WAFUNGUA KESI MAHAKAMA YA
A.MASHARIKI
Novemba 18,2013
Arusha-
WANASHERIA wakuu wa nchi za Kenya,Rwanda na Uganda wamefunguliwa
mashitaka katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kukiuka
vifungu vya Mkataba wa jumuiya hiyo.
Maombi namba 6 kesi namba 9/2013
imefunguliwa na wanajumuiya hiyo Ally Msangi,David Makata na John David Mbendo
wanaowakilishwa na wakili Jimmy Obedi wa kampuni ya Jimmy Obedi ya jijini Dar
es salaam imepokelewa leo na afisa masijala wa mahakama hiyo
Mbele ya waandishi wa habari
wakili Obedi amesema wamewasilisha maombi ya kutaka maazimio yote ya vikao
vilivyofanyika juni 24,25 mwaka huu Entebe Uganda,kikao cha agosti 28,2013
Mombasa na oktoba 28,2013 Kigali Rwanda bila kushirikisha nchi mwanachama
ambaye ni Tanzania.
“Lengo la maombi haya ni kuzuia
utekelezaji wa maamzi yaliyofikiwa kwenye vikao hivyo kwa kuwa ni kinyume na
vifungu vya mkataba wa jumuiya,ibara ya 71(f)71(b) na vingine….mahakama itoe amri ya kusitisha vikao vyote vinavyoendeshwa kinyume cha sheria ya jumuiya .... tumeomba
maombi hayo yasikilizwe upande mmoja na kutoa uamzi wa kusitisha utekelezaji
huo”amesema wakili.
Wakili huyo amesema wakati kesi hiyo ikisubiri kupangiwa jaji watu
wengine kutoka katika jumuiya hiyo wanaruhusiwa kujiunga na walalamikaji
hao ,kwa nia ya kuhakikisha mkataba wa shirikisho hilo unafuatwa kwa mjibu wa vifungu vya sheria iliyounda shirikisho hilo.
.
“Hapa walalamikiwa ni wanasheria
wakuu wan chi hizo tatu ambao marais wao wamekuwa wakikutana kinyume cha
mkataba wa shirikisho la jumuiya ya Afrika Mashariki….na sisi tunataka sauti ya
kimahakama ya kusitisha utekelezaji wa maazimio yao… mahakama ndio chombo kikuu
kitakachotoa tafsri si siasa tena…amebainisha wakili.
Kwa upande wake Msangi ambaye
amewakilisha walalamikaji wenzake mahakamani hapo amesema kuwa wamefikia uamzi
huo ili kupata ufafanuzi wa kisheria kwa kuwa taarifa zinazotolewa na wanasiasa
zinawachanganya wananchi wan chi zote ili kujua hatima ya shirikisho hilo.
mwisho.