Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Picha ya Maktaba
Na Editha Majura, Mwananchi
Posted Jumapili,Mei18 2014 saa 14:59 PM
Posted Jumapili,Mei18 2014 saa 14:59 PM
Kwa ufupi
Ashangaa kuasisi madai ya Serikali tatu, kuyapinga kwenye Mchakato wa
Mabadiliko ya KatibaMoja ya shughuli zilizoambatana na maadhimisho ya miaka 50 tangu nchi za Tanganyika na Zanzibar ziungane, ni kongamano lililojadili na kutathmini muungano huo, lililoandaliwa na Jukwaa la Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA).
Aina gani ya muungano kati ya serikali mbili au tatu, imekuwa hoja nzito kiasi cha kuligawa Bunge la Katiba, wanataaluma mbalimbali wamezungumza kuhusu CCM kukataa mapendekezo ya mfumo wa serikali tatu, unaopendekezwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Profesa Gaudence Mpangala, anashangazwa na hatua hiyo ya CCM akisema waasisi wa mfumo huo ni wanaCCM ambao walianza kudai Tanganyika tangu mwaka 1984
“Kiini cha kudai serikali tatu ni Tanganyika kumezwa na muungano. Mwaka 1984 Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kwa mara ya kwanza liliibua dai la Tanganyika, likifuatiwa na wabunge wa CCM (G55) kisha madai hayo yakaendelezwa na wananchi kupitia tume zinazoundwa na kuongozwa na wanaCCM,” anaeleza
Profesa Mpangala, anaamini wapinzani katika mchakato wa Katiba wameunga mkono uasisi wa CCM na kwamba inashangaza chama hicho kupambana kwa kila hali, kushawishi watu wakatae mfumo huo.
Anasema ni hatari Tanzania kubaki na mfumo wa serikali mbili, Tanganyika ikiwa imemezwa na muungano ilhali joto la kuidai likidhihirika kuongezeka kila linapopimwa.
Utaifa
Profesa Mpangala, anasema haiwezekani kukwepa utaifa ndani ya muungano ilhali umetokana na nchi mbili; “Sote ni Watanzania lakini ndani yetu kuna Tanganyika na Zanzibar, zenye asili ya Afrika na ambazo kihistoria, zimetokana na harakati za kumng’oa mkoloni.”
Utaifa wa Tanganyika na Zanzibar uweje?
Profesa Mpangala anasema tatizo ni aina ya muundo wa muungano. Lakini akaeleza kwamba historia ikiheshimika, suala hilo litatengemaa.
Anasema katika mfumo wa sasa, Tanzania imeimeza Tanganyika na kwamba ni hatari kwa usalama wa muungano. Historia ya hatari hiyo kuchomoza hadharani inaelezwa kuanza mwaka 1984.
Profesa anasema kwa mara ya kwanza, suala hilo lilijadiliwa ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kufuatiwa na hatua ya Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe, kupeleka madai ya serikali tatu kwa CCM, ikamgharimu kiasi cha kulazimika kujiuzulu.
Dk Kitila Mkumbo, akataka watu wahoji sababu ya Rais huyo, kuandika barua ya mbili badala ya tatu za kujiuzulu; “Alijiuzulu umakamu mwenyekiti wa CCM na umakamu wa kwanza wa rais tu. Barua ya kujiuzulu urais wa Zanzibar aliiandika baada ya kushinikizwa.
Madai ya Serikali tatu kwenye Mchakato wa Katiba
Profesa Mpangala anaona kuna msingi katika madai hayo ingawa yaliasisiwa na wanaCCM Zanzibar, sasa yameenea nchi nzima na kuungwa mkono na vyama vya siasa vya upinzani.
Anasema Rasimu ya Kwanza ya Katiba nchi iliyoungana na Zanzibar kwa jina la Tanzania Bara wananchi kupitia awamu ya kutoa maoni katika mabaraza ya wilaya ya Katiba wakahoji jina hilo, wakitaka upande huo uitwe jina lake la asili –Tanganyika ama sivyo, Zanzibar ifutwe na kuitwa Tanzania Visiwani.
“Marekebisho yamefanyika kwani Rasimu ya Pili inataja upande mwenza wa Zanzibar kwa jina la Tanganyika, tukiendelea kufichaficha Utanganyika, sidhani kama tuendako kutakuwa kuzuri,” anaeleza
Demokrasia
Anasema rasimu iliyoandikwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ndiyo yenye kukubalika kisheria na inaelekeza Tanzania kufanya mapinduzi ya kidemokrasia kwani wananchi wameshirikishwa.
“Mchakato umeanzwa kidemokrasia lakini ulipofikia,(Bunge Maalumu) mchakato umekuwa undemocratic process (demokrasia imekiukwa), hali hii haitaleta matokeo mazuri,” anaeleza.
Bungeni
Katiba ni kwa ajili ya taifa, msimamo wa CCM kutoendana na mapendekezo ya rasimu hususan mfumo wa muungano, haijengi msingi mzuri wa demokrasia.
Anasema hayo yangeeleweka enzi za mfumo wa chama kimoja, siyo sasa ambapo nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, demokrasia ni lazima.
“Madai kwamba serikali tatu zitaua muungano ni vise verser (kinyume) kwani serikali mbili zisizo na demokrasia ni hatari zaidi,” anaeleza.
Anaamini serikali tatu zitakomboa Tanganyika na Zanzibar
kiuchumi na anashauri mchakato wa Katiba kuheshimu utaifa wa watu wa pande zote
za muungano pamoja na rasimu, kwa kuiboresha bila kuibua rasimu mbadala. Hayo
yakizingatiwa, anasema itapatikana Katiba bora itakayodumu kwa miaka mingi
0 comments:
Post a Comment