Subscribe:

Ads 468x60px

VIWANJA 250 SERENGETI MMILIKI HAJULIKANI


MMILIKI WA VIWANJA  250 HAJULIKANI SERENGETI..
Februari 17,2013.
KAMATI ya ardhi wilaya ya Serengeti haina viwanja vya kugawa kutokana na halmashauri kutokuwa na uwezo wa kutunza maeneo na kuyafanyia mpango wa kuyapima kutokana na ukata unaoikabili idara ya ardhi.
Kutokana na ukata huo wakazi wengi wa mji wa Mugumu wamejimilikisha maeneo kinyamera  ama wengine wanagawiwakinyume cha utaratibu  na wataalam wa idara hiyo na kupelekea kukithiri kwa migogoro ya ardhi.
Kwa mjibu wa Taarifa ya afisa ardhi wilaya Orwaka Nyamususa kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo amebainisha kuwa vitalu J na K katika maeneo ya Magereza na Matare viwanja vina milikiwa kimila na wananchi ikiwa ni kinyume cha utaratibu.
Na kuwa serikali ilipaswa kuvitambua na kwa msingi huo haipati kodi ya ardhi ,na kikubwa ni kuwa hawana vifaa vya kupimia kama darubini ya kisasa ili wazalishe viwanja na matokeo ni ujenzi holela katika maeneo ambayo hayajapimwa.
“Halmashauri haina takwimu sahihi kuhusu kodi kwa mwaka…viwanja vyenye kumb.932 kitalu A,B,C,D,E,F,G,H,J,na K viwanja 250 kitalu A-G mmiliki wake hajulikani…vingine hakuna takwimu sahihi kodi wanayotakiwa kulipwa wala ukubwa wa viwanja”amebainisha.
Na kuwa kumbukumbu zinazotakiwa ni kubaini viwanja vilivyopimwa,andaliwa,hati miliki,barua za toleo,visivyoendelezwa,waliokiuka masharti ya uendelezaji,zinazolipiwa kodi ,zisizolipiwa ,maeneo hatari kwa makazi ,zenye mashauri mahakamani na migogoro ya umiliki.
Pia miliki zilizotolewa kituo cha uwekezaji(TIC)mashamba yaliyopimwa,hati miliki za kimila yaliyohaulishwa na kimilikishwa au yaliyotelekezwa.
Pamoja na kuwa na mchakato wa kuifanya mamlaka ya mji mdogo kuwa mamlaka maeneo mengi ya wazi yanavamiwa na kugeuzwa makazi kinyamera na wanaoongoza mchezo huo ni viongozi wa serikali hali ambayo inadaiwa kuchangiwa pia na idara hiyo ya ardhi.
Aidha inadaiwa kuwa watalaam wa idara hiyo wamejimilikisha viwanja vingi kinyamera ambavyo huvitumia kwa kuuza kwa watu na hiyo inachangia kutokuwepo kwa kumbukumbu sahihi za wamilikaji wa baadhi ya viwanja .
Licha ya kutambua matatizo hayo ambayo yanapelekea kukithiri kwa migogoro baadhi ya watumishi wanaohusika wanalindwa na baadhi ya madiwani kwa misingi ya ukabila ,na hatua huchukuliwa haraka kwa wale ambao si wazawa wa wilaya hiyo wanapobainika kukosea ,lakini kwa wazawa hulindwa na matokeo yake halmashauri hiyo inashitakiwa katika mabaraza ya ardhi na wananchi.
Mwisho.

1 comments:

Unknown said...

Hii kazi kwa mwendo huo tutafika kweli?

Post a Comment