Subscribe:

Ads 468x60px

Mnadani Nyamwaga Tarime

 wakazi wa nyamwaga na maeneo mengine wilayani Tarime wakiuza na kujipatia mahitaji kwenye mnada
Licha ya mvua kunyesha wajasiliamali na wanunuzi hawakujali kama inavyoonekana kwenye mnada wa Nyamwaga wilayani Tarime.

MATUKIO MBALIMBALI WILAYANI TARIME




 UKIFIKA ROSANA WILAYA YA TARIME UTAPOKELEWA NA AKINA MAMA WAJASILIAMALI WANAOUZA NDIZI,MKUNGU MMOJA NI KATI YA SH,5,000-7,000

 BIASHARA NI MAELEWANO MTEJA ANAOMBA KUPUNGUZIWA BEI.



WAKATIWENGINE WANAENDELEA NA BIASHARA,WENGINE WAKO KWENYE PILIKAPILIKA ZA KUSAKA NG'OMBE WALIOIBWA,WIZI UNACHANGIA KUZOROTESHA MAENDELEO WILAYANI HUMO KWA KUWA MUDA WA UZALISHAJI HUTUMIKA KUTAFUTA MIFUGO,HAO WAMENASWA NA KAMERA YETU WAKIWA KIJIJI CHA GIBASO WAKITOKEA MRITO.
HAWA NI WAKAZI WA KIJIJI CHA KITAWASI WILAYANI TARIME AMBAO WANADAI WANYAMAPORI KAMA TEMBO WAMECHANGIA MAISHA MAGUMU KWAO KWA KUWA MAZAO YAO HULIWA NA HIVYO SASA HIVI DEBE LA MAHINDI NI KATI YA SH,20,000-22,000 NA YANATOKA NCHINI KENYA.

 AAKINA MAMA WENGI NDIO WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA ZA KUUZA MBOGA,NYANYA NA MATUNDA KAMA INAVYOONEKANA HAPO KIJIJI CHA GIBASO WILAYANI TARIME

 OONGEZA PESA ANGALAU KIDOGO,NI MANENO YA MAMA NAYEUZA NDIZI KATIKA ENEO MAARUFU KWA JINA LA WAUZA NDIZI KIJIJI CHA ROSANA WILAYANI TARIME


 SSI LAZIMA GARI HATA BAISKELI INATUMIKA KUSOMBA MATOFALI KAMA ANAVYOONEKANA HUYO MWANANCHI NA MTOTO WAKE WILAYANI TARIME

 SSAFARI NI SAFARI MAANA HAPA WANAHABARI WAMEKWAMA BAADA YA GARI KUHARIBIKA,LAKINI WALIFANIKIWA KUSONGA MBELE.

Kikwete abebeshwa zigo la mawaziri dhaifu




CCM imemtwisha rasmi Rais Jakaya Kikwete jukumu la kukabiliana na mawaziri ‘mizigo’ wanaoshindwa kutimiza majukumu yao. PICHA | FIDELIS FELIX    
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Jumapili,Decemba15  2013  saa 5:12 AM
Kwa ufupi
  • Mawaziri 7 waliotajwa ni ‘mzigo’ kwa Serikali juzi walihojiwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM  chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete, ambapo jana Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema wamemshauri Rais Kikwete mambo matatu; kuwafukuza, kuwahamisha wizara au kuwahimiza wafanye kazi.
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia mpira Rais Jakaya Kikwete wa kuamua hatima ya mawaziri saba, wanaotuhumiwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Mawaziri hao waliotajwa ni ‘mzigo’ kwa Serikali juzi walihojiwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM  chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete, ambapo jana Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema wamemshauri Rais Kikwete mambo matatu; kuwafukuza, kuwahamisha wizara au kuwahimiza wafanye kazi.
“Kamati Kuu imetoa maazimio saba ambayo yote yanazihusu wizara saba zinazoongozwa na mawaziri hao. Tumemshauri Rais Kikwete, yeye ndiye ataamua nini cha kufanya kwa sababu ndiye aliyewateuwa mawaziri hao,” alisema Nape.
Wakiwa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika ziara ya chama hicho, Nape pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana aliwatupia lawama mawaziri hao wakati wakielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.
Nape alisema mawaziri hao waliitwa kuhojiwa na kutakiwa kutoa maelezo ya masuala yaliyoibuliwa wakati wa ziara hiyo ambayo pia iliwahusisha baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti.
Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari jana, Nape aliwataja mawaziri hao kuwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza, Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya (alihojiwa kwa niaba ya Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa).
Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.
Sakata la kutaka mawaziri ‘mizigo’ kutoswa limekuwa likiibuliwa na wabunge mbalimbali katika mikutano ya Bunge mjini Dodoma, huku baadhi wakipendekeza hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda naye atoswe kutokana na kushindwa kuwasimamia mawaziri.
Ushauri wa CCM kwa JK
Nape alisema kuwa kazi ya Kamati Kuu ni kushauri, “Kazi yetu ni kushauri na siyo kufukuza. Rais Kikwete ndiye amewateua mawaziri hao, ameupokea ushauri na yeye ndiye mwenye uwezo wa kuwafukuza, kuwahamisha au kuwasukuma watende kazi. Hiyo siyo kazi yetu”
Alipobanwa zaidi kueleza ushauri ambao Kamati Kuu ilimpa Rais Kikwete Nape alisema, “Kuna ushauri mwingine ambao tumempa Rais Kikwete hatuwezi kuuweka hadharani.”
Alisema kuwa wakati wa kuhojiwa kila waziri alikuja na majibu yanayoihusu wizara yake kutokana na udhaifu ulioelezwa na wananchi.

“Katika kikao kijacho cha Kamati Kuu moja ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na kuangalia utekelezaji wa mambo saba tuliyoishauri Serikali kupitia hizo wizara saba,” alisema.
Nape alisema kuwa walipoeleza udhaifu wa mawaziri hao hawakueleza kuwa ni mzigo kwa Serikali, bali walilenga kueleza upungufu wao katika kusimamia masuala mbalimbali.
“Mfano Waziri wa Kilimo kwa miaka minne hajawahi kwenda mkoani Ruvuma ambako kuna ghala la chakula pia hajawahi kushughulikia matatizo yanayowakabili wakulima wa korosho na mahindi,” alisema.
Hata hivyo, Nape alisema kuwafukuza mawaziri siyo dawa na kuweka mambo sawa kwa maelezo kuwa wakati mwingine utendaji kazi ndani ya Serikali unakwenda ovyo kwa sababu ya mfumo na sheria mbovu.
“Watu wanadhani ushauri tuliompa Rais Kikwete ni kuwafukuza mawaziri, wakati mwingine kufukuza siyo mwisho wa suluhisho. Kwa mfano tumebadili mawaziri Tamisemi lakini kila mwaka ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonyesha udhaifu katika wizara hiyo,” alisema Nape.
Maagizo
Nape alisema agizo la kwanza ni kuhusu kilimo cha pamba ambapo Kamati Kuu iangalie upya Serikali ipitie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa pamba nchini.
Alisema kuwa kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho ikiwamo kutowalazimisha.
“Kwa mfano Waziri husika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani Ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula na tulipofika Tunduma tulikuta foleni pale mizani huku watumishi wakiwa wanafanya kazi kwa saa tisa, lakini baada ya kueleza udhaifu huo sasa wanafanya kwa saa 24,” alisema.
Aliongeza, “Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton, badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu.”
Alisisitiza kuwa Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini,  hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira.
Kwa upande wa wakulima wa korosho, Nape alisema  kuwa Kamati Kuu imeisisitizia serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho na kuhakikisha inabanguliwa nchini.
“Serikali inatakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato kwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo, ili kuondoa makato yasiyo ya lazima na kuongeza kipato cha mkulima,”
“Kuhusu pembejeo za ruzuku Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa,” alisema.
 Kwa upande wakulima wa mahindi alisema kuwa serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.
“Utaratibu uwekwe wa kufanya tathmini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa,”alisema.
Nnauye alisema kwa upande wa madai ya walimu Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha uhakiki wa madai ya walimu na kuwalipa haki zao ikiwamo kuhakikisha madeni hayazaliwi tena.
Kamati hiyo pia imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye halmashauri mbalimbali nchini.
“Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye halmashauri mbalimbali nchini,” alisema Nnauye.
Kwa upande wa matatizo ya upatikanaji wa maji safi na salama serikali imeagizwa kufanya mkakati wa makusudi na wa dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wa kudumu tatizo hilo ikiwamo kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya ardhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.


UZINDUZI WA SIKU YA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Uzinduzi wa siku ya watetezi wa haki za binadamu Tanzania

Safari ya wanahabari vijijini

 wakazi wa kijiji cha Gibasonkata ya Nyarukoba wilayani Tarime wakiongea na timu ya waanidhi wa habari kuhusiana na ongezeko la wanyama waharibu wa mazao kwa wakazi waishio kando ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,mazungumzo hayo yalifanyika mbele ya jengo la Serena hoteli iliyokuwa imefunguliwa huku juu fundi akiezeka.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa hawana la kufanya baada ya gari walilokuwa wakilitumia kwenda kijiji cha Kegonga wilayani Tarime wkubadilika.

Bilal:Watoto waathirika zaidi ukiukwaji haki za binadamu


Na Elizabeth Zaya
12th December 2013

Makamu wa Rais,Dk. Mohammed Gharib Bilal
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema kundi la watoto ndiyo limekuwa likiathiriwa zaidi na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

Aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya haki za binadamu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Bilal alisema sababu kubwa inayochangia kundi hilo kukumbwa na suala la ukiukwaji haki za binadamu, ni kutokuwa na mtu wa kulisemea.

Alisema kuheshimu haki za binadamu, ni kioo cha kuonyesha nchi imekomaa kidemokrasia, hususan kwa kuwapa wananchi haki zao za msingi.

Alizindua mpango kazi wa kitaifa wa utekelezaji wa haki za binadamu wa miaka mitano utakaotoa mwongozo wa jinsi ya kusimamia utekelezaji wa haki za binadamu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema lengo kuu la mpango huo ni kukuza na kuimarisha haki za binadamu na kuimarisha uhusiano kati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Pia kupunguza upungufu uliopo katika kuheshimu, kulinda na kukuza haki za binadamu nchini pamoja na kukuza, kuimarisha na kuongeza uelewa wa haki za binadamu  baina ya wananchi wenyewe.
 
CHANZO: NIPASHE


Mawakili wamng`ang`ania Pinda kesi ya Kikatiba


Na Hellen Mwango
12th December 2013


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeambiwa kwamba kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ina mashiko ya kisheria na  inastahili kusikilizwa na mahakama hiyo na kutolewa maamuzi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Madai hayo yalitolewa jijini Dar es Salaam jana na upande wa walalamikaji kupitia kwa Makamu wa Rais wa TLS, Wakili Peter Kibatala, wakati akijibu hoja za pingamizi la awali la walalamikiwa kwamba kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa na haina mashiko ya kisheria na hivyo mahakama iitupilie mbali.

Kibatala aliwasilisha hoja zake mbele ya jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, akisaidiana na Jaji Augustine Mwarija na Dk. Fauz Twaib.

Upande wa walalamikiwa uliongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju, akisaidiana na Mawakili wa Serikali Wakuu, Gabriel Marata, Sarah Mlipano na Alesia Mbuya.

Wakili Kibatala alidai kuwa hoja za upande wa walalamikiwa kwamba kesi  isisikilizwe kwa madai ni ya kizushi na haina mashiko, hazina ukweli na kwamba inastahili kusikilizwa na kutolewa maamuzi.

"Kesi hii ina mashiko ya kisheria na tuna haki ya kuja mahakamani kusikilizwa hata kama Waziri Mkuu ana kinga lakini imepita ukomo wa kikatiba...walalamikiwa wamethibitisha kwamba ina mashiko na kwa sababu hiyo, Naibu Mwanasheria Mkuu aliomba mahakama kesi hii iendeshwe kwa lugha ya Kiswahili kwa maslahi ya umma," alidai.

Akifafanua zaidi alidai kuwa mahakama inatakiwa iseme kwamba kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda kama ni sahihi au la.

Alidai kuwa ili mahakama itoe maamuzi, ni lazima kesi isikilizwe kwa pande zote mbili na siyo itoe amri kwa kusikiliza pingamizi la awali.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa leo ambapo upande wa walalamikiwa watatoa hoja zao.

Katika madai ya msingi, LHRC na TLS, wanapinga kauli iliyotolewa na Pinda bungeni, Juni 20, mwaka huu, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

Pinda anadaiwa kutoa kauli inayolalamikiwa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, aliyetaka kujua msimamo wa serikali na mambo mengine, malalamiko dhidi ya vyombo vya dola katika baadhi ya maeneo kama Mtwara, kuwapiga wananchi.

UKATILI-AKATWA SIKIO NA SIME KWA KUKATAA KUFANYA NGONO NA SHEMEJI YAKE.

 Muuguzi wodi ya wanawake hospitali Teule ya Nyerere wilayani Serengeti akimtibu jeraha  Ghati Mikere(20)mkazi wa Kijiji cha Bisarara wilaya humo  anayedaiwa kukatwa shingo na sikio  na shemeji yake baada ya kukataa kufanya naye ngono. 
 Ghati Mikere akiuguza majeraha
 
Mratibu wa dawati la polisi la Jinsia WP Sajenti Sijali Nyambuche akichukua maelezo ya Ghati walipotembelea majeruhi mbalimbali hospitalini hapo

“Mwingine aliyeolewa na Mwanamke Nyumba Nthobu,anusurika kuuawa na mwanamme aliyemzalisha”
Desemba 7,2013
Serengeti:WAKATI wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali wakiwa katika kampeini za kupinga vitendo vya  ukatili wa kijinsia,Ghati Mikere(20)mkazi wa Kijiji cha Bisarara wilaya ya Serengeti amenusurika kufa kufuatia kukatwa shingo na sikio baada ya  kukataa kufanya ngono na shemeji yake .
Tukio hilo lililompelekea kulazwa wodi ya wanawake hospitali ya wilaya ya Nyerere limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali,linadaiwa kutokea novemba 30 mwaka huu majira ya saa 5:asubuhi nyumbani kwa majeruhi huyo.
Akiongea kwa kugugumia  kutokana na maumivu akiwa wodini alisema shemeji yake Chacha Kitari alimkata baada ya kukataa kushiriki tendo la ngono kwa madai ya kuondoa mkosi wa mme wake kufungwa jela ,alipokataa ikapelekea kukatwa sikio la kushoto na  shingo.
“Kabla ya kunishambulia kwa fimbo na kunikata kwa sime…alinitaka nifanye naye ngono kwa madai kuwa ni maamzi ya ukoo na itasaidia kuondoa mkosi kwenye ukoo…kisha amiliki mji na ndiye awe mme wangu ..yaani wameishajipanga kama mme wangu anafia huko”alisema kwa masikitiko.
Hata hivyo Ghati hakuwa tayari kusema mme wake kafungwa miaka mingapi na kwa kosa lipi,na ameanza kutumikia kifungo lini.
Alisema licha ya kupiga kelele kuomba msaada ,ndugu walimpuuza na ndipo akapata msaada kwa majilani wa kufika hospitali kwa kupitia polisi.
Mkuu wa kituo cha Polisi Mugumu ASP Joseph Maganga ambaye aliongoza dawati la jinsia akiwa hospitalini hapo alisema ,wanaendelea kumsaka mtuhumiwa kwa kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yameshamiri na kuomba jamii kutoyafumbia macho kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwenye familia na taifa.
Katika tukio jingine  mwanamke mmoja Mgosi Chacha (20) mkazi wa mtaa wa bomani mjini Mugumu naye amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya na mme wake wa kufikia kwa madai ya kukataa kurudisha  mahari iliyotolewa na mwanamke aliyemuoa(Nyumba Nthobu).
Akiwa wodi la wanawake mbele ya dawati la jinsia la polisi alisema desemba  2.majira ya saa tatu usiku mwaka huu akiwa nyumbani kwake mtaa wa  bomani mwanamme huyo  Chacha Charles mkazi wa kijiji cha Bonchugu alimfanyia unyama huo baada ya kudai hatarudisha mahari ya mwanamke huyo kwa kuwa aliolewa kwa mila na desturi za Kikurya.
“Nimeolewa kwa ng’ombe 12 kutoka kwa bibi Bhoke Charles …ndoa ya Nyumba Nthobu…huyo mwanamme yeye ameteuliwa na ukoo wa bibi ambaye alinitolea mahari…ambaye hakuzaa na ameishakuwa marehemu …amenizalisha watoto wanne ambao ni mali ya alinitolea mahar”alisema.
Alisema siku ya  tukio Charles akiwa nyumbani mtuhumiwa huyo alifika na kusema anataka  ng’ombe hao kwa kuwa amemweleza muda mrefu bila utekelezaji,na kumpa nafasi ya kujibu na alianza kumshambuli na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili,kana kwamba haitoshi alimchukuakua usiku huo akiwa ajitambui na kwenda kumtupa kwenye shimo refu umbali wa kilomita 2 kutoka nyumbani kwake ambapo aliokotwa asubuhi na wapita njia ambao walitoa  taarifa polisi na yeye alipata fahamu na kujikuta  amelazwa hospitali.
“Kwa sasa hali za wanawake hao zinaendelea vizuri na wanapata huduma ya matibabu ,  tofauti na mwanzo walipofikishwa Hospitali walikuwa katika hali mbaya”,alisema  Musa Wilison Muuguzi mwandamizi msaidizi .
Mwisho.

Kenyan Journalists hold protests over media law



By Lucas Barasa

Posted  Wednesday, December 4  2013 

In Summary
He said Parliament should raise at least 233 MPs to overturn the changes proposed by President Kenyatta or the Head of State should withdraw the proposed law and send a proper one to the House.
Nairobi.Journalists yesterday held protests in Nairobi and other major towns over changes in the media Bill that curtail press freedom. Editors’ Guild vice-chair David Ohito led journalists in peaceful picketing in Nairobi.
The protests were also held in Mombasa, Nyeri, Nakuru and Eldoret.
In Nairobi, the journalists converged outside Nation Centre before starting the procession on Kimathi Street, Moi Avenue and later joined Harambee Avenue before presenting their memorandum to the Office of the President, Deputy President, Attorney General and to Parliament.
The media personnel bound their mouth and camera lenses with tapes. Mr Ohito said journalists would move to court if Parliament passed memorandum proposed by President Uhuru Kenyatta “which worsened an already bad Bill.”
Mr Ohito said the country requires free and independent media and that regulations should only be through the Media Council or a professional body composed of journalists. “The clauses in the media Bill should be in tandem with the constitution and reflect modern society,” Mr Ohito said.
WITHDRAW PROPOSED LAW
He said Parliament should raise at least 233 MPs to overturn the changes proposed by President Kenyatta or the Head of State should withdraw the proposed law and send a proper one to the House.
Media Owners Association said President Kenyatta’s memorandum of refusal on the Kenya Information and Communications (Amendment) Bill, 2013, should be taken to a parliamentary departmental committee on Energy and Communication. MOA on behalf of the Nation Media Group, Radio Africa Group, Royal Media Services, Kass and Standard Group said the Bill as passed by the National Assembly on October 31 fundamentally violates the Spirit and Letter of Article 34, Freedom of the Media and is thus unconstitutional.

WAFANYABIASHARA WAWILI WAUAWA ,MMOJA KWA KUPIGWA RISASI NA MWINGINE KUPORWA.


Desemba 1,2013.
Serengeti:WAFANYABIASHARA wawili wilayani Serengeti  wameuawa katika mazingira na maeneo tofauti  mmoja kwa kupigwa risasi tatu  na watuhumiwa hawakuchukua kitu mwingine kwa kuporwa pikipiki,simu na maiti yake kutelekezwa   eneo la shule ya msingi Matare.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo kwa tarehe na maeneo tofauti na kumtaja aliyeuawa kwa kupigwa risasi tatu ni Mugaya Marwa Mnata(37)aliyekuwa na duka la dawa baridi kijiji cha Rung’abure na Thomas Marwa Nyahure mkazi wa Matare na aliyekuwa na duka mjini Mugumu.

Kwa mjibu wa taarifa za kipolisi matukio hayo yametokea Novemba 26 na 28 ambapo maiti ya Nyahure ilikutwa imelazwa kifudifudi  eneo la shule ya Msingi Matare huku kichwani kukiwa na jeraha la kupigwa na kitu cha ncha kali,na Mnata aliuawa Novemba 28 kwa kupigwa risasi tatu ubavuni majira ya saa 3:30 usiku na kufa hapo hapo,ambapo maganda yalionekana ni silaha ni Smg.

Akizungumzia tukio la Mnata Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Rung’abure Charles Kibure alisema alikutwa na mauti muda mfupi baada ya kufunga duka lake akielekea nyumbani.

“Aliuawa eneo la stoo ya kijiji kitongoji cha Kwanina…watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa wamejificha walimpiga risasi tatu ubavuni na moja kuchana masikio kisha wakakimbia…haijajulikana nia yao maana inaonekana hapakufanyika uporaji”alisema.

Alisema wananchi walijitokeza muda mfupi baada ya kusikia mlio lakini watuhumiwa hawakupatikana na kumkuta ameishakata roho,”haya mauaji yanaacha maswali sana …maana marehemu alihamia hapa kibiashara miaka mitano iliyopita akitokea kijiji cha Kebweye wilayani Tarime….alikuwa mfamasia mzuri na alikuwa na wateja wengi sana “alisema Mwenyekiti.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho alisema kutokana na matukio ya mauaji kama hayo kujitokeza mara kwa mara ,waliitisha mkutano wa hadhara na wananchi wameahidi kufuatilia na kutoa taarifa za siri ili wahusika waweze kukamatwa kwa kuwa wanakijiji wanajawa na hofu.

Naye msemaji wa familia ya Nyahure Samweli Marwa alisema mdogo wake alitoka novemba 25 asubuhi mwaka huu kuwa anaenda dukani na hakurejea mpaka maiti yake ilipookotwa novemba 26 asubuhi kijijini hapo.

“Hatujajua chanzo cha mauaji hayo…maana hakuna mtu anahisiwa ama amekamatwa…sisi tulikuta maiti imelazwa kifudi udi kichwani kaumizwa na kitu cha ncha kali…pikipiki,simu aliporwa,fedha hatujui kama alikuwa nazo ama la…lakini kila mara tunapewa taarifa kuwa pikipiki imeonekana maeneo Fulani tukienda hakuna mafanikio”alisema Marwa ambaye ni kaka wa marehemu.

Michael Mwita jilani wa marehemu alisema kuwa kutokana na matukio kama hayo kujiridia rudia mara kwa mara,ameomba polisi wafanya uchunguzi wa kina ili kukomesha mauaji kama hayo.
Polisi wanaendelea na uchunguzi na hakuna mtu anashikiliwa kwa matukio yote mawili.
Mwisho.