Subscribe:

Ads 468x60px

Bilal:Watoto waathirika zaidi ukiukwaji haki za binadamu


Na Elizabeth Zaya
12th December 2013

Makamu wa Rais,Dk. Mohammed Gharib Bilal
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema kundi la watoto ndiyo limekuwa likiathiriwa zaidi na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

Aliyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya haki za binadamu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Bilal alisema sababu kubwa inayochangia kundi hilo kukumbwa na suala la ukiukwaji haki za binadamu, ni kutokuwa na mtu wa kulisemea.

Alisema kuheshimu haki za binadamu, ni kioo cha kuonyesha nchi imekomaa kidemokrasia, hususan kwa kuwapa wananchi haki zao za msingi.

Alizindua mpango kazi wa kitaifa wa utekelezaji wa haki za binadamu wa miaka mitano utakaotoa mwongozo wa jinsi ya kusimamia utekelezaji wa haki za binadamu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alisema lengo kuu la mpango huo ni kukuza na kuimarisha haki za binadamu na kuimarisha uhusiano kati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Pia kupunguza upungufu uliopo katika kuheshimu, kulinda na kukuza haki za binadamu nchini pamoja na kukuza, kuimarisha na kuongeza uelewa wa haki za binadamu  baina ya wananchi wenyewe.
 
CHANZO: NIPASHE