (98) yameibiwa na kubaki 153,viti vya plastiki (33 )
kubaki 67 na magodoro (61) na kubaki 107.
Vifaa vingine anavyotuhumiwa kuiba
ni komputa mpakato(laptop) zote (6 )zilizotolewa na wafadhili mbalimbali kwa
ajili ya watoto kujifunzia,komputa kubwa desk top (1) na kubaki 7,Cpu (5)Monitor
(5)Keybod 5 zote zilizokuwepo.
Diwani wa kata hiyo Samweli
Gibewa ameiambia blog kuwa wizi huo umebainika mwaka jana wakati anahama,huku Mkuu wa sekondari aliyehamia hapo Emmanuel
Mgini akishiriki kuficha ukweli kwa kusaini makabidhiano vitu ambavyo havipo kwa
lengo la kumlinda.
“Niliita bodi ,pamoja na WDC
tukakaa na kubaini upotevu wa vitu hivyo… mtuhumiwa akawa hatoi ushirikiano
baada ya kuhamishiwa sekondari ya Mbalibali,Mgini alikiri kudanganywa na
mwenzake …nikatoa taarifa halmashauri,mkaguzi wa ndani alipotumwa akabaini
upotevu huo”anasema na kuongeza
“Leo(jana )tuna kikao cha WDC
nimemwalika Mwenyekiti wa halmashauri maana taarifa ya mkaguzi tunayo sasa
…maana suala hili linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu…wazazi
wanachangia vitu,walimu wanageuza miradi yao”anasema.
Mwalimu John alipoulizwa alikiri
vifaa hivyo kutoweka,”ni kweli havipo lakini viko kwenye nyumba za walimu…vitarudishwa
…maana wengine walikuwa masomoni….nikuahidi kuwa vitarudishwa hivyo vifaa maana
nimeishapata taarifa ya mkaguzi…nimeitwa kwenye kikao nitawaambia kuwa
nitarudisha”alisema.
Alipotakiwa kufafanua ilikuwaje
akabidhi vitu ambavyo havipo,na toka mwaka 2012 alipohama ameombwa arudishe
bila mafanikio,alisema,”nakwambia vifaa vitarudi baadhi kama magodoro yapo
yaliyokwisha “alisema bila kufafanua mangapi yalibaki.
Alipotafutwa siku moja baada ya
kikao kutoa ufafanuzi kama amerudisha kama alivyoahidi,alijibu kwa ujumbe mfupi
wa simu “kuwa na subira nitakujibu”.
Uchunguzi wa Blog hii umebaini mwalimu huyo aliandikiwa barua ya kutakiwa
kueleza mali hizo zilipo akapewa siku 30 ,hakujibu akaandikiwa barua ya kusudio
la kuchukuliwa hatua za kisheria ,lakini akarejesha Laptop 6 mbovu zikakataliwa.
Aidha mkuu wa shule aliyepo Mgini
ameazimiwa na kikao cha halmashauri achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushiriki
wizi huo kwa kusaini vitu hewa,hali
ambayo inaonyesha walikuwa na dhamira moja.
Uchunguzi zaidi umebaini katika
kikao cha kamati ya Uchumi,ardhi na Mazingira ya baraza la madiwani iliyoketi
juni 25 mwaka huu imeazimia Mwalimu huyo kuvuliwa madaraka,ndani ya siku 30 awe
amerudisha vitu vyote vilivyopotea,au apelekwe mahakamani.
Sekondari ya Machochwe ndiyo
inaongoza kwa kuchangia harambee nyingi,na ilikuwa miongoni mwa shule mbili na Natta zilizoandaliwa
kuwa kidato cha tano na sita,na baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kata hiyo
kuchukuliwa na Chadema , baraza la madiwani liikabadili uamzi na kuchagua shule
zingine ambazo hazikuwa zimeandaliwa .
Wimbi la wakuu wa shule kufuja
mali za umma linaendelea kutikisa wilaya hiyo hasa ,hivi karibuni aliyekuwa
mkuu wa sekondari Nyambureti Patrick Majige kwa kushirikiana na ofisa elimu
sekondari William Makunja walichota sh.mil.9 za ujenzi wa nyumba na
haikujengwa,baada ya ukaguzi kubaini alihamishiwa Mugumu sekondari,kisha
kusimamishwa.
Hata hivyo baada ya kusimamishwa aliwasilisha barua ya kustaafu na
kupitishwa,huku ofisa aliyeidhinisha fedha za ujenzi wa nyumba kutumiwa kwa
posho za safari akiendelea na kazi kama kawaida.
Sekta ya elimu ni miongoni mwa
sekta 6 za vipaumbele ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika semina ya wakuu
wa mikoa aliahidi atakaye shindwa kusimamia atafukuzwa kazi.
Mwisho.