Subscribe:

Ads 468x60px

Bulembo atuhumiwa matumizi mabaya ya madaraka



Na Richard Makore
10th May 2014
Mwenyeketi wa  Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdalah Bulembo, ametuhumiwa kuendesha taasisi  hiyo kama mali ya familia  na kuhusishwa na matumizi mabaya ya fedha.

Tuhuma hizo zilitolewa  jijini Dar es Salaam jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Taifa kutoka mkoa wa Mara, Jeremiah Wambura alipozungumza na wanahabari.

Wambura alisema Bulembo amezidi kuvuruga jumuiya hiyo, kwa kutumia fedha vibaya pamoja na kuamua mambo yake bila kushirikisha wanachama.

Alisema wakati wa kampeni za kuwania nafasi hiyo aliahidi kuifufua jumuiya hiyo ambayo ilikuwa hatarini kufutwa na CCM, ikiwamo kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vile vya zamani hasa shule.

Aidha, ahadi zingine alizoahidi ni pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi wa Jumiya hiyo na kumaliza kero zao za muda mrefu pamoja na  kuleta umoja na mshikamano jambo ambalo Wambura alisema Bulembo ameshindwa kulifanya.

Wambura ambaye  alikuwa meneja wake wa kampeni mwaka 2012, alisema Bulembo amekiuka kanuni za Jumuiya hiyo na sasa anaamua mambo mazito kwa kushariana na familia yake

"Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko" hiyo ni sehemu ya Katiba ya  CCM aliyoinukuu Wambura na kusema kwamba wananchama wengi walimchagua Bulembo ili atekeleze maslahi ya Jumuiya na siyo ya kwake binafsi kama anavyofanya sasa.

 Bulembo amedaiwa kuwa ni msaliti kwa kuwa ameshindwa kutimiza malengo  badala yake amewa chukia na kuwaona maadui wanaompinga.

"Wakati Bulembo anaingia madarakani kila shule ilikuwa inachangia makao makuu ya jumuiya hiyo Sh.10,000 kwa mwaka  lakini yeye akapandisha kiwango hicho hadi Sh.100,000 jambo ambalo linaweza kuwaumiza wazazi wanaosomesha watoto wao huko kwa kuwa lazima ada itapanda" alisema Wambura

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana kuhusiana na  tuhuma hizo, Bulembo alisema hana cha kujibu na kwamba mambo yote yanatakiwa kumalizwa kupitia vikao vya jumuiya.

Jumuiya hiyo imekuwa katika mgogoro wa muda mrefu huku sababu kubwa ikitajwa kwamba unatokana na baadhi ya viongozi kufuja fedhai
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment