Subscribe:

Ads 468x60px

MAAFISA WA POLISI NA USALAMA WA TAIFA WALIOKUTWANWAKICHIMBA DHAHABU HIFADHINI WAPANDISHWA KIZIMBANI

MAAFISA WA USALAMA WALIOKUTWA WAKICHIMBA DHAHABU WAPANDISHWA KIZIMBANI.

Na Mwandishi wetu- Machi 7,2013.
MUSOMA.

HATIMAYE maafisa  wa polisi na usalama wa Taifa waliokutwa wakichimba
dhahabu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara  wamefikishwa
katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mara  wakikabiliwa na
makosa 6 ya uhujumu uchumi.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni karibu mwaka mzima toka wamekamatwa katika tukio hilo lililohusisha raia watano ambao walifikishwa mahakamani baada ya siku 2 toka wamekamatwa,huku maafisa hao wakihamishwa vituo vya kazi.

Waliofikishwa mbele ya mahakama hiyo ni SSP Paulo Cathbert
Mng’ong’o(56)aliyekuwa Ocd Serengeti,Said Mussa(44)aliyekuwa ofisa
usalama wa Taifa na dreva wa polisi E 933 koplo  Frematus
Fredrick(42).

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wakili wa serikali Valensi Mahenga
mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Emmanuel Loitare Ngigwana
walitenda makosa hayo machi 24,2012 katika eneo la kilima fedha ndani
ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wakili huyo aliyataja makosa yanayowakabili kuwa ni kula njama kwa
lengo la kufanya kosa na kutenda kosa ,kuingia hifadhini kinyume cha
sheria.

Makosa mengine ni kukutwa na silaha ndani ya hifadhi kinyume cha
sheria ,kufanya uchimbaji wa dhahabu ndani ya hifadhi ya taifa kinyume
cha sheria,kupatikana na dhahabu ambayo haijasafishwa kinyume cha
sheria na kukutwa na zana za milipuko ndani ya hifadhi kinyume cha
sheria.

Washitakiwa wamekana mashitaka na wako nje kwa dhamana na kesi hiyo
itatajwa machi 19 mwaka huu.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limemfukuza kazi aliyekuwa dreva wa
polisi koplo Frematus Fredrick mwenye namba  E 933 huku aliyekuwa  SSP
Mng’ong’o  akiwa amesimamishwa kazi kutokana na cheo chake.

Katika tukio hilo maafisa hao pi a walikamatwa na raia watano
walioingia nao ndani ya hifadhi kwa ajili ya kutenda uharifu huo ambao
tayari walishafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa
wilaya ya Serengeti.

Washitakiwa wengine ambao ni raia walifikishwa mbele ya hakimu wa
mahakama ya wilaya Amon Kahimba machi 26,2012 wakikabiliwa na makosa 5
, huku kwa upande wa maafisa hao ikidaiwa kuwa uchunguzi na taratibu
za kijeshi zilikuwa zinaendelea.

Makosa hayo ikiwa ni  kuingia ndani ya hifadhi ya Taifa bila
kibali,kupatikana na silaha bila kibali,kufanya uchimbaji wa dhahabu
ndani ya hifadhi bila kibali na kupatikana namifuko 10 mawe ya madini
ya dhahabu kinyume cha sheria. Kosa lingine likiwa ni kukutwa na vifaa
vya milipuko ndani yahifadhi
.
Washitakiwa hao ni Mniko Nyamhanga Mwita (30)mkazi wa Matare,Jonas
Marwa Chacha (42)mkazi wa Mugumu mjini,Maiga James Maganjala(26)mkazi
wa Bunda .
Wengine ni Mwita William King’eti(30)mkazi wa Mugumu na Alex
Peter(29)Mwalimu wa sekondari Kambarage iliyoko mjini Mugumu

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi aprili mwaka huu baada
ya upande wa mashitaka kudai upelelezi umekamilika.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment