Subscribe:

Ads 468x60px

WENYE VVU JIJI LA ARUSHA KUWAPATIA MATIBABU BURE



Arusha
.Halmashauri ya Jiji la Arusha,imetangaza mpango wa kuwapatia bure huduma za Afya,wanachama wa chama cha wanaoishi na maambukizi ya Ukimwi cha Tumaini  positive(TUPO) na familia zao.
Wanachama hao wa TUPO zaidi ya 50 Watapewa huduma za afya ,baada ya kilipiwa fedha za uanachama katika mfuko wa Taifa wa bima ya Afya,kupitia mpango  wa uchangiaji wa familia wa (CHF).
Mwenyekiti wa kamati ya Afya na Uchumi ya halmashauri ya jiji la Arusha,Isaya Doita,alitangaza mpango huo,wakati akifunga,semina ya waandishi wa habari na TUPO,kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi na kupinga unyanyapaa iliyoandaliwa naTASWA  Arusha,Ms unique na Tupo.
Doita alisema ,kutokana na jiji la Arusha,kujiunga na mpango  CHF wanachama wa TUPO  watalipiwa kiasi cha Ts 12,000 kwa mwaka ili waweze kupatiwa huduma bure za Afya na familia zao.
"nawapongeza Taswa,TUPO na Ms unique kwa kuandaa semina hii ambayo ni ya saba kwa ufanisi mkubwa na sisi kama jiji tunawaunga mkono"alisema Doita.
Awali Afisa matekelezo wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya akitoa mada katika semina hiyo,Desderius Buhoye aliwataka wakazi wa Arusha kujiunga na mfuko wa CHF ili kuweza kupata huduma bora za Afya.
Semina hiyo,iliyofanyika palace hoteli ilidhaminiwa na mfuko wa pensheni wa PPF ,PSPF ,LAPF,NSSF,shirika la PINGOS forums na shirika la PSI.
Mwisho

ASOMEWA MASHITAKA YA KUBAKA NA KULAWITI MTOTO AKIWA WODINI



Novemba 30,2013.
SERENGETI.
MAHAKAMA ya Hakimu wa Wilaya ya Serengeti imelazimika kuhamia hospitali ya wilaya ya Nyerere na kumsomea mashitaka  Marwa Ibrahimu(30)mkazi wa Kijiji cha Matare wilayani hapo,anayekabiliwa na mashitaka mawili  ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 12.
Hakimu wa Mahakama hiyo Franco Kiswaga alilazimika kuhamia hospitalini hapo kutokana na mtuhumiwa kushindwa kufikishwa mahakamani kufuatia kupigwa na kuumizwa na wananchi walipomkuta anafanya unyama huo .
Mwendesha mashitaka wa polisi Jakobo Sanga akisoma maelezo ya shitaka hospitalini hapo alisema mnamo novemba 19 mwaka huu majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Bukore kijiji cha Nyichoka kata ya Kyambahi mtuhumiwa anadaiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka 12.
Akisoma hati ya mashitaka alisema kuwa mshitakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ikiwemo la ubakaji na kulawiti mtoto kinyume cha maumbile ikiwa ni kinyume cha sheria.
Na kuwa mtuhumiwa akijua kuwa ni kosa alimkamata mtoto huyo na kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia majeraha sehemu za siri na haja kubwa mtoto huyo.
Mwendesha mashitaka alisema kuwa upelelezi umekamilika,hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka  na hakimu kuamru apelekwe mahabusu atakapopona  hadi desemba 5 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwisho.

VYOMBO VYA HABARI VISAIDIE KUELIMISHA JAMII KUHUSU MAAMBUKIZI YA HIV






MEYA WA JIJI LA ARUSHA GAUDENCE LYIMO AKIFUNGUA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA HUO JUU YA UGONJWA WA UKIMWI.

 ,VYOMBO vya habari nchini,vimeombwa kusaidia Taifa katika vita dhidi
ya ugonjwa wa Ukimwi na unyanyapaa,kwani hivi sasa kumebainika kuanza
maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi.

Meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo,ametoa  wito huo ,wakati akifungua
semina ya siku moja ya waandishi wa habari,juu ya ugonjwa wa ukimwi na
kupinga unyanyapaa.

Katika semina hiyo,iliyoandaliwa na Taswa Arusha ,chama cha wanaoishi na
vvu mkoa wa Arusha(TUPO) na kampuni ya Ms unique na kudhaminiwa na shirika
la PSI,Mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF,PSPF,NSSF,LAPF na Shirika la
Pingos Forums meya Lyimo,amesema hali ya maambukizi ya vvu ni mbaya.

Amesema  kwa hali ilivyo sasa,ni muhimu vyombo vya habari,kushiriki
ipasavyo katika vita dhidi ya Ukimwi kwani hali sio nzuri.

Na kuwa  kila siku kukiwa na taarifa za HIV katika vyombo vya habari
kutasaidia kukumbusha jamii kuendelea kuchukua  tahadhali

Mapema  Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Arusha,Brandina Nkini ametoa taarifa
ya maambukizi ya  HIV yanavongezeka  jijini Arusha kutoka 1.6 mwaka
2007 hadi kufikia3.2 mwaka  2012..

Mwisho.

Plight of Tanzanian journalists with the advent of multipartism


By David Kisanga
28th November 2013




Tanzania electronic, print media doing news coverage
The Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) has completed its country’s security needs assessment survey for human rights, Non Governmantal Organizations (NGOs), and journalists.

According to their findings and what was recorded in the questionnaires distributed, media practitioners working for public media outlets are facing severe hatred from fractions of the citizenry or from supporters of certain political parties.

These have led to commotions during political rallies and in situations where there is a tug of war between the citizenry in one side and the government and investors on the other side.

Given this situation this coalition foreseen of worst scenario as this country is heading towards the 2015 General Elections. Incidents of hurling stones and other forms of humiliations to this group are a common practice according to leaders of the 16 regional press clubs that were visited by this coalition.

Good examples to elucidate this scenario are found in all regions which are strong mainstay of the opposition, or which are endowed with rich reserves of natural resources.

In this category regions like Mbeya, Iringa, Mtwara, Arusha, Kigoma and Dar es Salam have witnessed incidents of humiliating journalists like what happened to the TBC broadcaster Marin Hassani Marin when he was harassed by sympathizers to one of the main opposition parties in the country, when it was launching its presidential candidate in the 2010 General Elections at the Jangwani grounds following a sudden blackout of the national television coverage.

Happenings like these could hinder the work of media practitioners in public media outlets which are run on coffers money.

According to Tanzania Human Rights Defenders-Coalition (THRDC) National Coordinator Onesmo Olengurumwa any sudden blackout of this media outlets have always created a critical risky situation towards these journalists as the public at large tend to assume that it is the journalists who decide what should and should not be aired without any attempt to understand that reporters operate under orders from their managements and editors.

Just to mention a few, Olengurumwa pointed out that a similar blackout of news from the TBC led to the unprecedented violence against the Mtwara based TBC reporter Kassimu Mikongolo in May this year, whose house was set ablaze by the irate mobs condemning him for terminating this coverage deliberately.

He mentioned other similar incidents that also occurred in Arusha, where TBC reporters were sidelined during the Arumeru by-election, and in other rallies by CHADEMA. This has forced them to use stories which have been collected by their colleagues from such rallies.

He mentioned Journalists from public media outlets who faced difficulties as Leonard Manga, Sechela Kongola, Khalfan Mshana and Ben Mwaipaja.

Olengurumwa gave an example of Kigoma where journalists working in public media outlets have a working confidence with leaders from all parties. However, citizens at large do not have trust with such outlets. In Kigoma TBC reporter Dotto Elias once faced a stiff challenge at the CHADEMA rally where he was harassed by its sympathizers. In that occasion CHADEMA’s leaders came to his rescue.

Gervas Msigwa also with TBC has been facing harassments whenever he attends CHADEMA’s rallies he had a narrow escape from an attack during the by-election in Lisabon Songea in 2011.

“There is a need to improve managerial capacity to the runners of these institutions so that they can get well acclimatized to the multiparty era in which this country is now operating.”

The current chairman of the Iringa Press Club Frank Leonard, who is employed by a public media outlet publisher of Daily News and Habari Leo, says there is a problem with politicians who fail to construe journalists as members of the community and that whatever they report reflect people’s wishes.

Citing in the 2010 General Election the ruling CCM top leadership had substituted its candidate who emerged an overall winner and replaced him with the one who happened to be their own choice.

By reporting this discrepancy he was seen as an agent of the opposition so he was confronted by the CCM’s Green Guards on grounds that he was working against their party, at the end of the day the ruling party lost in the Iringa Urban Constituency. 
SOURCE: THE GUARDIAN
More News


ABAKA NA KULAWITI MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI


                                
.

MWANAFUNZI wa darasala tano mwenye umri wa miaka (12) shule ya msingi(Nyichoka)wilayani Serengeti amelazwa katika hospitali ya wilaya akiguza majeraha ya kubakwa na kulawitiwa na mkazi mmoja wa kijiji cha Matare wilayani humo.
Mratibu wa dawati la jinsia la polisi wilaya Wp Sijali Nyambuche amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Marwa Ibrahimu(33) ambaye anadaiwa kutenda unyama huo Novemba 20 majira ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Bukore kijiji cha Nyichoka kata ya Kyambahi.
Alisema mtuhumiwa huyo ambaye wanamshikilia alimfanyia ukatili(jina limehifadhiwa)baada ya kumkamata kwa nguvu na kumchania nguo zake  za siri  .
“Siku ya tukio mtuhumiwa ambaye anafanya kazi kwenye roli la kusomba mawe,walifika kijijini hapo ili kununua mawe na mchanga…mtoto huyo alikuwa na mawe aliyokusanya kwa ajili ya kuuza apate fedha za mahitaji yake ya shule…gari liliharibika wakashindwa kuondoka na kulazimika kulala….ndipo usiku akamfanya ukatili huo”alisema mratibu wa dawati.
Nyambuche alisema kuwa kabla ya kumfanyia unyama huo usiku mtuhumiwa aliombwa kuwa mlinzi wa gari hilo na kusindikizwa na  mtoto huyo kuelekea kwenye gari,ghafla akamkamata na kumwingiza ndani ya gari na kumtendea unyama huku akimtishia kumuua.
“Tulimpkea mtoto huyo na kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya kupata PF3 kwa ajili ya matibabu  na uchunguzi zaidi ili kubaini amejeruhiwa kiasi gani na kama amepata magonjwa ya zinaa”alisema Nyambuche.
Akiongea kwa kusita sita mtoto huyo alisema baada ya kufika kwenye gari mtuhumiwa alimlazimisha kupanda ndani ya gari,alipokataa  akanishika kwa nguvu na kumpandisha ndani ya gari  akafunga mlango na kuchana nguo zake za  ndani na kuanza kumlawiti na baadae kumbaka na kuchanika sehemu zote na damu pamoja na kinyesi kutoka mfululizo.
“Nilipochelewa kurudi nyumbani usiku huo mama alniifuatilia…nilipomsikia nilimwita nikilia…akamkuta  mtuhumiwa akiendelea kunifanyia maneno ya aibu..akapiga yowe wananchi wakajitokeza na kuanza kumpa kipigo mtuhumiwa na kumpeleka polisi.”alisema.
Waganga katika hospitali ye Nyerere wamesema hali ya motto huyo inaendelea vizuri na polisi wanasema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote.
Matukio hayo yanatokea ikiwa wanaharakati wametawanyika nchi nzima katika kampeini za siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.      
MWISHO.

MATUKIO YA UZINDUZI WARIPOTI YA TANZANIA HUMAN RIGHTS DEFENDERS

 BAADA YA KUZINDUA RIPOTI PICHA ZA PAMOJA ZIKAPIGWA
 MGENI RASMI JAJI MKUU WA TANZANIA OTHMAN CHANDE KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAJUMBE WA THRDS WALIOSHIRIKI UZINDUZI WA RIPOTI YA HALI HALISI ILIVYO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
PICHA YA PAMOJA

RIPOTI YA TANZANIA HUMAN RIGHTS DEFENDERS COALITION YAZINDULIWA

 JAJI MKUU WA TANZANIA OTHMAN CHANDE AKIZINDUA RIPOTI YA TANZANIA HUMAN RIGHTS DEFENDERS COALITIONS UKUMBI WA HOTELI YA KEMPISKI DAR ES SALAAM
 MRATIBU WA MTANDAO WA THRDS ONESMO OLENGURUMWA AKIMKABIDHI JAJI MKUU RIPOTI YA MTANDAO HUO .
 MWENYEKITI WA MTANDAO HUO BI MARTINA KABISAMA AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WAKATI WA KUFUNGUA RIPOTI YAMTANDAO HUO

 JAJI MKUU WA TANZANIA OTHMAN CHANDE KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA THRDS,MABALOZI NA WADAU WENGINE MARA BAADA YA KUZINDUA RIPOTI HIYO
BAADA YA UZINDUZI  WA RIPOTI KILA MMOJA NI FURAHA TU

ANG’ATWA NA SIMBA

 Novemba 24,2013

Serengeti:MKAZI  mmoja wa kijiji cha Rwamchanga kata ya Manchirawilayani Serengeti Jimoka Nyihocha (20)amenusurika kufa baada yakuvamiwa na Simba katika zoezi la kuwaua baada ya kuvamia kijijinihapo na amelazwa hospitali ya wilaya ya Nyerere.
Tuko hilo limethibitishwa na afisa maliasili na wanyama pori wilaya
John Meitamei ,diwani wa kata hiyo na uongozi wa hospitali ya wilayalimetokea novemba 21 majira ya saa 6 mchana katika eneo la Bwawa laManchira.
Afisa Maliasili na wanyama pori Meitamei alisema Nyihocha alijeruhiwabaada ya wananchi kufuatilia nyayo za Simba waliodaiwa kupita kijijinina kuwakuta katika kichaka eneo la bwawani wakiwa wawili,na katikapurukushani hizo mmoja akakimbia na aliyebaki ndiye akaleta madhara
hayo.
“Baada ya wananchi kumzingira ili wamuue baada ya jike kukimbia hilodume lilianza kuwatisha …ghafla likatoka kichakani na kumvamia huyokijana na kumng’ata matakoni na kwenye paja,lakini wananchi kwa kuwawalikuwa wengi wakasaidia akakimbia na kurudi kichakani”alisema.
Alisema askari wa halmashauri kwa kushirikiana na mapori ya Ikorongona Grumeti walifika eneo la tukio na kuanza kukabiliana na simba huyokwa muda mrefu ,na kufanikiwa kumuua.
“Toka saa sita hadi saa kumi ndio tukafanikiwa kumuua…maana alikuwaeneo baya kwenye kichaka na kuingia haikuwa kazi rahisi…alipopigwarisasi akaruka kuja kumvamia askari…wakamuwahi na kumpiga risasi yapili na kufa…vinginevyo angeleta madhara mengine”alisema.
Hata hivyo alisema wanaendelea na msako wa simba aliyekimbia asije akaleta madhara kwa wananchi na mifugo.
Diwani wa kata hiyo Marko Shaweshi alisema kijana huyo alishambuliwana Simba wakati anajaribu kukimbia”Simba huangalia mtu mwoga na hakuwana uzoefu…mara baada ya kuunguruma akajaribu kukimbia,hilo ni kosa kwasimba kumtega mgongo akamvamia…kama watu wasingewahi angemuua”alisema.
Alisema kukithiri kwa wanyama katika makazi ya wananchi ni kutokana nahali huko ndani kuwa ngumu ya kupata mawindo na chakula hivyohukimbilia maeneo ya watu ili kujipatia chakula.
Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo Neema Mechara amesema majeruhi huyoaliyelazwa kitanda namba moja wodi ya wanaume anaendelea vizuri na ameanza kufanya mazoezi baada ya kusafishwa vidonda na mifupa
haikupata madhara.
Mwisho.

AFA KWA KUJINYONGA BAADA YA KUTISHIWA NA BABA YAKE.


Aliambiwa akimuua ndama aliyekuwa ana mpiga atakula nyama yake mbichi,
Novemba 24,2013
Serengeti:
JULIANA MARWA(14)mkazi  wa kijiji cha nyamakendo katika wilaya ya serengeti mkoani mara amejinyonga  hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani baada ya kutishiwa na baba yake mzazi kuwa akimuua ndama aliyekuwa anampiga atakula nyama yake mbichi.
Tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi kwa wananchi limethibitishwa na diwani wa kata hiyo Samweli Gibewa na polisi wilayani kuwa limetokea mwanzoni mwa mwezi huu katika kitongoji cha Bwisabuka kijijini hapo.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 12.00 jioni msichana huyo akiwa anakamua maziwa ndama alikuwa anamsumbua kwa kutaka kunyonya ndipo akaanza kumpiga ,kitendo kilichomuudhi baba yake na kumtolea maneno kuwa  akifa atamla mbichi,kauli inayodaiwa kumuudhi na kuamua kwenda kunjinyonga.
“Alikutwa ndani ya shamba la mihogo mita 100 kutoka nyumbani kwao majira ya saa 1:00 asubuhi kesho yake kwa kuwa baada ya kugombezwa alitoweka kwao….Mama yake alipokwenda shambani kupalilia ndipo akamkuta ana ning’inia ameishakata roho na kulazimika kupiga kelele kuomba msaada”alisema diwani.
Mama mzazi wa marehemu  Mugosi Marwa akielezea tukio hilo alidai kuwa baada ya binti huyo kutoelewana na baba yake alitoweka nyumbani majira ya usiku  wakidhani ameenda kulala  kwa bibi yake ambaye wanaishi jirani hivyo hawakuwa na sababu ya kumfuatilia wakijua kuwa atarudi asubuhi mwenyewe kinyume chake akaenda kujinyonga.
Hata hivyo Marehemu hakuacha ujumbe wowote kuhusiana na uamzi wake wa kujinyonga ,jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi  kuhusiana na tukio hilo  baada ya kuhoji familia akiwemo baba mzazi Marwa Mwita Yahara.
Mwisho.

WANASHERIA(AG)KENYA,UGANDA NA RWANDA WAFUNGULIWA MASHITAKA MAHAKAMA YA A.MASHARIKI



 Wakili Jimmy Obedi kushoto akiwasilisha maombi ya kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kuitaka mahakama hiyo itoe amri ya kusitisha utekelezaji wa maazimio ya vikao vitatu vilivyoshirikisha Uganda,Kenya na Rwanda kwa kuwa ni ukiukwaji wa vifungu vya sheria ya jumuiya hiyo,anayepokea ni afisa wa masijala ya mahaka hiyo Richard Ogoti kwa niaba ya msajili wa mahakama hiyo




 Wakili Jimmy Obedi mwenye miwani akipokea hati maalum kutoka kwa karani wa masijala wa mahakama ya Afrika Mashariki Richard Ogoti mara baada ya kuwasilisha maombi na kufungua kesi namba 9/2013 iliyofunguliwa na watu watatu(picha zote na Blog hii)


WAFUNGUA KESI MAHAKAMA YA A.MASHARIKI
Novemba 18,2013

Arusha-
WANASHERIA wakuu wa nchi  za Kenya,Rwanda na Uganda wamefunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kukiuka vifungu vya Mkataba wa jumuiya hiyo.

Maombi namba 6 kesi namba 9/2013 imefunguliwa na wanajumuiya hiyo Ally Msangi,David Makata na John David Mbendo wanaowakilishwa na wakili Jimmy Obedi wa kampuni ya Jimmy Obedi ya jijini Dar es salaam imepokelewa leo na afisa masijala wa mahakama hiyo

Boniphace Ogoti  kwa niaba ya msajili.

Mbele ya waandishi wa habari wakili Obedi amesema wamewasilisha maombi ya kutaka maazimio yote ya vikao vilivyofanyika juni 24,25 mwaka huu Entebe Uganda,kikao cha agosti 28,2013 Mombasa na oktoba 28,2013 Kigali Rwanda bila kushirikisha nchi mwanachama ambaye ni Tanzania.

“Lengo la maombi haya ni kuzuia utekelezaji wa maamzi yaliyofikiwa kwenye vikao hivyo kwa kuwa ni kinyume na vifungu vya mkataba wa jumuiya,ibara ya 71(f)71(b) na vingine….mahakama itoe amri ya kusitisha vikao vyote vinavyoendeshwa kinyume cha sheria ya jumuiya .... tumeomba maombi hayo yasikilizwe upande mmoja na kutoa uamzi wa kusitisha utekelezaji huo”amesema wakili.

Wakili huyo amesema wakati kesi hiyo ikisubiri kupangiwa jaji watu wengine kutoka katika jumuiya hiyo wanaruhusiwa kujiunga na walalamikaji hao ,kwa nia ya kuhakikisha mkataba wa shirikisho hilo unafuatwa kwa mjibu wa  vifungu vya sheria iliyounda shirikisho hilo.
.
“Hapa walalamikiwa ni wanasheria wakuu wan chi hizo tatu ambao marais wao wamekuwa wakikutana kinyume cha mkataba wa shirikisho la jumuiya ya Afrika Mashariki….na sisi tunataka sauti ya kimahakama ya kusitisha utekelezaji wa maazimio yao… mahakama ndio chombo kikuu kitakachotoa tafsri si siasa tena…amebainisha wakili.

Kwa upande wake Msangi ambaye amewakilisha walalamikaji wenzake mahakamani hapo amesema kuwa wamefikia uamzi huo ili kupata ufafanuzi wa kisheria kwa kuwa taarifa zinazotolewa na wanasiasa zinawachanganya wananchi wan chi zote ili kujua hatima ya shirikisho hilo.
mwisho.