Subscribe:

Ads 468x60px

MICHUANO YA MARA DAY YAANZA

TIMUza Mugumu Star na Polisi Serengeti zimetoka sare baada ya kufungana goli 1-1 katika mchezo wa kuwania kikombe cha Mara day ,maadhimisho yatakayofanyika wilayani Serengeti mkoa wa Mara kuanzia septemba 9-15 siku ya kilele ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Ghalib Bilal.

Katika mchezo wa leo uliofanyika uwanja wa Sokoine ulihudhuriwa na watazamaji wengi,mashambulizi yalikuwa ya kila upande .lakini timu ya polisi inayoundwa na vijana wadogo ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa mshambuliaji mahiri Kessy Dyson dakika ya 35 kipindi cha pili.

Hata hivyo Mugumu Star timu inayoundwa na wachezaji wakongwe walizinduka na kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 2 kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wake Malima Chisumo.

Hata hivyo kutokufahamu sheria za mpira wa miguu ni mambo yaliyoonekana wazi kutoka kwa waamuzi wa mpambano wa leo ,hali iliyoibia kelele kutoka kwa washabiki na wachezaji.