MIKAKATI MIZURI YA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA MUGUMU WILAYANI SERENGETI KUONDOA TAKA MJINI,ZINAELEKEA KUSABABISHA MADHARA KWA VIBARUA HAO KUTOKANA NA MAMLAKA HIYO KUTOWAPA VIFAA MAALUM VYA KUJIKINGA WAFANYAPO HIYO KAZI,AMBAPO BAADHI WANASHIKA UCHAFU BILA VYOMBO VYA KUJIKINGA
VIBARUAWAKIWA KAZINI,HATA HIVYO WANALALAMIKIAUJIRA MDOGO UKILINGANISHA NA KAZI WAIFANYAYO.
MAMA HUYO HANA GLOVUS LAKINI ANAENDELEA NA KAZI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
Matokeo darasa la saba; Ufaulu waongezeka
Na Fredy
Azzah, Mwananchi
Posted Jumapili,Novemba3 2013
Kwa ufupi
- Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde
aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka
jana.
Dar es Salaam.
Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba
mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo
yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89
ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema jumla ya
watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia
50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.
Dk Msonde alisema
kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68
na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01.
Matokeo hayo pia
yanaonyesha kuwa, wanafunzi wengi wamefanya vibaya zaidi kwenye somo la
Hisabati huku wakifanya vizuri kwenye somo la Kiswahili.
Dk Msonde alisema
wavulana wamefanya vizuri zaidi kwenye mtihani huo ukilinganisha na wasichana.
Alieleza pia kuwa,
mwaka huu udanganyifu kwenye mtihani huo umeshuka kwa kiasi kikubwa, kwani
waliofutiwa matokeo ni 13.
Dk Msonde alisema
kati ya hao, watano walibainika kukariri mtihani huo jambo ambalo kisheria
hawaruhusiwi na wengine walikamatwa na karatasi za majibu kwenye vyumba vya
mtihani.
Ufaulu
Alisema miongoni
mwa waliofaulu, wenye ulemavu ni 476, kati yao wasichana wakiwa ni 219 sawa na
asilimia 46.01 na wavulana ni 257 sawa na asilimia 53.99.
Dk Msonge alisema
kuwa, mwaka 2012 watahiniwa waliopata zaidi ya alama 100 walikuwa ni asilimia
30.72, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 19.89.
Kuhusu sababu za
ongezeko la ufaulu, Dk Msonde alisema baraza bado halijafanya tathmini ya
kubaini chanzo cha ongezeko hilo.
isi
tulicholetewa ni kile kilichofanyika kwenye chumba cha mtihani na haya hapa
ndiyo majibu yake,” alisema Dk Msonde.Ufaulu kimasomo
Alisema mwaka huu ufaulu kwa masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya sita mpaka 28.06, ikilinganishwa na mwaka 2012.
Somo ambalo watahiniwa wengi wamefanya vizuri ni Kiswahili ambalo ufaulu wake umefikia asilimia 69.62 na walilofeli zaidi ni Hisabati ambalo ufaulu wake ni asilimia 28.62.
Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka 2012 ufaulu kwenye somo la Kiswahili ulikuwa ni asilimia 41.00 na Hisabati ulikuwa ni asilimia 18.74.
Kwenye somo la Kiingereza ufaulu mwaka huu ni asilimia 35.52 wakati mwaka jana ilikuwa ni asilimia 21.06, huku kwa Sayansi mwaka huu ufaulu ukiwa ni asilimia 47.49 na mwaka jana ilikuwa ni asilimia 41.48 na Maarifa ya Jamii mwaka huu ufaulu ni asilimia 53 na mwaka jana ilikuwa asilimia 28.61.
Usahihishaji wa mashine ni bora zaidi
Alisema ili kujiridhisha na usahihishaji wa kutumia Mashine Maalumu za OMR (Optical Mark Reader), sampuli 20,795 za karatasi za majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 za mikoa tisa ya Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga zilisahihishwa kwa mkono.
Alisema baada ya kufanya ulinganifu wa usahihi wa karatasi zilizosahihishwa kwa mkono na zile zilizosahihishwa kwa mashine, ilibainika kuwa zile zilizosahihishwa kwa mashine zilikuwa na usahihi wa hali ya juu.
“Usahihishaji wa kutumia kalamu ulikuwa na makosa machache ya kibinadamu, makosa hayo yalikuwa ya kukosea kusahihisha swali kwa kutumia mwongozo wa usahihishaji na dosari za kujumlisha alama,” alisema Dk Msonde.
Alibainisha kuwa, kati ya sampuli za karatasi za watahiniwa 20,795 zilizosahihishwa kwa mkono, 249 sawa na asilimia 1.2 ndizo zilizobainika kuwa na makosa aliyosema ni ya kibinadamu.
Mbali na usahihi wa usahihishaji, alisema pia mfumo huo umesaidia kupunguza wasahihishaji kutoka 4,000 waliokuwa wakitumika awali na kufikia 301 waliofanya shughuli hiyo mwaka huu.
Alibainisha pia kuwa, OMR imepunguza siku za kusahihisha mtihani huo kutoka 30 za awali mpaka 16 zilizotumika mwaka huu.
Waliofanya mtihani
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa ni 867,982 wakiwamo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.
Alieleza kuwa, kati ya watahiniwa hao walikuwemo wenye ulemavu wa kuona, 597 walikuwa na uono hafifu na wengine 88 ni wasioona.
“Watahiniwa 844,938 sawa na asilimia 97.34 ya waliosajiliwa walifanya mtihani huo. Wasichana walikuwa 446,115 sawa na asilimia 99.85 na wavulana walikuwa 398,823 sawa na asilimia 96.78,” alisema Dk Msonde.
Alisema kuwa, watahiniwa ambao walisajiliwa na hawakufanya mtihani huo ni 23,045 sawa na asilimia 2.66, kati yao wasichana wakiwa 9,781 sawa na asilimia 2.15 na wavulana 13,264 sawa na asilimia 3.22.
Alieleza kuwa utoro na ugonjwa ni miongoni mwa sababu za wanafunzi hao kutofanya mtihani huo.
Lengo la BRN halijafikiwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa akizungumza katika warsha ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN-Big Results Now), kwenye sekta ya elimu iliyotolewa kwa watendaji wa elimu ngazi ya kanda, mkoa na wilaya, Agosti 14, mwaka huu, alisema moja ya lengo la mpango huo ni ufaulu kwa darasa la saba mwaka huu kufikia asilimia 60 kutoka 31 ya mwaka jana.
“Katika kutekeleza vipaumbele hivyo, kila mmoja wenu atakuwa na eneo la kutekeleza na atapimwa kutokana na utekelezaji katika eneo lake, hii ni katika kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka huu ufaulu katika elimu ya msingi unaongezeka kutoka asilimia 31 hadi kufikia 60,” alisema Dk Kawambwa.
Mara baada ya Dk Kawambwa kutangaza suala hilo, baadhi ya wadau walisema itaongeza hali ya kupata matokeo yasiyo halisi kwani hakukuwa na muda wa kuandaa mikakati ya kufikia lengo hilo, kwani mpango huo ulitangazwa Agosti na Septemba watoto wa darasa la saba walikuwa wanaanza mitihani.
Kenyan MPs pass harsh media law
The East Africa News
Kenyan Parliament during a past session. Kenyan MPs
have passed a new draconian media law that imposes harsh penalties on
Journalists
By John Ngirachu, The Citizen
Posted Saturday, November 2 2013
Posted Saturday, November 2 2013
In Summary
- Journalists now face punitive measures for
violating the Code of Conduct for journalists, including fines of up to
Sh20 million.
Nairobi. Kenyan parliament
has passed a new draconian media law that imposes harsh penalties on
journalists.
Journalists now face punitive
measures for violating the Code of Conduct for journalists, including fines of
up to Sh20 million.
They also risk being deregistered and
their bank accounts frozen.
MPs Thursday evening voted to create
a tribunal that will handle complaints against the media and have power to
impose the harsh penalties.
This happened through the
introduction of a surprise change to the Kenya Information and Communication
Bill, which was passed last evening with 17 per cent of MPs (60) present in the
chambers in the National Assembly.
The House accepted a proposal by the
Energy, Information and Communication Committee for the creation of Communications
and Multimedia Appeals Tribunal.
The Tribunal would have the power to
“impose a fine of not more than Sh20 million on any respondent media
enterprise…adjudged to have violated either that law or the Code of Conduct for
the Practice of Journalism.”
It has the power to fine individual
journalists “not more than Sh1 million” for violating the same code.
It would also get worse because the
fine would be a debt, meaning the person or organisation found to have broken
the law would be liable to have his bank accounts raided or their property sold
off for misreporting.
The tribunal also has the power to
“recommend the suspension or removal from the register of the journalist
involved.”
It has also been granted the power to
make any orders it feels would be necessary to carry into effect the orders or
directives it would make. Proposed by Energy Committee chairman Jamleck Kamau,
the creation of this tribunal was among amendments introduced with a mere 28
MPs in the chambers.
Only a handful shouted aye when the vote
was called for but the fact that there was no one in opposition was taken as
evidence that all were in agreement.
As they were going
through the amendments, Majority Leader Aden Dualle and Mr Kamau detected that
the Bill was not going to be passed without the quorum of 50 MPs and they
rushed out to get the rest to come in.
“This is a
controversial and good law but the members are not here. This House is more
full when passing other Bills,” Mr Dualle would later say.
After that, the 32
who hadn’t been in the House came in and helped bring the numbers up to 60 and
then Speaker Justin Muturi called for the verbal vote, the ayes had it and the
Bill was passed.
MIKAKATI YA MATOKEO MAKUBWA SASA
BRN imezinduliwa agosti 14 mwaka huu.
1. Upangaji wa shule kwa ubora wa
matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule
iliyoongoza hadi ya mwisho. Lengo la mkakati huu ni kuongeza uwajibikaji na ushiriki wa
jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora.
2. Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi.
3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule kutekeleza majukumu yao kikamilifu
4. Upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata
5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili. Mafunzo atatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.
6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.
7. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu shuleni.
8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
9. Utoaji wa motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.
2. Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi.
3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule kutekeleza majukumu yao kikamilifu
4. Upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata
5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili. Mafunzo atatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.
6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.
7. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu shuleni.
8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
9. Utoaji wa motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.
Wasomi wadai mabadiliko mitihani ya sekondari ni siasa tu
Na Fredy Azzah, Mwananchi
Posted Novemba2 2013
Posted Novemba2 2013
Kwa ufupi
- Baadhi ya wadau hao
wakizungumza na gazeti hili jana, walisema Tanzania imeweka rekodi kwa
nchi za Afrika kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha ufaulu cha alama F
kuanzia 0 mpaka 19.
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Serikali kutangaza kupunguza viwango vya ufaulu kwa
mtihani ya kidato cha nne na sita, baadhi ya wasomi na wadau wa elimu wameponda
uamuzi huo na kusema una malengo ya kisiasa.
Baadhi ya wadau hao wakizungumza na gazeti hili jana, walisema Tanzania
imeweka rekodi kwa nchi za Afrika kwa kuwa na kiwango kidogo sana cha ufaulu
cha alama F kuanzia 0 mpaka 19.
Walisema, Serikali imechukua uamuzi huo kisiasa ili kuhakikisha kuwa,
wanatimiza lengo la Mpango wa Maendeleo Makubwa Sasa (BRN), ambalo ni
kuhakikisha matokeo ya ufaulu kwa Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu yanafikia
asilimia 60 kutoka 33 ya mwaka jana.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Herme Mosha
alisema kuwa kilichofanywa na Serikali ni kupanua wigo wa watu kufaulu.
“Wanataka watu ambao walikuwa wanapata daraja la nne wapate daraja la
tatu, daraja la tatu wapate la pili na la pili wapate la kwanza.
Hata hivyo, kwa muda wote, wadau wa elimu ambao wanataka siyo kuona tu
watu wanafaulu, wanataka elimu iliyo bora. Kwa hatua hii waliyoichukua
haitasaidia lolote katika kuongeza ubora wa elimu ambao umekuwa kilio cha muda
mrefu,” alisema Profesa Mosha.
Alisema kuwa, washikadau wengi wangependa kuona ubora wa elimu
umeongezeka na siyo kuongeza wigo wa ufaulu.
“Huku ni kujidanganya, jambo la kwanza wangetakiwa waende katika shule
mbalimbali waone ni nini walimu wanataka, tatizo lipo wapi halafu wachukue
hatua kwa sababu ukiangalia sasa ni kama kuna mgomo fulani hivi,” alisema.
Kwa upande wake Dk Kitila Mkumbo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Saikolojia
ya Elimu na Masomo ya Mitalaa ya Shule Kuu ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, alisema tatizo la elimu Tanzania halijawahi kuwa ni viwango vya
ufaulu.
“Wanataka tu kuona hiyo asilimia 60 waliyojipangia inafikiwa.
Walijiwekea lengo hilo wakijua kabisa kwenye elimu hakuna miujiza, lazima mtu
ufanye kazi ndiyo matokeo yaonekane,” alisema.
Alisema kiwango cha kufeli kilichowekwa kinaifanya Tanzania kuwa nchi
yenye viwango vidogo sana vya elimu kwenye bara hili.
“Burundi wenyewe mtoto akipata 50 ndiyo anakuwa amefeli, sisi huku
tumeweka mpaka 19 ndiyo tunasema amepata hiyo F, lakini bado tunaita amefaulu,
huu ni utani,” alisema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT),
Ezekia Oluoch alisema Matumizi ya Alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA) ni
suala la kupongeza.
Hata hivyo, alisema kuwa kuna matatizo ya msingi kwenye elimu na ni
lazima yafanyiwe kazi.
“Lengo lao la kushusha ufaulu ni ili ionekane kuwa BRN imefikia lengo,
watoto wamefaulu ndiyo iwe furaha yao,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania
(TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema wamepokea suala hilo kwa mikono miwili.
“Zamani mtu alikuwa amapata sifuri na mwingine 33 wote tunasema wamepata
F, lakini sasa kuna utofauti kwa hiyo unaweza kuona ni namna gani uwatumie hawa
watu.
Pia suala hili linatoa mwanya mpana hata kwa Serikali na taasisi
nyingine za elimu, ikitokea kwamba watu wa C wamekosekana unaweza kuona sasa
tutumie wapi,” alisema.
Alisema kuwa, kwa sasa sera ya elimu inasema watu watakaoingia kidato
cha tano wanatakiwa wawe na C tatu, lakini mwaka huu Serikali ilichukua C moja
na D mbili wakaenda kidato cha tano.
“Yote hii ni kwa sababu hakukuwa na njia mbadala, lakini kwa sasa
kutakuwa na mianya mingi sana.
Hata hivyo, tujue kuwa, tatizo la elimu Tanzania halikuwa madaraja, hii
ilikuwa ni sehemu tu, lazima tuhakikishe tunatafuta matatizo ya msingi ya elimu
yetu tuyafanyie kazi. Tukibaki kwenye hizi alama, basi nchi yetu itakwenda
shimoni,” alisema.
Polisi mbaroni kwa kupora Sh220 mil
Na Daniel Mjema,Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Wadaiwa kuwa wamesharejesha Sh80 milioni baada ya kubanwa na makachero
wa polisi.
Moshi. Askari polisi wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wametiwa
mbaroni kwa tuhuma za kula njama na kushiriki katika uporaji wa Sh220 milioni
za Kampuni ya Dot Services ya mjini Moshi.
Habari za uhakika zilisema baada ya kubanwa na makachero, askari hao
walirejesha Sh60 milioni na watuhumiwa wengine wawili ambao ni raia,
walirejesha Sh23 milioni. Askari hao ni wale walioko katika Kikosi cha Polisi
wa doria wanaotumia pikipiki na jana watuhumiwa wote walitawanywa katika vituo
mbalimbali ili wahojiwe kwa nyakati tofauti tofauti.
Habari za kipolisi zilisema askari hao hawakwenda eneo la tukio lakini
walifahamu mpango mzima kuhusu uporaji huo uliowawezesha kupata mgawo wa fedha
hizo.
Waliotiwa mbaroni wana vyeo vya Constable (majina tunayo) na inaelezwa
kuwa tukio hilo limewachukiza baadhi ya polisi wakidai ni kuwa mfululizo wa
matukio yanayochafua sura ya jeshi hilo.
Habari hizo zimebainisha kuwa tukio hilo ni mpango mahususi
uliowashirikisha watu wasiopungua 10 wakiwamo baadhi ya watumishi wa Kampuni ya
Dot Services waliovujisha mpango wa kuhamisha fedha hizo.
Kulingana na vyanzo vya habari, idadi ya walioshiriki katika mpango wa
kupora fedha hizo ni kati ya watu wanane na 10 na tayari polisi wameanzisha
msako mkali wa kuwatafuta.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alikaririwa akisema
kuwa fedha hizo ziliporwa Jumanne asubuhi katika makutano ya Barabara za Arusha
na Boma mjini Moshi.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, baada ya kufika katika makutano hayo,
wafanyakazi wa Kampuni ya Dot Services waliokuwa na gari aina ya Toyota Hilux
T.864 AZM walisimama kuruhusu pikipiki ipite.
Kamanda Boaz alisema wakati wakisubiri pikipiki ipite, ghafla
walijitokeza watu wawili wakafungua milango na kuingia ndani ya gari na
kuwateka wafanyakazi na kuwaamuru waelekee eneo la Shanty Town.
Hata hivyo mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo ya ujenzi yenye makao
yake makuu nchini Uganda, Shuresh Bab alifanikiwa kuruka kwenye gari hilo na
kutoa taarifa polisi.
Kamanda Boaz alifafanua kuwa msako wa kuwatafuta wahusika ulianza mara
moja ambapo polisi walifanikiwa kulipata gari hilo na wafanyakazi wakiwa
wametelekezwa mto Karanga mjini Moshi.
Mabadiliko makubwa mitihani ya sekondari
Posted Ijumaa,Novemba1 2013
Kwa ufupi
Akifafanua zaidi juu ya alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA), alisema
kuwa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 inayotumika mpaka sasa inataka alama hizo ziwe
50 na zile za mtihani wa mwisho ziwe 50.
Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kuanza
mtihani wa kumaliza ngazi hiyo ya elimu, Serikali imepunguza alama za ufaulu
kwa mtihani huo pamoja na ule wa Kidato cha Sita.
Pia imetangaza kuwa, mtihani wa taifa wa kidato cha nne na sita utakuwa
na alama 60 za ufaulu, huku alama 40 zilizobaki zitatokana na zile za maendeleo
ya mwanafunzi shuleni (CA).
Katika mfumo huo mpya, wizara hiyo pia imefuta daraja la sifuri na
badala yake kutakuwa na daraja la tano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni
Mchome alitangaza uamuzi huo wa Serikali jana kwa kueleza utekelezaji wa
utaratibu huo utaanza kwenye mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka huu.
“Hatua hii imechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza kuanzia
mwaka 2011. Tangu wakati huo kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo yamekuwa
yakifanyika,” alisema Profesa Mchome.
Alisema kuwa, alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la
Taifa (Necta) katika kupanga matokeo hayo, kwa kidato cha nne ni A=80-100,
B=65-79, C=50-64, D=35-49, F= 0-34 kwa upande wa kidato cha sita A=80-100,
B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alisema mfumo mpya, umehusisha alama za kidato cha nne na cha sita na
kuwa kuanzia sasa A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na
F=0-19.
“Alama A itakuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ itakuwa ni ufaulu bora
sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu
sana na F ufaulu usioridhisha kabisa,” alisema Profesa Mchome.
Alisema pia kuwa, wamebadilisha mfumo wa madaraja ambao awali kulikuwa
na daraja la kwanza, la pili, la tatu, la nne na sifuri.
“Lile la sifuri tumeliondoa, badala yake kutakuwa na daraja la tano,
lengo ni kuweka mlolongo mzuri zaidi,” alisema.
Alisema, alama hizo zitakuwa ni mgando (fixed grade range).
Profesa Mchome alisema kuwa, utaratibu wa sasa wa kupanga matokeo hayo
kwa madaraja, utabadilika muda wowote kuanzia sasa na kwamba utakaokuwa
ukitumika ni ule wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Point Average ‘GPA’).
Mfumo huu kwa sasa unatumika kwenye ngazi za
vyuo. “Huu mfumo wa madaraja unaotumika sasa ni wa mpito tu, mwakani ama hata
kabla ya hapo tunaweza kuanza kutumia mfumo wa GPA,” alisema.Akifafanua zaidi juu ya alama za Maendeleo ya Mwanafunzi (CA), alisema kuwa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 inayotumika mpaka sasa inataka alama hizo ziwe 50 na zile za mtihani wa mwisho ziwe 50.
Kwa upande wa Zanzibar, alisema CA ilikuwa alama 40 na mtihani wa mwisho alama 60, ingawa alisema utaratibu huo haukuwahi kutumika kwa Zanzibar wala Bara.
Aliongeza kuwa hali hiyo ilisababishwa na kutokuwa na utaratibu wa kupata alama sahihi alizopata mwanafunzi shuleni kwani walimu wengi wamekuwa wakituma alama za uongo kwa kuwaongezea wanafunzi alama.
Alisema, utaratibu mpya wa kupata CA itakuwa ni mtihani wa kidato cha pili utachangia alama 15 mitihani ya mihula miwili ya kidato cha tatu kila muhula utachangia alama tano, Mtihani wa Kanda wa kidato cha nne alama 10 huku kazi mradi (project) zikitoa alama tano.
“CA zitatumika pia kwa watahiniwa wa kujitegemea, zile CA zao ambazo walimaliza nazo kidato cha nne hazitatupwa, wakitaka kurudia mtihani hizo alama zao zitajumlishwa kwenye mtihani wa mwisho.
Hata hivyo, alisema kuwa, kwa kuwa tayari shule nyingi zimeshawasilisha CA Baraza la Mitihani, alama 40 kwa mwaka huu zitapatikana tu kwa kuangalia alama hizo zilizopelekwa na shule ambazo hupatikana kwa kuangalia mitihani ya mihula kuanzia ule wa kidato cha kwanza. Kwa wale waliofanya mtihani wa QT (Qualifying Test), alama zao hizo za QT zitachukuliwa 40 kuongezwa kwenye mtihani wa kidato cha nne,” alisema Profesa Mchome.
Alisema kuwa, mfumo huo mpya hautabadilika mara kwa mara na kuwa, utamaliza mzunguko mmoja ambao ni wa miaka minne.
Kidato cha nne kuanza mitihani
Katika hatua nyingine Profesa Mchome alisema, Novemba nne wanafunzi wa Kidato cha nne nchi nzima wataanza mitihani yao ya mwisho ambayo wataimaliza Novemba 21.
“Mitihani hiyo imetanguliwa na ile ya vitendo ya masomo ya Food and Nutrition iliyofanyika Oktoba 7, mpaka 24 mwaka 2013,” alisema.
Alisema kuwa, watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani huo ni 427,906
ambao kati yao 367,399 ni watahiniwa wa shule na 60,507 ni watahiniwa wa
kujitegemea.
Alisema kuwa, kati ya watahiniwa wa shule 367,399 wavulana ni 198,257
sawa na asilimia 53.96 na wasichana ni 169,142 sawa na asilimia 46.04.
Alisema kuwa, kati ya watahiniwa 60,507 wa kujitegemea walioandikishwa,
wanaume ni 30,456 sawa na asilimia 50.33 na wasichana ni 30,051 sawa na
asilimia 49.67.
Alisema kuwa, watakaofanya Mtihani wa Maarifa (QT) walioandikishwa ni
18,214, kati yao wavulana ni 7,222 sawa na asilimia 39.65 na wasichana ni
10,992 sawa na asilimia 60.35 .
Wadau
Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Habari na Utetezi, Nyanda Shuli
alisema anaipongeza wizara kwa kuamua kutumia CA ingawa alisema ni lazima kuwe
na mfumo wa kuhakikisha alama hizo zinaonyesha uwezo halisi wa mwanafunzi.
Kuhusu kushusha kiwango cha ufaulu, alisema kuwa Serikali inapaswa kutoa
sababu iliyoifanya kuchukua hatua hiyo.
“Kama wanahofia jinsi matokeo ya mwaka jana yalivyokuwa siyo sahihi,
dawa ni kufundisha kwa makini zaidi,” alisema Nyanda.
Dk Joyce Ndalichako
Katika mahojiano, ambayo Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako,
aliwahi kufanya na gazeti hili, alisema ni vigumu kutumia alama za Maendeleo ya
Mwanafunzi (CA) kwani kwa kiasi kikubwa walimu hudanganya.
“Wafanyakazi wa baraza ni wachache, hatuwezi kwenda kila mahali ili tuhakikishe
alama hizo, mwaka 2011 wale wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka kwenye
mitihani yao ya mwisho, kwenye CA walikuwa wana mpaka alama 75.
Tulipowauliza walimu
wengine walisema hawakuwa na walimu waajiriwa wa Serikali na waliokuwa
wanawatumia ni wale waliomaliza kidato cha sita kwa hiyo hawajui kupanga hizo
alama, wengine walisema mitihani hiyo haina usimamizi makini,” alisema Dk
Ndalichako
KULALIA JAMVI KWA MFANYA ACHOME GODORO LA JILANI YAKE NA KUMUUNGUZA MTOTO
MTOTO KELVIN MARWA WA MIAKA MIWILI AMELAZWA KTK HOSPITALI TEULE YA NYERERE WILAYA YA SERENGETI AKIWA NA MAMA YAKE JACKLINE ANAYEMUUGUZA MAJERAHA YA KUCHOMWA MOTO NA JILANI YAO KUTOKANA NA WIVU WA KULALIA GODORO WAKATI YEYE ANALALIA JAMVI
Serengeti:
WIVU wa kukosa godoro
umempelekea mwanamke mmoja wa
mtaa wa uwanja wa mbuzi mjini Mugumu wilayani Serengeti kuchoma godoro la
jilani yake na kumuunguza vibaya mtoto
wakati amelala.
Tukio hilo la aina yake
limethibitishwa na polisi wilayani hapa na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Esther Juma linadaiwa kutokea oktoba 30 majira ya saa 1:00 asubuhi ambapo
mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Kelvin Marwa(2)ameungua sehemu mbalimbali za
mwili na amelazwa hospitali ya wilaya kwa matibabu.
Akisimulia mkasa huo mama mzazi
wa mtoto huyo akiwa hospitalini
Jackiline Godfrey(20)alisema wamekuwa na ugomvi na mtuhumiwa ambaye ni
jilani yake baada ya kuwa amenunua godoro na yeye analalia jamvi,na siku hiyo akaamua kuchoma godoro na kumuunguza
mwanae.
“Nilitoka saa 12:00 alfajiri kuwahi
kibaruani stendi kwenye mgahawa ninakofanya kazi…nikaacha mwanangu
amelala…hurudi mapema kumwandalia chai ama uji…nikiwa kazini majira ya saa 1:00
asubuhi nilifuatwa na mtoto wa
jilani..akasema Kelvin ameungulia ndani---niliishiwa nguvughafla…kwenda
nikakuta majilani wamebomoa mlango na mtoto ameungua vibaya”alisema huku
akifuta machozi.
Alisema mbali na mtoto kuungua
pia nguo na vitu vingine viliungua vyote
kutokana na unyama huo uliofanywa na jilani yake ambaye amekuwa akimwapia
kumkomesha kwa yeye kununua godoro na kumwacha yeye akilalia jamvi.
Baadhi ya mashuhuda walisema
walimwona mtuhumiwa akitoka ndani ya chumba kilichoungua akikimbia ,ghafla
wakaona moshi na sauti ya mtoto ikisikika akilia kwa sauti kali ,katika
kufuatilia wakabaini mtoto anaungua wakabomoa mlango na kumnusuru mtoto huyo.
“Kilichomsadia mtoto baada ya
kuanza kuungua alijivuta hadi kwenye kona na kuacha godoro linaungua….kwa kweli
ni unyama mkubwa sana aliokuwa anaufanya huyo mwanamke….kulalia jamvi
kunampelekea kutaka kumuua huyo mtoto…kwa kweli kama polisi wasingewahi
angeuawa”alisema shuhuda.
Balozi wa nyumba 10 eneo hilo
Janet Samwel alisema baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa alianza kupigwa na kama
si polisi kufika eneo hilo mapema huenda angeuawa kwa kuwa wananchi walikuwa na
hasira kali dhidi ya ukatili huo.
Mratibu wa dawati la jinsia la
polisi wilaya WP 5665 D/S Sijali Nyambuche alisema walilazimika kufika haraka
eneo la tukio baada ya kupata taarifa za tukio ,wakabaini kuwa huenda kukatokea
maafa kwa mtuhumiwa kutokana na mazingira ya tukio na hasira za wananchi.
“Kama tusingewahi ingekuwa mbaya
zaidi…tulimnusuru mtuhumiwa na tunamshikilia ..taratibu zikikamilika
atafikishwa mahakamani wakati wowote”alisema.
Muuguzi wa zamu wodi ya watoto
Mwangwa Samson alisema mtoto huyo ameungua makalio,miguu na sehemu za siri kwa
asilimia 30 na kuwa hawezi kukaa kutokana na majeraha aliyopata,na juhudi za
madaktari na waganga zinaendelea kuhakikisha anapona.
Mwisho.
MAJAMBAZI YA MIFUGO YAJERUHI WAWILI KWA RISASI.
Serengeti:
WATU wawili wamelazwa katika
hospitali ya wilaya ya Serengeti baada ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa
kuwa wezi wa mifugo wakati wanafuatilia nyayo.
Mganga mwandamizi katika
hospitali hiyo Dk.Tanu Waryoba amewataja majeruhi hao kuwa ni Chacha
Megera(39)na Marwa Nyakimwi(21) wote wakazi wa kijiji cha Nyahende wilayani
hapa.
Amesema Megera alipigwa risasi
mguu wa kushoto na Nyakimwi kwenye nyonga mguu wa kulia na kutokea paja la mguu
wa kushoto,na kuwa wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu .
Megera akiwa kitanda namba 12
wodi ya wanaume alikolazwa alisema oktoba 28 majira kati ya saa 4-5 usiku mwaka
huu kulitokea wizi wa ng’ombe 9 nyumbani kwao wakati wamelala.
“Mke wa kaka yangu Kibibi Ntare
alipotoka nje kujisaidia alibaini wizi huo…alipiga yowe kwa kushirikiana na
wanakijiji tukaanza kufuatilia nyayo tukiwa tunakimbia…kufika eneo la mto
Nyahende …tukishangaa ghafla nikapigwa risasi mguu wa kushoto”alisema.
Alisema alishindwa kuendelea na
safari hiyo kutokana na maumivu makali na kulazimika kurudishwa nyumbani na
kupelekwa hospitali kwa matibabu.
“Mimi nilipigwa risasi kwenye saa
6 usiku nikiwa miongoni mwa vijana wenzangu tuliokuwa mstari wa mbele…tukiwa
tunakwenda kwa kasi baada ya kuwepo ishara kuwa wezi hawako mbali…ghafla
nilipigwa risasi upande wa kulia wa nyonga na kutokea kushoto…niliishiwa nguvu
na kulala chini”alisema Marwa Nyakimwi.
Nyakimwi aliyelazwa kitanda namba
8 alisema ilibidi akimbizwe hospitali,huku wenzake wakisonga mbele na
kufanikiwa kurudisha ng’ombe wote 9 na kukamata watuhumiwa watatu kati ya sita
waliohusika na tukio hilo.
Hata hivyo polisi walifanikiwa
kuwaokoa watuhumiwa watatu waliokamatwa na mmoja aliyetajwa kwa jina la Mwita
Malitwa(40)amelazwa hospitali ya wilaya chini ya ulinzi wa polisi.
Polisi wanasema wanaendelea na
mahojiano na baadhi ya watuhumiwa na inasemekana watuhumiwa waliofanikiwa
kutoroka walikimbilia maeneo ya Gibaso wilayani Tarime.
Kuhusu bunduki iliyohusika
walisema ni ya kivita kwa kuwa risasi zake zilibainika ni za SMG ambazo
zinatumiwa na bunduki aina ya SRA pia.
Mwisho.
KANISA KATOLIKI LAZINDUKA
ILI kukabiliana na changamoto za
kidunia zinazochangia kuporomoka kwa
Imani ,maadili na ukiukwaji wa utawala bora kwa waumini na viongozi kanisa
Katoliki hapa nchini limeanza kujitathimini na kuweka mikakati mipya.
Akitoa semina wakati wa ibada ya
misa kwa waumini wa kanisa katoliki Parokia ya Mugumu katibu wa baraza la
maketikisa jimbo la Musoma Antony Marwa alisema hatua hiyo ya haraka imetokana
na tafiti zilizofanywa na wataalam wa kanisa na kukabidhi baraza la maaskofu Tanzania.
Alisema licha ya waumini
kuongezeka ndani ya kanisa katoliki imani inazidi kushuka kwa kuwa hawajengwi
kwa misingi mizuri na wanayumbishwa na changamoto nyingi za kidunia ikiwemo
suala la madhehebu mengine.
“Kanisa limeruhusu dunia kuingia
ndani na kuporomosha imani za waumini…watu wanaingia kanisani wamevaa nguo
zisizo na staha …waumini hawasemi,viongozi wa kanisa wako kimya…lakini waumini
wakiulizwa wanasema kanisa linaruhusu….wapi kanisa limeruhusu uchafu kama
huo?”alihoji.
Alikwenda mbali zaidi na kudai
kuwa watakao ingia kanisa na vimini,wanaume wamevaa mregezo na heleni wafukuzwe
kabla ya kuingia,na kwa wanaotoa komnio wasiwape kwa kuwa hawana sifa stahiki.
“Suala la ulevi kuna watu
wanasema kanisa linaruhusu…wapi imeandikwa kwenye biblia kuwa wamewaruhusu
kulewa…muwe watu wa kiasi….haya si maadili mema kwa viongozi wa kanisa na
waumini lazima mageuzi yafanyike ili kujenga imani ya waumini”alisema na
kushangiliwa na kanisa zima.
Akizungumzia suala la utawala
bora kanisani alielezea kuwa viongozi wanaochanguliwa na waumini kuongoza
baraza la walei wanatakiwa kuwa wawazi kwa kutoa taarifa za mapato na matumizi
kwa waumini,ikiwemo vyanzo vyao na jinsi fedha wanazochanga zinavyofanya kazi.
“Kila wakati harambee harambee
kanisani hawasemi zinazochangwa
zinafanya nini…kanisa linakwenda bila bajeti,fedha zinakusanywa kila wiki
zinaishia mifukoni benki haziendi…wekeni bajeti za kuhudumia nyumba za mapadri
na watawa na huduma za kiroho zinazobaki zipelekwe benki”alisema.
Katekista huyo alisema kukosekana
kwa mipango kwenye makanisa kumepelekea elimu ya dini haifundishwi kwa kuwa
walimu wa dini hawalipwi,wanaishi maisha magumu huku fedha zikitumiwa vibaya na
imani ikiporomoka makanisani.
“Maktekista hawathaminiwi wakati
ndio wanafundisha waumini wakabatizwa na kupata kipaimara…shukrani wanachangia
mapadri na maaskofu waliofundisha hawapati kitu…wamekata tamaa ndiyo maana
hawafundishi..wanaingiza waumini wengi wakabatizwa lakini wasiokuwa na misingi
ya imani maana hawana mafunzo…wanawafanya walimu wa dini kama kibao cha
matofali kikimaliza kazi hutupwa”alisisitiza.
Alisema maazimio hayo
yanayotokana na semina ya wiki nzima iliyoshirikisha majimbo yote Tanzania
ilifanyikia Kurasini Dar es Salaam yanatakiwa kufanyiwa kazi ili ujumbe wa
Papa mstaafu Benedict wa 16 wa kutangaza
mwaka 2013 na 14 kuwa wa imani uweze kutimia.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)


