.
MWANAFUNZI wa
darasala tano mwenye umri wa miaka (12) shule ya msingi(Nyichoka)wilayani
Serengeti amelazwa katika hospitali ya wilaya akiguza majeraha ya kubakwa na
kulawitiwa na mkazi mmoja wa kijiji cha Matare wilayani humo.
Mratibu wa
dawati la jinsia la polisi wilaya Wp Sijali Nyambuche amemtaja mtuhumiwa huyo
kuwa ni Marwa Ibrahimu(33) ambaye anadaiwa kutenda unyama huo Novemba 20 majira
ya saa 2 usiku katika kitongoji cha Bukore kijiji cha Nyichoka kata ya Kyambahi.
Alisema
mtuhumiwa huyo ambaye wanamshikilia alimfanyia ukatili(jina limehifadhiwa)baada ya kumkamata kwa nguvu na
kumchania nguo zake za siri .
“Siku ya tukio
mtuhumiwa ambaye anafanya kazi kwenye roli la kusomba mawe,walifika kijijini
hapo ili kununua mawe na mchanga…mtoto huyo alikuwa na mawe aliyokusanya kwa
ajili ya kuuza apate fedha za mahitaji yake ya shule…gari liliharibika
wakashindwa kuondoka na kulazimika kulala….ndipo usiku akamfanya ukatili
huo”alisema mratibu wa dawati.
Nyambuche
alisema kuwa kabla ya kumfanyia unyama huo usiku mtuhumiwa aliombwa kuwa mlinzi
wa gari hilo na kusindikizwa na mtoto
huyo kuelekea kwenye gari,ghafla akamkamata na kumwingiza ndani ya gari na
kumtendea unyama huku akimtishia kumuua.
“Tulimpkea mtoto
huyo na kumpeleka hospitali kwa matibabu baada ya kupata PF3 kwa ajili ya
matibabu na uchunguzi zaidi ili kubaini
amejeruhiwa kiasi gani na kama amepata magonjwa ya zinaa”alisema Nyambuche.
Akiongea kwa
kusita sita mtoto huyo alisema baada ya kufika kwenye gari mtuhumiwa
alimlazimisha kupanda ndani ya gari,alipokataa akanishika kwa nguvu na kumpandisha ndani ya
gari akafunga mlango na kuchana nguo
zake za ndani na kuanza kumlawiti na
baadae kumbaka na kuchanika sehemu zote na damu pamoja na kinyesi kutoka
mfululizo.
“Nilipochelewa
kurudi nyumbani usiku huo mama alniifuatilia…nilipomsikia nilimwita
nikilia…akamkuta mtuhumiwa akiendelea
kunifanyia maneno ya aibu..akapiga yowe wananchi wakajitokeza na kuanza kumpa
kipigo mtuhumiwa na kumpeleka polisi.”alisema.
Waganga katika
hospitali ye Nyerere wamesema hali ya motto huyo inaendelea vizuri na polisi
wanasema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote.
Matukio hayo
yanatokea ikiwa wanaharakati wametawanyika nchi nzima katika kampeini za siku
16 za kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
MWISHO.