Subscribe:

Ads 468x60px

ANG’ATWA NA SIMBA

 Novemba 24,2013

Serengeti:MKAZI  mmoja wa kijiji cha Rwamchanga kata ya Manchirawilayani Serengeti Jimoka Nyihocha (20)amenusurika kufa baada yakuvamiwa na Simba katika zoezi la kuwaua baada ya kuvamia kijijinihapo na amelazwa hospitali ya wilaya ya Nyerere.
Tuko hilo limethibitishwa na afisa maliasili na wanyama pori wilaya
John Meitamei ,diwani wa kata hiyo na uongozi wa hospitali ya wilayalimetokea novemba 21 majira ya saa 6 mchana katika eneo la Bwawa laManchira.
Afisa Maliasili na wanyama pori Meitamei alisema Nyihocha alijeruhiwabaada ya wananchi kufuatilia nyayo za Simba waliodaiwa kupita kijijinina kuwakuta katika kichaka eneo la bwawani wakiwa wawili,na katikapurukushani hizo mmoja akakimbia na aliyebaki ndiye akaleta madhara
hayo.
“Baada ya wananchi kumzingira ili wamuue baada ya jike kukimbia hilodume lilianza kuwatisha …ghafla likatoka kichakani na kumvamia huyokijana na kumng’ata matakoni na kwenye paja,lakini wananchi kwa kuwawalikuwa wengi wakasaidia akakimbia na kurudi kichakani”alisema.
Alisema askari wa halmashauri kwa kushirikiana na mapori ya Ikorongona Grumeti walifika eneo la tukio na kuanza kukabiliana na simba huyokwa muda mrefu ,na kufanikiwa kumuua.
“Toka saa sita hadi saa kumi ndio tukafanikiwa kumuua…maana alikuwaeneo baya kwenye kichaka na kuingia haikuwa kazi rahisi…alipopigwarisasi akaruka kuja kumvamia askari…wakamuwahi na kumpiga risasi yapili na kufa…vinginevyo angeleta madhara mengine”alisema.
Hata hivyo alisema wanaendelea na msako wa simba aliyekimbia asije akaleta madhara kwa wananchi na mifugo.
Diwani wa kata hiyo Marko Shaweshi alisema kijana huyo alishambuliwana Simba wakati anajaribu kukimbia”Simba huangalia mtu mwoga na hakuwana uzoefu…mara baada ya kuunguruma akajaribu kukimbia,hilo ni kosa kwasimba kumtega mgongo akamvamia…kama watu wasingewahi angemuua”alisema.
Alisema kukithiri kwa wanyama katika makazi ya wananchi ni kutokana nahali huko ndani kuwa ngumu ya kupata mawindo na chakula hivyohukimbilia maeneo ya watu ili kujipatia chakula.
Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo Neema Mechara amesema majeruhi huyoaliyelazwa kitanda namba moja wodi ya wanaume anaendelea vizuri na ameanza kufanya mazoezi baada ya kusafishwa vidonda na mifupa
haikupata madhara.
Mwisho.