Subscribe:

Ads 468x60px

Msomi: CCM inapinga uamuzi wake



 


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Picha ya Maktaba 
Na Editha Majura, Mwananchi

Posted  Jumapili,Mei18  2014  saa 14:59 PM
Kwa ufupi
Ashangaa kuasisi madai ya Serikali tatu, kuyapinga kwenye Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba
Moja ya shughuli zilizoambatana na maadhimisho ya miaka 50 tangu nchi za Tanganyika na Zanzibar ziungane, ni kongamano lililojadili na kutathmini muungano huo, lililoandaliwa na Jukwaa la Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA).
Aina gani ya muungano kati ya serikali mbili au tatu, imekuwa hoja nzito kiasi cha kuligawa Bunge la Katiba, wanataaluma mbalimbali wamezungumza kuhusu CCM kukataa mapendekezo ya mfumo wa serikali tatu, unaopendekezwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Profesa Gaudence Mpangala, anashangazwa na hatua hiyo ya CCM akisema waasisi wa mfumo huo ni wanaCCM ambao walianza kudai Tanganyika tangu mwaka 1984
“Kiini cha kudai serikali tatu ni Tanganyika kumezwa na muungano. Mwaka 1984 Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kwa mara ya kwanza liliibua dai la Tanganyika, likifuatiwa na wabunge wa CCM (G55) kisha madai hayo yakaendelezwa na wananchi kupitia tume zinazoundwa na kuongozwa na wanaCCM,” anaeleza
Profesa Mpangala, anaamini wapinzani katika mchakato wa Katiba wameunga mkono uasisi wa CCM na kwamba inashangaza chama hicho kupambana kwa kila hali, kushawishi watu wakatae mfumo huo.
Anasema ni hatari Tanzania kubaki na mfumo wa serikali mbili, Tanganyika ikiwa imemezwa na muungano ilhali joto la kuidai likidhihirika kuongezeka kila linapopimwa.
Utaifa
Profesa Mpangala, anasema haiwezekani kukwepa utaifa ndani ya muungano ilhali umetokana na nchi mbili; “Sote ni Watanzania lakini ndani yetu kuna Tanganyika na Zanzibar, zenye asili ya Afrika na ambazo kihistoria, zimetokana na harakati za kumng’oa mkoloni.”
Utaifa wa Tanganyika na Zanzibar uweje?
Profesa Mpangala anasema tatizo ni aina ya muundo wa muungano. Lakini akaeleza kwamba historia ikiheshimika, suala hilo litatengemaa.
Anasema katika mfumo wa sasa, Tanzania imeimeza Tanganyika na kwamba ni hatari kwa usalama wa muungano. Historia ya hatari hiyo kuchomoza hadharani inaelezwa kuanza mwaka 1984.
Profesa anasema kwa mara ya kwanza, suala hilo lilijadiliwa ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kufuatiwa na hatua ya Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe, kupeleka madai ya serikali tatu kwa CCM, ikamgharimu kiasi cha kulazimika kujiuzulu.
Dk Kitila Mkumbo, akataka watu wahoji sababu ya Rais huyo, kuandika barua ya mbili badala ya tatu za kujiuzulu; “Alijiuzulu umakamu mwenyekiti wa CCM na umakamu wa kwanza wa rais tu. Barua ya kujiuzulu urais wa Zanzibar aliiandika baada ya kushinikizwa.
Madai ya Serikali tatu kwenye Mchakato wa Katiba
Profesa Mpangala anaona kuna msingi katika madai hayo ingawa yaliasisiwa na wanaCCM Zanzibar, sasa yameenea nchi nzima na kuungwa mkono na vyama vya siasa vya upinzani.
Anasema Rasimu ya Kwanza ya Katiba nchi iliyoungana na Zanzibar kwa jina la Tanzania Bara wananchi kupitia awamu ya kutoa maoni katika mabaraza ya wilaya ya Katiba wakahoji jina hilo, wakitaka upande huo uitwe jina lake la asili –Tanganyika ama sivyo, Zanzibar ifutwe na kuitwa Tanzania Visiwani.
“Marekebisho yamefanyika kwani Rasimu ya Pili inataja upande mwenza wa Zanzibar kwa jina la Tanganyika, tukiendelea kufichaficha Utanganyika, sidhani kama tuendako kutakuwa kuzuri,” anaeleza
Demokrasia
Anasema rasimu iliyoandikwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ndiyo yenye kukubalika kisheria na inaelekeza Tanzania kufanya mapinduzi ya kidemokrasia kwani wananchi wameshirikishwa.
“Mchakato umeanzwa kidemokrasia lakini ulipofikia,(Bunge Maalumu) mchakato umekuwa undemocratic process (demokrasia imekiukwa), hali hii haitaleta matokeo mazuri,” anaeleza.
Bungeni
Katiba ni kwa ajili ya taifa, msimamo wa CCM kutoendana na mapendekezo ya rasimu hususan mfumo wa muungano, haijengi msingi mzuri wa demokrasia.
Anasema hayo yangeeleweka enzi za mfumo wa chama kimoja, siyo sasa ambapo nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, demokrasia ni lazima.
“Madai kwamba serikali tatu zitaua muungano ni vise verser (kinyume) kwani serikali mbili zisizo na demokrasia ni hatari zaidi,” anaeleza.
Anaamini serikali tatu zitakomboa Tanganyika na Zanzibar kiuchumi na anashauri mchakato wa Katiba kuheshimu utaifa wa watu wa pande zote za muungano pamoja na rasimu, kwa kuiboresha bila kuibua rasimu mbadala. Hayo yakizingatiwa, anasema itapatikana Katiba bora itakayodumu kwa miaka mingi

JK kuongoza mashauriano ya mradi wa mabasi





Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Mei19  2014  saa 11:44 AM
Kwa ufupi
Ni yale yatakayofanya safari zake katika Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza mkutano wa mashauriano ya awamu ya kwanza ya uwekezaji katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) utakaowakutanisha wawekezaji wa ndani na nje Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa DART, Asteria Mlambo alisema mwishoni mwa wiki kuwa mkutano huo utakaofanyika mapema mwezi ujao utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa za uwekezaji zitakazopatika kwenye mradi huo.
Washiriki wa mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika benki na taasisi mbalimbali za kifedha, kampuni za kutengeneza mabasi, kampuni za mawasiliano, mifuko ya kijamii na wengine.
Mada kuhusu mradi wenyewe wa DART itatolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Jumanne Sagini.
Kabla ya mkutano huo, DART imeandaa mkutano wa wamiliki wa daladala Dar es Salaam, Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ili kuwafahamisha jinsi gani wanaweza kunufaika na mfumo huo mpya.
“Tutawaelezea faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini,” alisema Mlambo.
Mwezi uliopita Dart ilikamilisha shughuli ya kusajili mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo ikiwa ni moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo.
Kulingana na mpango huo wa Dart barabara hizo za Morogoro, Kawawa na Msimbazi zitatumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee kwa njia 64 Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na mradi huo.




MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU YAGEUZA MJI HUO KUWA MCHAFU KWA KUFUNGUA JALALA KATIKATI YA MJI

 LICHA YA KUTANGAZA MJI WA MUGUMU KUWA WA KITALII MAMLAKA YA MJI HUO IMEFUNGUA JALALA KATIKA MAENEO YA BIASHARA ZA NYUMBA ZA KULALA WAGENI,GROSERY NA ZAHANATI,MKAKATI UNAOPINGANA NA KAULI ZA VIONGOZI KWENYE VIKAO
 WAKATI UGONJWA WA DENGUE UNAZIDI KUSAMBAA ,MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU WILAYANI SEREGETI WANATENGENEZA BOMU LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KWA WAKAZI WAKE
 JALALA LILILOFUNGULIWA NA MAMLAKA YA MJI WA MUGUMU WILAYANI SERENGETI KATIKA MAENEO YA MAKAZI NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI
 WANAOTOA HUDUMA HAWAPEWI HATA VYOMBO VYA KUJIKINGA

Werema alikoroga, alinywa: Atoa kauli ya kuwabagua Wazanzibari



Posted  Ijumaa,Mei16  2014  saa 7:57 AM
Kwa ufupi

“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu,” alisema Werema.
Dodoma. Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na kulinywa mwenyewe’, baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.
Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15.
Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.
Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo.
“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu,” alisema Werema.
Mara baada ya Bunge kurejea, Mbarouk aliomba mwongozo wa Spika akitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya kibaguzi.
“Mheshimiwa Spika, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Mbarouk.
Alisema ubaguzi huo umewabagua wabunge ambao wamekula kiapo cha kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano na unaonyesha namna ambavyo Wazanzibari wanabaguliwa.
“Mheshimiwa Spika, yanapofanyika mambo kama hayo na wewe mwenyewe uko hapa unaona ni sawa na kubariki jambo hilo, huu ni ubaguzi unaoufanya wewe kwa kuwa lilifanyika ukiona bila hata ya kukemea,” alisema Mbarouk.
Hata hivyo, Spika alipinga na kusema: “Hakuna mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata nilipokuambia kaa chini umeendelea kuzungumza, tunaendelea.... Katibu (akimtaka Katibu wa Bunge kutoa mwelekeo wa shughuli iliyokuwa inafuata ambayo ilikuwa Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).”
Baada ya kauli ya Spika, wabunge wa Zanzibar walihamasishana na kuamua kutoka nje kwa wakati mmoja na huku wenzao wa upinzani wakiendelea kutafakari cha kufanya. Wakati huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alikuwa akisoma hotuba yake.
Muda mfupi baadaye, wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi nao walitoka na katika viti vya upinzani, alibaki John Cheyo wa UDP peke yake.
Baada ya kutoka
Akizungumza nje ya Viwanja vya Bunge, Mbarouk alisema wametoka kwa sababu Spika na Jaji Werema wamewadharau. “Hatutarejea ndani ya Bunge hadi hapo watakapotuomba radhi, wasipotuomba radhi hatutarejea bungeni,” alisema Mbarouk.
Hata hivyo, wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge, mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed aliwafuata na kuwaeleza kuwa amezungumza na Werema na amekubali kuomba radhi kwa wabunge na Watanzania.
“Ndugu zangu nimeongea na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amekubali kuomba radhi,” alisema Hamad Rashid jambo ambalo liliungwa mkono na wabunge wa CUF waliokuwa wamekaa katika makundi katika Viwanja vya Bunge.
Hata hivyo, wabunge hao baada ya muda wa dakika 15, walikwenda katika kikao cha dharura kwenye Ukumbi wa Kambi ya Upinzani ambako pamoja na mambo mengine, walijadiliana kusudio la kumuona Spika Makinda kumweleza mambo yasiyowaridhisha.
Werema aomba radhi
Muda mfupi kabla ya Bunge kuahirishwa, Jaji Werema alisimama na kusema: “Kwa imani yangu, ninaamini kila binadamu ana nyongo, isipokuwa watu wawili... Yesu Kristo na Mtume Muhammad (SAW), ndiyo pekee ambao hawakuwa na nyongo. Naomba maneno yangu yafutwe katika kumbukumbu za Bunge hili.
“Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.”
KULIKOROGA
“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu.”
KULINYWA
“Mimi ni Jaji kwa taaluma na kwa nafasi yangu nimekosea kwa kutoa maneno hayo. Nimetambua kosa langu na naomba radhi... kwanza kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rajab Mbarouk, Mheshimiwa Injinia Habib Mnyaa, Bunge hili na Watanzania kwa jumla.”



Maswali 10 tata kuhusu dengue
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2316486/highRes/746639/-/maxw/600/-/1j259wz/-/mbu.png
“Lakini si lazima wawe wanazaliana zaidi katika maji masafi kwa sababu wana tabia ya kubadili tabia. Kwa mfano, anopheles wanaoeneza malaria nao walipenda maji masafi awali, lakini kwa sasa wamebadilika wanazaliana hata kwenye maji machafu,”.PICHA|MAKTABA 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Mei16  2014  saa 7:53 AM
Kwa ufupi
Dk Govela alisema suala hilo bado linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kati ya aina tatu za mbu wanaosababisha dengue, hakuna utafiti uliofanyika kujua tabia zao wote.
Dar es Salaam.Tangu ugonjwa wa homa ya dengue uibuke mkoani Dar es Salaam na baadaye maeneo mengine ya nchi, wananchi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi yenye utata ambayo sasa yamepata majibu ya wataalamu.
1. Kwa nini mbu wengine wakiwamo wanaoambukiza malaria hawawezi kuambukiza dengue?
Mtafiti wa tabia za mbu kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), Dk Nicholaus Govela alisema mbu anayeambukiza homa ya dengue, Aedes Egypti, hawezi kubeba vimelea vya malaria wala yule anayeambukiza malaria hawezi kuambukiza dengue kutokana na maumbile yao.
Dk Govela alisema fiziolojia ya mwili wa mbu haiwezi kuruhusu Aedes Egypti kubeba virusi vya mbu mwingine.
“Ndiyo maana mbu hawezi kuambukiza Virusi vya Ukimwi,” alisema.
2. Kwa nini mbu wa dengue huuma mchana?
Dk Govela alisema suala hilo bado linahitaji utafiti zaidi kwa sababu kati ya aina tatu za mbu wanaosababisha dengue, hakuna utafiti uliofanyika kujua tabia zao wote.
Aina hizo ni Aedes Egypti, Aedes Albokictus na Aedes Africaans.
Alibainisha kuwa katika tafiti zinazofanyika, IHI iliwahi kubainika kuwa Aedes African ambaye pia anaambukiza dengue huuma usiku.
Alisema wengi wanamwelezea mbu huyu kwa kumlinganisha na tabia za mbu wa Japan, China na America ya Kusini lakini inawezekana huyu aliyepo hapa ni mpya tofauti na wa nchi za nje.
3. Je, dawa inayopulizwa inafaa kuwaangamiza?
Dk Govela alisema inawezekana ndiyo au hapana, lazima hili pia lifanyiwe utafiti kwa kuwa upo uwezekano wa mbu hawa kujenga usugu wa dawa kwa kuwa wamekuwapo nchini kwa miaka mingi.
Alipongeza uamuzi wa Serikali wa kupuliza dawa kwenye mabasi ya mikoani lakini bado alihoji iwapo imefikiria udhibiti kuanzia katika viwanja vya ndege na iwapo itawezekana kuzuia watu wanaokwenda mikoani wakiwa tayari wameambukizwa.
4. Je, kuna watu wanaougua dengue bila kuonyesha dalili?
Mtafiti huyo alisema wapo wanaougua bila kuonyesha dalili na wanaendelea kuambukiza... “Hawa mara nyingi hawaendi hospitali lakini wanakuwa na virusi mwilini,” alisema.
5. Kuna aina ngapi za virusi vya dengue?
Dk Govela alisema zipo aina nne za virusi vinavyoambukiza dengue. Alivitaja kuwa ni den 1, den2, den 3 na den 4. Hadi sasa, wanasayansi hawajaweza kubaini ni virusi vya aina gani vinasababisha homa hiyo kwa Tanzania.
“Ndiyo maana tunahitaji kufanya tafiti zaidi,” alisema.
6. Je, juisi ya majani ya papai ni tiba ya dengue?
Ofisa wa Taaluma na Udhibiti wa Magonjwa wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Grace Saguti alisema haijathibitishwa kisayansi.
Dk Saguti alisema ili tiba ikubalike, lazima ithibitishwe na hakuna namna mbadala ya kuiruhusu itumike kabla ya kujua madhara na faida zake. Alisema mpapai unaongeza vitamini A na hivyo kuimarisha kinga ya mwili, lakini si kutibu virusi vya dengue ambavyo kwa asili yake havina dawa.
7.Mbu wa dengue wako Dar es Salaam pekee?
Mtaalamu wa IHI alisema mbu huyo anaishi katika maeneo ya kitropiki, hivyo huenda yupo hata katika mikoa mingine. Alisema kwa tabia, aedes africans anafanana na mbu aina ya culex ambaye anapatikana katika mikoa mingine, hivyo hata huyo anaweza kuwapo huko pia... “Lazima ufanyike utafiti ili tujue iwapo mbu huyo hawezi kuzaliana katika mikoa mingine,” alisema.
8. Kwa nini aedes hupenda maji masafi yaliyotuama?
Dk Govela alisema ni kutokana na asili ya maumbile yao. Mbu hao huamini maji masafi yaliyotuama huwapa joto zaidi kwa ajili ya kutaga mayai.
“Lakini si lazima wawe wanazaliana zaidi katika maji masafi kwa sababu wana tabia ya kubadili tabia. Kwa mfano, anopheles wanaoeneza malaria nao walipenda maji masafi awali, lakini kwa sasa wamebadilika wanazaliana hata kwenye maji machafu,” alisema
9.Kwa nini wahudumu wa afya wanaathirika zaidi?
Daktari Kiongozi na Mtaalamu wa Homa ya dengue, Mrisho Lupinda alisema nao ni binadamu kama wengine na wanaishi maeneo hatarishi yenye mbu kama watu wengine.
10. Kwa nini panadol pekee ndiyo inatibu dalili za dengue?
Dk Lupinda alisema dawa nyingine za maumivu yaani Diclopar, Diclofenac na Aspirini huingiliana na mfumo wa chembe hai nyeupe za damu na huweza kusababisha chembe hizo kupungua mwilini. Dawa hizo huchochea kutengeneza sumu ambayo huathiri baadhi ya ogani za mwili.
Ugonjwa wasambaa
Homa ya dengue imesambaa katika maeneo mbalimbali nchini na kutoka Shinyanga, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Fredrick Mlekwa amesema kumetokea kifo cha mtoto aliyekuwa na dalili zote za ugonjwa huo.
Huko Arusha, mkazi wa Maji ya Chai, Frank Nnko (30) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akitokea Hospitali ya Wilaya ya Meru akiwa na dalili za homa hiyo.
Zanzibar, wagonjwa watatu wanaodhaniwa kuwa na homa ya dengue wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja. Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alisema wagonjwa hao wana dalili za ugonjwa huo.
Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Tumbi akiwa na dalili za dengue, akiwa na maumivu ya kichwa na kutoka damu puani, Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Gerald Chami alisema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 30, alitokea Mbezi Wilaya ya Kinondoni.
Imeandikwa na Florence Majani, Andrew Msechu, Stella Ibengwe na Happy Lazaro, Mwinyi Sadallah, Talib Ussi na Julieth Ngarabali.


SAFARI YA MWISHO YA MAMA YANGU MDOGO MWANAIDI ALIYEAGA DUNIA 10.5.2014 NA KUZIKWA 11.5.2014

 Tukio hili hutukumbusha maneno ya kitabu cha Yoeli,Lakini hata sasa asema bwana ,nirudieni sasa kwa mikoyo yenu yote....rarueni mioyo wala si mavazi,twapaswa kujiandaa....Upumzike kwa amani mama yetu.

 Umamavumbi na mavumbini utarejea tena,tutakukumbuka mama na tunamshukuru Mungu kwa kukujaliaa kuishi duniani miaka 73.
 Kwa heri mama ulitwaliwa mavumbini,na unarejea tena,Eee bwana utujulishe njia zako ili tujue kuzihesabu siku zako
Hapo watoto na wajukuu wakimaliza kuweka udongo kama ishara ya yeye kurudi mavumbini,wakati wa mazishi yaliyofanyikia kijiji cha Chumvi Majita wilaya ya Butiama

Bulembo atuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka



Na Richard Makore
10th May 2014
Mwenyeketi wa  Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo, ametuhumiwa kuendesha taasisi  hiyo kama mali ya familia  na kuhusishwa na matumizi mabaya ya fedha.

Tuhuma hizo zilitolewa  jijini Dar es Salaam jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa kutoka mkoa wa Mara, Jeremiah Wambura alipozungumza na wanahabari.

Wambura alisema Bulembo amezidi kuvuruga jumuiya hiyo, kwa kutumia fedha vibaya pamoja na kuamua mambo yake bila kushirikisha wanachama.

Alisema wakati wa kampeni za kuwania nafasi hiyo aliahidi kuifufua jumuiya hiyo ambayo ilikuwa hatarini kufutwa na CCM, ikiwamo kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vile vya zamani hasa shule.

Aidha, ahadi zingine alizoahidi ni pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa Jumiya hiyo na kumaliza kero zao za muda mrefu pamoja na  kuleta umoja na mshikamano jambo ambalo Wambura alisema Bulembo ameshindwa kulifanya.

Wambura ambaye  alikuwa meneja wake wa kampeni mwaka 2012, alisema Bulembo amekiuka kanuni za Jumuiya hiyo na sasa anaamua mambo mazito kwa kushariana na familia yake

"Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko" hiyo ni sehemu ya Katiba ya  CCM aliyoinukuu Wambura na kusema kwamba wananchama wengi walimchagua Bulembo ili atekeleze maslahi ya Jumuiya na siyo ya kwake binafsi kama anavyofanya sasa.

 Bulembo amedaiwa kuwa ni msaliti kwa kuwa ameshindwa kutimiza malengo  badala yake amewa chukia na kuwaona maadui wanaompinga.

"Wakati Bulembo anaingia madarakani kila shule ilikuwa inachangia makao makuu ya jumuiya hiyo Sh.10,000 kwa mwaka  lakini yeye akapandisha kiwango hicho hadi Sh.100,000 jambo ambalo linaweza kuwaumiza wazazi wanaosomesha watoto wao huko kwa kuwa lazima ada itapanda" alisema Wambura

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana kuhusiana na  tuhuma hizo, Bulembo alisema hana cha kujibu na kwamba mambo yote yanatakiwa kumalizwa kupitia vikao vya jumuiya.

Jumuiya hiyo imekuwa katika mgogoro wa muda mrefu huku sababu kubwa ikitajwa kwamba unatokana na baadhi ya viongozi kufuja fedhai
 
CHANZO: NIPASHE