,VYOMBO vya habari nchini,vimeombwa kusaidia Taifa katika vita dhidi
ya ugonjwa wa Ukimwi na unyanyapaa,kwani hivi sasa kumebainika kuanza
maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi.
Meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo,ametoa wito huo ,wakati akifungua
semina ya siku moja ya waandishi wa habari,juu ya ugonjwa wa ukimwi na
kupinga unyanyapaa.
Katika semina hiyo,iliyoandaliwa na Taswa Arusha ,chama cha wanaoishi na
vvu mkoa wa Arusha(TUPO) na kampuni ya Ms unique na kudhaminiwa na shirika
la PSI,Mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF,PSPF,NSSF,LAPF na Shirika la
Pingos Forums meya Lyimo,amesema hali ya maambukizi ya vvu ni mbaya.
Amesema kwa hali ilivyo sasa,ni muhimu vyombo vya habari,kushiriki
ipasavyo katika vita dhidi ya Ukimwi kwani hali sio nzuri.
Na kuwa kila siku kukiwa na taarifa za HIV katika vyombo vya habari
kutasaidia kukumbusha jamii kuendelea kuchukua tahadhali
Mapema Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Arusha,Brandina Nkini ametoa taarifa
ya maambukizi ya HIV yanavongezeka jijini Arusha kutoka 1.6 mwaka
2007 hadi kufikia3.2 mwaka 2012..
Mwisho.