Machi ,2014
Serengeti:WALIMU 37 wa shule ya Msingi Mapinduzi ‘A’iliyoko Mjini
Mugumu wilaya ya Serengeti,hulazimika kurudi kwenye makazi yao kujisadia kutokana
na shule hiyo kutokuwa na vyoo vya walimu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Ofisa Elimu wilaya hiyo William
Mabanga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo,na kudai kuwa ni shule nyingi hazina
vyoo vya walimu,kwa kuwa mkazo uliwekwa kujenga vyoo vya wanafunzi wakasahau
walimu,na kuahidi kuwa litashughulikiwa kwa kuwa athari yake ni kubwa kwa
walimu na watoto.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo James
Johannes amesema tatizo hilo lina muda mrefu,mamlaka husika zinataarifa lakini
hakuna hatua zilizochukuliwa kuwanusuru walimu
kwa kuwa wanaodharirika kwa kukosa vyoo na kuokoa muda wa vipindi ambao
huvitumia kurudi majumbani kujisaidia.
“ Mwalimu hutumia zaidi ya dakika 20 kutafuta eneo la kujistiri…hapa ni katikati
ya mji hawawezi kukimbilia vichakani…maana walimu 32 ni wakike , na wakiume 6 ,wanalazimika
kwenda kwenye miji yao ama majilani kujisaidia….na hii ndiyo shule ya
mjini,imeachwa hivi…tunaomba mamlaka zichukue hatua maana watoto wanakosa
mtiririko wa vipindi kwa tatizo hilo,”alisema Mwalimu kwa masikitiko.
Alisema awali walikuwa wanatumia
choo cha kanisa la Sayuni na baada ya kuweka uzio ,wakakosa sehemu ya
kujisaidia,na choo cha wanafunzi inakuwa vigumu kwa kuwa nacho kiko katika eneo
la mtu na matundu yaliyopo ni 12 kati ya mahitaji ya matundu 32 kwa watoto 890 waliopo
hapo shuleni.
“Baada ya kuweka uzio hatuna
sehemu ya kujisaidia…kwa mwalimu anayekaa shuleni anaye ana choo cha muda
ambacho kinadhalilisha maisha ya walimu….kuhusu vyoo vya wanafunzi tayari
tumeishapata notisi maana ni uwanja wa mtu anataka kuendeleza eneo lake….kuna
hatari ya shule kufungwa iwapo atazuia
hapatakuwa na jinsi,”alibainisha.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha NHC
,Elias Nyamraba anasema tatizo hilo linawadhalilisha walimu na kukosa morari ya
kufundisha ,na inapotokea amepata mchafuko wa tumbo hupata shida,hivyo Matokeo
Makubwa sasa hayawezi kupatikana katika mazingira kama hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Elimu,afya na Maji wilaya Daniel Kegocha alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwa
walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kukosa vyoo.
“Nilifika shuleni baada ya
kufuatwa na walimu,kweli hali ni mbaya …maana
wanaacha vipindi na kurudi nyumbani kutafuta vyoo kuna athari kubwa
kitaaluma…nitalifikisha hili tatizo halmashauri ya wilaya ili kuona jinsi ya kuchukua hatua za
haraka”alibainisha.
Kuhusu choo cha wanafunzi kuwa
katika eneo la mtu,diwani hiyo alisema hakuwa anajua na kubainisha yote
yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka ili kunusuru shule isijekufungwa.
Hata hivyo baadhi ya wananchi
walilaumu madiwani kwa kubadilisha matumizi ya eneo la mnada linalopakana na shule hiyo,viongozi
wakajigawia maeneo ambalo lingeweza kutumiwa na shule hiyo ili kuwanusuru
watoto wanaokwenda kujisaidia eneo la jilani kwa kuvuka barabara kuu,hali
ambayo ni hatari kwa usalama wao.
Kwa mjibu wa taarifa ya wilaya
,inabainisha kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo kwa
walimu 1,401,ambapo toka mwaka 2009 mpaka 2013 wamejenga matundu 25 tu,upungufu
wa madawati ni 16,460,ambapo zaidi ya asilimia 50 wanasoma wakiwa wamekaa
chini.
Mwisho.