Subscribe:

Ads 468x60px

Marekani yaiweka pabaya Tanzania, yaiita kitovu cha ‘biashara’ ya binadamu



Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba15  2013 
Kwa ufupi
  • Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.

Dar es Salaam. Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai  mwaka huu   na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
“Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na majumbani nchini Tanzania.
“Baadhi ya raia kutoka nchi  jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati,” inaeleza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya baruapepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.
Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.
“Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma. Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa kutoka kwao,” alisema.
Lawama kwa Serikali
Ripoti hiyo inaitupia lawama Tanzania kwa kutokuwa na sheria thabiti za kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu, huku ikitolea mfano namna ilivyoshindwa kuwasaidia raia wake waliokuwa wakinyanyaswa nje ya nchi.
“Kamati ya Serikali ya kupambana na usafirishaji binadamu, haijachukua hatua za kutosha katika kutekeleza mpango mkakati wa kupambana na vitendo hivyo,” inaeleza na kuongeza:
“Serikali imeshindwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa usafirishaji wa binadamu kama ambavyo inaelekezwa kwenye sheria ya kudhibiti biashara hiyo ya 2008.”
Taarifa hiyo inaitaka Tanzania kuongeza nguvu katika kutekeleza sheria ya kudhibiti biashara ya kusafirisha binadamu ya 2008 kwa kuwakamata na kuwashtaki wahusika wote, lakini ikaikosoa kwa kusema inatoa adhabu ndogo kwa mtu anayebainika kufanya makosa, ikiwa ni pamoja na kumhukumu kwenda jela miaka 10, kulipa faini au vyote viwili kwa pamoja.
“Sheria hiyo haifanani na nyingine kama za mtu anayepatikana na kosa la kubaka au kufanya kosa jingine la jinai. Mamlaka imesema ina kesi nne inazozichunguza, saba zipo mahakamani toka mwaka jana, zikiwepo mbili mpya,” inasema ripoti.
Pia, Serikali ya Tanzania imelaumiwa kwa kushindwa kuripoti maendeleo ya uchunguzi wa maofisa wake waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu.
LHRC na TGNP
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema tatizo la usafirishaji wa binadamu pia linachangiwa na wasichana kuwa na tamaa ya maisha mazuri, hivyo kukubali ahadi ambazo hupewa kwamba wanapelekwa kusoma, wasifahamu  wanarubuniwa.
“Wengi wanatamani kwenda ‘majuu’ wakidhani watapata elimu, lakini baadaye wanaingizwa kwenye vitendo vinavyowafedhehesha na kuwafanya wakate tamaa kabisa,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana waliochukuliwa vijijini kwenda mijini kufanya kazi.
Alisema pamoja na tatizo hilo kuongezeka hapa nchini, hakuna tafiti za kutosha ambazo zimefanywa na wadau mbalimbali kuonyesha madhara yaliyopatikana hadi sasa.
“Katika siku za usoni kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya kunyimwa chakula, kupigwa na kufukuzwa kazi huku wasichana wengine wakitumika kwenye biashara ya ngono,” alisema na kuongeza:
“Ripoti hii isiishie kwenye makabrasha bali  ifanyiwe kazi ili jamii yote ijue kuwa hili ni tatizo.”
Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu 47,000 pekee ndio walioweza kuokolewa mwaka jana kutoka kwenye mazingira ya utumikishwaji kati ya milioni 27 waliopo katika hali hiyo duniani.
Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 44 ambazo zinajaribu kupambana na biashara hiyo, lakini hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

ELIMU ,WAZAZI WANAWAJIBIKA KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO

 WAZAZI WAKILA PAMOJA NA WATOTO WAO KATIKA SHULE YA TWIBHOKI WILAYANI SERENGETI
 HAO NI WILBROADS NA ALICE ANTHONY WAKIWA TWIBHOKI
 HAWA NI FRANSISCA NA ALICE ANTHONY KATIKA MAZINGIRA YA SHULE
HAPO NI MSOSI NA KUULIZANA MAENDELEO YA TAALUMA KATI YA WAZAZI NA WANAFUNZI.

Kijazi awapa somo wabeba mizigo Kilimanjaro



  


na Grace Macha, Moshi

   





MKURUGENZI Mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini, (TANAPA), Allan Kijazi, amewataka wapagazi wanaosaidia kubeba mizigo ya watalii kwenye  Mlima Kilimanjaro kuhakikisha wanatunza mazingira ya mlima huo kwani ukiharibika na wao wataathirika kwa kukosa ajira.
 Aidha, alisema atawasiliana na wadau wa utalii ili kuona namna ya kuboresha utendaji wao kwa kuwatafutia ziara ya mafunzo kwenye moja ya nchi zenye milima mirefu.
 Aliyasema hayo jana wakati akifungua kongamano la kwanza la Chama Cha Wapagazi nchini (TPO) lililofanyika kwenye ukumbi wa YMCA ambalo lilikuwa likijadili changamoto wanazokabiliana nazo na namna ya kuzitatua.
 Kijazi alisema kuwa kwenye kongamano lao hilo mbali ya kujadili changamoto zinazowakabili ni vema wakaangalia namna ya kuutunza mlima huo ambao unawapatia ajira.
 “Kuna malalamiko yanakuja kuwa wakati mwingine nyie mnaacha taka huko mlimani kwa kushindwa kuzikusanya vizuri, ni vema mkautunza mlima huu kwani ukipoteza sifa na hadhi yake wageni wataacha kuja na nyie mtakosa ajira,” alisisitiza mkurugenzi mkuu huyo wa Tanapa.
Aliwataka viongozi wa TPO kujenga mfumo wa kufuatilia mienendo ya wanachama wao ili kuona kama wanafuata taratibu na maadili waliyojiwekea, kwani kuna wakati yanaibuka malalamiko kuwa kuna baadhi ya wapagazi si waaminifu na wengine hawazingatii uvaaji sahihi, jambo linalohatarisha usalama wa afya zao.
 Kijazi alisema kuwa anaangalia uwezekano wa kukutana na wadau wa utalii wanaoendesha shughuli kwenye mlima huo wakiwemo Chama cha Waongoza Watalii kwenye mlima huo, KIATO, na Wizara ya Maliasili na Utalii ili waweze kuona namna sheria zilizowekwa hasa kwenye udhibiti wa uzito wa mizigo zitakavyosimamiwa kwa ukaribu zaidi.
 Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, TPO, Richard Kessy, alisema changamoto kubwa zinazowakabili wapagazi ni kampuni za uwakala wa utalii  kubebeshwa mizigo mizito zaidi ya kiwango kilichowekwa na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ambacho ni kilogramu 20.
 “Wapagazi wakiwa huko mlimani kuna wengine wanapewa chakula mara moja kwa siku, wengine wanapewa mara mbili lakini kidogo sana ukinganisha na kazi ngumu ya kubeba mizigo yao na ya watalii wanayoifanya,” alisema Kessy.
 Naye Mwenyekiti wa TPO, Philip Mbise, alisema kuwa wana wanachama 2,820, ambapo kongamano hilo la siku moja limehudhuriwa na wapagazi 250 kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

WAZOA TAKA MJI MDOGO WA MUGUMU SERENGETI HATARINI KUAMBUKIZWA MAGONJWA YA MLIPUKO

 MIKAKATI MIZURI YA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA MUGUMU WILAYANI SERENGETI KUONDOA TAKA MJINI,ZINAELEKEA KUSABABISHA MADHARA KWA VIBARUA HAO KUTOKANA NA MAMLAKA HIYO KUTOWAPA VIFAA MAALUM VYA KUJIKINGA WAFANYAPO HIYO KAZI,AMBAPO BAADHI WANASHIKA UCHAFU BILA VYOMBO VYA KUJIKINGA
 VIBARUAWAKIWA KAZINI,HATA HIVYO WANALALAMIKIAUJIRA MDOGO UKILINGANISHA NA KAZI WAIFANYAYO.




MAMA HUYO HANA GLOVUS LAKINI ANAENDELEA NA KAZI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

Matokeo darasa la saba; Ufaulu waongezeka



 Na Fredy Azzah, Mwananchi

Posted  Jumapili,Novemba3  2013 
Kwa ufupi
  • Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.
Dar es Salaam. Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.
Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa, wanafunzi wengi wamefanya vibaya zaidi kwenye somo la Hisabati huku wakifanya vizuri kwenye somo la Kiswahili.
Dk Msonde alisema wavulana wamefanya vizuri zaidi kwenye mtihani huo ukilinganisha na wasichana.
Alieleza pia kuwa, mwaka huu udanganyifu kwenye mtihani huo umeshuka kwa kiasi kikubwa, kwani waliofutiwa matokeo ni 13.
Dk Msonde alisema kati ya hao, watano walibainika kukariri mtihani huo jambo ambalo kisheria hawaruhusiwi na wengine walikamatwa na karatasi za majibu kwenye vyumba vya mtihani.
Ufaulu
Alisema miongoni mwa waliofaulu, wenye ulemavu ni 476, kati yao wasichana wakiwa ni 219 sawa na asilimia 46.01 na wavulana ni 257 sawa na asilimia 53.99.
Dk Msonge alisema kuwa, mwaka 2012 watahiniwa waliopata zaidi ya alama 100 walikuwa ni asilimia 30.72, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 19.89.
Kuhusu sababu za ongezeko la ufaulu, Dk Msonde alisema baraza bado halijafanya tathmini ya kubaini chanzo cha ongezeko hilo.
isi tulicholetewa ni kile kilichofanyika kwenye chumba cha mtihani na haya hapa ndiyo majibu yake,” alisema Dk Msonde.
Ufaulu kimasomo
Alisema mwaka huu ufaulu kwa masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya sita mpaka 28.06, ikilinganishwa na mwaka 2012.
Somo ambalo watahiniwa wengi wamefanya vizuri ni Kiswahili ambalo ufaulu wake umefikia asilimia 69.62 na walilofeli zaidi ni Hisabati ambalo ufaulu wake ni asilimia 28.62.
Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka 2012 ufaulu kwenye somo la Kiswahili ulikuwa ni asilimia 41.00 na Hisabati ulikuwa ni asilimia 18.74.
Kwenye somo la Kiingereza ufaulu mwaka huu ni asilimia 35.52 wakati mwaka jana ilikuwa ni asilimia 21.06, huku kwa Sayansi mwaka huu ufaulu ukiwa ni asilimia 47.49 na mwaka jana ilikuwa ni asilimia 41.48 na Maarifa ya Jamii mwaka huu ufaulu ni asilimia 53 na mwaka jana ilikuwa asilimia 28.61.
Usahihishaji wa mashine ni bora zaidi
Alisema ili kujiridhisha na usahihishaji wa kutumia Mashine Maalumu za OMR (Optical Mark Reader), sampuli 20,795 za karatasi za majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 za mikoa tisa ya Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga zilisahihishwa kwa mkono.
Alisema baada ya kufanya ulinganifu wa usahihi wa karatasi zilizosahihishwa kwa mkono na zile zilizosahihishwa kwa mashine, ilibainika kuwa zile zilizosahihishwa kwa mashine zilikuwa na usahihi wa hali ya juu.
“Usahihishaji wa kutumia kalamu ulikuwa na makosa machache ya kibinadamu, makosa hayo yalikuwa ya kukosea kusahihisha swali kwa kutumia mwongozo wa usahihishaji na dosari za kujumlisha alama,” alisema Dk Msonde.
Alibainisha kuwa, kati ya sampuli za karatasi za watahiniwa 20,795 zilizosahihishwa kwa mkono, 249 sawa na asilimia 1.2 ndizo zilizobainika kuwa na makosa aliyosema ni ya kibinadamu.
Mbali na usahihi wa usahihishaji, alisema pia mfumo huo umesaidia kupunguza wasahihishaji kutoka 4,000 waliokuwa wakitumika awali na kufikia 301 waliofanya shughuli hiyo mwaka huu.
Alibainisha pia kuwa, OMR imepunguza siku za kusahihisha mtihani huo kutoka 30 za awali mpaka 16 zilizotumika mwaka huu.
Waliofanya mtihani
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa ni 867,982 wakiwamo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.
Alieleza kuwa, kati ya watahiniwa hao walikuwemo wenye ulemavu wa kuona, 597 walikuwa na uono hafifu na wengine 88 ni wasioona.
“Watahiniwa 844,938 sawa na asilimia 97.34 ya waliosajiliwa walifanya mtihani huo. Wasichana walikuwa 446,115 sawa na asilimia 99.85 na wavulana walikuwa 398,823 sawa na asilimia 96.78,” alisema Dk Msonde.
Alisema kuwa, watahiniwa ambao walisajiliwa na hawakufanya mtihani huo ni 23,045 sawa na asilimia 2.66, kati yao wasichana wakiwa 9,781 sawa na asilimia 2.15 na wavulana 13,264 sawa na asilimia 3.22.
Alieleza kuwa utoro na ugonjwa ni miongoni mwa sababu za wanafunzi hao kutofanya mtihani huo.
Lengo la BRN halijafikiwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa akizungumza katika warsha ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN-Big Results Now), kwenye sekta ya elimu iliyotolewa kwa watendaji wa elimu ngazi ya kanda, mkoa na wilaya, Agosti 14, mwaka huu, alisema moja ya lengo la mpango huo ni ufaulu kwa darasa la saba mwaka huu kufikia asilimia 60 kutoka 31 ya mwaka jana.
“Katika kutekeleza vipaumbele hivyo, kila mmoja wenu atakuwa na eneo la kutekeleza na atapimwa kutokana na utekelezaji katika eneo lake, hii ni katika kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka huu ufaulu katika elimu ya msingi unaongezeka kutoka asilimia 31 hadi kufikia 60,” alisema Dk Kawambwa.
Mara baada ya Dk Kawambwa kutangaza suala hilo, baadhi ya wadau walisema itaongeza hali ya kupata matokeo yasiyo halisi kwani hakukuwa na muda wa kuandaa mikakati ya kufikia lengo hilo, kwani mpango huo ulitangazwa Agosti na Septemba watoto wa darasa la saba walikuwa wanaanza mitihani.

Kenyan MPs pass harsh media law


The East Africa News

Kenyan Parliament during a past session. Kenyan MPs have passed a new draconian media law that imposes harsh penalties on Journalists 
By John Ngirachu, The Citizen

Posted  Saturday, November 2  2013 
In Summary
  • Journalists now face punitive measures for violating the Code of Conduct for journalists, including fines of up to Sh20 million.
Nairobi. Kenyan parliament has passed a new draconian media law that imposes harsh penalties on journalists.
Journalists now face punitive measures for violating the Code of Conduct for journalists, including fines of up to Sh20 million.
They also risk being deregistered and their bank accounts frozen.
MPs Thursday evening voted to create a tribunal that will handle complaints against the media and have power to impose the harsh penalties.
This happened through the introduction of a surprise change to the Kenya Information and Communication Bill, which was passed last evening with 17 per cent of MPs (60) present in the chambers in the National Assembly.
The House accepted a proposal by the Energy, Information and Communication Committee for the creation of Communications and Multimedia Appeals Tribunal.
The Tribunal would have the power to “impose a fine of not more than Sh20 million on any respondent media enterprise…adjudged to have violated either that law or the Code of Conduct for the Practice of Journalism.”
It has the power to fine individual journalists “not more than Sh1 million” for violating the same code.
It would also get worse because the fine would be a debt, meaning the person or organisation found to have broken the law would be liable to have his bank accounts raided or their property sold off for misreporting.
The tribunal also has the power to “recommend the suspension or removal from the register of the journalist involved.”
It has also been granted the power to make any orders it feels would be necessary to carry into effect the orders or directives it would make. Proposed by Energy Committee chairman Jamleck Kamau, the creation of this tribunal was among amendments introduced with a mere 28 MPs in the chambers.
Only a handful shouted aye when the vote was called for but the fact that there was no one in opposition was taken as evidence that all were in agreement.
As they were going through the amendments, Majority Leader Aden Dualle and Mr Kamau detected that the Bill was not going to be passed without the quorum of 50 MPs and they rushed out to get the rest to come in.
“This is a controversial and good law but the members are not here. This House is more full when passing other Bills,” Mr Dualle would later say.
After that, the 32 who hadn’t been in the House came in and helped bring the numbers up to 60 and then Speaker Justin Muturi called for the verbal vote, the ayes had it and the Bill was passed.

MIKAKATI YA MATOKEO MAKUBWA SASA


BRN imezinduliwa agosti 14 mwaka  huu.
 1. Upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza hadi ya mwisho. Lengo la mkakati huu ni kuongeza uwajibikaji na ushiriki wa jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora.

2. Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi.

3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule kutekeleza majukumu yao kikamilifu

4. Upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata

5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili. Mafunzo atatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.

6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.

7. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu shuleni.

8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.

9. Utoaji wa motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.

Wasomi wadai mabadiliko mitihani ya sekondari ni siasa tu




Na Fredy Azzah, Mwananchi

Posted  Novemba2  2013 
Kwa ufupi
  • Baadhi ya wadau hao wakizungumza na gazeti hili jana, walisema Tanzania imeweka rekodi kwa nchi za Afrika kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha ufaulu cha alama F kuanzia 0 mpaka 19.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Serikali kutangaza kupunguza viwango vya ufaulu kwa mtihani ya kidato cha nne na sita, baadhi ya wasomi na wadau wa elimu wameponda uamuzi huo na kusema una malengo ya kisiasa.
Baadhi ya wadau hao wakizungumza na gazeti hili jana, walisema Tanzania imeweka rekodi kwa nchi za Afrika kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha ufaulu cha alama F kuanzia 0 mpaka 19.
Walisema, Serikali imechukua uamuzi huo kisiasa ili kuhakikisha kuwa, wanatimiza lengo la Mpango wa Maendeleo Makubwa Sasa (BRN), ambalo ni kuhakikisha matokeo ya ufaulu kwa Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu yanafikia asilimia 60 kutoka 33 ya mwaka jana.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Herme Mosha alisema kuwa kilichofanywa na Serikali ni kupanua wigo wa watu kufaulu.
“Wanataka watu ambao walikuwa wanapata daraja la nne wapate daraja la tatu, daraja la tatu wapate la pili na la pili wapate la kwanza.
Hata hivyo, kwa muda wote, wadau wa elimu ambao wanataka siyo kuona tu watu wanafaulu, wanataka elimu iliyo bora. Kwa hatua hii waliyoichukua haitasaidia lolote katika kuongeza ubora wa elimu ambao umekuwa kilio cha muda mrefu,” alisema Profesa Mosha.
Alisema kuwa, washikadau wengi wangependa kuona ubora wa elimu umeongezeka na siyo kuongeza wigo wa ufaulu.
“Huku ni kujidanganya, jambo la kwanza wangetakiwa waende katika shule mbalimbali waone ni nini walimu wanataka, tatizo lipo wapi halafu wachukue hatua kwa sababu ukiangalia sasa ni kama kuna mgomo fulani hivi,” alisema.
Kwa upande wake Dk Kitila Mkumbo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Saikolojia ya Elimu na Masomo ya Mitalaa ya Shule Kuu ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema tatizo la elimu Tanzania halijawahi kuwa ni viwango vya ufaulu.
“Wanataka tu kuona hiyo asilimia 60 waliyojipangia inafikiwa. Walijiwekea lengo hilo wakijua kabisa kwenye elimu hakuna miujiza, lazima mtu ufanye kazi ndiyo matokeo yaonekane,” alisema.
Alisema kiwango cha kufeli kilichowekwa kinaifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwango vidogo sana vya elimu kwenye bara hili.
“Burundi wenyewe mtoto akipata 50 ndiyo anakuwa amefeli, sisi huku tumeweka mpaka 19 ndiyo tunasema amepata hiyo F, lakini bado tunaita amefaulu, huu ni utani,” alisema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekia Oluoch alisema Matumizi ya Alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA) ni suala la kupongeza.
Hata hivyo, alisema kuwa kuna matatizo ya msingi kwenye elimu na ni lazima yafanyiwe kazi.
“Lengo lao la kushusha ufaulu ni ili ionekane kuwa BRN imefikia lengo, watoto wamefaulu ndiyo iwe furaha yao,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema wamepokea suala hilo kwa mikono miwili.
“Zamani mtu alikuwa amapata sifuri na mwingine 33 wote tunasema wamepata F, lakini sasa kuna utofauti kwa hiyo unaweza kuona ni namna gani uwatumie hawa watu.
Pia suala hili linatoa mwanya mpana hata kwa Serikali na taasisi nyingine za elimu, ikitokea kwamba watu wa C wamekosekana unaweza kuona sasa tutumie wapi,” alisema.
Alisema kuwa, kwa sasa sera ya elimu inasema watu watakaoingia kidato cha tano wanatakiwa wawe na C tatu, lakini mwaka huu Serikali ilichukua C moja na D mbili wakaenda kidato cha tano.
“Yote hii ni kwa sababu hakukuwa na njia mbadala, lakini kwa sasa kutakuwa na mianya mingi sana.
Hata hivyo, tujue kuwa, tatizo la elimu Tanzania halikuwa madaraja, hii ilikuwa ni sehemu tu, lazima tuhakikishe tunatafuta matatizo ya msingi ya elimu yetu tuyafanyie kazi. Tukibaki kwenye hizi alama, basi nchi yetu itakwenda shimoni,” alisema.


Polisi mbaroni kwa kupora Sh220 mil


Na Daniel Mjema,Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba1  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi

Wadaiwa kuwa wamesharejesha Sh80 milioni baada ya kubanwa na makachero wa polisi.

Moshi. Askari polisi wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kula njama na kushiriki katika uporaji wa Sh220 milioni za Kampuni ya Dot Services ya mjini Moshi.

Habari za uhakika zilisema baada ya kubanwa na makachero, askari hao walirejesha Sh60 milioni na watuhumiwa wengine wawili ambao ni raia, walirejesha Sh23 milioni. Askari hao ni wale walioko katika Kikosi cha Polisi wa doria wanaotumia pikipiki na jana watuhumiwa wote walitawanywa katika vituo mbalimbali ili wahojiwe kwa nyakati tofauti tofauti.

Habari za kipolisi zilisema askari hao hawakwenda eneo la tukio lakini walifahamu mpango mzima kuhusu uporaji huo uliowawezesha kupata mgawo wa fedha hizo.

Waliotiwa mbaroni wana vyeo vya Constable (majina tunayo) na inaelezwa kuwa tukio hilo limewachukiza baadhi ya polisi wakidai ni kuwa mfululizo wa matukio yanayochafua sura ya jeshi hilo.

Habari hizo zimebainisha kuwa tukio hilo ni mpango mahususi uliowashirikisha watu wasiopungua 10 wakiwamo baadhi ya watumishi wa Kampuni ya Dot Services waliovujisha mpango wa kuhamisha fedha hizo.

Kulingana na vyanzo vya habari, idadi ya walioshiriki katika mpango wa kupora fedha hizo ni kati ya watu wanane na 10 na tayari polisi wameanzisha msako mkali wa kuwatafuta.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alikaririwa akisema kuwa fedha hizo ziliporwa Jumanne asubuhi katika makutano ya Barabara za Arusha na Boma mjini Moshi.

Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, baada ya kufika katika makutano hayo, wafanyakazi wa Kampuni ya Dot Services waliokuwa na gari aina ya Toyota Hilux T.864 AZM walisimama kuruhusu pikipiki ipite.

Kamanda Boaz alisema wakati wakisubiri pikipiki ipite, ghafla walijitokeza watu wawili wakafungua milango na kuingia ndani ya gari na kuwateka wafanyakazi na kuwaamuru waelekee eneo la Shanty Town.

Hata hivyo mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo ya ujenzi yenye makao yake makuu nchini Uganda, Shuresh Bab alifanikiwa kuruka kwenye gari hilo na kutoa taarifa polisi.
Kamanda Boaz alifafanua kuwa msako wa kuwatafuta wahusika ulianza mara moja ambapo polisi walifanikiwa kulipata gari hilo na wafanyakazi wakiwa wametelekezwa mto Karanga mjini Moshi.

Mabadiliko makubwa mitihani ya sekondari


Posted  Ijumaa,Novemba1  2013 

Kwa ufupi
Akifafanua zaidi juu ya alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA), alisema kuwa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 inayotumika mpaka sasa inataka alama hizo ziwe 50 na zile za mtihani wa mwisho ziwe 50.

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuanza mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu, Serikali imepunguza alama za ufaulu kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.
Pia imetangaza kuwa, mtihani wa taifa wa kidato cha nne na sita utakuwa na alama 60 za ufaulu, huku alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za maendeleo ya mwanafunzi shuleni (CA).
Katika mfumo huo mpya, wizara hiyo pia imefuta daraja la sifuri na badala yake kutakuwa na daraja la tano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alitangaza uamuzi huo wa Serikali jana kwa kueleza utekelezaji wa utaratibu huo utaanza kwenye mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka huu.
“Hatua hii imechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza kuanzia mwaka 2011. Tangu wakati huo kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika,” alisema Profesa Mchome.
Alisema kuwa, alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) katika kupanga matokeo hayo, kwa kidato cha nne ni A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F= 0-34 kwa upande wa kidato cha sita A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alisema mfumo mpya, umehusisha alama za kidato cha nne na cha sita na kuwa kuanzia sasa A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19.
“Alama A itakuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ itakuwa ni ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha kabisa,” alisema Profesa Mchome.
Alisema pia kuwa, wamebadilisha mfumo wa madaraja ambao awali kulikuwa na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne na sifuri.
“Lile la sifuri tumeliondoa, badala yake kutakuwa na daraja la tano, lengo ni kuweka mlolongo mzuri zaidi,” alisema.
Alisema, alama hizo zitakuwa ni mgando (fixed grade range).
Profesa Mchome alisema kuwa, utaratibu wa sasa wa kupanga matokeo hayo kwa madaraja, utabadilika muda wowote kuanzia sasa na kwamba utakaokuwa ukitumika ni ule wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Point Average ‘GPA’).
Mfumo huu kwa sasa unatumika kwenye ngazi za vyuo. “Huu mfumo wa madaraja unaotumika sasa ni wa mpito tu, mwakani ama hata kabla ya hapo tunaweza kuanza kutumia mfumo wa GPA,” alisema.
Akifafanua zaidi juu ya alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA), alisema kuwa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 inayotumika mpaka sasa inataka alama hizo ziwe 50 na zile za mtihani wa mwisho ziwe 50.
Kwa upande wa Zanzibar, alisema CA ilikuwa alama 40 na mtihani wa mwisho alama 60, ingawa alisema utaratibu huo haukuwahi kutumika kwa Zanzibar wala Bara.
Aliongeza kuwa hali hiyo ilisababishwa na kutokuwa na utaratibu wa kupata alama sahihi alizopata mwanafunzi shuleni kwani walimu wengi wamekuwa wakituma alama za uongo kwa kuwaongezea wanafunzi alama.
Alisema, utaratibu mpya wa kupata CA itakuwa ni mtihani wa kidato cha pili utachangia alama 15 mitihani ya mihula miwili ya kidato cha tatu kila muhula utachangia alama tano, Mtihani wa Kanda wa kidato cha nne alama 10 huku kazi mradi (project) zikitoa alama tano.
“CA zitatumika pia kwa watahiniwa wa kujitegemea, zile CA zao ambazo walimaliza nazo kidato cha nne hazitatupwa, wakitaka kurudia mtihani hizo alama zao zitajumlishwa kwenye mtihani wa mwisho.
Hata hivyo, alisema kuwa, kwa kuwa tayari shule nyingi zimeshawasilisha CA Baraza la Mitihani, alama 40 kwa mwaka huu zitapatikana tu kwa kuangalia alama hizo zilizopelekwa na shule ambazo hupatikana kwa kuangalia mitihani ya mihula kuanzia ule wa kidato cha kwanza. Kwa wale waliofanya mtihani wa QT (Qualifying Test), alama zao hizo za QT zitachukuliwa 40 kuongezwa kwenye mtihani wa kidato cha nne,” alisema Profesa Mchome.
Alisema kuwa, mfumo huo mpya hautabadilika mara kwa mara na kuwa, utamaliza mzunguko mmoja ambao ni wa miaka minne.

Kidato cha nne kuanza mitihani
Katika hatua nyingine Profesa Mchome alisema, Novemba nne wanafunzi wa Kidato cha nne nchi nzima wataanza mitihani yao ya mwisho ambayo wataimaliza Novemba 21.
“Mitihani hiyo imetanguliwa na ile ya vitendo ya masomo ya Food and Nutrition iliyofanyika Oktoba 7, mpaka 24 mwaka 2013,” alisema.
Alisema kuwa, watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani huo ni 427,906 ambao kati yao 367,399 ni watahiniwa wa shule na 60,507 ni watahiniwa wa kujitegemea.
Alisema kuwa, kati ya watahiniwa wa shule 367,399 wavulana ni 198,257 sawa na asilimia 53.96 na wasichana ni 169,142 sawa na asilimia 46.04.
Alisema kuwa, kati ya watahiniwa 60,507 wa kujitegemea walioandikishwa, wanaume ni 30,456 sawa na asilimia 50.33 na wasichana ni 30,051 sawa na asilimia 49.67.
Alisema kuwa, watakaofanya Mtihani wa Maarifa (QT) walioandikishwa ni 18,214, kati yao wavulana ni 7,222 sawa na asilimia 39.65 na wasichana ni 10,992 sawa na asilimia 60.35 .
Wadau
Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Habari na Utetezi, Nyanda Shuli alisema anaipongeza wizara kwa kuamua kutumia CA ingawa alisema ni lazima kuwe na mfumo wa kuhakikisha alama hizo zinaonyesha uwezo halisi wa mwanafunzi.
Kuhusu kushusha kiwango cha ufaulu, alisema kuwa Serikali inapaswa kutoa sababu iliyoifanya kuchukua hatua hiyo.
“Kama wanahofia jinsi matokeo ya mwaka jana yalivyokuwa siyo sahihi, dawa ni kufundisha kwa makini zaidi,” alisema Nyanda.
Dk Joyce Ndalichako
Katika mahojiano, ambayo Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, aliwahi kufanya na gazeti hili, alisema ni vigumu kutumia alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA) kwani kwa kiasi kikubwa walimu hudanganya.
“Wafanyakazi wa baraza ni wachache, hatuwezi kwenda kila mahali ili tuhakikishe alama hizo, mwaka 2011 wale wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka kwenye mitihani yao ya mwisho, kwenye CA walikuwa wana mpaka alama 75.
Tulipowauliza walimu wengine walisema hawakuwa na walimu waajiriwa wa Serikali na waliokuwa wanawatumia ni wale waliomaliza kidato cha sita kwa hiyo hawajui kupanga hizo alama, wengine walisema mitihani hiyo haina usimamizi makini,” alisema Dk Ndalichako