wanafunzi wa shule ya msingi Kisangura Serengeti wakifunga kuku walionunuliwa kwa ajili ya hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ,chini ya ufadhili wa New York Yearly Meeting la Marekani kwa usimamizi wa shirika la Zinduka la wilayani Bunda
Tunakufunga usitoroke usubiri kuchinjwa ,ndivyo inavyoonekana wanafunzi hawa wanasema huku wakiwafunga kuku kwa kamba wasijetoroka wasubiri kuchinjwa
|
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kisangura wilaya ya Serengeti wakiwa shuleni,huku baadhi yao wakisiburi kupokea msaada wa vifaa mbalimbali wanavyogawiwa kila mwaka kwa ufadhili wa kamati ya New York ya Marekani ,kwa usimamizi wa shirika la Zinduka lenye makao Makuu yake Nyamuswa wilayani Bunda,, |
|
Mmoja wa wanafunzi wa darasa la pili akipokea msaada wa vitu ,mbalimbali,ikiwemo sare mbili,viatu,soksi,kalamu,madaftari,na vitabu vya kiada na ziada ,msaada huo uelekezwa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu zaidi.jumla ya wanafunzi 125 wa shule ya msingi na sekondari Kisangura wamenufaika na msaada huo wenye thamani ya sh.mil.24,hata hivyo wafadhili wamekata misaada ya kulipia masomo ya elimu ya juu na ujenzi kufuatia wasimamizi kufanya ufisadi wa miradi hiyo. |