Subscribe:

Ads 468x60px

POLISI WAKANUSHA KUKAMATA MAGAIDI WENYE SILAHA WAKIKUSUDIA KUMUUA PAROKO BUTIAMA


POLISI WAKANUSHA KUKAMATA MAGAIDI WENYE SILAHA WAKIKUSUDIA KUUA PAROKO.
Na Anthony Mayunga-Musoma
Machi 9,2013.

JESHI la polisi Mkoani Mara limekanusha ujumbe unaosambazwa kwa njia ya simu  kuwa limekamata magaidi wawili toka Somalia wakiwa na bastola wilayani Butiama wakiwa na lengo la kumuua Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Butiama Matheus raia wa Poland kuwa ni uongo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma alisema ujumbe huo hauna ukweli wowote na unasambazwa na watu wenye ni uchochezi wa imani za kidini.
Alisema watu wanaosambaza ujumbe huo wanalenga kusababisha migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislam kwa kuwa wanadai kuwa magaidi hao walikuwa wamejificha kwa Shekhe mkuu wa wilaya ya Butiama kwa muda wa wiki nzima ili kutekeleza mauaji hayo.
“Habari hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa jeshi la polisi halijamkamata msomali wala silaha yoyote…huo uvumi unalenga kuwatia hofu wananchi”alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kutokuwa na hofu kuhusiana na watu wanaosambaza ujumbe wa uchochezi na kuwa watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili wahusika waweze kukamatwa.
Paroko na shehe hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia taarifa hiyo,juhudi za kuwatafuta zinaendelea.
Mwisho.








0 comments:

Post a Comment