Subscribe:

Ads 468x60px

AFA KWA KUJINYONGA BAADA YA KUTISHIWA NA BABA YAKE.


Aliambiwa akimuua ndama aliyekuwa ana mpiga atakula nyama yake mbichi,
Novemba 24,2013
Serengeti:
JULIANA MARWA(14)mkazi  wa kijiji cha nyamakendo katika wilaya ya serengeti mkoani mara amejinyonga  hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani baada ya kutishiwa na baba yake mzazi kuwa akimuua ndama aliyekuwa anampiga atakula nyama yake mbichi.
Tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi kwa wananchi limethibitishwa na diwani wa kata hiyo Samweli Gibewa na polisi wilayani kuwa limetokea mwanzoni mwa mwezi huu katika kitongoji cha Bwisabuka kijijini hapo.
Alisema siku ya tukio majira ya saa 12.00 jioni msichana huyo akiwa anakamua maziwa ndama alikuwa anamsumbua kwa kutaka kunyonya ndipo akaanza kumpiga ,kitendo kilichomuudhi baba yake na kumtolea maneno kuwa  akifa atamla mbichi,kauli inayodaiwa kumuudhi na kuamua kwenda kunjinyonga.
“Alikutwa ndani ya shamba la mihogo mita 100 kutoka nyumbani kwao majira ya saa 1:00 asubuhi kesho yake kwa kuwa baada ya kugombezwa alitoweka kwao….Mama yake alipokwenda shambani kupalilia ndipo akamkuta ana ning’inia ameishakata roho na kulazimika kupiga kelele kuomba msaada”alisema diwani.
Mama mzazi wa marehemu  Mugosi Marwa akielezea tukio hilo alidai kuwa baada ya binti huyo kutoelewana na baba yake alitoweka nyumbani majira ya usiku  wakidhani ameenda kulala  kwa bibi yake ambaye wanaishi jirani hivyo hawakuwa na sababu ya kumfuatilia wakijua kuwa atarudi asubuhi mwenyewe kinyume chake akaenda kujinyonga.
Hata hivyo Marehemu hakuacha ujumbe wowote kuhusiana na uamzi wake wa kujinyonga ,jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi  kuhusiana na tukio hilo  baada ya kuhoji familia akiwemo baba mzazi Marwa Mwita Yahara.
Mwisho.