Subscribe:

Ads 468x60px

MAHAFALI TWIBHOKI PRE PRIMARY-SERENGETI

MAANDAMANO YA KUINGIA UKUMBINI
WA KWANZA KULIA NI WILBROAD ANTHONY MAYUNGA

WILBROAD AKIONGOZA MAANDAMANO YA KUINGIA UKUMBINI
MAMBO YANAZIDI KUNOGA
HUYO NDIYE MAYUNGA JUNIORAdd caption

MAMA YAKE AKIMPONGEZA KIJANA WAKE
HONGERA MWANANGU KWA KUHITIMU NA KUIBUKA BINGWA WA TAALUMANI MANENO KUTOKA KWA MAMA YAKE
HONGERA NA PONGEZI HAZIKUACHANA


HUYO NI MDOGO WAKE NA WILBROAD ANAITWA FRANSISCA ANTHONY MAYUNGA AKISHUHUDIA HUKU NAYE AKIAHIDI KUFUATA NYAYO ZA KAKA YAKE MWAKA KESHO

KAKA NIMEKUKUBALI NI MANENO YA FRANSISCA

FRANSISCA AKIWA MENEJA WA MJADALA WAKATI WAKIONYESHA WAGENI WAALIKWA KUWA WANAWEZA ,
MJADALA UNAENDELEA MENEJA ANAUSIMAMIA VILIVYO
NI WAKATI MUAFAKA WA KUJALI AFYA WILBROAD ANAONGOZA WENZAKE
WAKATI MWINGINE HUAMUA KUPOOZI KAMA ALIVYO NASWA NA BLOG HII

WWAZAZI MBALIMBALI WALIKUWEPO KUWAPONGEZA WATOTO WAO

WWILBROAD ANAPOKEA CHETI CHA KUHITIMU PIA ALIPEWA CHETI CHA TAALUMA (HISTORY
KKAKA POKEA ZAWADI KUMBUKA MWAKANI NAMI MUNGU AKIJAALIA UJE UNITUZE,FRANSISCA AKIMWAMBIA KAKA YAKE
WILBROAD AKIWA NA MAMA YAKE NA MDOGO WAKE WA MWISHO ALICE AMBAYE ALIFIKA KUSHUHUDIA MAHAFALI YA KAKA YAKE.ption


HHONGERA WILBROAD

WAANDISHI WANOLEWA

 Amani Mustafa Mhinda akitoa mada ya Extractive Reseorce Governance Challenge and Policy Choices kwa wahariri wa habari na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa TMF Dar es Salaam
 Said Mmanga wa Changamoto akifuatilia mada
 Jamal Hashimu wa Tbc 1 akisikiliza kwa makini
 hapo tunafuatilia mada kwa makini ili kupata uwezo wa kufuatilia masuala mbalimbali
 Usikivu ni mmoja ya nguzo ya uelewa
John Bwire wa Raia Mwema ni miongoni mwa magwiji wanaojengewa uwezo wa masuala mbalmbali ya uchimbaji wa mafuta na madini

INTERNATIONAL CONFERENCE BOT


WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKTIKA PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WALIOWASILISHA UJUMBE KWA NJIA YA NYIMBO KUHUSU SERIKALI INAVYOUZA NCHI KWA WAGENI,KWENYE INTERNATIONAL CONFERENCE  KUHUSU LAND JUSTICE FOR SUSTINABLE PEACE IN TANZANIA UKUMBI WA BOT DSM
 WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ,KULIA KWAKE NI RAIS MSTAFU BENJAMINI MKAPA,WAZIRI WA ARDHI NA MAKAZI PROF.ANNA TIBAIJUKA ,KUSHOTO NI ASKOFU DR PETER MANGU,NA WACHUNGAJI NA WATAFITI
 HAPO KILA MMOJA ANABADILISHANA MAWAZO NA MWENZAKE
 MJADALA UNAENDELEA KILA MMOJA ANAFUATILIA
HAPA NI KUKUMBUSHANA HABARI ZA SIKU

UTALII NA MICHEZO

 VINYAGO VINGI NA VYA KISASA UNAVIPATA CULTURAL HERITAGE ARUSHA
 VINYAGO
 NAIBU KATIBU MKUU WA JOURNO TOURISM AKIWA CULTURAL HERITAGE
 WATALII WENGI HUFIKA HAPO KUNUNUA VINYAGO




 KATIBU WA TASWA MKOA WA ARUSHA MUSSA JUMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA DAR NA MANYARA WATAOSHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI JIJINI ARUSHA SEPT 8 MWAKA HUU KWENYE VIWANHA VYA GENERAL TYRE


 HAPO NI PALACE HOTEL VIONGOZI WA TASWA ARUSHA NA WADHAMINI WA BONANZA WAKIELEZA YATAKAYOJIRI SEPTEMBA 8 MWAKA HUU


HONGERA WIILY


 Willbroad akipongezwa kwa kufikisha miaka 12 ya kuzaliwa pia akiagwa na familia kwa ajili ya kurudi shule Twibhoki Pre English ambapo atakuwa miongoni mwa wanafunzi watakaofanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba septe 11,12 mwaka huu,Mungu azidi kumkirimia hekima,na afya azidi kukua na kumfungulia njia kwa yaliyo mema.
h





MAHAFALI YA HUDUMA YA INJILI SHULENI

LEOKADIA AKILISHWA KEKI NA SHANGAZI YAKE AMBAYE NI MYA WIFE
LEOKADIA AKIWA NA ALICE LAST BORN WETU SIKU YA MAHAFALI YAO YA KIDATO CHA NNE
WATOTO WANGU WALIKUWA MASHUHUDA

HAPO WANAMPA ZAWADI

MICHUANO YA MARA DAY YAANZA

TIMUza Mugumu Star na Polisi Serengeti zimetoka sare baada ya kufungana goli 1-1 katika mchezo wa kuwania kikombe cha Mara day ,maadhimisho yatakayofanyika wilayani Serengeti mkoa wa Mara kuanzia septemba 9-15 siku ya kilele ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Ghalib Bilal.

Katika mchezo wa leo uliofanyika uwanja wa Sokoine ulihudhuriwa na watazamaji wengi,mashambulizi yalikuwa ya kila upande .lakini timu ya polisi inayoundwa na vijana wadogo ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa mshambuliaji mahiri Kessy Dyson dakika ya 35 kipindi cha pili.

Hata hivyo Mugumu Star timu inayoundwa na wachezaji wakongwe walizinduka na kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 2 kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wake Malima Chisumo.

Hata hivyo kutokufahamu sheria za mpira wa miguu ni mambo yaliyoonekana wazi kutoka kwa waamuzi wa mpambano wa leo ,hali iliyoibia kelele kutoka kwa washabiki na wachezaji.

RAIS KENYATTA AZIDI KUWAPA UTAJIRISHO WANANCHI WA KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema licha ya wakazi wa Taita Taveta kutompigia kura lakini kwa kuwa aliahidi Wakenya kuwa akishinda atashughulikia tatizo la ardhi,ameanza na mkoa huo wa Pwani kwa kutoa hati za kumiliki ardhi ili kuhakikisha wananchi wanapambana na umaskini.

"Najua hamkunipigia kura ...wala hiyo si uongo...mlichagua watu tofauti na chama ya Jubillee ...hiyo ni haki yenu...sisi tuliahidi wakenya ..hivyo nimeanza na mkoa huu kugawa hati ...maana ardhi ni maisha ...ili tuondokane na umaskini lazima tutekeleze ahadi zetu.....nataka baada ya miaka mitano watu mil.3 wamepata hati kwa gharama za serikali....hii nafunga mjadala wa watu kuja kuomba kura kwa matatizo ya ardhi waje na mambo mengine"amesema.

Amesema wanataka kubadilisha maisha ya Wakenya kwa kutimiza ahadi walizoahidi,"ni miezi mitatu toka tumeanza kazi...na tumeanzia mkoa wa Pwani maana matatizo yake yanajulikana,nimemwambia Waziri wa ardhi kuhakikisha anaandaa hati zaidi ...leo nakabidhi 19,103 ...lazima tuwatumikie watu wetu bila kuangalia yeye ni chama gani maana wote tumechaguliwa na Wakenya na tujenge Kenya yetu"anasema Rais.

Makamu wa Rais William Ruto amesema mkoa huo una neema ya Madini,na maliasili hivyo wamepeleka sheria bungeni ambayo itasaidia wananchi kunufaika na madini ,na kuwa wananchi watakuwa wanufaika wa kwanza,jimbo na serikali kuu.

"Suala la Ujangili tutahakikisha tunaumaliza kabisa ..kwenye bajeti tumetenga ksh,mil.770 kwa ajili ya utalii...tutafanya operesheni kali kuhakikisha tunaondoa ujangili....na lengo letu ni kuelekeza nguvu kujenga uchumi wa watu wetu...tutatumia kilimo cha umwagiliaji pia ili kuondokana na aibu ya njaa na kuomba chakula"amebainisha.

Ili kuhakikisha wananchi wananufaika mapato yote yanayotoka eneo hilo asilimia 32 inabaki kwenye jimbo badala ya asilimia 15 iliyoandikwa kwenye katiba,fedha hizo zitasaidia kujenga uchumi wa jamii kwenye jimbo.

Waziri wa ardhi Charty Ngilu amewaambia wananchi kuwa mpango uliopo sasa ni kuwaweka wananchi wote kwenye senta moja watakapojengewa makazi na kupewa huduma zote ,kila mmoja atapewa hati ya kumiliki eneo lake,na mashamba yao yatabaki kwa kilimo badala ya kuishi mashambani.

Baadhi ya viongozi wa jimbo hilo akiwemo gavana alisema kwa miaka 52 hayo hayakuwahi kutokea lakini kwa miezi mitatu Kenya inabadilika kwa kuwajengea  uwezo wa kiuchumi wananchi wa taifa hilo.

Wamesema siasa zimekwisha sasa ni kufanya kazi kujennga Kenya,na wanaopiga siasa kuwa kazi anazofanya Rais za kugawa hati zilitakiwa kufanywa na karani wananchi wawapuuze.

WATENDAJI WA MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU WATAHADHALISHWA


MIONGONI MWA MAJALALA YANATAKIWA KUONDOLEWA NI HILI LILIKOANZISHWA UWANJA WA WAMICHEZO WA NHC 




MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU WAPEWA ONYO.
WATENDAJI wa Mamlaka ya  Mji Mdogo wa Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wameagizwa kuhakikisha huduma ya maji,kuwasha taa za barabarani na usafi wa 
mazingira inatolewa kwa uhakika .
Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe akiongea na wafanyabiashara wa Mji huo kwenye ukumbi wa bwalo la Magereza  kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya mto Mara ,amesema mji huo utapokea wageni zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya nchimwezi septemba.
Amesema hatawaonea aibu watendaji wasiotimiza wajibu wao,hivyo wanatakiwa kuhakikisha kuanzia sasa madampo waliyoanzisha kila  kona,yanaondolewa,maji yapatikane na taa za barabarani ziwashwe.
Aidha amewataka wafanya biashara wa mjini hapo kuchangamkia fursa hiyo ambapo wanatarajia kutumia zaidi ya mil.200 kwa wiki hiyo ya maonesho na maadhimisho hayo yatakayofanyika septemba 15 mwaka huu  ambayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Ghalib Bilal.
Amewataka kuboresha sehemu zao za biashara ikiwemo nyumba za kulala,hoteli,migahawa ili waweze kunufaika na maaadhimisho hayo yanayotaraji kushirikisha washiriki kutoka Nchini Kenya,na mikoa yote ya kanda ya ziwa ,ambayo pia yatahitimishwa kwa kushuhudia tukio la nyumbu wanavuka Mto Mara kutokea hifadhi ya Maasai Mara kuingia hifadhi ya Taifa yaserengeti.
Hata hivyo  baadhi ya wafanyabiashara wamemwambia kuwa kikwazo katika mji huo ni maji,umeme usiokuwa wa uhakika ikiwemo taa za barabarani kutowashwa kunapunguza usalama wa mji huo,na mamlaka kugeuza maeneo ya michezo  ya watoto kuwa madampo ya takataka.
Mwisho.