Subscribe:

Ads 468x60px

WENYE VVU JIJI LA ARUSHA KUWAPATIA MATIBABU BURE



Arusha
.Halmashauri ya Jiji la Arusha,imetangaza mpango wa kuwapatia bure huduma za Afya,wanachama wa chama cha wanaoishi na maambukizi ya Ukimwi cha Tumaini  positive(TUPO) na familia zao.
Wanachama hao wa TUPO zaidi ya 50 Watapewa huduma za afya ,baada ya kilipiwa fedha za uanachama katika mfuko wa Taifa wa bima ya Afya,kupitia mpango  wa uchangiaji wa familia wa (CHF).
Mwenyekiti wa kamati ya Afya na Uchumi ya halmashauri ya jiji la Arusha,Isaya Doita,alitangaza mpango huo,wakati akifunga,semina ya waandishi wa habari na TUPO,kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi na kupinga unyanyapaa iliyoandaliwa naTASWA  Arusha,Ms unique na Tupo.
Doita alisema ,kutokana na jiji la Arusha,kujiunga na mpango  CHF wanachama wa TUPO  watalipiwa kiasi cha Ts 12,000 kwa mwaka ili waweze kupatiwa huduma bure za Afya na familia zao.
"nawapongeza Taswa,TUPO na Ms unique kwa kuandaa semina hii ambayo ni ya saba kwa ufanisi mkubwa na sisi kama jiji tunawaunga mkono"alisema Doita.
Awali Afisa matekelezo wa mfuko wa Taifa wa bima ya Afya akitoa mada katika semina hiyo,Desderius Buhoye aliwataka wakazi wa Arusha kujiunga na mfuko wa CHF ili kuweza kupata huduma bora za Afya.
Semina hiyo,iliyofanyika palace hoteli ilidhaminiwa na mfuko wa pensheni wa PPF ,PSPF ,LAPF,NSSF,shirika la PINGOS forums na shirika la PSI.
Mwisho