Subscribe:

Ads 468x60px

JK kuongoza mashauriano ya mradi wa mabasi





Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Mei19  2014  saa 11:44 AM
Kwa ufupi
Ni yale yatakayofanya safari zake katika Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza mkutano wa mashauriano ya awamu ya kwanza ya uwekezaji katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) utakaowakutanisha wawekezaji wa ndani na nje Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa DART, Asteria Mlambo alisema mwishoni mwa wiki kuwa mkutano huo utakaofanyika mapema mwezi ujao utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa za uwekezaji zitakazopatika kwenye mradi huo.
Washiriki wa mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika benki na taasisi mbalimbali za kifedha, kampuni za kutengeneza mabasi, kampuni za mawasiliano, mifuko ya kijamii na wengine.
Mada kuhusu mradi wenyewe wa DART itatolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Jumanne Sagini.
Kabla ya mkutano huo, DART imeandaa mkutano wa wamiliki wa daladala Dar es Salaam, Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ili kuwafahamisha jinsi gani wanaweza kunufaika na mfumo huo mpya.
“Tutawaelezea faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini,” alisema Mlambo.
Mwezi uliopita Dart ilikamilisha shughuli ya kusajili mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo ikiwa ni moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo.
Kulingana na mpango huo wa Dart barabara hizo za Morogoro, Kawawa na Msimbazi zitatumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee kwa njia 64 Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na mradi huo.




0 comments:

Post a Comment