Desemba 1,2013.
Serengeti:WAFANYABIASHARA wawili
wilayani Serengeti wameuawa katika
mazingira na maeneo tofauti mmoja kwa
kupigwa risasi tatu na watuhumiwa
hawakuchukua kitu mwingine kwa kuporwa pikipiki,simu na maiti yake kutelekezwa eneo la shule ya msingi Matare.
Polisi wilayani hapa
wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo kwa tarehe na maeneo tofauti na kumtaja
aliyeuawa kwa kupigwa risasi tatu ni Mugaya Marwa Mnata(37)aliyekuwa na duka la
dawa baridi kijiji cha Rung’abure na Thomas Marwa Nyahure mkazi wa Matare na
aliyekuwa na duka mjini Mugumu.
Kwa mjibu wa taarifa za kipolisi
matukio hayo yametokea Novemba 26 na 28 ambapo maiti ya Nyahure ilikutwa
imelazwa kifudifudi eneo la shule ya
Msingi Matare huku kichwani kukiwa na jeraha la kupigwa na kitu cha ncha
kali,na Mnata aliuawa Novemba 28 kwa kupigwa risasi tatu ubavuni majira ya saa
3:30 usiku na kufa hapo hapo,ambapo maganda yalionekana ni silaha ni Smg.
Akizungumzia tukio la Mnata
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Rung’abure Charles Kibure alisema alikutwa
na mauti muda mfupi baada ya kufunga duka lake akielekea nyumbani.
“Aliuawa eneo la stoo ya kijiji
kitongoji cha Kwanina…watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa wamejificha
walimpiga risasi tatu ubavuni na moja kuchana masikio kisha
wakakimbia…haijajulikana nia yao maana inaonekana hapakufanyika
uporaji”alisema.
Alisema wananchi walijitokeza
muda mfupi baada ya kusikia mlio lakini watuhumiwa hawakupatikana na kumkuta
ameishakata roho,”haya mauaji yanaacha maswali sana …maana marehemu alihamia
hapa kibiashara miaka mitano iliyopita akitokea kijiji cha Kebweye wilayani
Tarime….alikuwa mfamasia mzuri na alikuwa na wateja wengi sana “alisema
Mwenyekiti.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho
alisema kutokana na matukio ya mauaji kama hayo kujitokeza mara kwa mara
,waliitisha mkutano wa hadhara na wananchi wameahidi kufuatilia na kutoa
taarifa za siri ili wahusika waweze kukamatwa kwa kuwa wanakijiji wanajawa na
hofu.
Naye msemaji wa familia ya
Nyahure Samweli Marwa alisema mdogo wake alitoka novemba 25 asubuhi mwaka huu
kuwa anaenda dukani na hakurejea mpaka maiti yake ilipookotwa novemba 26
asubuhi kijijini hapo.
“Hatujajua chanzo cha mauaji hayo…maana
hakuna mtu anahisiwa ama amekamatwa…sisi tulikuta maiti imelazwa kifudi udi
kichwani kaumizwa na kitu cha ncha kali…pikipiki,simu aliporwa,fedha hatujui
kama alikuwa nazo ama la…lakini kila mara tunapewa taarifa kuwa pikipiki
imeonekana maeneo Fulani tukienda hakuna mafanikio”alisema Marwa ambaye ni kaka
wa marehemu.
Michael Mwita jilani wa marehemu
alisema kuwa kutokana na matukio kama hayo kujiridia rudia mara kwa
mara,ameomba polisi wafanya uchunguzi wa kina ili kukomesha mauaji kama hayo.
Polisi wanaendelea na uchunguzi
na hakuna mtu anashikiliwa kwa matukio yote mawili.
Mwisho.