MIONGONI MWA MAJALALA YANATAKIWA KUONDOLEWA NI HILI LILIKOANZISHWA UWANJA WA WAMICHEZO WA NHC
MAMLAKA YA
MJI WA MUGUMU WAPEWA ONYO.
WATENDAJI wa
Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mugumu Wilaya ya
Serengeti Mkoa wa Mara wameagizwa kuhakikisha huduma ya maji,kuwasha taa za
barabarani na usafi wa
mazingira inatolewa kwa uhakika .
Kaimu Mkuu
wa wilaya hiyo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe akiongea na
wafanyabiashara wa Mji huo kwenye ukumbi wa bwalo la Magereza kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya siku
ya mto Mara ,amesema mji huo utapokea wageni zaidi ya 200 kutoka ndani na nje
ya nchimwezi septemba.
Amesema
hatawaonea aibu watendaji wasiotimiza wajibu wao,hivyo wanatakiwa kuhakikisha
kuanzia sasa madampo waliyoanzisha kila kona,yanaondolewa,maji yapatikane na taa za
barabarani ziwashwe.
Aidha
amewataka wafanya biashara wa mjini hapo kuchangamkia fursa hiyo ambapo
wanatarajia kutumia zaidi ya mil.200 kwa wiki hiyo ya maonesho na maadhimisho
hayo yatakayofanyika septemba 15 mwaka huu
ambayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Ghalib Bilal.
Amewataka
kuboresha sehemu zao za biashara ikiwemo nyumba za kulala,hoteli,migahawa ili
waweze kunufaika na maaadhimisho hayo yanayotaraji kushirikisha washiriki
kutoka Nchini Kenya,na mikoa yote ya kanda ya ziwa ,ambayo pia yatahitimishwa
kwa kushuhudia tukio la nyumbu wanavuka Mto Mara kutokea hifadhi ya Maasai Mara
kuingia hifadhi ya Taifa yaserengeti.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamemwambia kuwa
kikwazo katika mji huo ni maji,umeme usiokuwa wa uhakika ikiwemo taa za
barabarani kutowashwa kunapunguza usalama wa mji huo,na mamlaka kugeuza maeneo
ya michezo ya watoto kuwa madampo ya
takataka.
Mwisho.