Subscribe:

Ads 468x60px

Mwenyekiti wa Kijiji asomesha watoto wa mazingira magumu

 Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Majimoto Kata ya Maji Moto wilayani Serengeti Johannes Masioni kulia akikabidhi vifaa ,karo na michango kwa watoto wanne wa mazingira magumu ,alioamua kuwasaidia ili waanze masomo kidato cha kwanza Busawe Sekondari,msaada jumla ya msaada wake ni sh,420,000=
 Someni
 Saidieni watoto wasome si kuchangia harusi

watoto wanaahidi kusoma

SHULE KUKOSA VYOO WALIMU HULAZIMIKA KURUDI MAJUMBANI KUJISAIDIA.



Machi ,2014
Serengeti:WALIMU 37 wa shule ya Msingi Mapinduzi ‘A’iliyoko Mjini Mugumu wilaya ya Serengeti,hulazimika kurudi kwenye makazi yao kujisadia kutokana na shule hiyo kutokuwa na vyoo vya walimu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Ofisa Elimu wilaya hiyo William Mabanga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo,na kudai kuwa ni shule nyingi hazina vyoo vya walimu,kwa kuwa mkazo uliwekwa kujenga vyoo vya wanafunzi wakasahau walimu,na kuahidi kuwa litashughulikiwa kwa kuwa athari yake ni kubwa kwa walimu na watoto.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo James Johannes amesema tatizo hilo lina muda mrefu,mamlaka husika zinataarifa lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kuwanusuru walimu  kwa kuwa wanaodharirika kwa kukosa vyoo na kuokoa muda wa vipindi ambao huvitumia kurudi majumbani kujisaidia.
“ Mwalimu hutumia  zaidi ya dakika 20  kutafuta eneo la kujistiri…hapa ni katikati ya mji hawawezi kukimbilia vichakani…maana  walimu 32 ni wakike , na wakiume 6 ,wanalazimika kwenda kwenye miji yao ama majilani  kujisaidia….na hii ndiyo shule ya mjini,imeachwa hivi…tunaomba mamlaka zichukue hatua maana watoto wanakosa mtiririko wa vipindi kwa tatizo hilo,”alisema Mwalimu kwa masikitiko.
Alisema awali walikuwa wanatumia choo cha kanisa la Sayuni na baada ya kuweka uzio ,wakakosa sehemu ya kujisaidia,na choo cha wanafunzi inakuwa vigumu kwa kuwa nacho kiko katika eneo la mtu na matundu yaliyopo ni 12 kati ya mahitaji ya matundu 32 kwa watoto 890 waliopo hapo shuleni.
“Baada ya kuweka uzio hatuna sehemu ya kujisaidia…kwa mwalimu anayekaa shuleni anaye ana choo cha muda ambacho kinadhalilisha maisha ya walimu….kuhusu vyoo vya wanafunzi tayari tumeishapata notisi maana ni uwanja wa mtu anataka kuendeleza eneo lake….kuna hatari ya shule kufungwa iwapo  atazuia hapatakuwa na jinsi,”alibainisha.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha NHC ,Elias Nyamraba anasema tatizo hilo linawadhalilisha walimu na kukosa morari ya kufundisha ,na inapotokea amepata mchafuko wa tumbo hupata shida,hivyo Matokeo Makubwa sasa hayawezi kupatikana katika mazingira kama hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,afya na Maji wilaya Daniel Kegocha alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwa walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kukosa vyoo.
“Nilifika shuleni baada ya kufuatwa na walimu,kweli  hali ni mbaya …maana wanaacha vipindi na kurudi nyumbani kutafuta vyoo kuna athari kubwa kitaaluma…nitalifikisha hili tatizo halmashauri ya wilaya  ili kuona jinsi ya kuchukua hatua za haraka”alibainisha.
Kuhusu choo cha wanafunzi kuwa katika eneo la mtu,diwani hiyo alisema hakuwa anajua na kubainisha yote yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka ili kunusuru shule isijekufungwa.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walilaumu madiwani kwa kubadilisha matumizi ya eneo la mnada  linalopakana na shule hiyo,viongozi wakajigawia maeneo ambalo lingeweza kutumiwa na shule hiyo ili kuwanusuru watoto wanaokwenda kujisaidia eneo la jilani kwa kuvuka barabara kuu,hali ambayo ni hatari kwa usalama wao.
Kwa mjibu wa taarifa ya wilaya ,inabainisha kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo kwa walimu 1,401,ambapo toka mwaka 2009 mpaka 2013 wamejenga matundu 25 tu,upungufu wa madawati ni 16,460,ambapo zaidi ya asilimia 50 wanasoma wakiwa wamekaa chini.
Mwisho.

SHULE MBILI ZENYE WATOTO 1,005 ZINA WALIMU WATANO,



kati yao watoto 777 husoma wamekaa chini,kutokana na ukosefu wa madawati.
Machi 10,2014
Serengeti:WALIMU watano  wa shule za msingi Kitarungu  na Matanka kata ya Nyansurura wilayani Serengeti wanalazimika kufundisha  wanafunzi 1005 ,moja yenye watoto 557 ina walimu 2 na nyingine yenye watoto 448 ina walimu 3.
Mbali na upungufu wa walimu shule hizo zote mbili zina madawati 76 ambapo wanafunzi 777 kwa shule hizo mbili husoma wamekaa chini hali ambayo inabainisha changamoto kwa sekta ya Elimu ambayo ni miongoni mwa sekta 5 zilizokwisha zindua mikakati ya Matokeo Makubwa sasa(BRN).
Mratibu elimu kata hiyo Benard Misolo aliliambia Mwananchi kuwa kwa hali hiyo wastaraji miujiza kwa walimu wawili kufundisha wanafunzi 557 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba ,wakati huo Mwalimu mkuu ana majukumu ya utawala.
“Tatizo hili ni la muda mrefu ,ofisi ina taarifa ….kupitia uongozi wa kata na elimu toka mwaka 2007 shule ilipoanzishwa bila mafanikio…tukipata walimu sita watasaidia kupunguza tatizo ,kwa shule ya Matanka walimu watatu hawakidhi… wanaopata shida hapa ni watoto”alisema.
Kuhusu madawati alisema shule ya Kitarungu wanafunzi wanaosoma wamekaa kwenye madawati ni 108,huku wanafunzi 449 wanasoma wakiwa wamekaa chini,na shule ya Matanka wanaokalia madawati ni 120,huku 328 wanasoma wakiwa wamekaa chini.
“Kuna upungufu mkubwa wa vyumba vya Madarasa ,maana darasa moja watoto wanakaa kuanzia 50 hadi 120…wengi wakiwa wamekaa chini…hakuna usikivu hapo..hayo yote ni madhila yanayowakuta walimu wawili,”alisema.
Diwani wa kata ya Nyansurura Jackson Mwita(Chadema) aliliambia Mwananchi kuwa kata yake inahali mbaya kwa upande wa elimu kwa shule za msingi,kwa kuwa shule zote saba hazina walimu wa kutosha.
“Tumeomba sana walimu lakini hatupewi…wanadai hakuna nyumba za walimu…lakini hakuna kata yenye nyumba za walimu za kutosha….mjini shule moja ina watoto 800 ina walimu 37,hakuna nyumba wamepanga….hapa watoto zaidi ya 500 walimu wawili….uwiano gani huo…harafu mwisho unalaumu watoto na wazazi….nadhani kuna mitizamo hasi ya kisiasa,”alisema kwa masikitiko.
Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,afya na Maji halmashauri hiyo Daniel Kegocha amekiri kuwepo kwa upungufu huo na kuwa lilikwishatolewa agizo idara ya elimu kupitia vikao kuwa wapeleke walimu shule zenye upungufu.
“Walimu wapya watakaporipoti mwaka huu shule zenye upungufu zitapewa kipaumbele…si hizo hata Nyahende kata ya Kebancha bancha ina walimu watatu wanafunzi zaidi 500…maana shule za mjini wamerundikwa walimu wengi lazima uwiano uwepo,”alisisitiza.
Hata hivyo imebainika kuwa shule nyingi hazina nyumba za walimu,na hata vijijini wanakosa nyumba za kupanga hali ambayo inapelekea walimu kukimbia,ambapo mwaka 2013 walimu 80 walihama mkoa huo,wengi wakilalamikia mazingira magumu ya kazi.
Uongozi wa idara ya elimu wilaya wamekiri kuwepo kwa upungufu na kudai kuwa tatizo kubwa ni ukosefu wa nyumba ,hata nyumba za walimu kupanga baadhi ya maeneo ni changamoto na kuomba jamii kujitolea kujenga nyumba ,na kutengeneza madawati ili kuboresha elimu.
Mwisho.

M4C PAMOJA MUGUMU SERENGETI

Pamoja na jua kali wanasema wanataka mabadiliko 


 mkutano unaendelea
 Wananchi wakifuatilia mkutano wa M4C Katika uwanja wa Sokoine mjini Mugumu Serengeti
 DR.SLAA AKIONDOKA UWANJA WA SOKOINE MUGUMU SERENGETI

TANAPA KUENDESHWA KWA MFUMO WA KIJESHI ILI KUDHIBITI UJANGILI

Askari wapya waliomaliza mafunzo ya miezi mine katika Hifadhi ya Taifa Katavi wakipiga saluti kabla ya kuwasilisha risala yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliyekuwa mgeni rasmi
  
Katika kukabiliana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea kushika kasi ndani nan je ya mipaka ya nchi yetu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litaendeshwa katika mfumo wa jeshi-usu katika siku chache zijazo ambapo watumishi wake watalazimika kupitia katika mafunzo maalum ya kijeshi.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya askari wapya 96 walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi minne katika Hifadhi ya Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.

Kijazi alisema kuwa TANAPA imeanzisha utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka katika Vyuo vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na shirika kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya utendaji kazi katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa.


Tunakufunga usitoroke usubiri kuchinjwa

 wanafunzi wa shule ya msingi Kisangura Serengeti wakifunga kuku walionunuliwa kwa ajili ya hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ,chini ya ufadhili wa New York Yearly Meeting la Marekani kwa usimamizi wa shirika la Zinduka la wilayani Bunda
Tunakufunga usitoroke usubiri kuchinjwa ,ndivyo inavyoonekana wanafunzi hawa wanasema huku wakiwafunga kuku kwa kamba wasijetoroka wasubiri kuchinjwa
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kisangura wilaya ya Serengeti wakiwa shuleni,huku baadhi yao wakisiburi kupokea msaada wa vifaa mbalimbali  wanavyogawiwa kila mwaka kwa ufadhili wa kamati ya New York ya Marekani ,kwa usimamizi wa shirika la Zinduka lenye makao Makuu yake Nyamuswa wilayani Bunda,,
Mmoja wa wanafunzi wa darasa la pili akipokea msaada wa vitu ,mbalimbali,ikiwemo sare mbili,viatu,soksi,kalamu,madaftari,na vitabu vya kiada na ziada ,msaada huo uelekezwa kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu zaidi.jumla ya wanafunzi 125 wa shule ya msingi na sekondari Kisangura wamenufaika na msaada huo wenye thamani ya sh.mil.24,hata hivyo wafadhili wamekata misaada ya kulipia masomo ya elimu ya juu na ujenzi kufuatia wasimamizi kufanya ufisadi wa miradi hiyo.

Mbegu mbovu zatengeneza mafuta ya kula Mara





Meneja wa Kiwanda cha Bundaa, Roharl Parmar (kushoto) akiwa na Kaimu Afisa Shughuli wa kiwanda hicho, Paul Aaron wakati alipohojiwa na gazeti hili ofisi kwake. Na Mpigapicha Wetu. 


Posted  Jumatatu,Januari27  2014  saa 10:3 AM
Kwa ufupi
  • Uchunguzi uliofanywa gazeti hili ulibaini kuwa baadhi ya viwanda vya kuzalisha mafuta vimekuwa vikinunua mbegu hizo kwa bei nafuu kwa madai ya kuzitumia kutengenezea mashudu (chakula cha mifugo) na kuchomea
Bunda. Baadhi ya viwanda Mikoa ya Mara na Mwanza vinadaiwa kutumia mbegu za pamba zilizooza kwa ajili ya kuzalisha mafuta ya kula, hali ambayo inahatarisha afya za watumiaji wa mafuta hayo.
Uchunguzi uliofanywa gazeti hili ulibaini kuwa baadhi ya viwanda vya kuzalisha mafuta vimekuwa vikinunua mbegu hizo kwa bei nafuu kwa madai ya kuzitumia kutengenezea mashudu (chakula cha mifugo) na kuchomea
`boiler’ (chombo cha kuchemshia malighafi ya mafuta), lakini zimekuwa zikitumika kinyume.
Badala yake zimekuwa zikitumika kukamua mafuta ambayo kutokana na kuwa machafu, huchanganywa na mafuta mengine masafi kisha kuingizwa sokoni.
Uchunguzi ulibaini kuwa mchezo huo umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu, kabla ya kugunduliwa na wataalamu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), Kanda ya Ziwa, kutokana na kuwapo kwa malalamiko mengi kutoka kwa walaji.
Imebainika kuwa TFDA walifanya ukaguzi wa kushtukiza katika Viwanda vya Bundaa Oil Mill kilichoko wilayani Bunda mkoani Mara na Brichand Oil Mill Ltd kilichopo jijini Mwanza kutokana na kudaiwa kujihusisha na mchezo huo.
Meneja wa TFDA, Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe alisema: “Malalamiko ya walaji yalitusukuma kufanya msako wa kustukiza kwenye Kiwanda cha Brichand Oil Mill Ltd…Wakakiri kuuza mbegu zilizooza kwa Kampuni ya Bundaa Oil Mill Ltd na katika kufuatilia ndipo tulibaini ukiukwaji huo wa sheria huo,” alisema Mbambe.
Mbambe alisema uongozi wa Brichand Oil Mill Ltd ulisema kuwa mbegu hizo waliwapa Bundaa Oil Mill Ltd kwa madhumuni ya kutengeneza mashudu na siyo vinginevyo, lakini TFDA katika ukaguzi wao walibaini mbegu hizo zilitumika kwa ajili ya kuzalisha mafuta.
Mkaguzi wa Vyakula katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Bunda, Mafuru Madaraka alikiri kiwanda hicho kuhusika kutumia mbegu zilizooza kutengeneza mafuta ya pamba.
“Ni kweli tulivamia tukiwa na wataalamu wa TFDA na kukuta wakizalisha mafuta kwa kutumia mbegu zilizooza…mafuta mengine yakiwa yameshaingia sokoni na mengine yakiwa yamehifadhiwa stooni,” alisema Madaraka.
Alisema mbegu hizo zilichukuliwa na kuamriwa kuteketezwa chini ya usimamizi wao na TFDA, huku uongozi wa kiwanda hicho ukidai kuwa mbegu hizo waliuziwa na Kiwanda cha Brichand Oil Mill Ltd.
“Inaonekana ni mtandao licha ya kudai waliwauzia mbegu zilizooza lakini kulikuwa na ndoo za Kampuni ya Brichand Oil Mill Ltd…Ina maana mafuta yaliyokuwa yanazalishwa ilikuwa kampuni hiyo iyachukue…Hatujui wanayaingizaje sokoni yakiwa hivyo,” alisema Madaraka.
Viongozi wa viwanda
Meneja wa Bundaa Oil Mill Ltd, Rohan Parmar alikiri kukamatwa wakisaga mbegu chafu na kudai kwamba walipewa mbegu hizo na Kampuni Brichand Oil Mill Ltd.
Alipotakiwa kufafanua sababu za kukubali kupokea mbegu chafu wakati wakijua sheria hairuhusu alisema: “Kwanza muda huo nilikuwa Igunga sijui mambo mengi…Sisi tumepata shida sana tumekosa mbegu sasa tumesimamisha uzalishaji ….Hayo mengine sipendi kuyasemea.”
Baada ya gazeti hili kumbana kwamba alikuwapo kama msimamizi wakati TFDA walipowakamata, aling’aka akisema: “Sasa wewe unataka mambo mengi ya nini…Walikamata mbegu wakachoma ...Sisi sasa tumefunga kiwanda…Unataka nini tena…Mimi siwezi kusema mpaka mwanasheria wa kampuni awepo.”
Alipotakiwa kumtaja mwanasheria ili afuatwe kutoa ufafanuzi, Maramar alikataa akisema: “Siwezi kusema majina, wala alipo, wala namba…Wewe ‘tafuta’ sisi baada ya wiki moja.”
Jitihada za gazeti hili ziliwezesha kupatikana kwa Mwanasheria wa Kampuni, Denis Masami ambaye alipoulizwa kuhusu uzalishaji wa mafuta kwa kutumia mbegu zilizooza aliomba apewe nafasi ya kufuatilia kwa kuwa wakati wanakamatwa na TFDA alikuwa bado hajaajiriwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Brichand Oil Mill Ltd, Mohammed Sharif alikiri kiwanda chake kuwauzia Bundaa Oil Mill Ltd, mbegu chafu lakini kwa kwa ajili ya kusafisha `Boiler’.
“Walichukua kwa makubaliano kuwa wanakwenda kusafisha mashudu ili yawe meupe badala ya mafuta…Maana wana mtambo usio wa kawaida una uwezo wa kuchanganya mbegu zilizooza na safi ukasaga bila matatizo…Mitambo mingine haiwezi kufanya hivyo,” alisema.
Wasemavyo wananchi
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya wananchi walilalamikia mafuta yanayotokana na mbegu hizo, lakini kwa upande mwingine yalikuwa yakipendwa na wakaanga samaki kutokana na kuuzwa kwa bei rahisi ikilinganishwa na mafuta ya aina nyingine.
Mkazi wa Kijiji cha Migungani, Bunda ambao Kichere Gikaro (60 alisema kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa mafuta yalitoka katika Kiwanda cha Bundaa Oil Mill Ltd.
“Hapa kwetu sisi ndio tulitakiwa kuwa wateja wakubwa kwa kuwa kiwanda kiko hapa……lakini kutokana na malalamiko ya watumiaji wengi kuhusu ubora wake, tulilazimika kwenda kununua mafuta mengine mjini, malalamiko
aya yaliwafikia watu wa afya, lakini hatukupata majibu,” alisema Gikaro.
Muuzaji wa mafuta katika Soko Kuu la Bunda Mjini aliyejitambulisha kwa jina la Nashon alikiri kwamba alikuwa na wakati mgumu kuuza mafuta hayo kutokana na kulalamikiwa kwamba yalikuwa na uchafu pia harufu mbaya.
“Ilikuwa shida kweli maana licha ya kwamba bei yake iko chini lakini soko lake ni gumu sana, kama unavyojua sisi wafanyabiashara tunataka unaponunua mali basi itoke ili pesa yako izunguke,” alisema Nashon.
Naye Sundi Juma ambaye ni muuza samaki stendi Kuu ya Bunda, alisema yeye anayapenda mafuta hayo kutokana na ukweli kwamba ni mazito hivyo hayaishi haraka anapokuwa akikaanga samaki wake.
“Kwanza mafuta haya ni bei ni nafuu…Ni mazito, ukinunua kidogo unakaanga samaki wengi…unatumia gharama ndogo, ingawa wateja wanalalamika harufu hasa samaki wakila lakini kwetu ni nafuu…Maana mafuta mengine bei iko juu na ni mepesi,”alisema Juma.
Alisema bei ya mafuta hayo yanayozalishwa na Bundaa Oil Mill Ltd ni Sh 1,400 kwa lita moja, ikilinganishwa na mafuta aya aina nyingine ambayo yanauzwa Sh2,000 kwa kiasi hicho.
“Ukinunua mafuta ya bei kubwa unalazimika kuuza samaki pia kwa bei kubwa, wakaanga samaki hatuko tayari kununua mafuta ya bei ya juu…Kwa kuwa ukinunua wewe mwenzio anachukua ya bei ya chini, anauza samaki bei nzuri, wako wanabaki,” alisema.
Juma alikiri kuwapo kwa watu wanaolalamika kujisikia vibaya hasa wanapokuwa wanakaanga samaki kutokana na mvuke unaotokana na mafuta hayo kubadili hali ya hewa na kuwa nzito.
Madhara kiafya
Mmoja wa maofisa wa TFDA, Kanda ya Ziwa ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kutokana na kutokuwa msemaji wa taasisi hiyo, alisema miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata mtumiaji ni saratani.
“Uzalishaji wa mafuta hayo hutumia kemikali aina ya caustic soda ambayo kisheria lazima isimamiwe na mtaalamu, lakini hata mkemia hawakuwa naye…Wanazalisha mafuta kwa mbegu zilizooza…Wanawalisha watu vitu visivyo stahiki…madhara yake ni makubwa kiafya,”alisema.
Mfamasia na mmiliki wa zahanati binafsi wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Thomas Burito alisema madhara kwa watumiaji wa mafuta hayo ni makubwa kwa kuwa husababisha mishipa kuziba na matokeo yake ni watumiaji kuugua saratani na figo.
“Matumizi ya mafuta kama hayo ni hatari kwa maisha ya walaji, kiafya wanaathirika polepole na wengi hupata kansa, ugonjwa ya moyo, figo na hayo ni magonjwa hatari na mwisho kama hakuchukua hatua haraka ni vifo,” alisema Burito.
Ofisa Afya wa Wilaya Bunda, Fadhili Kinyogoli alisema matatizo ya kuzalisha mali zisizo na kiwango na kuziingiza sokoni ni kubwa kutokana na wananchi ambao ni walaji kutokutoa taarifa kwa wakati ili hatua ziweze kuchukuliwa.



ZABURI YA 72 ALIYOITUMIA DK,MATHAYO DAVID MATHAYO KUSALI WAKATI MAWAZIRI WALIPOWEKWA KITI MOTO KISHA KUMWAGWA


.1.Ee  mungu ,mpe  mfalme  hukumu   zako,  na  mwana  wa  mfalme   haki  yako.
2.Atawaamua  watu  wako kwa haki, na watu  wako   walioonewa  kwa  hukumu.
3.Milima  itawazalia  watu  amani,na  vilimaa  navyo  kwa  haki.
4.Atawahukumu  walioonewa  wa watu,atawaokoa  wahitaji  , atamseta  mwenye  kuonea.
5.Watakuogopa   wakati  wote  wa  kudumu  jua,na wakati  wa  kung’aa  mwezi  kizazi  hata  kizazi.
6.Atashuka  kama  mvua  juu  ya majani  yaliyokatwa,Kama  manyunyu  yainyweshayo  nchi.
7.Siku zake  yeye, mtu  mwenye  haki  atasitawi,na  wingi  wa  amani  hata  mwezi  utakapokoma.
8.Na   awe  na enzi  toka  bahari   hata bahari,Toka  mto  hata  miisho  ya  dunia.
9.Wakaao  jangwani  na wainame  mbele  zake;adui  zake  na  warambe  mavumbi.
10.Wafalme  wa tarshishi na  visiwa  na  walete  kodi,Wafalme  wa Sheba  na  Seba   na  watoe  vipawa.
11.Naam, wafalme  wote  na  wamsujudie,na  mataifa  yote   wamtumikie.
12.Kwa  maana atamwokoa  mhitaji  aliapo,na  mtu  aliyeonewa  iwapo  hana  msaidizi.
13.Atamhurumia   aliye  dhaifu  na maskini,na nafsi  za  wahitaji  ataziokoa.
14. Atawakomboa  nafsi  zao na  kuonewa  na  udhalimu,na  damu  yao  ina  thamani  machoni pake.
15.Basi na aishi;na  wampe  dhahabu  ya Sheba;na wamwombee  daima;  nakumbariki  mchana  kutwa.
16.Na  uwepo  wingi  wa  nafaka  katika  ardhi  juu  ya milima;matunda  yake  na yaweyawe  kama  lebanoni,
na  watu  wa  wastawi  kama  majani  ya  nchi.
17.Jina  lake  na  lidumu  milele,Pindi  ling’aapo  jua    jina  lake  liwe na wazao.
Mataifa  yote    na wajibariki  katika  yeye,na  kumwita  heri.
18.Na  ahimidiwe  Bwana,  Mungu,Mungu  wa  Israeli,atendaye  miujiza  yeye peke  yake.
19.Jina  lake    tukufu  na  lihimidiwe  milele;dunia  yote  na  ijae  utukufu  wake. Amina  na  amina.
20.Maombi  ya  Daudi  mwana  wa  yese  yamekwisha.
 

j



MISA YA SHUKRANI YA JUMUIA YA MT.MARIA NA KWAYA YA MARIA PAROKIA YA MUGUMU SERENGETI

 PAOKO WA KANISA KATOLIKI MUGUMU SERENGETI,AKIENDELEA NA MISA
 KWAYA YA MTAKATIFU MARIA MAMA WA MUNGU WAKIIMBA
 WAUMINI WA JUMUIA YA MT.MARIA WAKIPEANA AMANI
 TUNAIMBA
 POKEA MWILI WA KRISTO
 CHAKULA KINAPELEKWA UKUMBINI
NI WAKATI WA CHAKULA